GROLY
OF CHRIST TANZANIA CHUCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA –MOROGORO
PASTOR
DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI
MAY 20, 2018
Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akiwa tayari kutafuta na kuokoa kilichopotea. |
UTANGULIZI
Kwa miaka mingi jamii
za watu, kabila na lugha wamekuwa chini ya utumwa wa shetani, maisha yao
yakiongozwa naye. Wametawaliwa kimwili na kiroho, wamenaswa kwenye mashimo,
wamekuwa mawindo, wamezamishwa kwenye misitu ya uovu, wameibiwa mali na vitu
vyao na wamekosa msaada, lakini Mungu kwa upendo wake akamtoa mwanae mpenzi ili
watu waokolewe. Kwakuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile
kilichopotea.
“Kwa kuwa Mwana wa
Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” (Luka 19:10)
Mwana wa Adamu ni Yesu
Kristo mwenyewe (Yoh 1: 14). Hapo
mwanzo Yesu alikuwa ‘Neno’, alikuwa kwa Mungu, naye ‘Neno’ akavaa mwili akakaa
kwetu (Yohana 1:1-3). Ndiye aliyekuja kama Imanueli [Mungu pamoja
nasi] akazaliwa na mwanamke, akautoa uhai wake ili kupitia huo awaokoe wanadamu
ambao ni mimi na wewe kutoka katika mikono ya shetani.
Baadhi ya makutano haya wakifuatilia neno la Mungu kuhusu Oparesheni kutafuta na kuokoa kilichopotea |
Yesu Kristo alizaliwa
kama mwanadamu wa kawaida, aliishi kama mwanadamu wa kawaida. Ulipofika wakati
wake wa kuitenda kazi ya Mungu aliingia hekaluni, akisha kupewa kitabu, akafungua unabii uliokuwa umetabiliwa na nabii
Isaya, akasoma maandiko yafuatayo kudhihilisha lile alilojia hapa dunia.
“Akapewa chuo cha nabii
Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu
yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,
Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,Na kutangaza mwaka
wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo,
akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi
wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni
mwenu.” (Luka 4:17-21)
Maneno ya Bwana huwa yana
andikwa na kutunzwa kwa wakati wake, ukifika wakati wa utimilifu wa maneno hayo
matakatifu ya Mungu, Mungu humtuma mjumbe wake kuyatimiza. Unabii wa nabii
Isaya uliandikwa miaka mingi sana iliyopita, lakini wakati wa kutimia kwake
ulikuwa hujafika bado, ndipo Kristo alizaliwa baada ya muda kutimiza unabii
huo.
“Roho ya Bwana MUNGU i
juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari
njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru
wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana
uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;” (Isaya
61:1-2)
Tangu wakati wa nabii
Isaya watu walikuwa wanachukuliwa mateka, waliwekwa chini ya utawala wa giza na
kumezwa na mwovu pasipo msaada wowote. Ndipo mwana wa Adamu akaja duniani
kutafuta na kuokoa kile kilichochopotea, kuwafungua waliofungwa na kuonewa
chini ya utawala shetani Ibilisi.
Yesu anapokuja kutafuta
kwenye maisha ya wanadamu, huwa hatafuti lile linalo onekana, hutafuta ambalo
limepotea, limefichwa, limeibiwa na kuwekwa mahali pa siri. Ikiwa kuna kitu
ambacho ulikiweka mahali fulani ukategemea kesho ukichukue na ulipoenda siku
inayofuata ukakikosa ujue kuwa kimeibiwa. Mungu aliwaweka wanadamu duniani wakiwa
kamili, lakini watu hao wamepotea, wamepoteza mali zao, ndoa, mazao yao yameibiwa
na kufichwa mahali. Ndipo sasa Mungu akaja ili kuokoa na kutafuta kilichopotea.
Baadhi ya Makutano wakijifunza kwa habari ya kutafuta na kuokoa kilichopotea. |
Bwana uingia kwenye mashamba, kwenye mapori, mapango, nyumba za watu, juu ya dali. kwenye ofisi za watu, n.k, kutafuta na kuokoa kile ambacho kimeibiwa na kufichwa mahali. Yapo mambo mengi na vitu vingi vyako vimehamishwa mahali pake na kupelekwa sehemu nyingine. Mfano, amani yapasa kuwako ndani ya ndoa na familia lakini inaibiwa na kufichwa mahali hatimaye ndoa imekua uchungu, ndipo sasa anakuja kuitafuta ili kuirudisha mahali pake. Mchungaji mwema akiwa amepoteza kondoo mmoja ndani ya kundi la kondoo mia, huwaacha hao tisini na kenda na kuenda kumtafuta mmoja aliyepotea na akisha mpata anafurahi sana.
