GLORY OF CHRIST
TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA LA UFUFO NA
UZIMA MOROGORO
PASTOR DR. GODSON
ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 29 APRILI
2018
Mchungaji Dr. Godson Issa Zacharia akifundisha wakati wa Ibada ya leo. |
Mashimo ni mahali ambapo pamechimbwa kwa kazi maalum. Yawezekana ikawa
shimo kwa ajili ya Kisima au kuhifadhi taka na matumizi mengine. Lakini mashimo
haya ni mashimo ya rohoni yanayotumiwa kuleta uharibifu. Mashimo ya uharibifu
au, ni mashimo yapo katika ulimwengu wa roho hayaonekani kwa macho ya nyama. Mfalme
Daudi anasema alipandishwa kutoka shimo la uharibifu, Mungu alimpandishwa
kutoka kwenye shimo la uharibifu. Kupandishwa maana yake alikuwa amenaswa kwenye
shimo na alipotoka alikanyaga udongo wa utelezi na Bwana akamsimamisha. Katika
mashimo haya watu wengi wametumbukizwa na wamenaswa huko. Katika mashimo haya
ni mahali ambako shetani anakaa.
“Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka
udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.” Zaburi 40:2
“Malaika wa tano akapiga baragumu, nikaona
nyota iliyotoka mbinguni, imeanguka juu ya nchi; naye akapewa ufunguo wa shimo
la kuzimu.” Ufunuo wa Yohana 9:1
Ni shimo lililotengenezwa katika ulimwengu wa roho. Shetani
alikimbilia katika mashimo ya uharibifu au kuzimu. Mahali pengine mashimo haya
yanaitwa mashimo ya kichawi. Mchawi anaweza kutengeneza mashimo ya kukusanya
mizukule, au kukusanya mali na kuficha.
“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule
joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda,
wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa,
nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote;
akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu
mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na
mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye
awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya
MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata
kufa. Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na
bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya
kuwa ana wakati mchache tu.” Ufunuo 12:7-12
Hapa tunaona kulijuwa na vita mbingu na malaika waliosi wasiotii,
walipotaka kupandisha kiti chake juu zaidi ya kile cha Mungu, ndipo kukatokea
vita katika ulimwengu wa roho. Joka au Ibilisi alipigana na malaika lakini
hakushinda na akatupwa hata nchi. Biblia inasema alitupwa yeye na wale
waliokuwa wanashirikiana nao. Biblia inaposema nchi ina maana ni hapa duniani.
Hapa duniani angani, bahari na ardhini kuna mashimo ya roho. Mambo yote unayoona
katika ulimwengu wa mwili yameanzia katika ulimwengu wa roho. Mfano unapoona
meza, kiti au chochote kimeanzia ulimwengu wa roho. Tunakumbuka zamani wafalme
walikuwa wanachimba mashimo kuwatesa watu, mashimo yalikuwa na matope.
Baadhi ya Makutano wakimshangilia Bwana baada kuokolewa kutoka nguvu ya mashimo ya uharibifu. |
Shimo hili limetasfiriwa kama kuzimu au ulimwengu wa wafu kwa
kiebrania, pia limetasfriwa kama shafti ni shimo ambalo ukiiingia huwezi
kupanda. Maana yake yametengenezwa kwa kuchongwa sana. Na mahali pengine
limetasfiriwa kama Abis ni shimo lenye giza na taabu sana, kazi au masomo
yanakuwa na gizagiza. Shimo lisilokuwa na kimo, yaani ukidumbukia huoni ukifika
mwisho. Una kuta mtu anaota unadumbukia lakini hufiki mwisho. Unaona kazi, mume
, fedha zinatumbukia lakini leo Bwana atakutoa leo kwa jina Yesu. Mashimo haya
ni mabaya sana na kuna watu wengi wametumbukia kwenye haya mashimo.
“Hofu, na shimo, na mtego, vi
juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.” Isaya 24:17
Kila akaaye dunia anakumbana na hofu, shimo na mitego vipo kwa kila
mmoja anayeishi duniani. Mashimo haya wanaanda wachawi, waganga wa kienyeji na
mashetani ili kukupeleka shimo. Wachawi
hawakubebi mwili mzima bali wanaweza kuchukua nafsi yako na kupeleka shimonio.
“Lakini utashushwa mpaka kuzimu;
Mpaka pande za mwisho za shimo.” Isaya 14:15
Kijana huyu anaitwa Peter, hapa alikuwa anatoa ushuhuda namna alivyokuwa akitumikishwa kwenye shimo la uharibifu kule Musoma. |
Shimo hili ni refu sana wala huwezi kupanda, mashetani wametengenezwa
mashimo na kufanya kama makao makuu. Mizimu inaitwa mizimu kwa sababu ni viumbe
vilivyotoka kuzimu. Hii mizimu imewekwa ili ilete uharibifu, hasara, taabu,
shida, au kudhoohofisha kazi, afya na ustawi wako. Inawezekana ulishaambiwa
wewe hujafanikiwa kwa sababu hujaitumikia mizimu ya babu yako. Unapoweka agano
na mizimu ni unakuwa unawasiliana moja kwa moja na viumbe wa kuzimu. Kuzimu
linaitwa shimo la uharibifu kwa sababu linavuvia uharibu, kutoka kuzimu.
“Umeniinua nafsi yangu, Ee
Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.”
Zaburi 30:3
Mtu ni roho yenye nafsi inayokaa kwenye mwili. Kuna watu wameibiwa
nafsi zao na kupelekwa kuzimu au shimo.
