GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
UFUFUO
NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI
TAREHE 15.10.2017.
MHUBIRI:
MCHUNGAJI. STEVEN NAMPUNJU (Rp)
Mchungaji Mwandamizi akihubiri katika ibada ya leo. |
Mlango ni sehemu iliyoachwa
wazi ili kuingia, au kupitishia vitu kuingiza ndani. Ni kizuizi ambacho
kinazuia vilivyoko ndani visitoke nje bila utaratibu.Mathayo 16:18 Imeandikwa, “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu
ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda”.
Hizi ni habari za mtume Petro, alijibu jibu ambalo lilimshangaza Yesu. Yesu akasema
ni roho amekufunulia haya. Ndipo Yesu akasema juu yako nitalijenga kanisa wala
malango ya kuzimu hayatakushinda. Kumbe kuna milango ya kuzimu.Kwa kawaida
katika maisha yetu tunajenga kuta au uzio na kuweka mlango wa kuingia na
kutokea
Ufunuo 21:9 Imeandikwa, “Akaja
mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo
saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule
Bibiarusi, mke wa MwanaKondoo”. Yohana aliuona mji wenye milango mitatu
kila upande. Hii inatufundisha kuwa hata mbingu ina majina.Ezekieli 48:31 Imeandikwa, “na malango ya mji yatatajwa kwa majina ya
kabila za Israeli, malango matatu upande wa kaskazini; lango la Reubeni, moja;
lango la Yuda, moja; na lango la Lawi”. hata wana wa Israeli walikuwa
na malango. Kabila kumi na mbili za Waisraeli walikuwa na mlango wao.
MJI
WA SODOMA NA GOMORA
Mwanzo 19:1-10 Imeandikwa, “Basi,
wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa
Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. Akasema,
Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale,
mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema,
Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. Akawasihi sana, nao wakaja,
wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa
nao wakala. Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka
nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. Wakamwita Lutu,
wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate
kuwajua. Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.
Akasema, Basi,
nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. Tazama, ninao binti wawili ambao
hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema
machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari
yangu. Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu
kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe
vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje
mlango. Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani,
wakaufunga mlango. Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo
kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango”.
Makutano ya Ufufuo na Uzima wakisikiliza kwa makini katika ibada ya leo. |
MJI
WA YERIKO.
Yoshua 6:1 Imeandikwa, “Basi
Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu
aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia”. Mji huu ulifungwa milango yake
kwa ajili ya wana wa Israeli. Mji huu ulifungwa kwa sababu ya historia juu ya
maisha ya wana wa Israeli. Waliogopa habari za miujiza na maajabu ambayo Mungu
aliwatendea watu wake. Yoshua 5: 1
Imeandikwa, “Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng'ambo ya Yordani pande za
magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari,
waliposikia jinsi Bwana alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa
Israeli, hata tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo
roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli”.
Mji wa Yeriko ulifungwa baada ya kusikia
taarifa za ukuu wa Mungu. Watu wa nchi hii walijua kuwa wana wa Israeli
walikuwa ni hatari tupu. Hata sasa songa mbele maana wanaokuzuia na kukufungia
milango ya Baraka ni kwa sababu wamejua wewe ni hatari tupu. Kuna mahali
umekosa kazi, umekataliwa, umetukanwa na kunyimwa ruhusa kuingia ofisi Fulani,
si kwamba huna sifa bali adui amekujua kwamba ukipata wewe ni hatari tupu
kwenye ufalme wa shetani. Amua leo kuchukua hatua uvunje malango yote ya
ibilisi na walinzi wake, nawe utamiliki Baraka zako.
Wenyeji wa Mji walisikia
kwamba Mungu wa Israeli alivyowatendea wana wa Israeli. Wakajua jinsi Mungu
alivyowapa Maana kule jangwani, jinsi alivyowapa maji matamu katikati ya jangwa
na hata habari za miujiza ile ya kuigawanya bahari. Hata leo lipo neno la Mungu
ambalo ndio fimbo yetu. Waliposikia miujiza hii wakawekwa walinzi ili kulinda
malango ili wana wa Israeli wasiingie. Kwenye maisha haya tuna safari kutoka
hatua moja kwenda hatua nyingine. Wanadamu wanapoona mtu anabarikiwa wanaanza
kuona wivu. Kwa kawaida wachawi wakikuona wivu huchukua hatua ya kuanza
kukuzuia usifike kwenye hatima yako. Silaha yao ni kufunga milango ambayo
ungepita na kuifikia hatima yako. Shetani anatumia kizuizi cha muda au cha
milele kuzuia. Leo lazima uamue kung’oa malango ya uovu ili umiliki Baraka zako.
Platform Ministry wakiongoza sifa na kuabudu. |
Zaburi
24:1-10 Imeandikwa, “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na
juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo
mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea
baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha
wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi
malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni
nani Mfalme wa utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari, Bwana hodari wa vita.
Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele,
Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Bwana wa
majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu”.
Malango yaweza kuwa kizuizi
cha kielimu, kazi, biashara, Kiuchumi na familia. Malango haya haya yana wekwa
kwa namna ya kutokuwa tayari kuondoka. Haya ndiyo malango ya milele ambayo
tumepewa mamlaka kuyaondoa leo kwa jina la Yesu. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao
Bwana na Mungu wa Yakobo. Kwa kuwa unamtafuta Bwana naye atakupa nguvu ya
kuyainua malango ya milele. Waliokuzuia wote watakimbia kwa jina la Yesu. Ewe umtafutaye
Bwana unayo mamlaka ya kuyainua malango. Jifunze jambo kwamba KUINUKA NI ISHARA
YA KUONDOKA.
Malango haya ni mashetani
yanayoweza kuhoji. Shetani na mawakala wake hawaondoki kwa kuombwa ila kwa amri
kutoka kinywani mwa wale wamtafutao Bwana. Maana Bwana wa utukufu akiingia
shetani hawezi kukaa. Bwana wa Utukufu ndiye Mfalme wa Utukufu. Nenda kwa neno
la Bwana ukalikabili lango na kulibomoa kwa jina la Yesu. Lazima uyaondoe
malango yaliyoko mbele yako ili Baraka zako ziwe dhahiri. Kama malango
hayajatoka basi kuna mambo hutoyapata.
KWA
MSAADA ZAIDII NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK:
Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM:
pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL:
+255 719 798 778
(WhatsAssp
& SMS only)
BLOG:
Ufufuo na Uzima Morogorohttp://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/