Biblia inataja habari
za Mwana mpotevu aliye omba mali na fedha kutoka kwa baba yake , kwa kuwa baba
yake alimpenda akampa, akenda nchi ya mbali, akatapanya mali hizo kwa uzinzi na
uasherati. Njaa ikaingia kwake hata akaamua kujilisha pamoja na nguruwe, kwa
mateso hayo akapata akili na akawaza kurudi kwa baba yake, aliporudi baba yake
akafurahi sana kwa kumuona mwanae, (Luka
15:11-20). Hakika kuna furaha katika kurudisha, leo Bwana anataka kuokoa na
kurudisha vitu vyako vilivyofichwa na mwovu kwa jina la Yesu.
Biashara yako iliyokufa,
kazi yako iliyokufa, elimu iliyokufa, Bwana amekuja kuiokoa na kuirudisha
mahali pake. Mara nyingine unajikuta wewe ni mama, siku zako zimepotea; mwezi wa
kwanza, wapili hata watatu yamkini wamezipoteza ili hukose mtoto. Yesu Kristo
amekuja ili urudishe kile ulichopoteza kwa jina la Yesu.
Macho ya Mungu yanaona
kila mahali, huenda ukawa umechukuliwa kwa namna ya rohoni na kuweka kwa siri
kwenye mkoba wa mtu, kwenye uvungu wa mtu. Mara nyingine unaweza kuibiwa na
kuchukuliwa vitu vyako halali na kuwekwa mahali. Mfano, unaweza kuibiwa soksi
moja ikapelekwa mahali na tangu siku hiyo umekuwa unatabia mbaya, mambo hayaendi
kwakuwa umechukuliwa kwa namna ya kichawi.
Platform wakiongoza kipindi cha sifa na kuabudu. |
Nguo, nywele, kucha au
kitu chako chochote ni kiwakilishi chako. Yusufu alipomkimbia mke wa Potifa
aliacha sharti, na kupitia sharti hilo alikamatwa na kuweka gerezani. Hivyo
mali yako au sehemu yako inaweza kuchukuliwa na watu waovu ikapelekwa mahali na
ikawa kiwakilishi chako katika kutesa maisha yako yote. Leo Bwana anataka
kurudisha kile kilicho ibiwa, kurudisha kazi, ndoa,n.k. kwa jina laYesu.
Akili ya mtu pia
inaweza kuibiwa, kutekwa, upendeleo wako unaweza kuchukuliwa, kibali chako
kinaweza kutekwa mahali ili tu uharibikiwe. Kwakuwa Yesu alifahamu haya ndipo
akaja kutafuta na kuokoa kile kilicho potea.
Mtu aweza kuchukuliwa
na kutekwa, mali na mambo yako yanaweza kuchukuliwa na kutekwa. Vile vitu vyako
vinavyo haribika mara kwa mara ni kwasababu kunamtekaji amekuja kuvichukua na
kuviteka. Mtu anapochukuliwa mateka, na kwakuwa mtu huyo huwa haonekani
wanamwita msukule na mara nyingi huwa anakufa kabisa katika hali ya mwili na
ndipo wanamchukua na kumteka anakosa uhuru, na utumiwa kama anavyotaka mtekaji
wake kwakukosa maarifa.
“Kwa sababu hiyo watu
wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo
wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.” (Isaya 5:13)
Nabii Isaya alionyeshwa
na Mungu kwamba watu hawa wanao onekana; wanakula, wanatembea, walala na kumka,
kuoa na kuolewa, wameibiwa na kutekwa, wamechukuliwa na kunaswa kwenye mashimo.
Chanzo kikubwa cha kuchukuliwa kwao ni kukosa maarifa, kutokujua kamaa kunawachawi,
kuna waganga, majini. Kushindwa kufahamu kuwa kwa jina la Yesu ataokolewa.
Shetani siku zote anafanya kazi kwa siri sana ili asionekane, anapata nguvu
ikiwa anachomfanyia mtu hakijulikani.
“Lakini watu hawa ni
watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana
asemaye, Rudisha.” (Isaya 42:22)
Shetani alijaribu
kumwibia Ayubu mali, ndoa, kazi zake akashindwa kwakua Bwana alimzingira Ayubu
pande zote kwamaana alimtumikia Mungu kwa mwaminifu (Ayubu 1:1-3). Ndipo shetani akaenda mbele za Mungu akamwambia atoe
mikono yake ya ulinzi kwa Ayubu (Ayubu: 10),
Mungu alipotoa mikino ndipo mambo yakaharibika, mali zikaharibika na kila
alichokuwa nacho (Ayubu 1:13-20). Watoto wa Ayubu na mali zake ziliibiwa na watu
au mipango ya shetani si kwaajili ya Mungu. Kuna wakati shetani anavaa mwili
akatenda kazi kama binadamu ili aibe mali na vitu vya wanadamu.
