Pages

Sunday, November 12, 2017

KUVISHUSHA VILIMA VYA UHARIBIFU

GROLY OF CHRIST  TANZANIA CHURCH (GCTC).

[KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO].

JUMAPILI : 12 NOVEMBA 2017.

MUHUBIRI: MCHUNGAJI DKT.GODSON ISSA  ZAKARIA.
Mchungaji kiongozi Dkt. Godson Issa Zacharia akifundisha somo la leo kuhusu vilima vya uharibifu.

2 Wafalme 23:13
imeandikwa, “Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi”.
 Mfalme alijenga vilima vya uharibifu kwa ajili ya Israel akapabomoa. Kuna vilima vya uharibifu watu wanajengewa ili kuleta uharibifu. Milima ni mahali palikoinuka sana kuliko tambarare zote. Milima hii ni mahali ambapo waganga wa kienyeji, wachawi, wasihiri au wasoma nyota, wanapofanyia mipango ya kuleta uharibifu kwenye maisha ya watu duniani. Wachawi huwa wanatoka katika miili yao na kukutana ili kupanga mipango ya uharibifu kwenye ulimwengu wa roho. Kwenye vikao hivi wanafanya mapatano, ili wewe uharibikiwe, ufukuzwe kazi, uchumba uharibike, au uaibike. Kwenye milima hii kuna idara ya mawasiliano. Idara hii inahusika na usambazaji wa taarifa za uovu wao ambazo zinawapendeza wanadamu. 
Platform wakiongoza kipindi cha sifu na kuabudu.

Wapo waandishi wa habari za kichawi, na ndio maana habari mbaya inatembea kwa haraka mno, mfano habari uovu juu ya kiongozi wa kiroho inasambaa haraka sana mikoa mbalimbali. Lakini utaona jambo zuri limetokea kansiani labda mtu amefufuka, au alikuwa haoni sasa anaona, habari hizi zinasambaa taratibu kulinganisha na habari za uovu. Hii ni kwa sababu kuna mlima umewazuia watu wa Mungu kuyatangaza matendo makuu ya Mungu. Amka sasa na uzipeleke habari za ufufuo na uzima zisambae kwa kasi sana kwa jina la Yesu. Wewe unayesikia habari hii ya Yesu peleka  habari hizi katika vijiji, mitaa na mataifa yote kwa jina la Yesu. Leo tunapiga na kuruka juu kuwafuatilia wote ili kumwangusha chini anayeleta habari mbaya za maisha yako. Kwenye operesheni hakuna kuomba ruhusa ili kuvunja milima.

 Kazi yetu leo ni kuvunja vilima vyote na kuvishusha chini kwa jina la Yesu. Vilima hivi ni roho na hivyo havionekani kwa macho ya nyama. Tambua kwamba kila kitu kinaanzia rohoni. Tukibomoa leo utaona vitu vinarudi, milango inafunguliwa, kazi inapatikana, baraka na mafanikio utaanza kuyaona. Vilima ili vishushwe chini lazima vibomolewe. Yeremia 1:10 imeandikwa,  “angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.” Hapa umetajwa wewe kwamba umepewa mamlaka ya kubomoa na kuharibu za shetani. Mungu amekuita amekuweka juu ya mataifa na juu ya falme, juu ya vilima ili ubomoe kwa jina la Yesu. Vilima hivi tumeona ni sehemu wachawi wanakaa, wasoma nyoa ili kuleta uharibifu. Leo tusimama mimi na wewe ili tubomoe vilima vinavyotesa maisha yetu.

Majeshi ya Bwana wakisikiliza neno katika ibada ya leo

Ukiona kitu choche kibaya duniani jua kimetokea kwenye ulimwengu wa roho shetani. Waefeso 6:12 imeandikwa, “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Fanya vita kwenye ulimwengu wa roho. Milima hii inajengwa kwenye ulimwengu war oho. Lazima silaha zako uzielekeze rohoni na utapokea matokeo kwenye ulimwengu wa mwili.  Ukifanikiwa kubomoa rohoni jua na mwilini utaanza kufanikiwa.
Kwa nini vinaitwa vilima vya uharibifu.
Vinaitwa vilima vya uharibifu kwa sababu kuna muharibifu ambaye ndiye shetani anayetenda kazi. Analeta kuangamia, anayeharibu kabisa, anaitwa ibilisi au shetani na jina lake maarufu ni mwaharabu. Huyu ndo anatuma uharibifu uje kwako, anaweza kutuma kwenye moyo na  mtu anaanza kupata matatizo ya moyo, utasikia matundu kwenye moyo, pumu au kuharibika kwa figo. Mwaaharibifu furaha yake ni kukuona unaharibikiwa. Maombolezo 3:33 imeandikwa, “Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha”. Lazima uharibifu uondoke kwa sababu mabaya hayatoki kwa Mungu.
Mchungaji Kiongozi Dkt. Godson Zacharia akimfungua mtu kutoka vilima vya uharibifu.

