Pages

Sunday, August 13, 2017

KURUDISHA NYOTA - Semina Siku ya 4

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (G.C.T.C)
                 {KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ­- MOROGORO}
                              
                              JUMATANO: 09 AUGUST 2017

SEMINA SIKU YA 4

MHUBIRI:  PASTOR GODFREY MWAKYUSA (SNP-SHINYANGA) 


Nyota ni nini ?
Nyota ni kibali cha mtu anachopewa na Mungu tangu anapozaliwa
Yeremia 1:4-5
Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa
Hesabu 24:7
Maji yatafurika katika ndoo zake, Na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi. Na mfalme wake ataadhimishwa kuliko Agagi,
Na ufalme wake utatukuzwa.
Kabla hujazaliwa nyota yako inaanza kuonekana ,kuna watu walianza vizuri waliahidiwa mambo mazuri na ndugu ,waliota wana biashara nzuri lakini leo zimepotea zote
Mathayo 2:1-4
Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?
Yesu alipokua amezaliwa mama jusi wakaiona nyota yake wakaanza kuifuatilia na kuisujudia na kutoa uvumba na mane mane,lakini usiku walipolala malaika akawatokea akawaonya wasimrudie tena Herode maana anataka amuangamize mtoto.Kumbe Herode alikua na nia mbaya, nyota ya mtu inapoonekana lazima .wakufuate ,kwenye familia ni lazima kuna mtu ambaye Mungu anamuinua ili aje awainue wengine,wachawi wanapoiona nyota wanaanza kuifuatilia.
Njia mbili zinazotumiwa na wachawi kufunika nyota ya mtu au kuichukua:
Njia ya kwanza mtoto anapozaliwa huwa wanachukua vile vitovu vya watoto wanapozaliwa na kwenda kuvifunga kiuchawi hata kama watoto wangesoma vipi hawatafanikiwa maana wachawi wameshikilia vitovu vyao.
Mwingine ulilala usiku wakakunyoa nywele,mtu anashambuliwa tangu akiwa anaanza maisha yake,nyota ya mtu inaonekana tangu akiwa mdogo wanaanza kuona mtu huyu atakua mfanyabiashara mkubwa ,mtu huyu atakua na ndoa njema.Kuna mtu una watu wanaotakiwa wakupigishe hatua,nyota ya mtu inapoonekana unakua na upendeleo kibali kinaanza kuonekana ,unapookoka ndani yako unakua umembeba Yesu anasubiri tu wewe useme na yeye atende,kuna mtu mwingine nyota yake ni mbunifu,mwingine ni muombaji lakini leo huombi tena wachawi wameiba nyota yako lakini leo tunakwenda kuirudisha kwa jina la Yesu,kuna faida kubwa sana ya kuwapiga adui zako wewe mwenyewe.
MAOMBI :
Katika jina la Yesu natembea kwenye ulimwengu wa roho nayafuata mashimo yote yaliyoficha nyota yangu nayabomoa kwa jina la Yesu,nawakamata wachawi wote walioshikilia nyota yangu nawapiga wote kwa jina la Yesu,nyota ya kazi njooo kwa jina jina la Yesu,nyota ya upendeleo njooo kwa jina la Yesu……………