Pages

Sunday, July 23, 2017

KUTOROKA KUTOKA KWENYE GEREZA LA KIDIPLOMASIA

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA → MOROGORO}

JUMAPILI: 23 JULY 2017

MHUBIRI:  PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)

Mch. Godson Issa Zacharia akifundisha katika ibada ya leo.
Leo ni siku ya kutoroka kutoka kwenye gereza la kidiplomasia na kwenda kwenye usalamawetu kwa Jina la Yesu. Maana yaKutoroka ni kuondoka bila ruhusa.  Gereza la kidiplomasia ni gereza kama yalivyo maferza mengine.ulimwenguni kote kazi kuu ya gereza ni kumnyima mfungwa uhuru wa kufanya yale anayotaka kufanya. Mfano, ukiwa gerezani muda wa kulalautapangiwa, ratiba ya kula chakula unapangiwa n.k. Kwa kawaida mfungwa huwekwa gerezani kwa sababu ya makosa aliyofanya. Hata hivyo, shetani humtupa mtu gerezani siyo kwa sababu aliiba au kufanya kosa kubwa namna gani la hasha!! Shetani huwaweka watu gerezani kwakosa tu la wao kumufata Yesu.

Upo muda wa mfungwa kukaa gerezani na kutumikia kifungo fulani. Wafungwa wengine hutumikia kifungo kwa mwaka mmoja,miaka miwili,wengine 30 na wengine kifungo cha maisha yao yote. Anayeamua utendewe nini ni mkuu wa gereza, ambaye huitwa Bwana Jela. Gereza tunalozungumzia hapasiyo yale ya kimwili kama lilivyo Ukonga, au Kingulwira au Kilakala-Morogoro. Tunazungumzia gereza la Kiroho na ambalo kismingi hufanya kazi kama yalivyomagereza ya kimwili. Tunaposoma katika ISAYA 14:17, neno laMungu linasema hivi “Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao? ” Tunajifunza kuwa wanadamu wanawezamkufungwa na ibilisi na kuwekwa jela,  na baadae kukosa uhuru wa kuishi maisha ya uhuru.
1.      Ulikuwa zamani unapenda kula vyakula fulani, lakini leo hii ibilisi amekuweka kwenye jela ya kisukari, na sasa unachagua chakula.
2.      Ulikuwa zamani unapenda kusuka nywele lakini leo hii ibilisi amekuletea ugonjwa wakansa na nywele hazioti tena!!

Imeandikwa katika ISAYA 42:22Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.”. Kwa hiyo mtu aingiapo kwenye haya magereza hawezi kuachiliwa tena, hadi pale atakapotokea mtu  wa kusema “Rudisha”.

Kwa kawaida wafungwa wa magereza mengine hupata mateso ya viboko na chakula cha shida magerezani. Gereza la Kidiplomasia (Diplomatic prison) ni gereza la tofauti kidogo na pengine ni maalumu. Gereza la Kidiplomasia ni gereza la starehe. Mtu anakuwa amefungwa lakini bado zile anasa za kidunia mtu huyo anaendelea nazo. Ni kifungo kwa watu walioheshimika sana. Chumba cha gereza hili kina vitu vyote muhimu kama vile godoro, TV, AC, simu, chakula cha starehe n.k. Hata walinzi wanaolinda wafungwa wa kidiplomasia ni walinzi maalumu.  Pamoja na starehe zake, mfungwa wa kidiplomasia anakosa ule uhuru wa kufanya baadhi ya mambo aliyotaka kuyafanya binafsi. Mbaya zaidi, mfungwa wa kidiplomasia huwa hajitambui kuwa yupo gerezani. Mara zote mtu anayesababisha wewe kufungwa katika gereza la aina hii anakuwa ni ndugu  au  jamaa wa  karibu.

Majeshi ya Ufufuo na Uzima Morogoro wakisikiliza mafundisho ya leo.
Mtu anaweza kuwa na mali na kila anasa anayoitaka. Watu wa aina hii wanatumia hela hiyo hiyo kuwafanya wawe walevi, au waasherati, kuwa na nyumba ndogo mitaani, kuambukizwa maradhi yasiyotibika, kuwa watumiaji dawa za kulevya n.k.  Wewe uonapo watu wa aina hii ufahamu kuwa ni watu waliopo katika magereza ya kidiplomasia.

Tunasoma katika UFUNUO 2:10Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”. Kwanza tujue kuwa kuna kifungo, anayeweka watu gerezani ni ibilisi, mateso yatakuwepo  uwapo gerezani, nnekuna muda wa siku kumi kukaa gerezani na tano atakayevumilia hadi mwishjo atapata taji ya uzima. Kumbe upo muda fulani ambao mtu anaweza kuwepo katika gereza la kidiplomasia, na ni pale tu mtu atakapovumilia hadi mwisho atakuja kupewa taji.

