GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SNP DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPIL: 4 FEBRUARI, 2018
MHUBIRI: MCHUNGAJI, DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
“Basi hawa ndio wakuu wa mashujaa
aliokuwa nao Daudi, waliojitia nguvu pamoja naye katika ufalme wake, pamoja na
Israeli wote, ili kumfanya awe mfalme, sawasawa na neno la Bwana alilonena juu
ya Israeli.” 1 Mambo ya Nyakati 11:10
Shujaa ni mtu jasiri, asiyeogopa
chochote, ni mtu ambaye yuko tayari kutetea haki yake au kile kitu
anachokiamini. Ni mtu ambaye hawezi kunyamza mpaka kile anachoomba kitokee
kwenye maisha yake. Ni mtu anayejiamaini na ana udhubutu yeye mwenyewe ili
kuleta ushindi katika nyumba yake au kanisani. Ni mtu mwenye uwezo wa kukabili
na kuvumilia dhiki ili kufika kwenye mafanikio yake.
Shujaa wa ufalme ni mtu ambaye ni
jasiri kuelekea nchi ya ahadi ili
amiliki ahadi ya nchi kama Mungu alivyoagiza. Kuwa shujaa wa ufalme ni agizo la
Bwana. Kwenye ufalme wa mwanakondoo kuna mashujaa wanatakiwa watengenezwe.
Mungu alimuagiza Joshua kuwa shujaa na moyo wa uhodari.
“Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe
utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote
aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa
kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. Kitabu hiki cha torati kisiondoke
kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia
kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha
njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe
hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako,
yu pamoja nawe kila uendako” Yoshua 1:6-9.
Joshua aliambiwa awe hodari na moyo wenye
ushujaa. Watu wote ambao ni hodari wana moyo wa ushujaa. Mungu anataka
ufanikiwe, upate mali, usome ili upate haya ni lazima ushike sheria yake katika
njia iliyonyooka. Kupata moyo wa shujaa ni lazima kuondoa woga. Kuwa shujaa
katika nchi ni agizo la Bwana.
“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate
kuweza kuzipinga hila za Shetani.” Waefeso 6:11
Ushujaa hauji kwa
sababu ya ukoo uliotokea, au umesoma sana, au una fedha nyingi. Ili uwe shujaa
na hodari unahitaji uwezo na nguvu kutoka kwa Bwana kwa kuvaa
silaha zote za Mungu. Kumbuka Moyo wa ushujaa ni agizo la Bwana. Moyo wa
ushujaa unapokelewa, huu moyo kuna sehemu upo. Unapokuwa na jambo la kufanya
Bwana anakupa moyo wa shujaa.
“Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe
nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;” Yeremia 51:20
Wewe ni rungu na silaha za Bwana, kila unapokwenda uende kama
silaha, wewe ni upanga, moto, kifaru, wewe ni kisu cha Bwana. Kinachokupa
wasiswasi ni kwa sababu hujajua wewe ni nani. Leo ujue kwamba wewe ni shujaa.
Duniani kuna matatizo mengi lakini yanahitaji apatikane mtu ambaye ni shujaa.
“Basi Daudi akaondoka huko, akakimbilia pango la Adulamu; na
ndugu zake na watu wote wa mbari ya baba yake waliposikia habari hiyo,
wakamwendea huko. Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu
aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika
kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama watu
mia nne.” 1 Samweli 22:1-2
Daudi alikuwa ni mtu kabisa lakini ndani yake aliwekewa moyo
wa ushujaa na moyo wa kusaidia. Daudi alikuwa na moyo wa kuwasaidia watu waliofungwa. Daudi alimuua Goliath,
wanawake wakatunga wimbo, ambao ulikuwa ulikuwaunasema Sauli ameua maelfu
lakini Daudi ameua makumi elfu. Roho ya wivu ikamwingia Sauli na akaanza
kumwinda Daudi kwa ajili ya ule moyo wa ushujaa aliokuwa nao, Daudi akakimbilia
pangoni. Kwa kuwa alikuwa na moyo wa ushujaa watu walimfuata Daudi pangoni.
Watu hawa walijua Daudi anao uwezo wa kuwaondolea madeni, uchungu, na kuachwa
na watu. Daudi alifanyika kuwa jemerdari (kiongozi) wa watu hao. Jemedari kwa
kingereza ni ‘Captain’, hii ni nafasi ya juu katika nafasi za uongozi jeshini. Kuna
watu wakipata shida wanakimbilia kwa mganga wa kienyeji, au mchawi, ndugu
lakini wewe mkimbilie Daudi wako wa leo. Kuna mtu ambaye Mungu amemweka ili
akusaidie wewe.
Katika ulimwengu wa leo watu wanapenda watu wenye mafanikio
ila ni mashujaa peke yao wanaweza kukaa na watu wenye dhiki. Watu hawa
wakishafanikiwa wataambatana na Daudi.
“Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu
Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo
aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja. Na baada yake
kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa
watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa
wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao;
huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake
ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu
wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu. Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana
wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo
konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti; ila huyo alisimama
katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya
wokovu mkuu. Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu
wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi
cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai. Naye Daudi
wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako
Bethlehemu.” 2 Samweli 23:8-14
“Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu
wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa
na jina kati ya wale watatu. Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa
Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, k
pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji; huyo naye
akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini
yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa
mkuki wake mwenyewe. Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa
na jina kati ya wale mashujaa watatu.” 2 Samweli 18, 20-22
Daudi alikuwa mfalme kwa muda mrefu ni kwa sababu alisimama
na watu wenye dhiki na shida na watu wale walikuwa mashujaa wa Daudi. Kama una
dhiki ya ndoa, ya watoto, kazi, biashara leo Bwana atakutoa kwenye dhiki hiyo. Bwana
anataka uwe shujaa wa ufalme.
Yesu akasema njooni kwangu nyie wasumbukao na wenye kulemewa
na mizigo. Hii ni tabia ya Ufalme wa watu wa mbinguni. Ilikuwa tabia ya Daudi
kuwaonea huruma wale walioonewa na wenye uchungu. Hata sasa Yesu anawaita na
amekusadia kuwafundisha na kuwabadilisha ili wawe mashujaa wa ufalme. Omba,
pambana na shindana na falme za giza ili umiliki Baraka zako katika ulimwengu
wa roho na hatimaye utastawi kwa jina la Yesu.
“Njoni kwangu, ninyi
nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami 0nitawapumzisha.” Mathayo
11:28
Shujaa wa Bwana akifunguliwa kutoka kwenye vifungo. |
KWA
MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa
Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson
Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)