GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH, (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO
JUMAPILI:
08 OCT, 2017
Kuna
mtu au kiumbe ambacho kipo duniani ama katika ulimwengu wa mwili ama rohoni
amesimama kukuzuia kwa lengo Fulani, kiumbe huyu anaweza kuwa binadamu au
shetani anaweza kukuzuia katika jambo Fulani. Sasa viumbe hawa wanazuia nini
basi, wanazuia elimu yako usisome, wanazuia ndoa, wapo walio inuka na kusimama
ili wazuie usizae watoto, wengine walitakiwa wasafiri lakini hawaja safiri
wamezuiliwa ama katika ulimwengu wa roho ama katika ulimwengu wa mwili.
Watu
au viumbe wanajua kuwa kuna mahali unaenda kwenye Baraka zako, lakini wazuiaji
hawa wanajua wana zuia ili usifanikiwe, ukipata hela kwa ajili ya ujenzi
matatizo yaanza magonjwa ama misiba, ukiona hivyo ujue yupo azuiaye leo
namwondoa aondoke kwako na kwenye familia yako kwa jina laYesu. Wazuiaji hawa
hawakai ila wamesimama ili waone vizuri ili wakuzuiye, lakini neno linasema Yeremia 1:5 imeandikwa, “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na
kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” Mungu
alikujua tangu mda lakini leo haupo hivyo kama Bwana alivyo kujua lakini mimi
nasema utafanikiwa kama neno linavyo
sema kwa jina la Yesu.
Kuna mama mmoja namjua miaka mingi kidogo iliyo pita
lilimpata jambo la ajabu kidogo, mama huyu alifanya kazi miaka ishirini katika
ofisi Fulani bila kupandishiwa mshahara wala kupanda cheo, siku moja mama huyu
alikuja kanisani kwa huduma ya maombi na kuombewa, siku ya pili yake akaenda
ofisini kama kawaida yake, alipo fika ofisini akaanza kufanya usafi katika
ofisi ya bosi wake jambo la ajabu katika droo ya bosi wake akakuta vijeneza
viwili kimoja chake na kimoja cha dereva wake na majeneza hayo yalikuwa na
majina yameandikwa, alipo fungua ndani akajikuta yeye yumo ndani ya jeneza...
unaona jinsi watu wanavyo zuiliwa, mama huyu alizuiliwa asipandishwe cheo, sasa
leo wapo watu wengi walio zuiliwa kwa jinsi hii lakini Yesu atawafungua kwa
jina la YESU.
Baadhi ya Makutano wakifuatilia neno la Mungu katika Ibada ya Leo. |
2Wathesolonike 2:6-7 imeandikwa, “Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate
kufunuliwa wakati wake. 7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi;
lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.”
wazuiaji hawa wapo hata sasa wanafanya
kazi, na kazi yao ni kuharibu masomo, kazi, mafanikio watu hawa wapo lakini
uwezo wa kumwondoa tunao na tutamwondoa kwa jina la Yesu. 1wathesolonike 2:18 imeandikwa, “Kwa
hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na
Shetani akatuzuia.” Huyu ni Paulo ambaye ameandika karibu nusu ya
vitabu vya agano jipya lakini Paulo huyo anasema shetani amemzuia, sasa mimi na
wewe hapo je tupo salama, lazima tuombe na kuondoa vizuizi vyote kwa jina la
Yesu. Biblia inasema hivi, nawapenda wanipendao, lakini wale tu wanao nitafuta
kwa bidii wataniona uso, kama ukimtafuta Yesu kwa bidii Yule anaye kuzuiya
usiolewe, usioe, usisome ataondolewa kwa jina la Yesu. Kuna watu wengi leo wapo kanisani lakini ni wagumu kufanya maamuzi,
hii ni kwa sababu yupo anayepinga na kukuzuia, leo kataa kwa jina la Yesu.
Ukiri: sema leo katika jina la Yesu, ninakataa
kuzuiliwa kwa jina la Yesu, Yule aliye nizuia namwondoa kwenye maisha yangu kwa
jina Yesu, iwe ni mtu, jini, nina mwondoa atoke kwangu kwa jina la YESU AMEEN.
Shetani
hawezi kuja kukuzuia bila mipango, na ndio maana ni lazima ujue kuwa shetani
anao watu anao watumia ambao ni wachawi na waganga mfano utamwona mfalme Ahabu 2 Nyakati 18:19-21 Imeandikwa, “Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya
Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramothgileadi akaanguke? Basi huyu akasema
hivi; na huyu hivi. 20 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi
nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? 21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo
wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki
pia; ondoka, ukafanye hivyo.” Wanao
zuia ni watu ambao ndani yao kuna mashetani amabao kazi yao ni kuzuia jambo
rohoni ama mwilini, una ona pepo huyu aligeuka akawa pepo wa uongo ndani ya
kinywa cha manabii, inawezekana uliacha kazi kwa sababu ya maneno ya mtu, wengine
wana kauli mbaya na wamekutenga, usilo
jua wewe kuna pepo ameingia kwenye kinywa na pepo huyo amefunga na kuzuia
Baraka zako. LEO NAMTANGAZIA AKUACHIE MARA MOJA NA AONDOKE POPOTE ALIPO KAA KWA JINA
LA YESU.
Kuna
wengine wakipanga leo tunaomba gafla usingizi unakuja ujue kuna wazuiaji hapo.