UKIRI
Ewe ibilisi uliyejipanga kuniwekea kifungo cha kidiplomasia kwa muda maalumu leo na kushambulia kwa Jina la Yesu. Mimi leo ninatoroka kwenye gereza hilo kwa Jina la Yesu. Amen

Kwa kawaida Mungu wetu anakuwa amekusudia mambo mazuri sana katika maisha ya watu mbalimbali.
1.      Mathalani ulikuwa binti mzuri, na Mungu alikusudia uolewe na upate watoto watakaokuwa mawaziri, wabunge, majaji, Wakurugenzi au Katibu Mkuu wa baadae. Hata hivyo, katika kipindi kile cha umri wa miaka 18-35 binti huyu akaringia kila kijana aliyekuja kwake akitaka kumuoa. Maana yeke ni kuwa shetani alikuweka katika gereza la kidiplomasia, na sasa hawapo vijana wanaokufuata tena wakitaka kukuoa. Miaka imepita na sasa umri wako ni miaka 40 muda wa kukaa katika gereza la kidiplomasia umeisha na wanaotaka kukuposa ndiyo wameanza kukujia tena. Ni kweli  kuwa utaolewa lakini hautafaidi  matunda ya uzao wako, hata kama utazaa watoto mawaziri wa baadae kwa sababu upo  nje ya muda wa Mungu wa baraka zako.

2.      Mfano mwingine ni pale ambapo mtu anaitwa kwa ajili ya usaili wa kazi fulani lakini siku moja kabla ya usaili huo anavitafuta vyeti vyake na havipati, mtu huyu anakuwa amefungwa katika gereza la kidiplomasia. Baada ya siku ile ya usaili, mfungwa huyu anavikuta vyeti vyake vikiwa sehemu ya wazi kabisa, viko chini ya Biblia na kumshangaza mbona hakuviona? Uonapo mtu wa aina hii jua walikuwepo walinzi wa gereza la kidiplomasia ili mtu uyo asipewe kazi iyo na hatimaye kufanikiwa. Na ukimwona mtu asiyejua kabisa kusoma au kuandika wala usimlaumu kwa sababu ni mashetani yalitumika kumfunga katika gereza la kidiplomasia. Na mtu fungwa kwa sababu ya ile hatima iliyo ndani yake.

Platform ministry wakiongoza sifa na kuabudu katika ibada ya leo
Imeandikwa katika YEREMIA 1:4-6Neno la Bwana lilinijia, kusema, 5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. 6 Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni motto”. Mungu anatuhakikishia kuwa alitujua kabla ya kutuumba katika matumbo ya mama zetu. Tena Mungu alitutakasa hata kabla ya kututoa ndani ya matumbo ya mama zetu. Ni sawa na kusema, Mungu alituwekea UHESHIMIWA ndani yetu kabla ya kutuumba. Yeremia katika utoto wake alitaka kukataa lakiniMungu akamsisitiza kuwa. Kumbe watu wengi ni waheshimiwa lakini hawatambui hilo. Ndiyo maana Mungu anasema katika ISAYA 43:4Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako”. Kumbe Mungu anatutambua sisi kama waheshimiwa, na zaidi sana Mungu ametupenda.

Lipo jambo la ajabu sana na halivumiliki ambalo mtunzi wa Kitabu cha Mhubiri aliliona kwamacho yake likifanyika duniani. Katika MHUBIRI 10:5-7 imeandikwa “Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; 6 ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. 7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa”. Tunajifunza kuwa wapo watu wasiostahili kabisa lakini ndiyo wanaendesha magari ya kifahari, na wapo watu waliookoka, wenye kuheshimiwa na Mungu lakini wanatembea kwa miguu mabarabarani!!!! Wewe uliyeokoka unakaa nyumba ya kupanga tena isiyo na umeme na wale wasiostahili wanakaa kwenye nyumba za kifahari!!! Leo hii tukatae kuishi katika magereza ya kidiplomasia kwa Jina la Yesu.

Katika ZABURI 8:4-8 neno la Mungu linasema hivi “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. 7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini”. Yawezekana wewe unajiona ni mtumwa, kwa kuwa bado unatembea kwa miguu. Kumbe tunajifunza kuwa Mungu huwa anawaangalia wanadamu. Mtunga Zaburi anasema “Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu” kumaanisha kuwa Mungu amemfanya Mwanadamu kuwa kidogo sawa naye, na ndiyo maana “tukitamka mambo kwa vinywa vyetu lazima mambo hayo yatokee”. Wewe siyo mtu wa kawaida. Kutokujua kwako ndiyo kunamfanya ibilisi akuweke kwenye magereza ya kidiplomasia. Leo lazima tutoroke kwenye magereza ya biashara, miradi, elimu, ndoa n.k. Katika Biblia,  Danieli alikuwa hana kosa lolote lenye  kuweza kumfanya afungwe gereza la kidiplomasia. Maadui zake walipokosa sababu ya kumfunga, wakatafuta namna ya kumshitaki kwa habari za Mungu wake na ndipo akatupwa kwenye gereza lenye samba wakali.

Majeshi ya Yesu, yakimfungua mtu kutoka katika gereza.
Leo tutatoroka kutoka kwenye magereza yote ya kidiplomasia ambayo shetani alituweka. Ili kufanya haya, lazima apatikane  mtu wa kukusaidia ili  utoroke. ISAYA 42:6-7Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; 7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa”. Leo lazima tuhame kutoka vifungo hivi vya  kidilomasia kwa Jina la Yesu.

Mfungwa yeyote anapotaka kutoroka hapaswi kuomba ruhusa au kumuaga mtu yeyote. Ni muda wa mfungwa kuchungulia walinzi wa gereza walivyokaa na kuwaruka walinzi hawa bila wao kufahamu. Jambo la muhimu la kufanya ni kumpa Yesu Kristo maisha yako (kwa maana ya kukubali kuokoka). Baada ya leo kumpa Yesu maisha yako kila neno utakalotamka kwa kinywa chako litatokea vilevile kwa Jina la Yesu.

========== AMEN ========


KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)

BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/