Pages

Sunday, July 16, 2017

NDOA ZA KIROHO ZA KISHETANI (Sehemu ya 5)


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA → MOROGORO}

JUMAPILI: 16 JULY 2017

MHUBIRI:  PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)

Mch. Godson Issa Zacharia akifundisha katika ibada ya leo.
Kuanzia Jumapili iliyopita, tumekuwa tukichambua dalili, vyanzo na sababu mbalimbali za kuwepo kwa ndoa za kiroho za kishetani.  Yapo madhara mabalimbali yawapatayo watu walioingia katika ndoa hizi ikiwemo. Leo tena tutamalizia somo hili kwa upana zaidi na hakika Bwana Yesu atakuweka huru kwa Jina la Yesu.

Kwa nini tunazungumzia uwepo wa hizi ndoa za kiroho za kishetani? Hii ni kwa sababu, tunaposoma katika MWANZO 6:1-4, Biblia inasema hivi (Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 Nao Wanefili (Wanefili maana yake ni majitu) walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.). Tunaona katikamaandiko haya uwepo wa watu wa aina mbili: Wana wa Mungu (ambao ni  malaika) na binti za wanadamu (ni mabinti kweli wa wanadamu kama sisi). Biblia inasema wana wa  makundi  haya mawili waliingiliana (kwa maana ya kujamiiana), na hivyo walizaa watoto ambao ni mchanganyiko wa mbegu za kibinadamu na  malaika (majini) ambao walikuwa hodari sana, wakaitwa wanefili.  


Pia tunasoma katika EZRA 9:2 (Maana wametwaa binti zao kuwa wake zao, na wake za watoto wao; basi mbegu takatifu wamejichanganya na watu wa nchi hizi; naam, mkono wa wakuu na mashehe umetangulia katika kosa hili.). Mungu ameliona hili jambo  kuwa ni  kosa,na ndiyo maana katika Mwanzo 6 Mungu alisema roho yake haiwezi  kushindana  na mwanadamu. Malaikawapo  wa aina  mbili: Malaika  watakatifu  (hawa ndiyo tunaowatumia) na Malaika wachafu (hawa ndiyo  waharibifu, wanaoingiliawatu kuwaletea magonjwa, umaskini n.k). Ndiyo maana katika YUDA 1:9 imeandikwa hivi (Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu. 7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.) Kundi  hili la malaika waasi walitaka kumpindua Mungu katika kiti chake cha enzi. Malaika hawa walifuata uasherati kwajinsi moja kama vile Sodoma na Gomora, wakijichanganya kwa kufanya mambo yasiyo ya asili (sodomization).


Inawezekana hata wewe kwa kujua au kutokujua umeunganishwa na ndoa za aina hii, kati ya wanadamu na malaika waasi (majini). Leo tutaiangalia milango inayo ruhusu mume au mke wa kiroho na kufunga ndoa za aina hii na kisha tutaifunga yote kwa Jina la Yesu Kristo.



Majeshi ya ufufuo na Uzima Morogoro wakisililiza somo la leo

MILANGO INAYORUHUSU MUME AU MKE WA KIROHO KUINGIA NA KUFUNGA NDOA ZA KIROHO ZA KISHETANI.

1.      Ulinzi wa Kichawi:

Hii hutokea tu endapo mtu aliwahi kwenda kwa waganga wa kienyeji kuomba ulinzi wa kumfunga mwenza wake au mchumba wake ili asimkimbie. Ndoa hailindwi kwa madawa bali kwa Jina la Yesu Kristo. Mtu huyu hupewa masharti magumu sana na waganga wa aina hii, pengine kumwagiwa maji ya maiti au hata kuamriwa kuvua nguo zote na kulala nao. Kupitia madawa haya, mume au mke wa kiroho hupatikana. Mwisho wa watu kama hawa ni kukosa furaha, ndoa kuvunjika na ugomvi wa kila mara kutokea.

2.      Damu ya Hedhi

Hii ni ile damu ya kila mwezi kwa akina mama. Damu hizi zinapaswa kutupwa kwa  uangalifu  sana, hivyo ni vyema damu hizi zihifadhiwe kwa umakini  sana ili  zisifikie mikono ya wachawi au  waganga wa kienyeji. Biblia inatukataza ”usile nyama na damu yake kwa sababu katika damu kuna uhai”. Kupitia damu za hedhi, wanawake wengi wamejikuta wakifungwa kutozaa watoto baada ya waganga wa kienyeji kuzitumia damun hizi kuwaloga. Damu hizi ni muhimu sana kwa sababu zinahusisha mambo ya uzazi (idadi ya watoto na taarifa zinginezo za ndoa). Endapo damu hii ikifika mikonoi mwa waganga wa kienyeji, uchumba utaharibika, maumivu ya tumbo la uzazi, ndoa kuvunjika, damu kutoonekana kwa miezi kadhaa kwa mtu asiye mjamzito n.k. Dalili nyingine ni mume wa mwanamke aliyefungwa kupitia alama hii kuwa na mahusiano nje ya ndoa (michepuko).




