GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO
SNP DR.
GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 7
JANUARI 2018
MHUBIRI: SNP
DR GODSON ISSA ZACHARIA
Mchungaji Kiongozi Daktari Godson Issa Zacharia akifundisha neon la Mungu katika Ibada ya leo. |
Uharibifu ni mpango kazi wa ibilisi. Shetani ndio
mungu muovu wa dunia hii. Huyu mwaribbifu alikuja ili kuharibu. “Mwivi
haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele.” (Yohana 10:10).
Huyu mwaharibufu anafanya kazi ya kuiba nyota, kinywa, mikono,
kazi, ndoa, na akisha iba anaharibu. Uharibufu ni mambo maovu. Shetani hajaja
ili upate kibali/uoe/kuolewa bali uharibikiwe. Leo tutaipasua madhabahu ya
uharibifu ili nyota yako irudi kwa jina la Yesu. Mwaka 2018 ni mwaka wa furaha
kuu, ni mwaka wa kucheka tena, kwa jina la Yesu.
Mungu anasema ipasueni madhabahau ya uharibifu. Uharibifu ni
matendo yale yanayokupelekea uharibikiwe, katika maisha yako. Shetani ndiye
anayesababisha uharibifu. Uharibbifu huu unatokea kwenye madhabahu. Madhabahu ni
daraja linalounganisha vitu vya ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho.
Ulimwengu wa mwili ni vile vitu vilivyoumbwa vinaonekana mfano mto, milima,
dhahabu na n.k. Ulimwengu wa roho ni ulimwengu ambao vitu vyake havionekani kwa
macho ya kawaida. Asili yake ni roho, havionekani hata utumie vitu vya
kisayansi mfano, majini, mapepo, na n.k.
Shetani yeye ni roho na hawezi kufanya kazi pekee yake. Mungu na yeye ni roho.
Ili tuweze kuwasiliana na Mungu ni lazima kuwepo na daraja. Daraja
linalotuunganisha na Mungu ndio linaitwa Madhabahu ya Mungu. Vitu vyote
vinavyoonekana asili yake ni ulimwengu wa roho. Dunia na vyote vinavyoonekana
vinatokana na ulimwengu usionekana. Kila kitu kinachoonekana leo vilitokana na
ulimwengu usionekana.
Baadhi ya Makutano wakisikiliza neno la Mungu wakati wa Ibada. |
“Hapo mwanzo Mungu aliziumba
(mbingu) na nchi. Nayo nchi ilikuwa (ukiwa) tena utupu, na giza lilikuwa juu ya
uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema,
Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru
na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na
giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji,
likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo
juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni
ikawa asubuhi, siku ya pili. Mungu
akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu
paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji
akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao
mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo
ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa
jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi
yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu. Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la
mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na
siku na miaka. tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya
nchi; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale
mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie
nuru juu ya nchi; na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu
akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne. Mungu akasema,
Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya
nchi katika anga la mbingu. Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe
chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na
kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni,
mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.Ikawa jioni
ikawa asubuhi, siku ya tano. Mungu
akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho
kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya
mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila
kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.Mungu
akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa
baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba
mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.”
(Mwanzo 1:1-27)
Tunaona katika mstari wa 3, 6, 7, 9, 11, 14, 20, 24 alisema na
vikawepo kama alivyosema. Huu ni ulimwengu wa roho ukisema vitu vinatokea. Kama
Mungu alihitaji daraja ili kutekeleza yale aliyekusudia ndivyo hivyo shetani
anahitaji madhabahu ili kutenda yale anayokusudia. Kama unahitaji biashara,
kazi, gari, watoto, nyumba, ili vije lazima kuwepo na madhabahu na kuhani wa
madhabahu ili upokee katika ulimwengu wa mwili. Mungu alimwambia Yeremia kabla
sijakuumba nalikujua, kabla hujazaliwa nalikutakasa, hii ina maana kwamba
katika ulimwengu wa roho alionekana tayari ni shujaa wa Bwana.
Platform team wakiongoza kipindi cha sifa na kuabudu. |
“Bali wote waliompokea aliwapa
uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;” Yonaha 1:12
Madhabahu ni daraja, ili shetani afanye kazi anahitaji (binadamu).
Huyu ndiye kuhani wa madhabahu nap engine wanajulikana kama mawakala mfano ni
wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota. Kuhani wa madhabahu anaunganisha
ulimwengu wa roho na mwili. Ulimwengu wa roho una wakazi wa aina mbili. Wakazi ambao
ni watakatifu hawa ndio wale wamwanio na kumtumikia Mungu Yehova. Na wakazi
waovu mfano mapepo, mashetani, majini. Mfano mtu anapoota ndoto anafukuzwa kazi
ghafla anafukuzwa kazi kweli. Hii ni kwa sababu kwenye ulimwengu wa roho majini
yalishaharibu yanatumwa kwenye ulimwengu wa mwili ili kulitekeleza ilo na
inakuwa hivyo.
