Pages

Wednesday, August 23, 2017

KIJANA JOSEPHAT ASHUHUDIA ALIVYOLOGWA BAADA YA KUFANIKIWA KUJENGA NYUMBA

                                               UFUFUO NA UZIMA MOROGORO.

wa tatu tokea kulia ni kijana Josephat, wa kwanza toka kulia ni dada yake akidhibitisha.
Kama maandiko yasemavyo katika kitabu cha kutoka 22:18 ``usimwache mwanamke mchawi kuishi”hii ni alama sahihi ya kuonesha hasira ya MUNGU juu ya wachawi. Hii imedhihirika baada ya kijana Josephat Steven kutoa ushuhuda kuhusu namna alivyologwa kwa mafanikio aliyoyapata baada ya mda mrefu wa kuhangaika na maisha yake.kijana huyu alikuwa akiishia maneneo ya Doma mkoani Morogoro,amesimulia namna alivyologwa baada ya kufanikiwa kujenga nyumba akiwa anafanya kazi yake ya kukata mkaa na kuuza.

Josephat akitoa ushuda huo namna alivyologwa anasema``baada ya kuwa nimefanya biashara zangu za kuuza mkaa,nilifanikiwa kujenga nyumba ambayo ia vyumba viwili na sebule,mara usiku mmoja  nikaota ndoto kuna mtu ananifukuza na nikawa nakimbia,tangu siku hiyo nikawa nawaogopa watu, na nkawa sitaki kutoka nje ya nyumba, na hivyo nikawa nakaa uvunguni mwa kitanda changu’’amesema kijana Josephat. Kijana huyo amesema ,hata alipokuwa akikaa humo ndani ya hiyo nyumba bila ya kutoka nje hakuwa hata akihisi kuwa na haja kubwa wala ndogo kiasi cha kujaribu kutoka nje, maana hakuwa anakula chochote. Zaidi saana alikuwa akiogopa kuonana na watu, hivyo alikaa ndani siku zote chini ya kitanda, na alikuwa akitoka nje usiku tu ili kukwepa kuonana na watu.

Baada ya kuonekana kuwa na hali hiyo, ndipo ndugu zake walipoanza kuhangaika kwa waganga wa kienyeji,amabapo wakiwa wanaelekea kwa mganga wa mwisho maeneo ya kingulwira mkoani Morogoro ambaye aliwapa utaratibu wa kuleta kuku mwekundu na pesa kiasi cha shilingi laki moja. Badaye wakiwa katika kujiandaa kuelekea kwa huyo mganga,mtu mmoja akawaambia nendeni ufufuo na uzima wanaweza kumwombea na akawa sawa,wakapitia kanisa la ufufuo na uzima Morogoro na kuombewa na kurudia hali yake ya kawaida kama binadamu wengine.

Kijana Josephat kwa sasa amekwisha funguliwa na kuwa na akili zake timam  kama vijana wengine na anaendela kuabudu na kujifunza  katika kanisa la ufufuo na uzima Morogoro linaloongozwa na Askofu Dr.Godson Issa Zacharia.

Watu wote ambao wanapata mateso ya kulogwa na wachawi na kuharibiwa mipango na mifumo ya maisha, kanisa la ufufuo na uzima lipo kwa ajili ya kushughulika na mambo hayo,na kudhihirisha ukuu wa Mungu aliye hai. Karibu ufufuo na uzima Morogoro, eneo la mkundi minara mitatu.