Pages

Sunday, October 8, 2017

KUMWONDOA ALIYE SIMAMA KUKUZUIA

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH, (GCTC)

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO

JUMAPILI: 08 OCT, 2017
  
MHUBIRI: MCHUNGAJI Dr. GODSON ISSA ZACHARIA, (SNP).

Mchungaji Dr. Godson Issa Zacharia
Kuna mtu au kiumbe ambacho kipo duniani ama katika ulimwengu wa mwili ama rohoni amesimama kukuzuia kwa lengo Fulani, kiumbe huyu anaweza kuwa binadamu au shetani anaweza kukuzuia katika jambo Fulani. Sasa viumbe hawa wanazuia nini basi, wanazuia elimu yako usisome, wanazuia ndoa, wapo walio inuka na kusimama ili wazuie usizae watoto, wengine walitakiwa wasafiri lakini hawaja safiri wamezuiliwa ama katika ulimwengu wa roho ama katika ulimwengu wa mwili.

Watu au viumbe wanajua kuwa kuna mahali unaenda kwenye Baraka zako, lakini wazuiaji hawa wanajua wana zuia ili usifanikiwe, ukipata hela kwa ajili ya ujenzi matatizo yaanza magonjwa ama misiba, ukiona hivyo ujue yupo azuiaye leo namwondoa aondoke kwako na kwenye familia yako kwa jina laYesu. Wazuiaji hawa hawakai ila wamesimama ili waone vizuri ili wakuzuiye, lakini neno linasema Yeremia 1:5 imeandikwa, “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” Mungu alikujua tangu mda lakini leo haupo hivyo kama Bwana alivyo kujua lakini mimi nasema  utafanikiwa kama neno linavyo sema kwa jina la Yesu.

Kuna mama mmoja namjua miaka mingi kidogo iliyo pita lilimpata jambo la ajabu kidogo, mama huyu alifanya kazi miaka ishirini katika ofisi Fulani bila kupandishiwa mshahara wala kupanda cheo, siku moja mama huyu alikuja kanisani kwa huduma ya maombi na kuombewa, siku ya pili yake akaenda ofisini kama kawaida yake, alipo fika ofisini akaanza kufanya usafi katika ofisi ya bosi wake jambo la ajabu katika droo ya bosi wake akakuta vijeneza viwili kimoja chake na kimoja cha dereva wake na majeneza hayo yalikuwa na majina yameandikwa, alipo fungua ndani akajikuta yeye yumo ndani ya jeneza... unaona jinsi watu wanavyo zuiliwa, mama huyu alizuiliwa asipandishwe cheo, sasa leo wapo watu wengi walio zuiliwa kwa jinsi hii lakini Yesu atawafungua kwa jina la YESU.


Baadhi ya Makutano wakifuatilia neno la Mungu katika Ibada ya Leo.
2Wathesolonike 2:6-7 imeandikwa, “Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. 7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.”  wazuiaji hawa wapo hata sasa wanafanya kazi, na kazi yao ni kuharibu masomo, kazi, mafanikio watu hawa wapo lakini uwezo wa kumwondoa tunao na tutamwondoa kwa jina la Yesu. 1wathesolonike 2:18 imeandikwa,Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.”  Huyu ni Paulo ambaye ameandika karibu nusu ya vitabu vya agano jipya lakini Paulo huyo anasema shetani amemzuia, sasa mimi na wewe hapo je tupo salama, lazima tuombe na kuondoa vizuizi vyote kwa jina la Yesu. Biblia inasema hivi, nawapenda wanipendao, lakini wale tu wanao nitafuta kwa bidii wataniona uso, kama ukimtafuta Yesu kwa bidii Yule anaye kuzuiya usiolewe, usioe, usisome ataondolewa kwa jina la Yesu. Kuna watu wengi leo wapo kanisani lakini ni wagumu kufanya maamuzi, hii ni kwa sababu yupo anayepinga na kukuzuia, leo kataa kwa jina la Yesu.

