GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
PASTOR
DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI:
4 MACHI, 2018
MCHUNGAJI,
DR. HAPPINESS GODSON (RP)
Mchungaji Dr. Happiness Godson akifundisha somo kwa nini wakristo wasiotoa zaka huwa masikini.
Utangulizi:
Mara nyingi tumejifunza mambo mengi ya
rohoni lakini sio mambo ya sadaka. Lakini
biblia inatufundisha utii kwa habari ya kutoa zaka. Zaka ni agizo la Mungu
kumtolea. Wakristo maana yake ni watu wanaomfuata Yesu, wenye tabia za Kristo
na wanaoenenda na tabia za Kristo. Mtume Paulo anatusihi tuwe na nia kama
iliyokuwa ndani ya Kristo. Imeandikwa, ‘Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya
Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;
bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa
wanadamu;’ Wafilipi 2:5-7
Yesu alikuwa Mungu lakini akaamua
kuiacha mbingu ilia je duniani kutuokoa. Yesu alitii mamlaka ya Mungu na
akakubali yote. Lakini Yesu aliazimishwa, aliinuliwa baada ya kutii mpaka mauti
ya msalaba. Watumishi wa Mungu wanapofundisha kwa habari za utoaji watu huwaona
kama vile wanampango wa kuwataka watu wawape pesa kwa ajili ya mahitaji yao.
Mungu aliwai kumwambia Ezekieli kuwa naona watu wako wanafurahi kuyasikia
maneno ya uzima lakini hawayatendi. Anasema watu wamemwona Mungu kama wimbo
mzuri maana wanayasikia maneno yako lakini hawawezi kuyatendea kazi. Tupone leo
ili tuyatendee kazi maneno ya uzima.
Imeandikwa, ‘Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa
mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa
vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta
faida yao.’ Ezekieli 33:31
Ni sadaka maalaum tofauti na sadaka
nyingine. Hii ni moja ya kumi ya sehemu
ya mapato yako kama mwanadamu. Imeandikwa,
‘Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya
nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.’ Mambo ya Walawi 27:30
Sadaka ya Zaka pengine inaitwa Kodi ya
Mungu. Kama serikali za wanadamu wanaweza kuchukua kodo kwa nguvu zote, Mungu
je si zaidi ya wanadamu. Imeandikwa, ‘Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu,
kumletea Bwana kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani.
Wakafurahi maakida wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hata
wakaisha.’ 2 Nyakati 24: 9-10
SABABU ZA UMASIKINI WA WATU WASIOTOA
ZAKA
·
HAWANA CHA KUVUNA.
Mungu anasema kwa Yule
asiyetoa zaka hawezi kupanda na akavuna. Kwa yeyote asiyetoa zaka kila
atakachokipanda hakiwezi kuzaa kwa sababu hukuwai kupanda kwa Mungu. Mungu
anasema kwa kutokutoa zaka ni dhahili mtu anakuwa amaejitenga na kanuni ya
kupanda na kuvuna. Hii ndio inasababisha kila unachofanya hakiwezi kuendelea
wala kuongezeka. Kuna miradi umeanza lakini hakuna matunda. Tufani huwa ina
nguvu kuliko upepo wa kawaida. Tufani ni mbaya zaidi maana inaambatana na
uharibifu wa hali ya juu sana.
Imeandikwa, ‘Kwa maana wao
hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi
masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.’ Hosea 8:7
·
HAWAVUTI BARAKA ZA MUNGU KWENYE MAISHA YAO.
Kwa kutoa zaka kamili
unakuwa unavuta Baraka maana unakuwa umeitimiza sharia ya Mungu. Kwa kutokutoa
zaka unakuwa unajiweka mbali na Baraka za Mungu. Kwa kutoa zaka unakuwa
unafungua madirisha ya mbinguni ili Baraka zije juu yako.
Malaki 3:10
Hapa duniani tunaishi
maishe yenye ugumu na zimejaa taabu. Na tuko chini ya laana ya dhambi ya Adamu
kwa sababu wote tu wanadamu. Sasa ukichukua dlaana ya Adamu na laana ya Zaka,
huwezi kupata Baraka juu ya maisha yako. Kumbe kwa kutokutoa zaka huwa
tunafunga madirisha ya mbinguni ili Baraka zisiachiliwe juu yangu. Unaweza
kujaribu kila biashara lakini hakuna hata biashara moja iliyowai kukufanya ufurahi.
