Pages

Sunday, August 13, 2017

KURUDISHA ASILI YETU - Semina Siku ya 5

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (G.C.T.C)
                 {KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ­- MOROGORO}
                              
                              ALHAMIS: 10 AUGUST 2017

MHUBIRI:  PASTOR GODFREY MWAKYUSA (SNP-SHINYANGA) 


Asili ni ile hali ya kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza, Mungu alivyomuumba mwanadamu alimleta duniani akiwa na asili yake ya kule alikotoka yaani mbinguni
Mwanzo 1:1-3 Imeandikwa, “Hapo mwanzo Mungu aliziumba (mbingu) na nchi. Nayo nchi ilikuwa (ukiwa) tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwenuru; ikawanuru.”.
Mwanzo 1:26-27 Imeandikwa “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”
Mwanzo 2:7Imeandikwa, “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Mungu akasema kwa asili mwanadamu ni roho kutoka kwa Mungu. Kwa hiyo roho ya mtu ndio mtu mwenyewe. Mungu baada ya kuumba akawabariki wanadamu.
Mwanzo 1:28 Imeandikwa, “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, nakuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”…lazima uzae kwa sababu ni asili yetu kuzaa hapa duniani. Kwa hiyo kutokuzaa hapa duniani huwakuna roho inayosababisha tatizo hilo. Ndiyo roho ya utasa. Mpango wa Mungu kwa wanadamu ni kuzaa, kutawala na kutiisha. Tumepewa asili ya kutiisha kila kiumbe. Kwa hiyo usiogope wachawi au waganga.
1Wakorintho 15:47-48 Imeandikwa
47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, niwa udongo. Mtu wapi liatoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.
Hapa tunajifunza kwa asili sisi tunatoka mbinguni. Kwa hiyo lazima uishi, utembee au utende kama ilivyo asili yako. Lazima kila unachokifanya kiongezeke na sio kuanza na kuishia njiani. Tamka na utende kama baba wa mbinguni atendavyo. Kama alivyo baba ndivyo atakavyokuwa mwana. Kwa asili ni haki yetu kumiliki mali, afya, kutawala tukiwa hapa hapa duniani. Lazima ulime na kula matunda ya nchi. Kwa hiyo asili ya mtu inaweza kuibiwa na shetani.
Shetani aliwadanganya Adam na Hawa wakala tunda, ule utukufu ukaondoka. Baada ya kula lile tunda ndipo utukufu wa Bwana ukawaondoka. Baada ya hapo mwanadamu akalaaniwa.Taabu zote zimeanzia kwenye dhambi. Kumbe dhambi ndiyo inayoondoa asili yetu.
1Wakorintho 15:38 Imeandikwa
38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.
Lakini Yesu alikuja ili kurudisha asili yetu kwa kufa msalabani.
Yohana 3:16 Imeandikwa,
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
“….Baada ya kuona wanadamu wamepoteza asili yake akamtuma mwanae wa pekee.
Ufunuo 5:9-10 Imeandikwa
,9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
“Hapa tunaona Yesu alikuja kufungua na kuturudishia asili yetu. Asili ikirudi ukianza biashara, kazi, mradi, unafanikiwa.
Zaburi 82:6-7 Imeandikwa, “Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia. Lakini mtakufa kama wanadamu, Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.”
Shetani anaweza kuwapandia wanadamu asili ya ugonjwa, kukataliwa, kuonewa, kuibiwa au madeni. Lazima ukatae na kuvua asili ya kuzimu kwa jina la Yesu.
MAOMBI:
Katika jina la Yesu kuanzia leo narudi kwenye asili yangu ,asili ya kufanikiwa ,asili ya kuolewa ,asili ya uzao ,asili ya kufanya biashara kwa jina la Yesu.