GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA
{MOROGORO}
JUMAPILI:
22 OKTOBA, 2017
Huyu ni binti mdogo tu, aliletwa kanisani wakati wa ibada ya katikati
ya wiki kwa maombi. Mama yake anaitwa Evelina
Msumba anaishi mtaa wa Mkundi. Siku ya Jumanne mwanae alidondoka shuleni, na mama
akapewa taarifa hii. Kilichotokea ni kuwa, alikosa fahamu akiwa shuleni, baada ya
mtu mmoja aliyeanza kumuita Jina Lani, Lani. Hapo shuleni kuna mwalimu ameokoka,
ambaye alianza kumuombea na akapata nafuu. Siku ya Jumatano tatizo hili lilijirudia
tena.
Aliyesimama Kushoto ni Bethra, kulia ni mama yake mzazi akitoa ushuhuda, katikati ni Mchungaji kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia. |
Siku ya Alhamisi mama yake
aliitwa shuleni na kusimuliwa yaliyotokea. Kwamba Bertha alikuwa anakimbia tu kwa kuwa anamuona huyo mtu
anayeitwa Lani. Bertha alikuwa miongoni mwa watoto zaidi ya 370 waliopata Kipaimara
katika Kigango cha Kihonda, Kanisa Katoliki. Lakini miongoni mwa hao watoto kuna
mmoja wao ambaye anakuwa anatoa cheche akiangaliwa usoni. HuyoLani alimkataza asisimulie
kitu chochote kwa mtu yeyote.
Siku ya maombi, Bertha anasema
kuwa kwa wiki 2 zilizopita alikuwa amechukuliwa hadi baharini. Je, aliyekula sakramenti
ya kipaimarani ni nani? Bertha alisema Lani alikuwa amekuja na kuvaa sura ya
Bertha na kuwa ndiye alikuwa anafanya kila kitu na hata kwenda
shuleni (Top Star) na kula sakramenti siku ya Kipaimara.
Bertha akihojiwa na Mchungaji kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia katika ibada ya leo. |
Huko Baharini anasema alikuwa na
wanaume wengi sana huko, wakiwa wanamchezea kwa kupiga ngoma na nyimbo asizozijua.
Je, alitokaje huko baharini? Wakati anafanyiwa maombi hapa katika nyumba ya Ufufuo
na Uzima Mkundi Morogoro, yale maombi yalifanya wale waliokwuwa wanamshikilia waungue
kwa moto. Waliomshikilia walisema wanamuachia kwa sababu Yesu wake amekuja mle baharini
na hivyo wanamuogopa na kumuachia.