Kwa kumtolea Mungu unakuwa unaweka mvuto wa Baraka kutoka mbinguni zije juu ya
maisha yako. Imeandikwa, ‘Farao
akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi? Yakobo akamjibu
Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya
maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka
ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.’ Mwanzo 47:8-9
Kama madirisha ya mbinguni
yamefungwa jua nchi unayoishi haiwezi kuzaa kwa ajili yako. Kila unachokifanya
hakiwezi kuongezeka kwa sababu hakuna mkono wa Mungu. Imeandikwa, ‘Na mbingu
zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako
itakuwa chuma.’ Kumbukumbu la Torati 28:23
·
WAKO CHINI YA LAANA.
Laana ni mbaya sana maana
kwa asili palipo na alaana hakuna kufanikiwa. Mungu amesema mnaniibia kwa zaka
na dhabihu. Usipotoa zaka unakuwa umejiweka chini ya laana ya Mungu mwenyewe.
Laaana zingine unaweza kuziondoa kwa kuomba na kushindana na shetani na
ukashinda. Lakini laana ya zaka haiondoki kwa kushindana bali kwa KUTUBU NA KUTII NENO. Mtu akiwa chini
laana ya zaka anasababisha laana ndani ya kanisa. Mungu anatutaka tututbu na
kumtii yeye. Laana hii inasababisha mtu
kukosa amani ya moyoni. Na mtu anakosa ujasiri wa kumwendea Mungu wakati wa
maombi.
Imeandikwa, ‘Je!
Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema,
Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa
laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.’ Malaki 3:8-9
Platform team wakiongoza kipindi cha sifa na kuabudu wakati wa Ibada ya leo. |
·
WAHARABU HULA MAZAO WAKATI WOTE.
Baraka za Mungu kwa mtu
anayetoa zaka ni hakika. Neno la Mungu linasema Mungu atatuma malaika ili
awapige wale wanaoharibu mazao. Yule anayekula matunda ya kazi ya mikono yako,
kazi na miradi yako. Hata kwenye nchi kuna laana kwa sababu nchi na viongozi
wake hawamtolei Mungu zake kama sharia ya Mungu inavyomtaka kila mwanadamu.
Kuna nchi ni ndogo lakini uchumi wao uko vizuri. Unakuwa na matobo kwenye
mifuko yako na kila unachopata huwa unapoteza. Umasikini huu wa leo ni kwa
sababu ya laaana ya zaka. Imeandikwa, ‘Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye
alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha
matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.’
Malaki 3:11
·
MATUNDA YA MASHAMBA YAO HUARIBIWA WAKATI
WOTE
Kila unachofanya huwa kinaharibika.
Ukilima huwezi kuvuna kwa sababu hakuna ulinzi juu ya kazi za mikono yako. Kuna
matukio ya kutisha kwa sababu ya kutokutoa fungu la Kumi. Watu wanamatukio
kwenye familia zao kwa sababu hawana ulinzi wa Mungu. Malaki 3:11
MATUNDA YANAPOTEA KABLA YA KUVUNA.
Hapa utaona hakuna uwiano wa mapato na
kile ulichokiwekeza. Mtaji uloweka unaisha kabla ya kuzalisha kitu chochote.