Ukiri: sema leo katika jina la Yesu, ninakataa kuzuiliwa kwa jina la Yesu, Yule aliye nizuia namwondoa kwenye maisha yangu kwa jina Yesu, iwe ni mtu, jini, nina mwondoa atoke kwangu kwa jina la YESU AMEEN.
Shetani hawezi kuja kukuzuia bila mipango, na ndio maana ni lazima ujue kuwa shetani anao watu anao watumia ambao ni wachawi na waganga mfano utamwona mfalme Ahabu 2 Nyakati 18:19-21 Imeandikwa, “Bwana akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu mfalme wa Israeli, ili akwee Ramothgileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. 20 Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? 21 Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo vinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka, ukafanye hivyo.”  Wanao zuia ni watu ambao ndani yao kuna mashetani amabao kazi yao ni kuzuia jambo rohoni ama mwilini, una ona pepo huyu aligeuka akawa pepo wa uongo ndani ya kinywa cha manabii, inawezekana uliacha kazi kwa sababu ya maneno ya mtu, wengine wana kauli mbaya na  wamekutenga, usilo jua wewe kuna pepo ameingia kwenye kinywa na pepo huyo amefunga na kuzuia Baraka zako. LEO NAMTANGAZIA AKUACHIE MARA MOJA NA AONDOKE POPOTE ALIPO KAA KWA JINA LA YESU.
Platform Ministry weakiongoza kipindi cha sifa na Kuabudu.
Kuna wengine wakipanga leo tunaomba gafla usingizi unakuja ujue kuna wazuiaji hapo.
NJIA KUU MBILI AMBAZO SHETANI ANAZUIA MTU
Shetani anatumia njia zifuatazo kumzuia mtu ;
1: SHETANI ANAWEZA KUZUIA AKIWA NDANI YA MWILI
Sasa mtu ni nani, mtu ni roho yenye nafsi inayo kaa ndani ya nyumba na nyumba hiyo ndio inaitwa mwili. Shetani akiwa ndani ya mwili naanza kukutawala, na shetani asili yake ni mabaya hivyo kila utakalo panga yeye anazuia kutokea ndani. Kumbuka wewe ni roho na shetani anakumiliki au (demon possession). Ni kama hivi, unatakiwa uende kwenye usahili mahala fulani saa mbili ila ikifika mda huo gafla unaanza kuumwa tena sana, hii ni kwasababu Yule wa ndani anayetawala maisha yako hataki uende kwa sababu anajua hapo kuna Baraka zako. Leo kataa kutawaliwa na kuzuiliwa kwa jina la Yesu. LEO NAMTANGAZIA YULE MTAWALA ANAYE TAWALA MAISHA YAKO LEO, NAMFYEKA KWA JINA LA YESU, HATA KUZUIA TENA MILELE YOTE KWA JINA LA YESU.
UKIRI:
Katika jina la Yesu shetani uliye kaa ndani ya moyo, kichwa, macho nakung’oa kwa jina la Yesu, mkono wangu huu naugeuza uwe na moto nakufyeka kwa jina la Yesu, niachie kuanzia leo, achia maisha yangu, ndoa, yangu, kazi yangu kwa jina la Yesu.

Kadiri unavyo jitunza kwa utakatifu ndivyo unavyo zidi kufanikiwa. Dhambi inaleta mauti, ndio maana Bibilia inasema miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu 1Wakorintho 6:16 imeandikwa, “Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.”  Unapo fanya dhambi jengo lina haribika leo kataa kuwa mtumwa wa dhambi kwa jina la Yesu. Utamwona Yuda Luka 22:3-4 imeandikwa, “Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.”
Roho ikikamatwa, mwili unaanza kuhangaika hangaika unakosa mwelekeo, ndio maana utaona watu leo wana vaa vimini, mlegezo, hii ni kwa sababubu mwili unatawaliwa. Jifunze jambo kwamba siku zote vitu vizuri huwa vimefichwa au kusitiriwa. Hata dhahabu inapatikana  chini, Almasi mpaka ichimbwe chini ya udongo ndo mtu aanze na kupata hela. Sasa kwanini vijana mnavaa nusu uchi, maana yake ni kwamba mwili una tawaliwa leo kataa kwa jina la Yesu. Sisi binadamu tumeumbwa kwa namna ya ajabu na kutisha. Hivyo usikubali kuliharibu hekalu lako kwa namna yeyote ile. Shetani alipo mtoka Yuda akajinyonga kwa nini alipo gundua amemuuza Yesu akajiua, na mimi naagiza shetani anaye kutawala akutoke uanze kumiliki na kutawala kwa jina la Yesu. Kuna mashetani wana mzuia mtu hata usimtolee Bwana mfano, mtu kaja kanisani akatoa shilingi mia tano lakini mwimbaji akiimba unatoa elfu ishirini unaanza kujiuliza kumbe alikuwa nayo mbona hajatoa kwa  Bwana? Kumbe shida ipo mashetani wana mzuia asitoe kwa bwana leo kemea kwa jina la Yesu.
Showers of Glory Morogoro
2: MASHETANI WANAO ZUIA KUTOKEA NJE YA MWILI
Hii ni njia ama mbinu nyingine ambayo shetani anaitumia ili kukugandamiza usitoke hapo na mtu ana kuwa hana mwelekeo, mashetani hawa wana kufuatilia mahali popote pale unapo kwenda, ndio maana mwingine halipuki mapepo lakini hafanikiwi anasema mimi sina mapepo kumbe asicho kijua huyu kuna mashetani wana kuzui kutokea nje ya mwili. Kuna mwingine kaomba kazi hapati ni kwa sababu shetani ametangulia nje kuzua asipate kazi. Mwingine anataka kuolewa wazazi wamekubali ila tatizo linatokea kwa ndugu wakagoma shida ni shetani katangulia kule akazuie, leo fanya ukaguzi wa rohoni na kuwaondoa hawa wazuiaji kwa jina la Yesu. Mfano utaona Zakaria 3:1 imeandikwa, “Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye”.  huyu ni kama askofu mkuu mashetani alishindwa kumwingia lakini wakashindana nae kutokea nje, kuna wengine mambo hayaendi kumbe nje kuna pepo yupo ana zuia biashara, leo nakataa kutawaliwa kutokea nje kwa jina la Yesu.
Wageni waliotutembelea kutoka nchini Ujerumani.
Matendo 13:6-12 imeandikwa, “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake BarYesu;7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 11 Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazungukazunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza. Ndipo Yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.”Huyu mmoja anatamani kuisikia injili lakini mmoja anazuiya asisikie injili ya Yesu, kuna mishale inarushwa kutokea nje ili uache jambo Fulani ambalo umelianza ama unalo kusudiwa kulianza wao wanazuia.

©/  MEDIA & INFORMATION MINISTRY,
GLORY OF CHRIST (T) CHURCH
MOROGORO CHURCH