GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SNP DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 11 FEBRUARI, 2018
MHUBIRI: MCHUNGAJI, DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
Duniani kuna falme 2 zinazofanya kazi.
Falme hizi 2 zinapingana. Ufalme wa Mungu, huu ni ufalme halali ambao
hautikisiki, Ufalme huu ndio watu wanatakiwa kufanya kazi hapa duniani. Ufalme huu
ulitoka mbinguni na kuletwa duniani.
“Akawaambia,
Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako
uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]” Luka11:2
Hapa
Yesu alikuwa anawafundisha wanafunzi wake namna ya kusali. Aliwaambia kwamba
Baba yetu yupo mbinguni, jina lako litakaswe, ufalme wako uje, na mapenzi yako yatimizwe hapa duniani
kama huko mbinguni. Ufalme uliombwa kutoka mbinguni na ukaja kutoka mbinguni.
Hapa
duniani tunapoishi uraia wetu si hapa bali ni mbinguni ni kwa sababu mtu ni
roho na anakaa kwenye nyumba ambayo ni mwili na alipuliziwa pumzi kutoka
mbinguni. Mfano wamarekani wana ufalme wao wakitaka kuja Tanzania wanatengeneza
ubalozi.
“Basi
kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa
hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho;” Waebrania 12:28
Ufalme
wa Mungu hautetemeshwi.
Kuna
ufalme wa uharibifu/na ufalme wa shetani, ufalme huu ni batili (hauna kibali)
ni mtu aliyejiapisha mwenyewe, ni ufalme
ambao haujaruhusiwa na aliyeumba mbingu na nchi. Ni ufalme unaofanya kazi hapa
duniani.
“Mwivi
haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele.” Yohana 10:10
Hapa
tunajifunza mfalme wa uharibifu kwamba ni mwivi haji ila aibe na kuchinja na
kuharibu. Ila Yesu alikuja ili tuwe na uzima huyu ni mfalme wa ufalme wa
mbinguni.
“Na
juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu, jina lake kwa Kiebrania ni
Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni.” Ufunuo wa
Yohana 9:11
Biblia inasemaa yupo mfalme ambaye ni
Ibilisi kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani analo jina lake Apolioni au
muharabu.
“Sisi
tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu.
Yeye asiyependa, akaa katika mauti.” 1 Yohana3:14
Sisi
tukiamini tumepita toka mautini na kuingia uzimani. Kuna ufalme unatawala
mautini.
Ukiri: Kwa jina la Yesu, ingawa nina maumivu makali
najua ya kwamba nimepita toka mautini na kuingia uzimani.
“Amin,
amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka
yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini
kuingia uzimani.” Yohana 5:24
Kuna
watu wapo duniani wanatembea lakini wameshakufa, lakini Biblia inasema yeyote
atakayeamini yu na uzima tele na amepita kutoka mautini na kuingia uzimani. Biblia
inasema tumekuwa wafu ni kwa sababu ya makosa na dhambi zetu. Ili uvuke kutoka mautini
na kuingia uzimani ni lazima uvuke kwa
kumwamini Yesu.
Mfalme
wa uharibifu ni kama mvuvi haramu, Mfalme huyu wa uharibifu amevua vitu vingi
sana, amevua mimba, watoto, kazi, ndoa, amevua watu na kuwaweka msukuleni
amewaweka mashimoni.
“Kulikuwa
na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka
naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao
hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani,
aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na
malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufunuo 12:7-9
Mfalme wa uharibifu amevuna vitu vingi sana,
“Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota
ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha
mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti
changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa
kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za
mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema,
Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; Aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?”
Isaya 14:12-17
Maelfu ya makutano wakisikiliza somo la leo la kuhama kutoka ufalme wa uharibifu. |
Mfalme huyu ameangusha mataifa, mfalme huyu
anatakiwa apigwe, amepanga shida,matatizo, lazima tumpige na arudi kuzimu. Ufalme
wa uharibifu una makao makuu matatu, Baharini, nchi kavu na angani. Ufalme huu
wa uharibifu una gereza au shimo na kuzimu.
“Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na
kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa
mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.” Isaya 42:22
Watu wametekwa waishi kule wanalishwa nyama za
watu, wana kunywa damu za watu. Ufalme huu
wa uharibifu unaandaa mpango kazi ambao utachagua nani aoe/kuolewa, nani
atapata kazi. Kwenye ufalme huu kuna uchawi, wizi, na anachinja na kutengeneza
mizoga.
“Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo
na unyang'anyi; mateka hayaondoki. Kelele za mjeledi, kelele za magurudumu
yafanyayo kishindo; na farasi wenye kupara-para, na magari ya vita yenye
kuruka-ruka; mpanda farasi akipanda, na upanga ukimeta-meta, na mkuki
ukimemetuka; na wingi wa waliouawa, na chungu kubwa ya mizoga; mizoga haina
mwisho; wanajikwaa juu ya mizoga yao. Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule
kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na
jamaa za watu kwa uchawi wake.” Nahumu 3:1-4
Japokuwa umetekwa, Bwana akusimamishe tena. Ufalme
wa uharibifu umejaa hila, na wasaidizi wake ni mashetani, majoka.
“hata mfalme mwingine akainuka juu ya Misri,
asiyemfahamu Yusufu. Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya
baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi.” Matendo
7:18-19
Unakuta mtu anajifungua mtoto anaambiwa
ameshakufa, au amezaliwa baada ya mwezi anakuwa na degedege. Hizi ni hila za
mfalme wa uharibifu. Mfalme huyu wa uharibifu ni muuaji.