“Aliyeufanya ulimwengu ukiwa,
akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?” Isaya 14:17
Mtu anapelekwa shimoni na anatumikishwa. Mashetani wanabeba roho yake
na mwili wanaweka roho ya joka ya kusumbua watu ili wamtumie. Hii roho
inayotolewa inatumiwa kuangusha magari, na katika mwili lile joka linafanya
kazi.
“Lakini watu hawa ni watu
walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana
asemaye, Rudisha.” Isaya 42:22
Mungu alimwonyesha Isaya kuna watu wanatenda kazi lakini amechukuliwa
wako mashimo, wamefichwa na wamekuwa mawindo, mateka lakini hapana aokoaye. Kumbe
mashimo haya ni kwa ajili ya kuficha na kuteka watu.
“Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini
kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai? Wazalisha wakamwambia
Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa
kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia. Basi Mungu
akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na
kuzidi kuwa na nguvu nyingi. Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa
wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba. Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake,
akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto
mwanamke mtamhifadhi hai.” Kutoka 1:18-22
Mfalme Farao aliona wana wa Izraeli wanaongezeka sana na kwa kasi,
basi akaongea na wazalishaji wakiwa wanazalisha kama mtoto wa kiume muueni na
wa kike waache waishi. Mashetani wana uwezo wa kuchungulia na kujua kama mtoto
huyu akizaliwa atakuwa mkuu, waziri mkuu kumbe kuna mauti imetengenezwa ili
mtoto apelekwe shimo. Inawezekana kuna mambo yako yanazaliwa lakini yanakufa
haraka haraka, ndoa inaanza, kazi inaanza
zinakufa. Mapepo yanapoona kesho yako unaanza kufanikiwa wanaiua haraka.
Wale wazalishaji walikuwa wacha Mungu walikataa kuwaua.
“Maana bila sababu wamenifichia
wavu, Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.” Zaburi 35:7
Shimo linaweza kuchimbwa na mtu kwa ajili yako au watoto wako. Kuna
baadhi ya watu wameshachimbiwa shimo, afya yako imenasa, kukataliwa, shida na
huwezi, wamekufichia wavu.
“Amechimba shimo, amelichimba
chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!” Zaburi 7:15
Shimo limechimbwa chini sana, unaona ukianza kujenga nyumba imekwama.
“Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo
la madhara; Katika midomo yake mna moto
uteketezao.” Mithali 16:27
Mtu asiyefaa kitu ni watu kama wachawi, mganga wa kienyeji, anapanga
kukuua wewe. Wewe upo lakini kuna watu wamekuchimbia shimo ili usitoke. Ukiri: Leo
natoka kwa jina la Yesu, shimo nililochimbiwa na rafiki, ndugu, bosi wako, au
baba nalifukia kwa damu ya mwanakondoo. Mtu anaweza kutengeneza shimo likakaa
ndani yako.
“Kinywa cha malaya ni shimo
refu; Anayechukiwa na Bwana atatumbukia
ndani yake.” Mithila 22:14
Kinywa cha Malaya ni shimo refu. Kuna binadamu barabarani wanatembea
kawaida lakini ni shimo refu na ukiambatana naye unadumbukiwa. Mtu anayefanya
uzinzi hawezi kuacha kwa sababu alipofanya kwa mara ya kwanza na hawezi kuacha,
mara leo yupo na huyu kesho na yule. Hilo ni shimo limeachia likakumeza. Shimo
la uharibifu linaweza kuwa mtu mwenyewe.
“Kwa maana kahaba ni shimo
refu; Na malaya ni rima jembamba.” Mithali 23:27
Anayefanya kahaba ni shimo refu, wanakutengenezea ukianza kitu
chochote kiharibike.
“Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na
vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa. Asubuhi mfalme
akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba. Naye
alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme
akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu
wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danieli
akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.” Daniel 6:18-21
Daniel alitupwa kwenye shimo la Simba, mfalme hakulala na usingizi
ulimpaa, mfalme anaweza kukutoa kwenye tundu la samba, yeye anayekuweka ndiyo
anayeweza kukutoa. Mfalme hakulala kwa sababbu mtakatifu wa Bwana ametupwa
shimoni, Daniel hakuonekana na kosa wala hatia.
Lakini leo tunaye Mfalme Yesu Kristo, ambaye alitoa maisha yake kwa
ajili yetu. Yesu halali akiona nyumba, ndoa, kazi ipo shimoni mpaka vyote
vimetoka. Mfalme Dario alipoamka asubuhi akamuuliza Daniel Mungu unayemtumikia
je amekuokoa? Mungu aliye hai akuokoe na shimo la uharibifu kwa jina la Yesu.
“Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana
mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye
thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na
nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo
cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; na
mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya
mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari,
na miili na roho za wanadamu.” Ufunuo 18:11-13
Hizi ni bidhaa ambazo wafanyabiashara wa nchi wanazozifanya. Kuna biashara
ya miili ya na Roho za wanadamu inaendelea kwenye ulimwengu wa roho. Kumbe mashimo
haya ni sehemu ya kutunzia roho za wanadamu waliobiwa. Leo lazima tuwatoe kwa
jina la Yesu.
KWA
MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI:
FIKA
KANISANI,
KANISA LA
UFUFUO NA UZIMA MKUNDI MINARA MITATU MOROGORO
AU
WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK:
Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us
on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us
on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255
719 798 778
BLOG:
Ufufuo na Uzima Morogoro