GROLY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA
UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO
SNP DR.
GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 21
JANUARI 2018
MHUBIRI:
MCHUNGAJI: JOYCE GABRIEL (SNP DUMILA)
(MILANGO
INAYOMPA NAFASI MME AU MKE WA KIROHO)
Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akisisitiza jambo kabla hajamkaribisha Mchungaji Joyce Gbriel. |
Ndoa ni muunganiko wa maisha yote kati ya
mwanaume na mwanamke unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii. Ndoa huwa inawafanya
waliokuwa wawili kuwa mtu mmoja. Ndoa huwa inampa mtu uwezo wa kumiliki kile
ambacho hakikuwa haki yake kabla ya ndoa. Lakini shetani naye bado anaweza kuwa
na ndoa na wanadamu. Ndoa za kishetani ni jambo linalowapata watu wa dini na
kabila zote. Lakini ijulikane kuwa shetani hawezi kummiliki mtu isipokuwa mtu amefungua
mlango fulani. Ipo milango ambayo inamfanya shetani aanzishe ndoa za kishetani
kati yake na wanadamu. Ifuatayo ni baadhi MILANGO;
i)
Kupitia Ulinzi kwa waganga wa kienyeji. Kuna wakati watu wanapokwenda kwa waganga
wa kienyeji kupewa ulinzi. Lakini kinachoitwa ulinzi huwa ni malaika wa shetani
ambao kwa mujibu wa neno la Mungu hawa ndio walioamua kuwaingilia wana wa
wanadamu. Kwa hiyo anakuja kama mlinzi lakini anaamua kujimilikisha kama mke au
mme wa kiroho.
Mchungaji Joyce Gabriel akiwa katika uwepo wa Bwana |
ii)
Kucheza ngoma za Kimila. Kila
kabila lina taratibu zake. Mfano kwa watu wa Pwani wana taratibu za kumtoa
mwali. Kwa hiyo kupitia sherehe hizo kuna mambo fulani yanafanyika kwenye
ulimwengu wa roho. Kuna sadaka zinatolewa ambazo zinasababisha watu
kuungamanishwa na mashetani. Katika sherehe hizi watu wanatoa kafara ya damu
ambayo inasababisha mashambulizi . kupitia vyakula na vinywaji katika
sherehe vinawaungamanisha watu na mashetani
pasipo kujua. Matukio haya yanampa shetani kuwamiliki watu kama mke na
mme kwenye ulimwengu wa roho. Imeandikwa 1Wakorintho
10:20-21 “Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala
si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea
kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya
Bwana na katika meza ya mashetani.”
iii)
Matendo
ya Uzinzi na Uasherati. Jambo hili
limekuwa jambo la kawaida hata kwa waliookoka. Anaweza kuwa ni kijana lakini
ana wapenzi au mke au mme wa mtu lakini anamiliki nyumba ndogo. Miili yetu ni hekalu la Mungu na Roho
Mtakatifu. Kwa kufanya uzinzi na uasherati ni mlango ambao shetani anawamiliki
watu kwa kasi sana. Kumbuka Mungu anatuonya kwamba zinaa haikemewi bali sharti
uikimbie. Si wote wazinio walitaka kwa
hiari yao, bali wengi kwa sababu ya roho ya uzinzi walijikuta wameungana na
mashetani. Mashetani yanatengeneza ndoa ili waweza kuzaa kwa ajili ya kuzimu. Ndio
maana ndoa zilizokumbana na mashetani hawa lazima ziwe na ugomvi siku zote. Wanagombana kwa sababu kisa mmoja wao ana
wapangaji kutoka kuzimu ndani yao. Imeandikwa 1Wakorintho 6:15 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya
Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!”.