Kuna watu wanafanya kazi masaa mengi lakini malipo yao ni kidogo sana. Wengine
kila wakifanya kazi wazulumiwa na kuonewa sana. Kila ukilima huwezi kuvuna kwa
sababu yupo Yule mwarabu. Kuna mambo yanakupata kwa sababu ya laana ya
kutomtolea sadaka. Kila unachoaanza kinaishia njiani. Malaki 3:11
Kumbe Mungu anaangalia moyo wetu wa kutii ili atubariki
kwa kila tunachofanya. Faida ya kutii
ni kusababisha upenyo kwenye njia zako. Hakika mafanikio yako yanategemea sana
moyo wako wa Utii. Imeandikwa, ‘Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;’
Isaya 1:19
Kwa nini wachungaji
wakifundisha kuhusu sadaka watu hawaachangamki sana? Ni kwa sababu mioyo yao
iko mbali na sharia ya Bwana. Mungu anamwambia Ezekieli watu wangu wamekuwa
wanakuja kwako wanasikiliza neno langu lakini hawayatendi yaani wewe umekuwa
kama wimbo mzuri. Mungu atuponye leo kwa jina la Yesu sisi tuyasikie na
kuyatenda maneno yake. “Nao huja kwako
kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno
yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi,
lakini mioyo yao inatafuta faida yao. Na tazama, wewe umekuwa kwao kama wimbo
mzuri sana, wa mtu mwenye sauti ipendezayo, awezaye kupiga kinanda vizuri;
maana, wasikia maneno yako, lakini hawayatendi.” Ezekieli 33:31-32
Makutano wakimimina Roho zao mbele za BWANA ili wasamehewe dhambi ya kumwibia Mungu Zaka. ulikuwa wakati mwema sana kwa ajili kubadilisha maisha yetu. Hakika Mungu amesamehe. |
MAANA
HALISI YA KUMWIBIA MUNGU
Ø Sisi
kama wakristo tunauelewa gani kama tunamwibia Mungu; Mungu anasema 10% ni mali
yake, vitu vyote ulivyonavy ya mapato yako, ya mifugo na kila kitu ni mali ya
Mungu. Mfano una maguni 10 ya mpunga, gunia 1 ni la Mungu. Hii si zawadi, si
chagizo balimali ya Mungu, hii unatoa kwanza halafu matumizi mengine
yanaendelea. Ukimtolea Mungu sadaka bila kutoa zaka, Mungu anaona kuwa ni zile
pesa zake ulizoiba na kumpelekea kanisani. Mfano ni kama umeniibia pesa zangu
halafu ile hela unanunua keki unaniletea. Usichukue fungu la 10 ukamnunulia
mchungaji zawadi. Kwa sababu biblia haijasema kuhusu kumwibia mchungaji bali ni
kumwibia Mungu. Fungu la 10 si zawadi.
Ø Mungu
ametoa Onyo kali sana kwa wezi Imeandikwa, “bali
jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi
hawavunji wala hawaibi;” Mathayo 6:20
Ø Kuiba
fungu la 10 kunaharibu ushirika wako na Mungu, Mara nyingi si salama sana
kuishi karibu na mwizi. Mfano katika jamii anayeiba anawekwa jela ili akae
mbali na jamii. Kwa hiyo usipotoa fungu la 10 unaharibu mahusianao yako na
Mungu. “Lisikieni neno la Bwana, enyi
wana wa Israeli; kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu
hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ila
kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka,
na damu hugusana na damu.” Hosea 4:1-2.
Ø Kuiba
fungu la 10 unasababisha kanisa lisifanye matumizi yake kawaida. Kwa kuiba
maana yake hupendi mikutano ya injili, hupendi kiwepo chakula kiwepo nyumbani mwa
Bwana. Kanisa linatembea kwenye laana, kanisa linakosa mvuto.
Ø Kuiba
kunaleta hasira ya Mungu iwke juu yako, “Watu
wa nchi wametumia udhalimu, wamenyang'anya kwa nguvu; naam, wamewatenda jeuri
maskini na wahitaji, nao wamewaonea wageni bila haki. Nami nikatafuta mtu
miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali
palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. Kwa
sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira
yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.”Ezekieli 22:29-31, Mungu amekuacha
uende katika njia zako mwenye kwa sababu umekataa kukubali na kutii. Wewe kama
unamwibia Mungu unataka Mungu akufanye nini.
MATATIZO
YA KIROHO KWA WATU WASIOTOA ZAKA
§ Watu
wasitoa zaka ni kwa sababu hawatii mamlaka kuu/mamlaka iliyopo, hamtii Mungu,
mchungaji hawalipendi kanisa. “Basi Yuda
Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti,
akasema, Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini?
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye
ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.” Yohana 12:4-6 Yuda
alikuwa hamtii Yesu, lakini Yuda alipoona yule mama anapomimina yale mafuta
anapoteza hela, lakini alionekana anawahurumia maskini na yale mafuta yangeuzwa
angefaidika kwa sababu alikuwa mtunza mkoba.
