Pages

Sunday, August 13, 2017

NGUVU YA KURUDISHA - Siku ya 2

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (G.C.T.C)
                 {KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ­- MOROGORO}
                              
                              JUMATATU: 07 AUGUST 2017

MHUBIRI:  PASTOR GODFREY MWAKYUSA (SNP-SHINYANGA) 



Mathayo 10:5-8 (Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. 6 Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. 7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. 8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure).

Kondoo ni nani? Ni mimi na wewe tuliyopetea. Kuna kondoo waliotakiwa kuwa kanisani leo ila wamepotea, wanateswa mahali, wanabeba zege, wanafanya biashara. Kuna maduka ya kichawi yanayouza bidhaa za kichawi. Na bidhaa zao ni za kutengeneza.

Ufalme wa mbinguni ukikaria wagonjwa wanapona, wafu wanafufuka, wakoma wanatakasika, mapepo wanatoka kwa jina la Yesu. Tunaposema unafufua wafu,wachawi hawapendi kuona watu wanafufuka.

Luka 24:49
Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Leo unapokea uwezo utokao juu, kuwarudisha waliochukuliwa,ukipokea uwezo huitaji kutabiriwa, au uende kwa mtume na nabii, ni wewe mwenyewe unaingia kwanye shamba la kurudisha, shamba la kukata mapori na kurudisha, ukisema njoo wanakuja kwa jina la Yesu.
Kama una ndugu yako amekufa na anakutokea , utakapomwona sema katika jina la Yesu, nakugandisha hapo hapo, na nakurudisha kwenye umbo lako la mwili wako na tuongee.
Imeandikwa katika Waefeso 3:20
20 Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Imeandikwa katika,Matendo ya mitume, 1:8
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Ukisoma katika Yohana 14:12
14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.
Imeandikwa katika Luka 9:1
9 kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.
Tunapotaka kurudisha, ni kwamba ufalme wa giza nao una nguvu,na kwenye ulimwengu wa roho tunaposema njoo, wanahoji ni nani anayeita? Ana uwezo gani,ana jeshi gani, ni askari wa cheo gani? Mgambo, koplo au ni nani?. Wanaangalia, na ndio maana wengine wanapata matatizo makubwa, mashambulizi.
Ukiri
Baba katika jina la Yesu, leo mtu yeyote aliyeshikiliwa, njooo, katika jina la Yesu.