Sunday, July 21, 2013

SOMO: UMEKUFA UNGALI UNAISHI


Na Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia | Morogoro | Jumapili 21 July 2013

Neno la Msingi1TIMOTHEO 5:6”  Bali yeye asiyejizuia nafsi yake, amekufa ingawa yu hai.” Yeyote asiyeweza kuzuia nafsi yake amekufa ingawa anaishi.
 
Kwanza nafsi ni nini? MWANZO 2:7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai.
 Mtu ni nini? 
Mch.Kiongozi Dr. Godson akifundisha mapema leo hapa Kanisani
Ni roho yenye nafsi inakaa ndani ya nyumba na nyumba inaitwa mwili. Nyumba zinatofautiana wiki chache zilizopita tulikuwa na wajapani weupe, na pia kuna wahindi wekundu wanaishi marekani. Mwanadamu angekuwa ni mwili, basi tungekosa maana halisi ya kile ambacho Mungu alisema kuwa tuumbe mtu kwa mfano wetu. Alikuwa anamaanisha roho. Na mara baada ya mwili na roho kuungana, ikaleta kitu kinachoitwa nafsi. Na kama roho ikitengana na mwili nafsi hupotea.

Nafsi ya mtu kimsingi ndiyo chanzo na msingi wa utu wake, maana nafsi ikiwepo ndo tunaona uhalisia wa utu wako ndo maana hata tunapowaleta watu kwa Yesu kwa kiingereza inaitwa SOUL WINNING. Na nafsi inatupatia vitu kama vitatu vya msingi:

1.NIA/MIND
 Hii ni sehemu ya fikra/department of thoughts, ni sehemu ambayo unafikiria na kukupa uwezo ufanye nini. Rumi 12:2 “wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza, na ukamilifu.

2.UTASHI/WILL
Shemu hii ya nafsi inahusiana na maamuzi, unapoona mtu anapoamua vibaya ujue utashi wake umeshavamiwa na shetani. Hivyo utashi ni sehemu muhimu sana ya maisha yako maana maamuzi yako ndiyo yatakufanya uwe nani

3.HISIA/EMOTIONS
Ukimuona mtu ana hasira, ana jazba, ana furaha ujue haya yote yanaaanzia kwenye hisia. Hapandipo utasikia mtu anaexpress upendo, kuna namna ambayo unaweza kuonyesha hisia zako na mtu anaweza kukujua kupitia hisia zako na mashetani wanaweza kugeuza fikra zako ndipo hata wale ambao walikuwa tayari kukusaidia wanaacha
.
Yohana 11:25-26 “Yesu akawaambia, mimi ndimi huo ufufuo na uzima……." na kuna mauti ya aina mbili, ya kwanza ni ile ambayo mwanadamu ametengana na Mungu, na mautiya pili ni ile ambayo mtu anatupwa jehanum.

Tuna watu wengi sana ambao wanatembea wakiwa wamekufa ingawa wako hai “watu wapo lakini hawapo” maana pale ambapo mtu anashindwa kuizuia nafsi yake amekufa ingawa amekufa. Mtu asiyeweza kujitawala, hawezi kuamua mambo yanayomhusu yeye mwenyewe, anaweza akawa mfanyakazi, huyo amekufa ingawa anaishi. Au mwingine alitakiwa aende shule kusoma amelipiwa ada yote ukimuuliza moja jumlisha moja anajibu kumi na moja, mtu kama huyu hayupo ndani kabisa, unaweza ona handsome boy lakini kila siku anashindwa kujizuia kwenye mambo  ya uzinzi, mtu kama huyo amekufa ingawa anaishi, na watu wa namna hii ni wengi saana tena sana. Utakuta mtu alitakiwa kuolewa, wamepanga kukutana na mchumba wake kanisani utakuta binti anasema maneno ambayo Yule mchumba wake anakata tamaa, kumbe nafsi yake Yule  binti nafsi yake imeshikiliwa na majini, hivyo nafsi yako inafanya ambayo wewe mwenyewe hupendi, hivyo umekufa ingawa unaishi. Ukiona huwezi kuamua kufanya mambo yanayokuhusu mwenyewe unasubiria mpaka uamuliwe na watu ujue unaishi ingawa unaishi
.
Mch.Kiongozi Dr. Godson akimhoji  binti Anna aliyekuwa amechukuliwa msukule akiwa anashuhudia
Kuna binti mmoja anaitwa Ruth ambaye alichukuliwa msukule na mjomba wake na alikuwa akifanya kazi ya kuwapikia uji misukule wengine. Anasema alichukuliwa msukule akiwa darasa la sita na ndani yake kuliwekwa joka ambalo ndo lilikuwa linalinda mwili wake. Anasema alikuwa anapika uji na mjomba wake alikuwa anawapelekea misukule ambao walikuwa wanalima kwenye mashamba hayo na cakula chao kingine kilikuwa ni pumba. Na wakati mwingine walikuwa wanaenda kupalilia mashamba ya huyo mzee. Ila kiuhalisia huyu binti amesoma mpaka form four na muda wote huo akiwa anasoma mwili wake ulikuwa unalindwa na joka. Alikuwa amekufa, ingawa anaishi

.
Pia kuna dada mwingine anaitwa Agness ambaye alirudishwa msukule alikuwa amewekwa mto Nile na anasema ndani yake alikuwa anaishi babu yake ambaye alikuwa anampa maelekezo ya kila kitu anachofanya. Na anasema alikuwa ameolewa na mume wake, na mara nyingi mume wake alikuwa akimwona alikuwa anamwogopa maana alikuwa anaonekana kama babu. Na wakatimwingine alikuwa akimchagulia nguo ya kuvaa, lakini majeshiya BWANA yalipoanza kuita njooooo alijikuta anatapikwa na huyo babu na ndiyo ikawa kufunguliwa kwake huyo dada, alikuwa amekufa angali anaishi.

Mch.Kiongozi Dr. Godson akimhoji  Agness akishuhudia alivyokuwa amechukuliwa msukule na kupelekwa mto Nile
 MUNGU WETU NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE
UFUFUO NA UZIMA-MOROGORO
Share:
Powered by Blogger.

Pages