UKIRI
Kwa Jina la Yesu, Ninamfukuza jini aliyeingilia ndoa kwa njia ya Damu ya Hedhi. Ewe shetani ninakufukuza kwa Jina la Yesu. Ewe shetani uliyenifunga kwenye ndoa ya kiroho nakufyeka  kwa Jina la Yesu. Amen 


3.      Uvaaji wa Nguo Mbaya za Kimahaba

Njia hii humfanya mtu aliyevaa nguo kuonekana amevaa lakini viungo vyote vya mwili na sehemu za siri zinakuwa zinaonekana. Uvaaji wa nguo za aina hii huyafanya majini yamgundue haraka kuwa wewe ni mwenzao.  Kwa njia hii, mashetani haya hupata upenyo wa kumuingilia mtu anayevaa mavazi ya aina hii. Kwa wanaume ni pale mtu anavaa shati kwa kuachakifua wazi au kama ni wanawake ni wale wavaao nguo fupi sana au zinazoonesha maumbile yake.

4.      Ngoma za Asili

Hizi ni ngoma za asili zinazochezwa na baadhi ya makabila (kama vile Waluguru). Aina ya ngoma hizi ni VIGODORO na MDUNDIKO. Uchezaji wa ngoma hizi huambatana na uchezaji usio na staha, wakati mwingine uchezaji-nusu uchi. Mashetatni hupata nafasi kuwaingia wafuasi wa hizi ngoma na kuoana nao. Ngoma nyingine ni ile ya CHAKULAGA (kwa Wasukuma) ambayo huchezwa na watu kuchaguana wakati wa uchezaji. Majini nayo hujipatia watu wa kuwachagua na kufunga naao ndoa za kishetani.  


Showers of glory wakicheza mbele za Mungu


5.      Mlango kupitia Uzinzi au Ukahaba au Uasherati

Imeandikwa katika 1WAKORINTHO 6:15 (Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!). Unapofanya ukahaba unajiungamanisha na mtu usiyemjua, na hatimaye mashetani kjukutamia wewe kama mume aumke wa ndotoni.

6.      Mlango kupitia Mbegu za Uzazi za Kiume

Kwa mtu ambaye hujaoa au hujaolewa, na kutenda tendo la ndoa (uasherati) au kama umeoa na una mke na kufanya tendo la ndoa nje ya mke wako (uzinzi), unakuwa umejichimbia kaburi lako mwenyewe. Biblia inasema ikimbieni zinaa. Imeandikwa katika 1WAKORINTHO 6:15-16 (Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!16 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.) Mara nyingi mashetani yanakuwa yanakusanya mbegu hizi nakwenda nazo baharini ili kuzalisha watoto wa kijini. Wengi wetu tuliwahi kusikia habari za uwepo wa mashetani yakiitwa POPO-BAWA ambayo huwaingilia watu usiku na kutoa sharti la mtu aliyeingiliwa kujitangaza rasmi kwamba umeshaingiliwala sivyo yaendelee kukujia usiku.


Kama ambavyo damu ya hedhi inatumika na mashetani, vivyo hivyo mbegu za kiume ni njia ya kumuunganisha mwanaume na majini, na kumfanya aolewe na wanawake wa kijini. Yapo maeneo ambayo ni hatari, yanatumika kwa shughuli za ukahaba. Hata mahotelini pia uvaajji wa nguozakikahaba upo  na lengo ni kuwavuta wateja wa ukahaba na wakeshalala pamoja mbegu hizi hukusanywa na mashetani  na kuolewa  na majini.


MADHARA YANAYOMPATA MTU MWANAUME WA AINA HII NI: 

·        Mambo ya kifedha huharibika ghafla (miradi kufa, biashaara kuyumba)

·        Kukosa hamu ya tendo la ndoa na mke wake wa ndoa.

·        Mwanaume kuchanganyikiwa kila anapomuona mwanamke au binti amekatisha mbele yake.

·        Mwanaume anakuwa hapati ujauzito kwa sababu mwanaume anakuwa hana mbegu za kutosha (low sperm count) baada ya mashetani kuzigema na kuzipeleka baharini.