Children Ministry wakiimba na kucheza katika ibada ya leo. |
“Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za
baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala
hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo,
husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.” Yohana
8:44
Kwenye
ufalme wa uharibifu mipango yao ni kuchinja, kuua ,a kuharibu. Na hata wachawi
wakikutana mahali mipango yao ni kuua, kuchinja na kuharibu. Yamkini umeibiwa furaha yako haipo, kumbe
yupo muharibifu amepanga ili uibiwe, lakini leo kwa jina la Yesu Kristo yeye
alikuja ili tuwe na uzima tele, leo namfuata kwa jina la Yesu namkamata nakukanyaga kwa jina la Yesu achia
kwa jina la Yesu.
Kila
kitu kinachotokea kwenye ulimwengu wa mwili kinaanzia katika ulimwengu wa roho hapahapa
duniani. Ufalme wa uharibifu unaiba akili.
Wakazi
wa ufalme wa uharibifu.
1. Wakazi wa ufalme huu wana magonjwa mengi
ambayo hayaponi, ni kwa sababu mkuu wa ufalme anapanda magonjwa.
2. Wakazi wa ufalme huu wamejawa na tabu, tabu
imekuwa kama makazi yako.
3. Umasikini; wakazi wa ufalme huu wamejawa
umaskini, unaweza kumkuta mtu ameokoka lakini ni masikini.
4. Majuto; wakazi wa ufalme huu wana majuto
mengi, unakuta mtu anasema najuta kuzaa watoto, hii ni kwa sababu unaishi
kwenye ufalme wa uharibifu.
5. Kukataliwa & Mikosi; wakazi wa ufalme huu
wamejaa mikosi na kukataliwa.
6. Msukule, kuibiwa, mauti; wakazi wa ufalme huu
wamejawa na kuchukuliwa msukule, wanaibiwa ndoa, kazi, mchumba, safari. Pia wamejawa
na vifo, vifo vya kazi.
7. Huzuni; wakazi wa ufalme huu wamejawa na
huzuni.Lakini Yesu alikuja ili kutuondolea huzuni.
Muumini akifunguliwa kutoka kwenye ufalme wa uharibifu. |
8.
Chuki; wakazi wa ufalme wamejaa chuki sana.
WAKAZI WA UFALME WA MUNGU
Huu
ni ufalme halisi ambao Bwana aliuleta kutoka mbinguni. Bwana aliutengeneza kama
ubalozi ili ukae kwetu. Mimi na wewe tumeumbwa kutoka kwenye ufalme wa Mungu
ambao hautikisiki.
Ufalme huu wa Mungu huwa unakuja kwetu na
kuupokea, kwa kuwa tunapokea ufalme huu tumtolee Bwana ibada ya kutengeneza. Kwenye
ufalme huu kuna uzima. Yohana 10:10
“Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji
wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu
mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya
kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.” Waebrania 12:22-24
Hawa ni wakazi wa ufalme wa Mungu, Mungu
Baba mwenyewe, majeshi ya malaika elfu nyingi, kanisa la wazaliwa wa kwanza,
Mungu mwamuzi wa watu wote, roho za watu wenye haki, Yesu Kristo, na damu
inayonena mema.
Kwenye
ufalme huu hakutakiwi magonjwa kwa sababu ipo damu inayonena mema. Magonjwa haya
ni mapando ya ufalme wa uharibifu
“Maana
moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha” Maombelezo 3:33
Hapa
Mungu hapendi kuwahuzunisha watu, huzuni ni pando la ufalme wa uharibifu. Kwenye
ufalme huu hakuna mikosi. Mungu wakati anatuumba alituwekea uwezo wa kumiliki
na kutawala mipango hii iliwekwa kabla ya kuzaliwa. Kuishi, kufanikiwa,
kuoa/kuolewa, utamiliki na kutiisha.
“Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa
mataifa.” Yeremia 1:5
Ufalme
huu unapanga mipaka.
Mamia ya waumini waliompokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao katika ibada ya leo. |
“Bwana
akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba
yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa
kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki
wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia
watabarikiwa.”Mwanzo 12:1-3
Hapa Mungu anakupa mipaka ya kumiliki, pia atakufanya uwe
taifa kubwa.
“Angalieni, nawawekea
mbele yenu hivi leo baraka na laana;”Torati 11:26
Hapa Mungu anasema ukiyashika maagizo yake ameweka Baraka mbele
yako.
“Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi
alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi
mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.” 2 Wakorintho 8:9
Yesu alifanyika kuwa masikini ili mimi na wewe tuwe matajiri,
ukiona wewe si tajiri ujue unaishi kwenye ufalme wa uharibifu.
“ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu
Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.” Wagalathia 3:14
Ibrahim kama baba yetu
alikuwa na mali nyingi, na sisi yatupasa kumiliki na kuwa tajiri kama
Baba yetu wa Imani.
Inawezekana umeokoka na unatakiwa uishi kwenye ufalme wa
Mungu, lakini wakakuzunguka na wakakuweka katika ubalozi wa kishetani.
“Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa
hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu
kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa
ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.” Ufunuo 5:9-10
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa
takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye
aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;” 1 Petro 2:9
Shetani anaitwa mungu wa dunia hii, lakini Mungu aliamua
kushusha ubalozi wake ndani yangu na ndani yako. Lakini wakakuiba na kuwekwa
kwenye ufalme wa uharibifu.
KWA
MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa
Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson
Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/