KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA- MOROGORO
SNP
DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI:
31 DISEMBA 2017
MHUBIRI:
SNP DR. GODSON ISSA ZACHARIA
Mchungaji kiongozi Godson Issa Zacharia akifundisha somo la panua hema lako kupokea Baraka zako za mwaka 2018 |
Mungu wetu ni Mungu wa
ajabu sana na ametupatia imani ambayokwayo tunashinda na kufanya mambo makubwa
kama nini.Imani ina tabia ya plastiki, inaweza kuongezeka kadili tutakavyo,
imani yako utakavyo ipanua kupokea baraka zako ndivyo Mungu atakavyo kupatia. Ukifungua
imani yako kama kikombe Mungu nimwaminifu naye atakupa kadili ulivyo weka,
ukiweka jagi naye Mungu atajaza jagi lako. Kadiri utakavyo mwomba Mungu akujaze
ndivyo atakavyo kupatia,kama pipa Mungu atakujazia pipa.kwa jina la Yesu.
Nabii Isaya aliona
mambo mabaya yawapatayo watu katika maisha yao, ya kwamba maisha yao ni tasa,
hakuna kuongezeka wala kufanikiwa, kila wanacho fanya hakizai .biashara zao
hazileti faida, kazi zao hazina matunda, akatabiri kuongezeka kwa baraka za
watu kwa kadiri watakavyo fungua mioyo yao kupokea kwa imani. Imeandikwa..
“ Imba, wewe uliye
tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na
utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye
aliyeolewa, asema Bwana. Panua mahali pa
hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa
kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na
upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji
iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.
Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa;
kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako
hutayakumbuka tena. Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo
jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa
dunia yote. Maana Bwana amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni,
kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. Kwa kitambo kidogo
nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya. Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu
dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi
wako. Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama
nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika
nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea. Maana milima itaondoka, na
vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la
amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye.” (ISAYA 54:1-10)
Maelfu ya waumini wakisikiliza neno katika ibada ya leo |
Bwana anasema na wewe
leo ambaye umefunga kamba fupi kwa ajili ya mafanikio yako, wewe uliyeandaa
kapu dogo kwaajili ya kupokea baraka zako,uliyeandaa hema dogo kwa kupokea
utajiri wako, yeye anasema hama hapo panua kamba yako, panua hema yako upate
kupokea kadiri ya ukubwa wa chombo chako .Anataka upanue hema yako leo, andaa
mahari kwa ajiliya kuwekea baraka zako,
panua biashara yako kwaajiri ya faida kubwa, panua mashamba yako kwa maana
utaenda kuvuna kwa kiasi kikubwa, panua mtaji wako kwa maana Bwana anaenda
kukupa kadiri ya ulivyo andaa chombo chako cha kupokelea, na utapokea kwa jina la Yesu.
Mungu alisema na Joshua
kwa habari ya mipaka ya wana wa Israeli, alisema kila mahali watakapo kanyaga
amewapa wao, wala hakusema kwa eneo dogo,aliwamilikisha maeneo makubwa hata
nchi ya Lebanoni hata mto flati.
“Kila mahali
zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa.
Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati,
nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo
ndipo patakapokuwa mpaka wenu.”
(YOSHUA 1:3-4)
Mungu anakutaka upanue
mipaka yakoleo kama alivyo sema na wana wa Israeli anasema na wewe leo kuwa
kila mahala utakapo kanyaga amekupa upamiliki, hivyo panua mipaka ya maeneo yako,
panua mipaka ya biashara yako, panua mipaka ya elimu yako, mipaka ya kazi yako kwa maana Bwana
amekupa kila mahala utakapo kanyaga kuwa
milikiyako. Hutakufa hadi umiliki baraka zakokwa jina la Yesu. Hakuna wa kuzuia wewe panua
hema yako, panua njia zako kwa maana uwezo wa kujaza si wako, uwezo wa kujaza
ni wa Bwana naatakujaza kwa jina laYesu.
Hakuna aliye acha vyote
akamfuata Yesu akakosa kitu, Kwa maana Bwana anasema yule atakaye acha vyote na
kumfuata atapata mara mia, kwahiyo sisi tuliye acha vyote nakuambatana na Yesu hatutakosa
kitu tutapata mara miamoja kwa maana yeye alifanyika maskini ili sisi tuwe
matajiiri kwa jina la Yesu.
Platform ministry wakiongoza sifa na kuabudu katika ibada ya leo |
Ayubu alikua ni mtu
mwenye mwili kama sisi, yeye alikua mkamilifu, na mwenye kumcha Mungu na
kuepukana na uovu. Alikua mtakatifu na hata Mungu akakubali utii wake naye Mungu akambarikia kwa mali , wanyama na
utajiri wa kila namna ,alimbarikia akawa na watoto wengi sana. Wewe ni nani ata
usibarikiwe kama umemtumikia Mungu kwa kuacha vyote na kuishi maishamatakatifu?, kimsingi panua hema yako ili upokee baraka
zako kwa jina la Yesu.