§ Uasi mtu asiyetoa zaka ni
muasi, “Ila watu waliteka nyara, kondoo
na ng'ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu
kwa Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda
sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na
kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na
ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye
amekukataa wewe usiwe mfalme.” 1
Samweli 15:21-23, unatakiwa
utafakari kama umemuasi Mungu kwa kutotoa zaka
§ Wachoyo; watu wanatamani kupitiliza, wnatamani vitu
visivyokuwa vya kwao, zaka ni mali ya Mungu, “Tutapata mali yote ya thamani, Tutazijaza nyumba zetu mateka. 19 Ndivyo
zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.” Mithali
1:13, 19 watu wanauwawa kwa kutoyoa zaka kwa sababu injili haiwafikii.
§ Watu hawaenendi kwa roho; Kama
huenende kwa roho ni vigumu kuenenda kwa roho. Kama Roho mtakatifu yupo
atakusukuma utoe na utapata amani.
Imeandikwa “Kwa kuwa nia ya mwili ni
mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.” Warumi 8:6
§ Wamerudi nyuma, watu
wsiotoa zaka wanarudi nyuma, yupo kanisani kama mshirika wa jengo lakini si
mshirika wa MUngu, ukitengeneza vizuri na Mungu utaona nguvu. “Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana
wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na
huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.” Luka 16:13
§ Unampenda Mungu kwa kiwango kidogo sana;
Ni
vigumu sana kwa mtu anayempenda Mungu kwa kiwango kidogo kumpenda Mungu kwa mali
zake na vitu vyake vyote “Nami tena kwa
kuwa nimeiwekea nyumba ya Mungu wangu shauku yangu, nami ninayo hazina yangu
mwenyewe ya dhahabu na fedha, naitoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu, zaidi
ya hiyo akiba niliyoiwekea tayari nyumba takatifu;” 1 Nyakati 29:3
§ Watu wasiotoa zaka wanawaza wanamwadhibu
mchungaji; mtu anawaza kwamba anamwadhibu mchungaji, kama
mchungaji anataka kufanya kitu atumie fedha zake. Ukiwaza hivyo ni mawazo ya
kiumaskini na uukiendelea hivyo hutaon aBaraka za Mungu.
Mchungaji Dr. Godson Issa Zacharia akiongoza maombi ya Toba wakati wa Ibada ya leo. |
MAWAZO
MABAYA YA WASIOTOA ZAKA/WANA SABABU ZAO
o
Napata
kidogo sana hivyo siwezi kutoa zaka, mtu anakuwa maskini ni kwa
sababu anawaza kinyume na maandiko, “Maana
aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.” Mithali
23:7, usipowaza mawazo chanya, ukiwaza ndivyo ulivyo na ndiyo
yatakayokupata. Mtu akiwaza kuwa ana
kidogo hii ni dalili ya wizi, na mawzo ya mwizi ni kwamba hupata kidogo sana.
Katika habariya utoaji hakuna habari ya kidogo au kingi.
o
Napata
sana siwezi kutoa zaka; “Lakini
mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani
vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.” 1 Nyakati
29:14, Unakuta kuna mtu amepata milioni 20, na 10% ya milioni 20 ambayo ni
milioni mbili, anaona ni kubwa sana anawaza hiyo hela angefungua kamradi
kingine. Lakini anasahau huo uwezo wa kutafuta milioni 20 ameupata kwa Mungu.
Hutakiwi kumlinganisha Mungu na vitu vyako.
o
Pesa
amepata kwa shida, hivyo hawezi kumtolea Mungu zaka; “Bwana, moyo wangu hauna
kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala
na mambo yashindayo nguvu zangu.” Zaburi 131:1 unatakiwa
ujue myoni mwako unamtolea yeye na usitake kujua matumizi ya pesa/zaka hiyo.
o
Wachungaji
wanatumia pesa zake kwa anasa; watu wengine wanawaza pesa
zinatumiwa na wachungaji kwa anasa/kwa faida zao, unatakiwa uwaze hiyo zaka
unafaidika mwenyewe. Hataki kumwona kiongozi wake amefanikiwa au amepiga hatua.
Huyu mtu anatamani mchungaji amevaa viatu vimetoboka na ndipo ataona pesa zake
zinatumika vizuri.
o
Wachungaji
wote ni matapeli na wezi; mtu mwenye mawazo mabaya anaona
wachungaji ni wezi, hutakiwi kuwasulubisha wema na waovu. Maandiko yanatupa
maonyo ya kuwaza huyu ni mwema na kumbe ni mwovu, wewe unatakiwa umtii Mungu.