NJIA KUU MBILI AMBAZO SHETANI ANAZUIA MTU
Shetani
anatumia njia zifuatazo kumzuia mtu ;
1: SHETANI ANAWEZA KUZUIA AKIWA NDANI YA MWILI
Sasa
mtu ni nani, mtu ni roho yenye nafsi inayo kaa ndani ya nyumba na nyumba hiyo
ndio inaitwa mwili. Shetani akiwa ndani ya mwili naanza kukutawala, na shetani
asili yake ni mabaya hivyo kila utakalo panga yeye anazuia kutokea ndani. Kumbuka
wewe ni roho na shetani anakumiliki au (demon possession). Ni kama hivi,
unatakiwa uende kwenye usahili mahala fulani saa mbili ila ikifika mda huo
gafla unaanza kuumwa tena sana, hii ni kwasababu Yule wa ndani anayetawala
maisha yako hataki uende kwa sababu anajua hapo kuna Baraka zako. Leo kataa
kutawaliwa na kuzuiliwa kwa jina la Yesu. LEO NAMTANGAZIA YULE MTAWALA ANAYE TAWALA
MAISHA YAKO LEO, NAMFYEKA KWA JINA LA YESU, HATA KUZUIA TENA MILELE YOTE KWA
JINA LA YESU.
UKIRI:
Katika jina la Yesu shetani uliye kaa ndani ya moyo,
kichwa, macho nakung’oa kwa jina la Yesu, mkono wangu huu naugeuza uwe na moto
nakufyeka kwa jina la Yesu, niachie kuanzia leo, achia maisha yangu, ndoa,
yangu, kazi yangu kwa jina la Yesu.
Kadiri
unavyo jitunza kwa utakatifu ndivyo unavyo zidi kufanikiwa. Dhambi inaleta
mauti, ndio maana Bibilia inasema miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu 1Wakorintho 6:16 imeandikwa, “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba
ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.” Unapo fanya dhambi jengo lina haribika leo kataa kuwa mtumwa wa dhambi kwa
jina la Yesu. Utamwona Yuda Luka 22:3-4
imeandikwa, “Shetani akamwingia Yuda,
aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda
akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi
mwao.”
Roho
ikikamatwa, mwili unaanza kuhangaika hangaika unakosa mwelekeo, ndio maana
utaona watu leo wana vaa vimini, mlegezo, hii ni kwa sababubu mwili
unatawaliwa. Jifunze jambo kwamba siku zote vitu vizuri huwa vimefichwa au kusitiriwa.
Hata dhahabu inapatikana chini, Almasi
mpaka ichimbwe chini ya udongo ndo mtu aanze na kupata hela. Sasa kwanini vijana
mnavaa nusu uchi, maana yake ni kwamba mwili una tawaliwa leo kataa kwa jina la
Yesu. Sisi binadamu tumeumbwa kwa namna ya ajabu na kutisha. Hivyo usikubali
kuliharibu hekalu lako kwa namna yeyote ile. Shetani alipo mtoka Yuda
akajinyonga kwa nini alipo gundua amemuuza Yesu akajiua, na mimi naagiza
shetani anaye kutawala akutoke uanze kumiliki na kutawala kwa jina la Yesu.
Kuna mashetani wana mzuia mtu hata usimtolee Bwana mfano, mtu kaja kanisani
akatoa shilingi mia tano lakini mwimbaji akiimba unatoa elfu ishirini unaanza
kujiuliza kumbe alikuwa nayo mbona hajatoa kwa Bwana? Kumbe shida ipo mashetani wana mzuia
asitoe kwa bwana leo kemea kwa jina la Yesu.
2: MASHETANI WANAO ZUIA KUTOKEA NJE YA MWILI
Hii
ni njia ama mbinu nyingine ambayo shetani anaitumia ili kukugandamiza usitoke
hapo na mtu ana kuwa hana mwelekeo, mashetani hawa wana kufuatilia mahali
popote pale unapo kwenda, ndio maana mwingine halipuki mapepo lakini hafanikiwi
anasema mimi sina mapepo kumbe asicho kijua huyu kuna mashetani wana kuzui
kutokea nje ya mwili. Kuna mwingine kaomba kazi hapati ni kwa sababu shetani
ametangulia nje kuzua asipate kazi. Mwingine anataka kuolewa wazazi wamekubali
ila tatizo linatokea kwa ndugu wakagoma shida ni shetani katangulia kule
akazuie, leo fanya ukaguzi wa rohoni na kuwaondoa hawa wazuiaji kwa jina la
Yesu. Mfano utaona Zakaria 3:1 imeandikwa, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa
Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye”. huyu ni kama askofu mkuu mashetani
alishindwa kumwingia lakini wakashindana nae kutokea nje, kuna wengine mambo
hayaendi kumbe nje kuna pepo yupo ana zuia biashara, leo nakataa kutawaliwa
kutokea nje kwa jina la Yesu.
Wageni waliotutembelea kutoka nchini Ujerumani. |
Matendo 13:6-12 imeandikwa, “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu
mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu;7 mtu huyu alikuwa
pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba
na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini Elima, yule
mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule
liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa
Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu
wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana
zilizonyoka? 11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu,
usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na
kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo Yule liwali, alipoyaona
yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.”Huyu
mmoja anatamani kuisikia injili lakini mmoja anazuiya asisikie injili ya Yesu,
kuna mishale inarushwa kutokea nje ili uache jambo Fulani ambalo umelianza ama
unalo kusudiwa kulianza wao wanazuia.
©/ MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T)
CHURCH
MOROGORO CHURCH
|