Pages

Sunday, July 2, 2017

KUMTUPA NJE MKUU WA ULIMWENGU

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI TAREHE 02.07.2017
MHUBIRI: PATOR, GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
  
Mch. Godson Issa Zacharia akifundisha ibada ya leo
Yohana 12: 31 Imeandikwa,“Sasa hukumu ya Ulimwengu huu ipo;sasa mkuu wa Ulimwengu huu  atatupwa nje”  Kutupwa nje maana yake atupwe nje ya shamba, ndoa, kazi, shule, huduma, masomo na biashara pia. Mkuu wa ulimwengu huu anaitwa shetani. Shetani anayo majina mengi. Pengine anaitwa ibilisi, nyoka wa zamani, baba wa uongo, mshitaki wa ndugu,  na majina mengine anaitwa mwizi.  muuaji tangu zamani, mkuu wa pepo- belzebuli. Na pengine ameitwa mkuu wa giza katika ulimwengu wa roho. Pengine ameitwa mwarabu ambaye ndiye mkuu wa uharibifu wote Swali litakuwa ni kwa nini tumtupe wakati hatumwoni? Ijulikane ya kuwa shetani ni roho na anaweza kukaa mahali popote. Unaweza usimwone kwa sababu yeye hukaa katika roho.

 Imeandikwa Ufunuo 2: 13 “Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.”  Shetani huwa anakaa kokote. Anaitwa Mwarabu kwa sababu ya uharibifu. Na akiingia mahali basi ujue uharibu umefika. Shetani huwa anakaa ndani ya watu. Shetani hawezi kufanya kazi isipokuwa amepata mahali pa kukaa. Asipotupwa utamwona wa faida ila kazi zake zimejaa uharibifu.

Ufunuo 12: 7-21 Imeandikwa  “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.


Majeshi ya Bwana Yesu yakimwimbia Mungu.
 Shetani alitupwa katika nchi baada ya vita. Vita hii ilipiganwa kupitia malaika Mikaeli, tena neno linasema ya kuwa  malaika wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo. Neno linasema mbingu ikafurahi baada ya kumtoa shetani kutoka mbinguni ametupwa katika nchi. Tena ilikuwa nguvu kwa sababu shetani na malaika zake wameondolewa na kutupwa nje.

Baada ya shetani kutupwa katika nchi, Mungu alijua hila za ibilisi siku zote huwa ni uharibifu.  Baada ya kuona jambo ili ndio Mungu akatoa matibabu. Silaha ya kumshinda ibilisi ni Damu ya Mwanakondoo. Silaha hii hutumiwa na watakatifu. Ndio maana neno linasema Kuhani Joshua wakati akiwa kazini, shetani alisimama pembeni kumpinga. Kwa hiyo  shetani  aweza kuwa ndani ya mtu au nje ya mtu. Lakini ukiwa na utakatifu, malaika wa Bwana atakulinda dhidi ya mkono wa ibilisi.  

Ufunuo 12: 12 Imeandikwa : Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. Shetani anafanya kazi masaa yote kwa sababu anajua muda wake ni mchache. Asipoweza biashara atahamia kwenye macho, mikono, shule, mashamba au kazi. Shetani na wasaidizi wake wana hasira sana ndio maana wanaweka watu mashimoni. Utaona mtoto aliyekuwa na akili na fahamu nzuri anabadilika ghafla. Badala ya kuwa namba moja anakuwa wa mwisho, mwenye magonjwa ya kila namna. Lazima uamue kuchukua hatua ya kupambana kwa nguvu zote.Mateso haya tunayoyaona kwa watu hayatoki kwa Mungu isipokuwa kwa shetani. Magonjwa ya ajabu Ukimwi, Kisukari na Pressha na taabu zote havitokani na Mungu.

 Maombolezo 31-33 Imeandikwa: Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. 32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. 33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha. Si mapenzi ya Mungu kuona tukiwa na huzuni. Huzuni ya ndoa, kazi, shule, njaa au hali ya uchumi. Haya yanatokana na shetani na mawakala wake waliotupwa nje.


Platform ministry wakiongoza sifa na kuabudu.
Mapepo hawapendi kukaa hewani. Kumbe siku zote wanapenda kukaa ndani ya watu. Ndio maana wakati wa Yesu walipo mwona walisema tuna nini nawe mwana wa Mungu. wakauliza kwanini anataka kuwatoa kabla ya muhula wao. Leo ndio siku au muhula wa kuwatupa nje mashetani waliokaa ndani yako siku zote. Silaha yetu ni kwenda kwa damu ya Yesu maana ndio iletayo ushindi katika maisha yetu. Ukiwapiga

USHAHIDI WA KUWA SHETANI YUPO DUNIANI.
Yohana 14:30 Imeandikwa, “Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.”  Ukikaa vizuri na Yesu, shetani hawezi kufanya chochote kwako. Si mchawi wala mganga atakayeweza kutenda lolote juu yako. Luka 4:1 Imeandikwa, “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, 2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. 3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate.  4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu.  5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.  8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. 9 Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; 10 kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; 11 na ya kwamba, Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 12 Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. 13 Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda.”  Shetani yupo hapa hapa duniani. Hapa alimjaribu Yesu mwana wa Mungu, je wewe? Watu hawaamini lakini yako matukio yanayowapata watu lakini hayatokani na Mungu. Mtu akiombewa leo kesho anavamiwa tena, kwa sababu shetani anapenda kukaa ndani ya mwanadamu.

2 Korintho 4:4 Imeandikwa, “ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.” Mbinu ya shetani ni kupofusha fikra za wanadamu ili wasijue hila zake. Yohana 16:11 Imeandikwa, “kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa”… shetani yupo na alikwisha kuhukumiwa. Makao yake ni kuzimu. U nani wewe usikubaliane na neno la Mungu, kama Yesu anamwita Mungu muovu wa dunia hii, utakataaje kwamba shetani yupo duniani.

Showers of Glory wa morogorogo wakicheza mbele za Mungu.
 Ayubu 1:6-9 Imeandikwa, “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. 7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. 8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. 9 Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure.” Hapa ina maana kabla shetani hajasema kwa Mungu, alikuwa ameishajaribu kuharibu mali za Ayubu ila akashindwa. Kumbe shetani ni roho inayoweza kuyachunguza maisha ya wanadamu na kuwajua kwa undani zaidi. Mali, kazi, biashara, mashamba, mifugo na ustawi wako shetani anajua. Pambana kwa jina na damu ya Yesu ili kumtupa nje ibilisi. Ibilisi akitupwa nje furaha urudi katika maisha ya wanadamu. Utarudishiwa vyote shatani akaiondolewa ndani yako. Ustawi, afya, upendo, maendeleo na kicheko kitasikika tena kama mbingu ilivyoshangilia baada ya shetani kutupwa nje.

Maombi:
Kwa mamlaka ya jina la Yesu namtupa nje adui wa maisha yangu,kila kilichofunga maisha yangu nakitupa nje kwa damu ya mwanakondoo,nakamata roho zote zilizofunga maisha yangu,ndoa yangu,biashara yangu maanikio yangu nazitupa nje kwa jina la Yesu.namkamata mkuu wa ulimwengu aliyeshikilia maisha yangu aliyezuia hatua zangu namtupa nje kwa jina la Yesu.


                                          ========== AMEN ========

KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KIPITIA:

FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG:UfufuonaUzimaMorogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/