7.      Kuirithi Mikoba ya Ukoo

Katika Bara la Afrika, zaidi ya miaka 100iliyopita wengi wa wazee wetu walikuwa siyo Wakristo. Kuna wabibi huwaita wajukuu zao wakiume kuwa ni wachumba zao. Au kuna wababu au wanaume watu wazima katika ukoo huwaita binti wadogo kuwa ni wachumba zao. Maneno kama haya huumbika katika ulimwengu wa roho.


SHETANI HUWEZAJE KUMUINGIA MTU?

Kama tulivyosoma katika MWANZO 6:1-3, zipo alama ambazo mashetani humwekea mtu mwilini au rohoni na kuwezakumuingia mtu. Katika kitabu cha MWANZO, Mungu alimwekea alama Kaini ili watu watakaomuona wasimdhuru. Kwa hiyo zipoalama zakuwafanya mashetani wamuingilie mtu:

Platform ministry wakiongoza sifa na kuabudu.

Imeandikwa katika UFUNUO 3:16-18 (Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.) Hizi ni alama za kimwili kabisa ambazo mpinga Kristo anaweza kumwekea mtu.

1.      Alama katika Paji la Uso

Alama hii huweza kuwa ya kuonekana au kutoonekana. Majini huwa rahisi kuiona alamahii wanayomwekea mtu.  Wakati mwingine hata katika magariau daladala, unaweza kuziona alama au maandishi yaliyowekwa ndani mle kumbe ni alama inayotumiwa na majini kuwasiliana.


2.      Alama katika Viungo vya Uzazi

Kwa wanawake, alama za aina hii huwekwa kifuani karibu na maziwa, au katika magotini, au chale shingoni n.k. Pengine mtu anakuwa anajua au hajui. Majini humuingia mtu  kwa sababu wanapoiona hiyo alama inakuwa rahisi kukutambua.


UKIRI
Ewe jinni unayenimiliki, niachie kwa Jina la Yesu Kristo. Hizo alama futikaleo kwa Jina la Yesu. Ewe jinni unayeingia ndani yangu kwa sababu ya alama leo naifuta kwa Jina la Yesu. Amen


3.      Alama kwenye Miguu

Shida hii huwapata sana wanawake kwa sababu miguu yao huwa wazi na kuonekana. Baadhi ya akinamama huvaa chain wakidhani ni fasheni kumbe tayari wanakuwa wamemilikiwa.  Chain hii huvaliwa zaidi mguu wa kushoto. Kuna wanawake wengine huvaa pete miguuni wakidhani ni urembo lakini kumbe ni alama za kishetani za kumfutailia. Mtu wa aina hii atakapotembea popote majini husema ni mtu wao, na nyakati za usiku majini haya humuingilia mtu huyu kimapenzi.


4.      Alama inayowekwa kwenye kiuno

Kuna wanawake wanaofundishwa namna ya uvaaji wa shanga kiunoni kwa matumizi ya unyumba. Mashetani humuingilia mwanamke wa aina hii kwa sababu ya kuiona hiyo alama kiunuoni.  Kwanza jiulize swali: Kwa nini shanga hizi hutengenezwa na jamii ya aina moja? Wale wale wanaotengeneza shanga hizi ni wale wale wanaouza dawa za kuongeza nguvu za kiume.

5.      Alama ya vazi la Hijabu

Alama hii ya Hijabu hata kuanzia utotoni kwa wenye utamaduni huu huanza kuvaliwa na kuyafanya mashetani yapate upenyo wa kumuingilia huyu mttoot na kukaa naye hadi ukubwani mwake.  


KWA NINI MTU UWEKEWE ALAMA HIZI?

Shetani huziweka hizi alama ili kazi yake iwe rahisi. Biblia inaasema katika WARUMI 12:2 (Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu). Kwa hiyo hatupaswi kufuatisha kila kitu kinachofanywa na watu wa dunia hii. Zipo taratibu za dunia hii ambazo ukizifuatisha utajikuta unapata madhara.


UKIRI
Kwa Jina laYesu, kama Damu yangu imechukuliwa kwa mimi kukubaliana na waganga wa kienyejji, leo nayakataa makubaliano. Alama ya damu kwenye vidole vangu, alama ya damu usoni mwangu, leo nazifuta kwa Jina la Yesu. Amen


Ili  kuwa salama,  yapo mambo mawili  ya kufanya: Jambo la kwanza ni kumpa Yesu maisha yako (kwa maana ya kukubali kuokoka), pili ni kufanya maombi ya kujifungua viungo vyako vilivyowekewa alama na tatu ni kutoa talaka na kuachana na hizo  ndoa za kiroho  za kishetani na mwisho ni kuifunga milango yote iliyoruhuhsu wewe kuingiliwa kirahisi.


========== AMEN ========

KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:

FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia

Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson

Follow us on YOUTUBE: pastor:dr.godson

TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)

BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/