Pages

Sunday, August 13, 2017

SOMO: NGUVU YA KURUDISHA - Siku ya 3

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (G.C.T.C)
                 {KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ­- MOROGORO}
                              
                              JUMANNE: 08 AUGUST 2017 

(Semina Siku ya 3)


MHUBIRI:  PASTOR GODFREY MWAKYUSA (SNP-SHINYANGA) 


Isaya 26:19
19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Isaya anasema ilishatabiriwa kwamba ardhi itawatoa wale wote waliokufa.
Hosea 6:2
2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.
Mungu tunayemtumikia ni Mungu wa kufufua,yani ile mizigo yote iliyofichwa kwake inafichuliwa,wachawi wanapotaka kumchukua mtu kwanza wanatuma mashetani ili wamvune mtu huyo,na ndo maana
Waefeso 6:12
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Inasema ni lazima tushindane katika ulimwengu wa roho,aliyepoteza kazi lazima inarudi,aliyepoteza ndugu yake lazima arudishwe ,asiyekua na ndoa lazima apate ndoa ,kama wao walivyotuma mashetani na sisi leo tunawatuma malaika watasafiri kwenda milimani kuwaleta wale wote waliochukuliwa na watawarudisha tena.
Danieli 6:10-11
10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
11 Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danieli akiomba dua, na kusihi mbele za Mungu wake.
Mungu alimsikia Danieli na ndo maana alimtuma malaika na kumwambia nenda ukamwambie Danieli tangu siku ya kwanda alipoanza kuomba niliyasikia maombi yako,na leo Bwana anaongea na wewe ya kwamba tangu siku ile ya kwanza tulipoanza semina Bwana aliyasikia maombi yako,kumbe tuna uwezo wa kuwatumia malaika
Waamuzi 6:11-12
11 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.
Hapa tunaona jinsi ambavyo malaika alimtokea Gidioni baada ya kuona amepata hofu,akamwambia Gidioni wewe ni shujaa,na Bwana leo anakutangazia tena wewe ni shujaa,simama na uende wale adui zako waliokutesa miaka mingi utawapata na kuwaangamiza kabisa.
Luka 2:9-10
9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. 10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
Hawa ni watu ambao walikua wanalia baada ya Yesu kuondoka ,lakini malaika walikuja kuwaletea taarifa njema,kumbe tunapoona mambo yetu hayaeleweki tunaweza kuwatuma malaika waende wakapeleke habari njema.
Luka 1:11
11 Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.
Tunaona jinsi ambavyo malaika wa Bwana alimtokea Zakaria na kumpa habari njema ya kumpata mtoto Yohana,jioni ya leo kila aliyepoteza kazi ,aliyepoteza ndoa malaika wa Bwana asimame tena ili vyote vilivyopotea virudi kwa jina la Yesu,mtu wa Mungu unaposema jambo linaumbika ,linakua vile vile maana sisi tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.
Mathayo 28:1-4
1 Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
2 Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.
3 Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.
4 Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu.
Malaika wa Bwana alitumwa aende akaliondoe jiwe,na sisi leo tunawatuma malaika wakaliondoe jiwe,jiwe la mateso ,jiwe la magonjwa leo lazima liondoke kwa jina la Yesu,ingawa walichochea magonjwa,walikuletea huzuni,taabu, wale wale watakuja kwako kwa aibu na Yesu anakuinua tena,kuna watu walikucheka,walikudharau lakini Yesu amekununua tena kwa damu yake ya thamani.
UKIRI:
Katika jina la Yesu nawatuma malaika nenda mashimoni,anza kukusanya mali zangu, leta ndoa ,leta kazi,leta afya yangu,leta nyota yangu.leo ninatembea katika ulimwengu wa roho ninawakamata wachawi wote mlionitaabisha ninawakalia kwa jina Yesu. Kuanzia sasa chochote nilichopoteza kwenye maisha yangu nakiamuru njooo kwa jina la Yesu.