Hukumu unatakiwa kumwachia Mungu, wewe unatakiwa utoe zakakwa ajili yakufungua
madirisha ya mbinguni. Kwa habari ya kwamba mchungaji anaiba mwachie Mungu. Imeandikwa,“Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na
kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; watiao
uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu!” Isaya 5:20.
o
Fungu
la kumi ni kubwa sana siwezi kutoa; kuna mtu anawaza 10% ni
kubwa sana anaanza kutoa 5% au 1% na akiona ni kubwa anazidi kupunguza. Lakini
serikalini tunalipa kodi 18%. Pia waza kama Mungu akaruhusu kiwanda unachofanya
kazi kikifungwa utapata wapi mapato. Utalala kanisani uombe Mungu atende, na
maombi ya mwenye dhami ni kelele mbele za Mungu.
o
Najenga
nyumba yangu hivyo siwezi kutoa zakazangu; lakini Mungu hajawi
kutanguliza tujenge nyumb zetu kabla yak wake. “Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, Je!
Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo
nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?” Hagai 1:3-4. Unaweza ukawa unajenga
nyumba na ukawa unaibiwa na mafundi.
o
Nina
msiba/sherehe ya kuchangia hivyo siwezi kutoa zaka; lakini serikali huwezi
kuiambia serikali wasikate kodi kwa sababu una msiba.
o
Nina
madeni mengi sana hivyo siwezi kutoa zaka; unawaza una mkopo
CRDB, VICOBAna Mchezo, na kwa nini usiache kuchangia ili utoe zaka.
o
Mimi
ni mjane hivyo siwezi kutoa zaka; wajane wanatakiwa
kuhurumiwa kabisa, Biblia inasema tusiwaonee wajane. Tunajifunza hata Eliya
alienda kwa mjane na alitaka kujua kama huyu mtu kama atatii. Mama Yule alipofanya
mkate Eliya akamwambia akakusanye vyombo. Maana yake muujiza wake ulikuwa
tayari baada ya utii. Hapa tunajifunza kila mtu anaweza kumtolea kawa nafasi
bila kujalisha hali aliyonayo. “Naye
akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi mkutano watiavyo mapesa
katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. Akaja mwanamke mmoja, mjane,
maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. Akawaita wanafunzi wake,
akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote
wanaotia katika sanduku la hazina;” Marko 12:41-43,
Baadhi ya makutano walioamua kumpa Yesu maisha yao ili waondokane na laana ya sadaka ya Zaka. |
o
Mimi
ni mwanafunzi siwezi kutoa zaka Wanafunzi wengi wanamwibia
Mungu kwa kujiteteta hawana kipato, ili hela unayopewa ya matumizi unatakiwa
utoe 10% maana ni sehemu ya Mungu. Neno la Mungu halijaweka matabaka bali
linawataka watu wote kumtolea Mungu zaka. Imeandikwa, “Mheshimu Bwana kwa mali yako,
Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.” Mithali 3: 9.
o
Sijaajiriwa
siwezi kutoa; hata ukiajiriwa huwezi kutoa kwa sababu umekosa utii. ukikosa
uaminifu ukiwa haujaajiriwa na hata ukiajiriwa hautakuwa mwaminifu. “Basi wale mitume waliporudi walimweleza
mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja
uitwao Bethsaida.” Luka 9:10.
o
Nimestaafu
niko kwenye pensheni siwezi kutoa zaka; kuna wastaafu wengine wanapesa nyingi
kuliko walioajiriwa. Hatutoi zaka kwa sababu ya wingi wa pesa
bali tunatoa kwa sababu ni agizo la Mungu.
o
Nasaidia
maskini, nafanya miradi hivyo siwezi kutoa zaka, kusaidia
maskini ni jambo zuri lakini hakuzuii wewe kutoa zaka, ili kuvunja umaskini katikati ya wakristo lazima tujifunze kutoa zaka.
Kuwa mtii wa sharia za Ufalme wa Mungu.
Showers of Glory Morogoro wakimsifu Mungu baada ya maombi ya toba wakati wa ibada ya leo. |
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK:
Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL:
+255 719 798 778
BLOG:
Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.co m/