Maranyingine waweza kumuona
mtu mwenye afya nje, cheo na mali lakini ametekwa, ameibiwa fedha, mali, kazi
n.k. Wamefungiwa huko hata hawawezi kujiongoza wenyewe, wamewekwa kwenye nguvu
za shetani na utawala wake hata hakuna msaada. Wakati mwingine mtu anaweza
kuibiwa tumbo, akili, moyo n,k vikawekwa mahali kifungoni.
Baadhi ya Makutano waliamua kumpa Yesu maisha yao ili waweza kutafuta, na kuokoa kilichopotea. |
Unaweza kuibiwa sura
yako au akili yako. Wanaenda kwa waganga
nakuchukua kile wanacho kitaka kwako, sasa yule aliye ibiwa anakuwa katika
kundi la kukataliwa, hakuna anaye msemesha, hakuna anaye mtaka kwakuwa sura au
kibali chake kimeibiwa. Leo Bwana arudishe kibali chako kwa jina la Yesu.
Jambo la kushangaza
chini ya nchi nikuwa wale walio ibiwa na kutekwa ni wengi sana kuliko walio
huru. Mtumishi wa Mungu Stephano alipigwa kwa mawe hadi kufa (Matendo 7:59), wengine walichomwamoto,
na kukatwa vichwa (Marko 6:24-25).
Kimsingi si wote wanaokufa, wanaopotea, wanaokaa kifungoni ni mapenzi ya Mungu,
hapana! ni kazi za wovu. Ndipo bwana anasema siwezi kukaa ikiwa watu wake wanatekwa,
wanauawa, wanapelekwa utumwani ndipo akasema.
“basi sasa, nafanya
nini hapa, asema Bwana, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanao watawala
wanapiga yohe, asema Bwana, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa”(Isaya
52:5)
Mwanadamu ni kazi ya
Bwana, lakini wachawi wanamtumia binadamu huyo kama ndondocha na kuwatumia
wanavyotaka, kwa kufanya hivyo jina la Bwana linatukanwa (Zaburi 138:8).
Watu wanaweza
kuchukuliwa mateka kwa namna tatu. Kumbuka mtu ni roho anaka kwenye nyumba
inaitwa mwili. Kwakuwa mtu ni roho anaweza
kuchukuliwa kwa namna tofauti kuwekwa kifungoni kama ifuatavyo;
1.Anaweza
kuchukuliwa mzima kabisa. Wachawi wakimuona mtu anafaa
kwenye mambo yao, wanakuja wanafanya uchawi wao kisha wanamchukua kwa kumtoa
kwenye mwili wake kisha wanaleta gogo likavaa sura ya mtu huyo. Wakati watu
wanahangaika na gogo ili walizike wao wanakuwa wamemchukua mtu huyo kumfanya
watakavyo.
Sikumoja Askofu mkuu,
Dr. Josephati Gwajima alikwenda msibani mahali, alipokuwa anapita kuaga mwili
wa marehemu akaona mgomba umevalishwa suti umewekwa kwenye jeneza, akapita mara
ya kwanza na ya pili, akasimama akawambia watu wote walikuwa mahali hapo huyu
simtu bali mgomba, wakambishi ndio akasema ‘kwa jina la Yesu’ yule kijana
akatoka ndani ya nyumba na kwenye jeneza ukaonekana mgomba kabisa.
Binti huyu alifunguliwa kutoka alikokuwa ametekwa, hakika amewekwa huru kwa jina la Yesu |
Jana msavu stendi
Morogoro alionekana kijana anaumwa mguu, watu wa stendi wakaamua kuchanga ili kumpeleka
hospitali, wakati wanampeleka akatokea mtu anasema jamani mtu huyu si alikufa tanga?
Wakamkatalia, lakini walipokwisha mpeleka hospitalini akapotea katika mazingira
ya kutatanisha hadi leo hayupo.
Kwa mifano hiyo jifunze
kuwa watu wanaweza kuchukuliwa na kufichwa, katika mwili akaonekana amekufa na
wakamzika kabisa na kuandika jina lake kwenye msalaba, kumbe mtu huyo amechukuliwa
amepelekwa mahali kufanya kazi kichawi. Wanaweza kumchukua mtu na mara nyingine
wakamzika kumbe yuko Uganda anafanya kazi benki.
2.
