Sunday, October 22, 2017

BINTI BERTHA MWANJA ASHUHUDIA NAMNA ALIVYORUDISHWA KUTOKA CHINI YA BAHARI

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA

{MOROGORO}

JUMAPILI: 22 OKTOBA, 2017

Huyu ni binti mdogo tu,  aliletwa kanisani wakati wa ibada ya katikati ya wiki  kwa maombi. Mama yake anaitwa Evelina Msumba anaishi mtaa wa Mkundi. Siku ya Jumanne mwanae alidondoka shuleni, na mama akapewa taarifa hii. Kilichotokea ni kuwa, alikosa fahamu akiwa shuleni, baada ya mtu mmoja aliyeanza kumuita Jina Lani, Lani. Hapo shuleni kuna mwalimu ameokoka, ambaye alianza kumuombea na akapata nafuu. Siku ya Jumatano tatizo hili lilijirudia tena.
Aliyesimama Kushoto ni Bethra, kulia ni mama yake mzazi akitoa ushuhuda, katikati ni Mchungaji kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia.

Siku ya Alhamisi mama yake aliitwa shuleni na kusimuliwa yaliyotokea. Kwamba Bertha  alikuwa anakimbia tu kwa kuwa anamuona huyo mtu anayeitwa Lani. Bertha alikuwa miongoni mwa watoto zaidi ya 370 waliopata Kipaimara katika Kigango cha Kihonda, Kanisa Katoliki. Lakini miongoni mwa hao watoto kuna mmoja wao ambaye anakuwa anatoa cheche akiangaliwa usoni. HuyoLani alimkataza asisimulie kitu chochote kwa mtu yeyote.

Siku ya maombi, Bertha anasema kuwa kwa wiki 2 zilizopita alikuwa amechukuliwa hadi baharini. Je, aliyekula sakramenti ya kipaimarani ni nani? Bertha alisema Lani alikuwa amekuja na kuvaa sura ya Bertha na kuwa ndiye alikuwa anafanya kila kitu na hata kwenda shuleni (Top Star) na kula sakramenti siku ya Kipaimara.
Bertha akihojiwa na Mchungaji kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia katika ibada ya leo.

Huko Baharini anasema alikuwa na wanaume wengi sana huko, wakiwa wanamchezea kwa kupiga ngoma na nyimbo asizozijua. Je, alitokaje huko baharini? Wakati anafanyiwa maombi hapa katika nyumba ya Ufufuo na Uzima Mkundi Morogoro, yale maombi yalifanya wale waliokwuwa wanamshikilia waungue kwa moto. Waliomshikilia walisema wanamuachia kwa sababu Yesu wake amekuja mle baharini na hivyo wanamuogopa na kumuachia.





Share:
Powered by Blogger.

Pages