“Palikuwa na mtu katika
nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na
mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti
watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni
kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda
wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni
mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.” (AYUBU1:1-4)
Tunajifunza wanawa
Israeli walipokua utumwani Misri walikua wanateseka kwa mambo mabaya waliokua
wanafanyiwa na Farao na majeshi yake.Mungu akasikia kilio chao akatuma mtu
aende kuwatoa, wakapita katika bahari ya shamu huku majeshi ya Farao yakiendelea
kuwafuatilia, hata hivyo wote wakaangamia katika bahari ya shamu.
Mtu ambaye hajaokoka nisawa
na wana wa Israeli nchini misri, lakini akisha okoka kuingia kwenye wokuvu
hutoka Misri kuingia kwenye baraka zake lakini shetani uendelea kumfuatilia na
kufunga hatua zake na mafanikio yake, biashara yake inapungua, kazi zake
kuelekea mafaniko yake zinafungwa. Kama vile Bwana alivyowatosa majeshi Farao
baharini ndivyo atawatosa bahariniadui zako nawe utavuka kuingia kwenye Baraka
zako, kwenye nchi ya ahadi yenye maziwa na asali kwa jina la Yesu.
Hakuna aliyewahi
kumiliki pasipo kupigana; tunajifunza hata malaika walipigana kumwondoa shetani
mbinguni, hata katika hali ya kawaida watu hupigana ili kumiliki. Idi Amini
alipigana naTanzania chini ya Rais Julias Nyerere kwaajili ya kumiliki mipaka
ya kagera. Nasisi wakristo ilitupate
kumiliki baraka zetuni lazima tupigane kwa njiaya kiroho, tunapigana kwa maombi
ili wale wazuiaji waondoke kwenye mipaka yatu, tunakataa kutawaliwa nashetani katika maisha yetu, kwa kupigana tuna panua hema ya mafaniko, tunapanua mipaka
kwa jina la Yesu.
Mtu anapozaliwa ana
kuwa na baraka zake , lakini nivigumu kumiliki baraka hizo pasipo kupigana.
Katikabiblia kuna mfano wa mwanamke mjane ambaye hakupanua hema yake kupoke baraka
zake
“Basi, mwanamke mmoja
miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako
mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na
aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.Elisha
akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi
mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta. Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa
jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache. 4 Kisha uingie ndani,
ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo
vilivyojaa ukavitenge. Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao
wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina. Ikawa, vilipokwisha kujaa vile
vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo.Akamwambia, Hakuna tena
chombo.Mafuta yakakoma. Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema,
Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe
na watoto wako.”(2WAFALME
4:1-7)
Showers wakicheza na kumsifu Mungu katika ibada ya leo |
Mume wa mwanamke huyu
alikua anapenda sana madeni na mumewe alipokufa aliacha madeni hata kufika
watoto wake kuuzwa kwa ajili ya madeni, pale alipokutana na nabii Elisha
mwanamke huyu mjane alimwambia nabii habari za taabu yake. Elisha akamwambia
nenda ukatake vyombo kwa majirani zako tena sio vichache na utie hayo mafuta.
Lakini huyu hakuwa mwaminifu kwa nabii, yeye aliomba vichache na pale vilipojaa
mafuta yakakata na akapata kadili ya alivyo andaa. Yaani alipata dili la kuwa
bilionea akaanda mpango wa kuwa milionea.
Imani ndio itendayo
kazi, kadili utakavyo amini ndivyo utakavyo pokea usitegemee maneno au uwezo wa
mwanadamu, Mungu pekee ndiye atakaye nyoosha mapito yako na kukubariki.
Inagharimu tu kuambatana.vile unakua mwaminifu kwa Bwana ndivyo atakavyo
kubariki na kukuzidishia atakujaza kulingana na ukubwa wa hema yako, hivyo
panua hema yako kwa jina la Yesu.
Mshirika akifunguliwa kutoka katika vifungo |
Tunajifunza habari za
Elisha jinsi alivyo ambatana na Eliya akaacha vyote na mwisho akapata Baraka,
Elisha alipata vizuizi vingi lakini ile nguvu ya kuambatana aliyokua nayo ndiyo
ilimwimalisha na kusonga mbele, mwishoni Eliya akamwambia Elisha omba utakacho
nitakupatia,nayeElisha akaomba kupata nguvu mara mbili ya Eliya, naye Eliya
alipochukuliwa vazi lake lilianguka chini naye alipolivaa akaingiwa na nguvu kadili
alivyoomba. Nawe usimwache Yesu kwa maana ukiambatana na Yesu utapata baraka
zako maradufu, yoyote atakaye ambatana na Bwana atapokea mara mbilikwa jina la
Yesu.
======== AMEN ========
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor
Dr Godson Issa Zacharia
Follow us
on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us
on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson
Zacharia
TEL: +255 719
798778 (WhatsApp&Sms only)