GLORY OF CHRIST
TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFUO NA
UZIMA MOROGORO
JUMAPILI TAR, 19
NOVEMBA 2017
MHUBIRI: MCHUNGAJI KIONGOZI
DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
Mchungaji Kiongozi Dkt. Godson Issa Zachari akifundisha neno la Mungu. |
Kuteka nyara ni kumnyima mtu uhuru wake wa kutenda kama apendavyo. Kumteka mtu ni tendo linalotokea katika mazingira maalum. Mtu aweza kutekwa kwa sababu ya matendo ya kigaidi katika ulimwengu wa wanadamu. Kutekwa yawezekana kukawa kwa kutekwa rohni au mwilini. Lakini hapa tutajifunza kwa habari ya kuwateka nyara walinzi wa rohoni. Kwa kawaida shetani anatenda kazi katika ulimwengu na ufunga maisha ya watu kupitia rohoni usikoweza kuona kwa macho.
2 Wakorintho 10:3 – 5 imeandikwa, “Maana ingawa tunaenenda katika mwili,
hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili,
bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila
kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila
fikira ipate kumtii Kristo;” Paulo anasema ingawa tunaenenda katika mwili ila vita vyetu
ni katika ulimwengu wa roho. Paulo ni mtume aliyeandika karibia ya nusu ya
vitabu vya Agano Jipya. Paulo anasema ingawa tunaenenda katika mwili, vita yetu
si juu ya mwil na nyamai. Mtume Paulo anatujulisha kwamba kwenye maisha haya
kuna vita. Kuna vita kubwa sana, ingawa tunaenenda katika mwili vita si juu ya
mwili. Ukubwa wa kile ulichopewa na Mungu ndio ukiubwa wa vita yako.
Tuna silaha, na silaha
zetu si za kimwili, ila zina uwezo wa kuangusha ngome katika ulimwengu wa roho.
Hizi silaha zinauwezo katika Mungu, kuangusha ngome, kuangusha hata mawazo. Kuangusha
kitu chochote kinachojiinua juu ya elimu ya Mungu. Vita ipo na silaha zipo.
Silaha hizi tunaziona kataika Waefeso 6:
10 – 12 Imeandikwa, “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na
katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga
hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali
ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo
wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Neno la Mungu linasema vita yetu ni ya kiroho. Kuna wafalme,
wenye mamlaka, na majeshi ya pepo mabaya. Shetani amegawa majeshi yake katika
ngazi tofautitofauti, kama tunavyoona majeshi ya majini, angani, nay a nchi
kavu. Leo tunatakiwa kuwateka nyara hawa mashetani, wakuu wa giza, mapepo wote
katika ulimwengu war oho. Unaweza ukawa umefungwa kwenye tatizo, halafu
aliyekufunga ametoa kafara ndogo, mapepo yanayokuja ni ya ngazi ya nchi na
kumfungua ni rahisi kuliko aliyetolewa kafara kubwa mapepo yanayokuja ni ya
ngazi ya mfamle na anayetakiwa kumfungua anatakiwa awe na ngazi ya kifalme.
Baadhi ya makutano wakisikiliza neno la Mungu wakati wa Ibada |
Mashetani kazi yao kubwa kabisa ni kukulinda na kuharibu maisha yako. Hawa walinzi usipowateka nyara na kuwateketeza wanaenda na kurudi na utajikuta unarudia tatizo hilohilo. 1 Petro 5:8 Imeandikwa, “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzungukazunguka, akitafuta mtu ammeze.” Yaani ibilisi ni mshtaki wetu, tena anazungukazungua akitafuta mtu ammeze. Walinzi hawa wanaouwezo wa kumeza, ndoa, biahshara na ukabaki huna kitu kumbe amemeza. Tunajifunza kwa Yona alivyoacha njia ya Bwana akamezwa na samaki. Na Baadae alirudishwa na samaki akamtapika na Yona akaanza kuhubiri. Kuna watu wamemeza kazi, ndio maana huna kazi au kila ukitafta kazi hupati, huna watoto, nyumba kumbe wamemeza. Leo kwa jina la Yesu waliomeza macho, akili, nyumba, kama ni kazi lazima uwateke na kuwatapisha kwa jina la Yesu. Mungu si mwanadamu hata aseme uongo, ni dhahiri kwamba wapo waliomeza hatima yako. Wateke nyara hao na wewe utamiliki kwa jina la Yesu.
Yohana 5:25 Imeandikwa, “Amin, amin, nawaambia, Saa
inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale
waisikiao watakuwa hai.” Saa ipo wafu watafufuka kwa jina la Yesu.
Mwana wa Mungu ni wewe na kama ilivyoandikwa
katika Yohana 1:12, “Bali
wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake;” Leo waliomeza vitu vyako watatekwa nyara. Kuteka
nyara ni kumnyima mtu uhuru wake wa kutenda kama apendavyo. Wachawi wanaweza
kumeza miguu, au mikono, fedha, tumbo, macho, kichwa. Amua kuwateka nyara maadui
zako na majeshi yao kwa jina Yesu.
Wanakulinda wewe ubaki kwenye matatizo, wanaweza kulinda kazi
yako, maisha yako kwa umilele. Tatizo ulilo nalo sio tatizo la mwenzako. Na
ahawa walinzi wanamlinda kila mtu kwenye tatizo lake. Ili ukae kwenye tatizo
hilo wanakudhohofisha kwanza kimwili wanakupiga ili ukose nguvu. Waamuzi
16:21 Imeandikwa, “Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho;
wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa
akisaga ngano katika gereza.” Tunaona Samsoni alikamatwa na akafungwa kwanza
kabla ya kuwekwa gerezani. Baada ya kumfunga kinachofuata ni mateso na
kuhakikisha hatoki shimoni. walinzi majini au mapepo ndio wanaohakikisha hawezi
kutoka kwenye vifungo vya ibilisi. Mateso haya hayatokani na Mungu, Maombelezo 3:33 imeandikwa, “Maana
moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.” Mungu hapendi
uteseke. Kumbe mabaya yanayokukabili hutoka kwa shetani.
Kutoka 3:7 Imeandikwa, “Bwana akasema, Hakika nimeyaona
mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya
wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; ” Mungu anasema amesikia
kilio chako kwa ajili ya walinzi wako, Mungu atakutoa leo katika jina la Yesu. Isaya 14: 17 imeandikwa, “Aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?”
Ni kanuni ambayo imewekwa katika utawala wa shetani kwamba kila aliyefungwa
hatoachiwa. Hawa walinzi hawataki hata mara moja uondoke kwenda kwenye furaha, Baraka
na utele wa maisha yako.
Marko 5: 1- 12 imeandikwa, “Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka
nchi ya Wagerasi. Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu,
ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa pale
makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa
minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo,
akaikata ile minyororo, na kuzivunjavunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa
na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na
milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe. Na alipomwona Yesu kwa
mbali, alipiga mbio, akamsujudia; .. akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema,
Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.
Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako
nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, a kwa kuwa tu wengi. Akamsihi sana
asiwapeleke nje ya nchi ile. Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la
nguruwe, wakilisha. Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe,
tupate kuwaingia wao.” Tunaona
pepo aliomba wasitolewe, mapepo yalikuwa ndani ya mtu. Na mtu huyu alikuwa na
nguvu za ajabu, na hakuwa na msaada, kwa sababu walinzi walimlinda akae na
shida yake.
Unaweza ukawa na ndugu yako aliye na tatizo la akili, kumbe
sio kichaa ila ni walinzi wanamlinda kwenye shida hiyo, kwa sababu wameona
uwezo wake wa akili. Usikubali kumwita ndugu yako kichaa tena sema ni mzima kwa sababu kuna nguvu
katika kukiri. Unakuta unatafuta kazi hupati, tatizo si kazi, shughulika na
walinzi wanaokulinda usipate kazi. Yawezekana hujawai kupata mimba, kuanza
ujenzi au biashara ni kwa sababu kuna walinzi wanaokulinda ili usiingie kwenye Baraka
zako.
Unakuta wewe mwenyewe unakataa maombi, kumbe lengo lao hao
walinzi wanakulinda usiende kwenye kesho yako kupitia maombi. Unalindwa ili
ukianza kitu kishindikane, uharibikiwe, ushindwe na ukianza tu ndugu wanageuka
kuwa adui. Unaweza pata msaada ila baadae unageuka. Anaonekana kama mwenye
mwelekeo wa kukusaidia ila kumbe ana kusudio la uovu nyuma yake. Ukiri: kuanzia
leo, mizimu, roho za watu waliokufa zamani, wanaonilinda katika shida
niliyonayo nawashinda kwa jina la Yesu, Amen. Mashetani mlioniingiza katika
shida nawashinda kwa damu ya Mwankondoo, leo nakataa kuwa mateka bali nawateka
nyara adui zangu kwa jina la Yesu.
Showers of Glory wakimsifu Mungu wakati wa Ibada. |
========== AMEN ========
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI TUWASILIANE KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr
Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson
Zacharia
TEL: +255 719
798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo
na Uzima