Mtu anaweza kuchukuliwa na kupotea kabisa, asife wala
asionekane mahali kumbe amechukuliwa kwa namna ya kichawi wakamtowesha
kumpeleka sehemu kufanya kazi. Tunajifunza mfano wa Yusufu aliyeuzwa na ndugu
zake wakasema kuwa amekufa kumbe wamemuuza misri. Hivyo inawezekana mtu
kutoweshwa katika mazingira ya kutatanisha kisha akapelekwa mahali pasipo
julikana.
3.
Mtu anaweza kuchukuliwa kwa namna ya rohoni. Kwakuwa mtu ni
roho wanakuja kiuchawi na kumtoa ndani ya mwili kisha kumpeleka wanako taka (Yohana 6:63). Roho ndiyo itiayo uzima
mwili haufai kitu, kwakua mwili bila roho umekufa, wanapochukua roho yake
wanapanda roho ya mashetani ndani ya mwili. Ndipo matatizo kadha wa kadha
yanamtokea mtu huyo.
Ndiomaana tukimrudisha
mtu toka msukuleni anasema nilikuwa Tanga nalima mashamba ya katani, unapo
muuliza sasa nani alikuwa kwenye mwili wako? Anasema jini, au paka au mbwa. Unaweza
kuona mtu ndani ya familia anasababisha shida, ugomvi kwakuwa si mtu bali ni
pepo aliye ndani ya mwili wake.
Mchungaji Dr. Godson Issa akimfungua binti huyu na kumweka huru. |
Kuna wakati unaweza
kumwona mtu anasumbua kwenye mtaa, mwingine anaacha kazi anatumia fedha vibaya,
pia unaweza kuzaa mtoto kwenye familia hatari mno anasumbua sana ukaamua
kumchapa kila siku, usimwaribu mtoto huyo kwamaana anaweza kuwa si mtu. Kristo
alikuja kuokoa na kurudisha kile kilochotekwa na kuibiwa na leo amekuja ili
wewe uokolewe kwa jina la Yesu.
Ulifunga ndoa na mume
wako alikuwa safi, mtulivu, mpole lakini gafla anaanza kurudi usiku amelewa, anatoa
maneno ya ajabu, unamuuliza umekuwaje? Hana jibu, mtu asiye na maarifa akiona
mume wake yuko hivyo anaenda kwa mganga. Usifanye hivyo, mchawi hawezi
kukusaidia, acha kwenda kwa mganga wa kienyeji tena mganga wa kienyeji ni mbaya
kuliko mchawi, yeye anajua kuweka na kutoa uchawi. Njoo kwa Yesu, yeye amekuja kuokoa na
kurudisha kile kilichopotea, kuna uwezo wako umepotea, kibali chako kimepotea
hata huwezi kufuatilia mambo yako, ndoa yako imepotea lakini Kristo amekuja
kukuoka wewe kwa jina la Yesu.
Biblia inasema
usimwache mwanamke mchawi kuishi (Kutoka
22:18), si kama Mungu alikosea bali ni kwasababu hawa wachawi ni wabaya wanaweza
kumchukua mtu, mali yake na uwezo wake wakautumia watakavyo. Siku moja niliwahi
kumkuta mtu kwenye kibao cha kanisa, nilipomwoji akawa mkali mno, nikamchukua
nikamleta kanisani kisha nikamwombea, baada ya siku mbili mama yake akaja
anataka mtoto wake, akasema kuwa alikuwa anapata msaada kupitia mtoto huyo,
kumbe walimchukua wanamtumia kichawi. Leo Bwana anataka akutoe kwenye utumwa wa
kichawi kwa jina la Yesu.
Showers of Glory Morogoro wakiimba na kucheza mbele za Bwana. |
Sababu zinazo
sababishwa mtu achukuliwe msukule ni kukosa maarifa, biblia inasema watu wangu wanapotea
kwa kukosa maarifa (Hosea4:6),
sababu nyingine inasabaibisha mtu kuchukuliwa mateka ni wivu (Matendo 5:17-21),
sababu ya tatu ni dhambi. Dhambi inamfanya mwanadamu kukosa ulinzi wa Mungu na
kuwa rahisi kwa shetani na mawakala wake kumchukua.
“nikasema, Ee Mungu
wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa
maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu
imeongezeka na kufika mbinguni. Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia
kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na
makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa
upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang'anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso
zetu, kama hivi leo.” (Ezra 9:6-7)
Ili uweze kuwekwa chini
ya ulinzi wa Mungu lazima umkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako,
ukisha mpokea Yesu utajifunza maarifa ya Neno la Mungu kwa namna hiyo unakuwa
chini ya ulinzi wa Mungu na shetani hawezi kukuchukua mateka wewe kihurahisi, watoto
wako na kile ulicho nacho. Mungu akubariki kwa moyo wako uliyo tayari kumfuata
Kristo na kuwawaokoa waliotekwa. Ameni.