Tabia za uzinzi na uasherati ni chanzo cha
migogoro katika ndoa. Kila mtu kabla ya ndoa aliyonayo leo alikuwa na wapenzi
wengi na wote aliungwa pamoja naye. Chunga
sana tabia zako na mienendo yako. “Amani
ya ndoa yako itategemea sana namna ambavyo wewe ulianza. Kwa hiyo namna ya kumaliza
kwako itategemea sana na namna ulivyoanza. Kumbe ni heri uanze na Bwana na
umalize na Bwana”. Kataa kuwa
kahaba kwa jina la Yesu. Amua kujikana leo na ujitie bidii kumtafuta Mungu,
nawe utakuwa imara kwa jina la Yesu. Maana kwa kumtafuta Mungu utaishinda roho
ya ukahaba. Imeandikwa ``Ufunuo wa
Yohana 17:1-2 “Akaja mmoja wa wale
malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku,
nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; ambaye
wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya
uasherati wake.”
Baadhi ya Makutano wakisikiliza neno la Mungu wakati wa Ibada ya leo. |
Watu walio kwenye ndoa za kishetani hawawezi
kufanikiwa katika maisha yao. Watu hawa ni msukule katika ulimwengu wa roho. Nndio
maana talaka ni nyingi katika dunia ya sasa. Kumbe wengi waliovunja ndoa zao si
kwamba walitaka, bali ni kwa sababu yapo mashetani walio sababisha ugomvi kati
yao. Watu hawa hawajawai kufanya kazi na ikazaa matunda. Akianza biashara,
kazi, mradi au shule hawezi kufikia mwisho wa jambo hilo.
Mama huyu akifunguliwa kutoka vifungo vya Ndoa za Kishetani. |
iv)
Kurithi Mikoba ya Uchawi ya Ukoo. Kila
aliyerithi huwa anapata haki juu ya mambo yote. Kila aliyerithi mambo ya
familia au ukoo huwa anarithi na miungu ya familia na koo husika. Mtu anaweza
kuwa anaonekana kama mwanadamu lakini ndani yake ni mashetani. Ndio maana mtu
alioa kwa tamaa zake, lakini baada ya kuanza ndoa ni vita kubwa. Hii ni kwa sababu
ndani hao wanaoonekana ni wazuri lakini ndani yao wamejawa mashetani. Imeandikwa
2 Wakorintho 12:2 “Namjua
mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa
katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo
alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.”
v)
Zawadi. Kuna vitu unaweza kupewa na vikageuka
na kuwa mlango wa kukuletea matatizo, hasa chanzo cha ndoa za kishetani. Tabia ya
kupenda vitu vya kupewapewa mara nyingi vinagharimu sana maisha ya watu. Yawezekana
ilionekana kama zawadi lakini ndani yake imebeba mauti. Kuna mtu aliwai kupewa
ua zuri na usiku wake akaota mtu anakuja na ni mzuri kama lile ua alilopewa
asubuhi. Mwangalie Bwana awezaye kukupa vyote vya mwilini na rohoni. Achana na
tabia ya kujipenda kuliko Mungu. Maana watu wengi wameibiwa na kuolewa kwa
sababu ya kupenda vitu vya duniani. Litumikieni kusudi la Bwana lililo ndani
yako.
vi)
Mavazi. Wengine wametekwa kwa sababu ya
mavazi na stahili za kuvaa. Mavazi yanachukua sehemu kubwa ya kuwafanya watu wamjue
au wamkatae Mungu. Wengine wametekwa kwa sababu ya kuomba au kuazima nguo za
wenzao. Nguo nyingine zina manuizo ya mashetani ndani yao. Mwingine amepatwa na
mabaya kwa sababu nguo aliyovaa imezoelewa na mashetani na kila wakimwona
usababisha mabaya kwake. Kumbe kwenye nguo za kuazima unaweza kuazima na
matatizo ya mmiliki wa nguo.
Chunguza maisha yako ni wapi ulifungua mlango
mpaka shetani akakuingilia. Mabaya huja kwa sababu ya kwenda kinyume na mapenzi
ya Mungu. Shetani hawezi kukuvamia isipokuwa umemfungulia mlango. Amua kumrudia
Mungu maadamu anapatikana. Tengeneza na
Bwana, tubu maana Mungu anapenda roho ya toba na hapendezwi na kiburi cha
uzima.
======== AMINA
========Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akimfungua mtu kutoka ndoa za kishetani |
KWA MSAADA
ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)