Pages

Sunday, August 20, 2017

BIASHARA YA KICHAWI

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO

JUMAPILI: 20 AUGUST, 2017


MHUBIRI: PASTOR, Dr.  GODSON ISSA  ZACHARIA (Snp)



Biashara ni shughuli inayotambulika kisheria kwa ajili ya kuuza au kununua bidhaaa fulani ili mtu apate faida. Kwenye biashara kuna mfanya biashara, bidhaa, na lengo lake ni kupata faida. Kwa hiyo biashara ya kichawi ni ile biashara inayofanywa na mawakala wa kishetani. Wafanya biashara wake ni wachawi ambao ni wanadamu. Siku zote wanawadanganya watu na kuwapokonya mali zao. Kwenye biashara hii kuna taaaluma nyingi, mfano: Afisa usafirishaji, Afisa mawasiliano, wataalam wa udanganyifu na wachumi wanaoangalia kipi kifanyike ili wapate fedha. Wapo wataalam wa kuteka na kuhakikisha wapate watu wa kuwateka.

Wachawi kupitia wataalam wa uchawi, watu wanakuwa masikini, fukara, wenye taabu na mateso ili wao watumie nyota zao. Biashara ya kichawi huwa inalenga kuleta mauti katika maisha ya watu. Mchawi ni mtu mwenye roho ya uchawi ndani yake. Wachawi ndio wachuuzi katika biashara hii.

Habakuki 2:5 Imeandikwa, Naam, pamoja na hayo, divai ni mchumi mdanganyifu, mtu wa kiburi asiyekaa nyumbani mwake; huongeza tamaa yake kama kuzimu, naye huwa kama mauti, hawezi kushibishwa; bali hujikusanyia mataifa yote; hujiwekea kabila zote chungu chungu.   

Kutoka 22:18 Imeandikwa, Usimwache mwanamke mchawi kuishi. Hii ni biashara inayovuviwa lakini ina wasimamamizi. Divai ndio mchumi mdanganyifu. Uchami watu wengi uharibikia kwenye ulevi.

Ufunuo wa Yohana 18:11:13 Imeandikwa,  ‘Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; 12 bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; 13 na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.’ Hapa neno la Mungu linataja baadhi ya bidhaa katika biashara, zaidi unaweza kujifunza kuwa mtu anaweza kuibiwa na kuuzwa ama mwili wake au roho yake. Watu waliokufa katika mazingira tata wanaweza kuuzwa kutoka kwa mchawi mmoja na kwenda kwa mwingine.

Baadhi ya makutano wakifuatilia mafundisho ya neno la Mungu  katika nyumba ya Ufufuo na Uzima Morogoro.
Walawi 20:27 Imeandikwa, ‘Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.’ Kadri unavyowapiga ndivyo watakavyokimbia na kuondoka maishani mwako. Sisi tunabeba neno la Bwana ndio jiwe letu. Kwa jina la Yesu wachawi lazima wapigwe.
Wachawi siku zote wana waloga watu kwa sababu ya Wivu tu.kwahiyo hapa tunajifunza kuwa chanzo cha wachawi kumloga mtu ni wivu. Kwa kawaida kila taarifa njema unayowapa marafiki zako, si wote wanaofurahia. Kumbuka taarifa zako za kushinda, faida katika biashara zako, mavuno na ustawi, tangu ulipozitoa ndipo matatizo yalipo anza. Mateso na shida unazoziona zinatoka kwa wachawi.

Kumbukumbu la Torati 18:10-11 Imeandikwa, ‘Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.’ Mungu hapendi mambo ya uchawi na wasoma nyota. Uchawi una madhara kuliko ambavyo tunaweza kuwaza. Mfano, mtu alikuwa mwenye miguu iliyojaa Baraka lakini ghafla anaugua miguu. Mtu akisha ugua basi hawezi kutembea na kukutana na Baraka zake.
Kuchukua watu Misukule. Hii ni madhara ya biashara za kichawi. Uchawi unaweza kusababisha nyota, kazi, fursa zikapotea na hatimaye mtu anakua masikini.  Mtu anaibiwa eneo moja na kuuzwa eneo lingine,

Nahumu 3:1-4 Imeandikwa, ‘Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki. 2 Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye kuruka-ruka; 3 mpanda farasi akipanda, na upanga ukimeta-meta, na mkuki ukimemetuka; na wingi wa waliouawa, na chungu kubwa ya mizoga; mizoga haina mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yaoKwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake..’ Kuna watu leo wametekwa na wanapigwa mijeledi na wachawi. Misiba na machozi imekuwa mingi katika miji kwa sababu ya biashara ya uchawi. Watu wanalia na kuomboleza kwa sababu ya uchawi. Watoto hawawezi kusoma tena, vijana wamependa anasa kuliko Mungu kwa sababu ya uchawi. Mchawi anaweza kuuza taifa moja kwa nchi nyingine. Kama mchawi anaweza kuuza mtu mwingine au taifa, basi mchawi anaweza kuuza nyota, miguu na mikono yenye Baraka, uso au kinywa chenye kibali. Macho yanaweza kuuzwa ndio maana una matatizo ya macho.

Biashara ni kubadilishana. Kwa baishara za kichawi, wakiiba uso au nyota lazima waweke pepo wa balaa na mikosi. Wanaweza kuuza kibali cha mtu na ukawekewa roho ya kukataliwa. Ezekieli 13:18-19 Imeandkiwa,’ useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? 19 Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. 20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege. 21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.’ Wachawi wanawinda roho za watu. Mtu akiwa na nyota nzuri au kibali, akiwindwa utaona anaanza kuchanganyikiwa. Kumbe kuna mambo yaliyokupata kwa sababu ya nyota, kibali au Baraka ulizopewa na Mungu. Wasimamizi wa biashara ya kichawi wanauza kilicho bora ili kitumike kuzalisha katika ufalme wa shetani.

Platform wakimsifu Mungu wakati wa Ibada.
MAOMBI
Katika jina la Yesu Imeandikwa hapana uchawi juu ya Yakobo wala uganga juu ya Israeli nakufuata ewe mchawi uliyeshikilia nyota yangu,akili yangu ya biashara,miguu yangu,mikono yangu,kibali changu, nakufuata popote ulipo nakupiga kwa jina la Yesu ,nawashambulia kwa mawe achia akili yangu,leta nyota, leta mikono yangu ya kufanya biashara.

Leo ni siku ya kushambulia biashara za kichawi na kufuta kabisa nguvu zao kwa Jina la Yesu. Endapo kuna mtu ambaye hajampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yake binafsi, leo ni muhimu kufanya maamuzi hayo ya kuokoka ili kufanyika kiumbe kipya.


©  MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH