Sunday, August 13, 2017

KURUDISHA ASILI YETU - Semina Siku ya 6

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (G.C.T.C)
                 {KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ­- MOROGORO}
                              
                             IJUMAA: 11 AUGUST 2017

MHUBIRI:  PASTOR GODFREY MWAKYUSA (SNP-SHINYANGA) 

Yohana 3:16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Mungu akaupenda ulimmwengu na ndio maana alimtuma mwanae wa pekee,kumbe upendo unaambatana na kutoa,huyu mwana aliyetolewa naye akaamua kujitoa .
2 Wakorintho 8:9
9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
Huyu mwana aliyetolewa alikua tajiri ,ingawa alikuja kwetu lakini alijifanya masikini ili sisi tuwe matajiri ,huyu alikua na asili ya utajiri,kumbe umasikini sio asili yetu.
2 Wakorintho 9:8
8 Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;
Mungu anapoona watoto wake tukifanikiwa huwa anafurahi sana,Ayubu alikua na ng,ombe wengi sana ,alikua na kondoo wengi,alikua na watoto wazuri lakini vyote vilikwisha ,hapa tunajifunza kuwa asili hii ya matukio yaliyompata Ayubu ni ya kishetani ,lakini Ayubu aliweka msimamo wake kwa Mungu wake na ndipo aliporudishiwa asili ya utajiri wake.
Kuna mambo tumewekewa lakini sio asili yetu,kuna mtu akiingia tu kanisani mzima akirudi nyumbani mgonjwa maana yake kuna mahali wachawi wametuma mashetani kwamba nendeni mkaweke magonjwa ndani yake au kwenye familia yake ,hapo wameshagundua asili yako ni ya mafanikio wanachofanya wanataka wakucheleweshe,lakini jioni ya leo we mng,ang,anie Yesu na asili yako itarejeshwa tena.
Wagalatia 6:17
17 Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.
Waefeso 1:3
3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
Yaani kwa asili Baraka zote tunazo,Baraka za uzao ,Baraka za ndoa ,Baraka za mafanikio, lakini zipo kwenye ulimwengu wa roho,unachotakiwa kufanya wewe ni kupakua zije katika ulimwengu wa mwili na uzimiliki.tuna asili ya kufanikiwa,mtu anapozaliwa anazaliwa kutoka kwenye ukoo,na hizi koo zetu zimejaa matambiko na ndio maana mtu akisema kwenye familia ya kwamba umeokoka wana ukoo wanainuka wanamwambia wewee ulimuona nani kwenye ukoo wetu ameokoka wanaanza kukupinga.
Kuna mwingine una magonjwa yalitoka kwa mama yako leo unaugua wewe unaambiwa ni magonjwa ya kurithi,kuna watu leo wana asili ya vifo vya kufanana kwenye familia, mnawekewa kalenda ya kichawi ili muwe mnakufa tarehe za kufanana familia yote,asili ya mtu pia inaweza kuibiwa kupitia zawadi ,yani mtu anaweza kukuletea zawadi we ukaona jamani huyu ndugu yangu ananipenda kweli kumbe nyota yako ndio imeshaibiwa,yani una asili ya kufanya mambo mazuri lakini unasahau,wanakuwekea asili ya kusahau wanaondoa kumbukumbu zako,kuna mwingine ni mtendaji kazi mzuri lakini ukimpa hela hana uaminifu ni mwizi wamekupandia asili ya kuiba ,kuna mambo mengine shetani amekuwekea asili kupitia kinywa chako wewe mwenyewe unaharibu unakua ni mtu wa kuropoka tu.
3 Waraka wa Yohana1:1-4
1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.
2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
3 Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.
4 Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.
Huyu mzee Gayo alifanikiwa rohoni aliku imara sana lakini mwilini alikua dhaifu ,sasa Paulo akamwambia naomba ufanikiwe zaidi kama vile roho yako ifanikiwavyo.
2 Timotheo 1:5
5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.
Paulo anamwambia Timotheo kwamba akiikumbuka imani iliyokua kwa bibi yake Loise ikahama ikaja kwa mama kisha ikaja kwa mtoto,kumbe imani inaweza kuhama ikatembea kwenye familia ,leo tunataka tuhame kwenye asili ya maneno tuliyotamkiwa kama uliambiwa hutafanikiwa leo unakwenda kufanikiwa kwa jina la Yesu,kama ulitamkiwa hutazaa leo tunakwenda kufuta maneno hayo na utazaa kwa jina la Yesu .
MAOMBI:
Katika jina la Yesu leo nakataa asili ya magonjwa ,asili ya kukataliwa ,asili ya utasa ,asili ya madeni ,nawapiga mashetani wote mlioshikilia asili yangu achia kinywa changu,achia miguu yangu nakataa leo kwa damu ya mwanakondoo tumbo langu halitawekwa mikoba ya kichawi.
Share:
Powered by Blogger.

Pages