Pages

Sunday, August 13, 2017

KUJIONDOA KWENYE KITABU CHA UKOO - Semina Siku ya 7

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (G.C.T.C)
                 {KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ­- MOROGORO}
                              
                              JUMAMOSI: 12 AUGUST 2017

MHUBIRI:  PASTOR GODFREY MWAKYUSA (SNP-SHINYANGA) 


Kama unavyojua kila mahali unapoenda iwe kwenye maofisi au mahali popote unapofika mapokezi lazima ujiandikishe kwenye kitabu. Imeandikwa katika Kutoka 32:33
33 Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.
Tunaona Mungu ana kitabu ambacho majina ya watu wake yaani watakatifu yameandikwa. Utaona pia katika kitabu cha Mwanzo 5:1 1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; Unaona Adamu alipoumbwa akawa na kitabu kilichoandikwa kizazi chake. Imeandikwa pia katika Mwanzo 6:9
9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu. Nuhu alikua mtu wa haki na ndio maana sifa yake inazungumziwa hapa
Mwanzo 9:1
1 Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.
Mungu alipotaka kumbariki Nuhu alimbariki Nuhu na wanawe,kumbe Baraka huanzia kwa baba kwenda kwa mtoto.Kuna koo wanaruhusiwa waolewe lakini wasidumu kwenye ndoa unakuta dada mkubwa karudi nyumbani ,dada mdogo ,na wote ndoa zimevunjika mpo nyumbani alafu mnaona ni maisha ya kawaida kabisa ,familia hii tayari wameshaandikwa kwenye kitabu,kuna mwingine unatembea lakini kwenye ulimwengu wa roho kuna kitabu kimeandikwa hakuna kufanya biashara,wengine mmewekewa masharti ya kutokula vyakula fulani fulani kwamba ukoo hauruhusu.
Kuna mwingine umeingizwa kwenye kitabu cha mganga wa kienyeji,ulipoenda akakuchanja chale tayari ameshakusajili kwenye kitabu chake ,hata makampuni kuna makampuni yameajiri watu unakuta unalipwa mshahara mdogo sana lakini upo tu hata kujenga huwezi tena kumbe kampuni hiyo imeshawaandika majina yenu hamtakiwi kujenga wala kuwa na maaendeleo .Kuna ukoo wanakufa kwa ajali tu familia nzima kuanzia mkubwa hadi mdogo,wengine vifo vyao ni kujinyonga unakuta majina yenu yameandikwa kwenye kitabu cha kichawi kwamba wote mfe vifo vya kufanana.
Imeandikwa katika Mathayo 1:1
1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo,hata Yesu alikua na kitabu unaweza ukakuta mtu ana kipawa kizuri tu lakini mashetani wakapanda tabia zinazokufanya uchukiwe na watu,maisha ya mtu yana umuhimu sana na kitovu chake,kitovu kinaweza kikanuiziwa maneno kikafungwa na kuwekwa kwenye chungu hapo ndipo maisha yako yatakapoanza kuharibika tayari wameshakuandika kwenye kitabu chao.
Agano ni baina ya Mungu na wanadamu,na mkataba ni baina ya mwanadamu na mwanadamu,kuna uwezekano wewe upo hapo lakini jina lako lipo kwenye madhabahu za kichawi,kuna vitabu vya aina mbali mbali kuna kitabu cha mafarakano yani siku haipiti ulishagombana na mume wako tayari,kuna kitabu cha madeni wewe kazi yako ni kukopa tu.
MAOMBI:
Katika jina la Yesu ninakifuata kitabu mahali popote kilipo kilichoandika jina langu nakichoma moto ,nakiteketeza kwa jina la Yesu,naivunja mikataba iliyowekwa na baba ,bibi navunja leo kwa damu ya mwanakondoo ,nahama kwenye ukoo,nahama na familia yangu .