Madhabahu hii tunayoongelea leo ni madhabahu za kichawi ambazo
wanazitumia kufanya uharibifu. Madhabahu nyingine zinawezekana zipo nyumbani
kwako leo kwa jina la Yesu zitapasuka. Kuna mwingine akiamua kuja kanisani
madhabahu inamsemesha, au inaweza kumwingia mtu ili akuzuie, huyo mtu anakuwa
amebeba madhabahu ya udhaifu/magonjwa
ya ukoo anaona unataka kutoroka hivyo anakuja
kukuzuia.
Baadhi ya Makutano walioamua kukata shauri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao. |
Jinsi madhabahu inavyofanya kazi, madhabahu ya kichawi wanapoona
unaendelea vizuri au unaenda kupona wanaongeza kafara. Kafara hizi hutolewa juu
ya madhabahu za kichawi na kunuiziwa mabaya. Mfano kama walitoa njiwa wanatoa
kuku. Kila wanapoongeza kafara ndivyo
nguvu ya kifungo kinavyozidi. Hata nyumba ya Ufufuo na Uzima ina
madhabahu ya damu ya mwanakondo. Nguvu ya madhabahu inaongezeka kwa maombi. Maana
imeandikwa maombi ni kama uvumba mbele za Mungu.
Wachawi wanaweza kujenga madhabahu. Tunaposema kuvunja ni kwa
sababu madhabahu imejengwa. Ukitaka kufanya kazi lazima ujenge madhabahu
watumishi wengi katika Biblia walijenga madhabahu, Musa, Ibrahimu na wengine
wengi. Wewe mwenyewe unaweza kutengeneza madhabahu ndani yako. Ukiongeza nguvu
za maombi kwa kuomba kwa bidii na
unanena madhabahu yako inaongezeka nguvu. Je hamjui miili yenu ni
hekalu la Roho mtakatifu.
Leo tutapasua madhabahu ya kichawi na kuvunja mikono ya kuhani mwaribifu.
Maana mikono yake ndo inafanya kazi kuchanganya dawa ili ubaya ukupate wewe.
“Ndipo Yeroboamu akajenga Shekemu
katika milima ya Efraimu, akakaa huko. Akatoka huko akajenga Penueli. Yeroboamu
akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. Kama watu hawa
wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, ndipo
mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao
wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. Kwa hiyo mfalme akafanya
shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu
kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli,
iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili
akamweka katika Dani. Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu
mbele ya kila mmoja, hata huko Dani. Tena akafanya nyumba za mahali pa juu,
akafanya na watu wo wote, watu wasio wa wana wa Lawi, kuwa makuhani. Yeroboamu
akaamuru kushika sikukuu katika mwezi wa nane, siku ya kumi na tano ya mwezi,
mfano wa sikukuu iliyokuwa katika Yuda, akapanda juu ili kuiendea madhabahu.
Akafanya vivyo katika Betheli akiwatolea dhabihu wale ng'ombe aliowafanya;
akawaweka katika Betheli wale makuhani wa mahali pa juu alipokuwa amepafanya.
Akatoa dhabihu juu ya ile madhabahu aliyoifanya katika Betheli, siku ya kumi na
tano ya mwezi wa nane, mwezi aliouwaza moyoni mwake mwenyewe; akawaamuru wana
wa Israeli waishike sikukuu hiyo, akapanda kuiendea madhabahu, ili kufukiza
uvumba.
(1Wafalme 12:25 -33)
Mchungaji Kiongozi akimfungua mtu kutoka Madhabahu ya uharibifu. |
“Na tazama, akatoka mtu wa Mungu
katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa
akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya
madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema
hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu
yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na
mifupa ya watu itateketezwa juu yako. Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii
ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo
juu yake yatamwagika. Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu
wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake
pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha
ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena. Madhabahu ikapasuka, majivu ya
madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la
Bwana.” (1 Wafalme 13:1-5)
Majivu yalimwagika kwa sababu ndani ya majivu kuna fedha, kazi,
dhahabu, biashara, ndoa, masomo, afya, leo madhabahu ikipasuka utapokea kwa
jina la Yesu. Yeroboamu alikasirika baada ya kusikia maneno ya yule mtu wa
Mungu, mfalme akanyoosha mkono wake pale madhabahuni, basi mkono wa mfalme
ukakatika. Mchawi anayekufuatilia maisha yako leo mkono wake ukatike kwa jina
la Yesu. Huyu kuhani wa madhabahu alikuwa na kiburi kwa kuwa alikuwa anategemea
majoka, mkono ulivyokatika kashuka chini akanyenyekea.
Showers of Glory wakimsifu Mungu na kucheza wakati wa Ibada ya Leo. |
"Mfalme akajibu, akamwambia yule
mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono
wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena,
ukawa kama ulivyokuwa kwanza.” (1
Wafalme 13:6)
Hapa mfalme aliomba mkono wake na akarudishiwa, hii ni ishara ya
mammlaka, ukiamini utapokea nguvu na mamlaka. Ili kile wanachokitegemea
kivunjike au kiondoke kabisa kwa jina la Yesu. Amua leo kuwakata mikono
waliokuandalia madhabahu ya ubaya maishani kwako. Tumia nguvu iliyomo katika
jina na damu ya Yesu ili upasue madhabahu ya watesi wako.