1 Wakorintho 10:10 imeandikwa, “Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.” Bwana anasema usinung’unike leo kwa jina la Yesu maana kile kifaa cha kung’oa kipo tayari. Njooni kwangu asema Bwana njooni kwangu msumbukao na kulemewa na mizigo naye atawapumzisha.  Unaweza ukawa umeamka na hasira, hiyo ni roho iiyopandwa na mwaharabu baada ya vikao milimani.  Yohana 10:10 imeandikwa, “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. ” Huyu mwivi ana malengo 3 makubwa,  kuiba, kuchinja na kuharibu. Ndo maana hujawahi kuona wachawi mchana kwa sababu lazima watende kazi usiku wakiwa rohoni.  
Ufunuo wa Yohana 9:11 imandikwa, “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.” Makao makuu ambayo shetani anakaa ni baharini, nchi kavu au angani. Wachawi wanakutana milimani ili kutoa kafara ya damu, halafu wanaanza kuyaita majini na mizimu. Na kama jina lao linavomaanisha uharibifu wanakuja kuharibu baada ya kunywa damu iliyotolewa. Tunaposema kuvishusha vilima vya uharibifu, ni kubomoabomoa katika ulimwengu wa roho na si kwenda kukodi magreda au mapanga kuwachinja watu. Maana kushinda kwetu si juu ya damu na nyama bali katika  kila falme na wenye mamlaka na  majeshi ya mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Wachawi wanapokuwa kule kilimani wanaita majini au mashetani wanawachomea ubani, halafu wanawatuma. Leo tutaomba mpaka wachawi wanapokutana kwenye hivyo vilima tutavisawazisha mpaka kuwe sawa, tambare.

Showers of Glory Morogoro wakicheza na kusifu mbele za Mungu.

Waefeso 6:11
imeandikwa, “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.” leo tutaazima vifaa ikibidi ili kuteketeza vilima vyote. Inawezekana vifaa unavyo ila hujui kutumia leo tutavaa vifaa hivyo katika ulimwwengu wa roho.
Luka 3:5 imeandikwa, “Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa; ” leo tutakipiga hiko kilima mpaka kiondoke, kilima kilichonitangazia uharibifu, lazima kishuke leo ktk jina la Yesu.
Yeremia 51:20 - 21 imeandikwa, “Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa;  Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote;  Na Israeli ni kabila ya urithi wake;  Bwana wa majeshi ndilo jina lake. Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;” Maandiko haya Matakatifu yanakwambia wewe ni Rungu la Bwana na silaha  za Bwana za vita. Mungu anataka akutumie wewe kuvishusha vilima vyote vya kichawi.  Inawezekana umekaa kwa furaha na kwa amani lakini kuna wachawi wapo vilimani wanakupangia uharibifu, na wengine wanataja majina yako yote kwenye hicho kilima wanaona nyota yako wanakasirika na kung’ata meno wanakasirika na kuanza kunena uharibifu.

Wanafanyaje ili uharibifu ukupate  
Wanakutenga, waachawi au waganga wa kienyeji wanafanya mambo ili utengwe: Wanajenga mlima wanakutenga, mfano wewe ulitakiwa kukutana na mchumba mwakani wanajenga mlima kwenye ulimwengu wa roho ili usikutane naye. Au unakuta mtu anatengwaa na kazi yake, ni kwa sababu  wamejenga mlima kati yako. Unawezaukawa na vyeti vingi lakini hupati kazi. Au unaweza kutengwa na elimu, unakosa hamu yakusoma, wanajua ukisoma utakuwa mkubwa au utafanikiwa mbeleni. Ukiri: ewe mlima uliwekwa kati yangu na mchumba, kati yangu na rafiki, ewe mlima bandia nakuvunja, ewe shetani uliyegeuka kama mlima nakuvunja kwa jina la Yesu.Isaya 43:4 imeandikwa, “Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako”. Wachawi wanapokuchungulia kwenye ulimwengu wa roho wanakuona kuna Neema kwenye maisha yako, inawezekana ni mchina, au mluguru au mataifa mbalimbali yakikutana na wewe watakuunganisha na kazi, watakuunganisha na ndoa, wakiona hivyo wanaweka mlima kati yako. Ukiona mlima umeanguka usipumzike, unapoona dalili ya kujengwa tena pambana usambaratishe na weka walinzi wa kiroho.
Mchungaji Hapiness Mhimbula akimfungua mtu kutoka vilima vya uharibifu.

Yeremia 51:25
imeandikwa, “Tazama, mimi ni juu yako, Ee mlima uharibuo, asema Bwana; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukufingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa.” Zakaria 4:7 imeandikwa, “Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.” Luka :4 – 6 imeandikwa, “kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake. Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa;  Na wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu.” Njia nyingine wanazotumia kuharibu maisha ya watu kupitia milima ni pamoja  na  kutoa laana juu ya mtu.

========== AMEN ========
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA :
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro