Pages

Sunday, October 1, 2017

MICHORO YA UOVU

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH [GCTC]
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI: 01, OKTOBA, 2017.
MHUBIRI: MCHUNGAJI: DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)  

Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akifundisha na kuwaombea Makutano.

Utangulizi;
Basi ni hakika kwamba hakuna michoro bila mchoraji. Uchoraji ni sanaa ya kuweka alama kwa kutumia vifaa mbalimbali kama Kalamu ya wino, brashi na Penseli. Pengine kuchora kunaelezwa kuwa kuandika kwa kupaka rangi katika karatasi, Kitambaa, Ubao, Mwamba au ngozi. Matokeo au (picha) ndio huitwa MCHORO. Huu ndio uwakilisha kitu au wazi fulani. Mchoro waweza kuchorwa kwa makusudi mema au baya au waweza kutoka kwa Mungu au Shetani. Tunaposema Michoro ya Uovu maana yake ni ile michoro iliyotoka kwa shetani na mawakala. Michoro hii imelenga kazi iondoke, afya iondoke, ndoa ife, na wachoraji hawa wakichora hawaishii hapo unaenda katika hatua nyingine ya ujenzi, ambao ni mashetani wanajenga kuwa mtu huyu asizaee, asiolewe, au asisome.


 Kwa kawaida Mungu akitaka kuwasaidia watu huwa anawatumia mtu kuwasaidia. Yohana 1:6-7 Imeandikwa, “Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.  Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye”. Kabla kitu chochote hakijatokea huwa kinaanzia kwenye mchoro. Kila unachokiona leo kilianzia kwenye akili ya mtu mmoja na baadae kikawekwa kwenye mchoro na hatimaye kikawekwa kwenye uhalisia. Yawezekana ni nyumba, gari, duka, kanisa, Meli, Ndege na vinginevyo vingi vilianzia katika michoro. Michoro ya Uovu inalenga kazi iondoke, afya iondoke, ndoa ife, watoto wafee, uzae mapooza, na wachoraji hawa wakichora hawaishii hapo unaenda katika hatua nyingine ya ujenzi, ambao ni mashetani wanajenga kuwa mtu huyu asizaee, asiolewe, au asisome, ila leo ninaufuta michoro yao kwa jina la Yesu.

KUNA MCHORAJI. Ili mchoro uwepo lazima awepo mchoraji. Hata kwenye uovu nako mambo huanza na michoro. Yawezekana shetani na mawakala wake wakaona namna ambavyo umepewa nyota ya mafanikio, kibali, utajiri mchawi anaona wivu. Mchawi akishaona wivu basi anachukua hatua ya kutafuta mchoraji wa mchoro wa uovu/uharibifu.

Baadhi ya Makutano Wakipokea hatima zao wakati wakiendelea kusikiliza somo la Michoro ya Uovu.

WASAIDIZI WA MCHORAJI
. Ili wachawi au waganga waweze kuchora michoro ya uovu lazima watoe kafara kwa majini na majoka. Majini hawa ndio wenye ujuzi wa namna nzuri ya kuvunja miguu, kumrudisha mtu nyuma  kiroho na mengine mengi. Ili kufanikisha uovu huo shetani anatumia majini au mapepo kulingana na ngazi zao kwenye ulimwengu wa roho. Waefeso 6:12 Imeandikwa, “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”. Kama mtu ni mwombaji sana, basi anatokea mchawi au jini ambaye alimfahamu kabla hajaokoka. Basi wanapanga namna ya kumtega huyo kwa kumtumia msichana wa aina yake. Baada ya mchoro huu kumnasa utaona nguvu ya kuomba inapungua na hatimaye mtu anamwacha Yesu. Mtu anahamishwa kwenye nafasi yake anapelekwa kwenye kujua habari za mambo mabaya, muziki wa dunia na mengine mengi. Tambua katika hali kama hii fahamu kuna mchawi au mganga anakutafuta ili akumeze. Lazima ufute michoro hiyo kwa jina la Yesu. 


MTEKELEZAJI WA MCHORO.   Baada ya Kuchora Mmchoro lazima awepo mtekelezaji wa mchoro. Maana yake ni kwamba hawa ndio wanahamisha mchoro kutoka kwenye maandishi na kuuweka kwenye uhalisia. Hawa wakishaanza ujenzi wa uharibifu  mtu anaonekana kama mtakatifu lakini ndani yake roho ya shetani inatenda kazi ndani yake. Wajenzi hawa huwa wanatumia mabati/uzio ili uharibifu ndani yako usionekane. Kumbe hakuna tukio la ghafla bali ni kwa sababu yalikuwako mabati ya uzio ili usijue kama ujenzi ndani ulikuwa unaendelea. Kila tatizo unaloliona lilianzia kwenye ujenzi wa rohoni. Na ukuta ukishakamilika ndipo uovu unatokea mfano ajali, kifo, magonjwa ya ghafa; unashangaa kwa sababu hukujua walikuwepo wachoraji na wajenzi wa mchoro. Jenga utamaduni wa kuomnba siku zote za maisha yako ili uwe salama. Lazima uombe siku zote ili uvunje michoro ya uharibifu na uovu wa kila namna. Kila unapoomba, Mungu anasikia kilio chako na hivo husikia na kuzuia mabaya.


Jifunze kwa nini mtu anaweza kuacha kazi mwenyewe kwa hiari yake. Hii ni kwa sababu kuna mtu aliyeweka mchoro na akatuma majini wa kumpandia roho ya kuacha. Mashetani yakiingia yanaongea ndani yake na hatimaye mnaona anaamua kuacha kazi mwenyewe. Na ndio maana baadae utamwona anajutia uamuzi wake, kwa sababu hakuwa yeye bali watekelezaji wa mchoro ule. Kwenye kuachwa, kuvunjika kwa ndoa, kuibiwa, kukataliwa fahamu kuna mchoro ulioanza kabla halijatokea jengo la uharibifu kama kujiua, kakataliwa na kuibiwa.

Platform Team wakiongoza kipindi cha Sifa na Kuabudu wakati wa Ibada ya Leo.

Yeremia 5:26-27
Imeandikwa, “Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu.  Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.” Katika uumbaji wa Mungu kuna watu waovu ambao kazi yao ndio wachoraji na watekelezaji wa mchoro husika. Watu hawa na nyumba zao wamejaa hila. Maana yake ni kwamba ukiingia ndani ya nyumba yao utaona ramani za umasikini, ufukara, mateso, ufuska, ajali na matukio mabaya yamechorwa kinyume na maisha ya watu. Hizi ndio kazi za waovu, kuna michoro ya uzinzi, kuzaa kabla ya ndoa, na kuzaa mapooza maana kuna michoro ya kichawi ili mtu aaibike. Wachawi wanayo michoro ambayo bado haijatekelezwa, imewekwa akiba waweza kuitekeleza wakati wowote. Lazima uamue kuwapinga kwa nguvu ya maombi katika jina la Yesu.
  
Ndani ya nyumba za waovu kumejaa hila. Mtu akiona wivu anaenda kwa mchawi na kutaka mchoro wa uharibifu. Anaweza akapewa mchoro wa makengeza, kushindwa, ufukara, harufu mbaya, bahati mbaya na kifo cha ghafla. Kwa kawaida mchoraji kama bado yuko hai, ukifuta leo basi kesho anachora mwingine. Lazima na yeye avunjwe kwa sababu yeye ndiye mchoraji.


Matendo ya Mitume23:12-16 Imeandikwa, “Kulipopambauka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo. Na hao walioapiana hivyo walipata zaidi ya watu arobaini. Nao wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo tusionje kitu hata tumwue Paulo. Basi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua habari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia.  Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari.” Huu ulikuwa ni mchoro kwa ajili ya kumuua mtume Paulo. Mchoro uliandaliwa baada ya kujua kazi aliyokuwa amepewa mtume huyu kwa ajili ya kuwafungua wanadamu kutoka mikononi mwa shetani.


Watu hawa waliapiana kufunga. Maana yake hawa walijua nguvu ya kufunga. Ili mchoro wao ufanikiwe ni lazima wafunge. Hii ilikuwa hatua ya kwanza ili kuutekeleza uovu wao. Pili waliamua kukubaliana na kuapiana maana yake Kiapo. Tatu wakaenda kwa Wazee na Makuhani ili kupata kibali cha wazee. Wenye michoro walienda kumshawishi Jemedari ili amshushe chini ili kumuua. Hii yote ilikuwa namna au mbinu ya kutekeleza mbinu ya uovu. Ilikuwa kidogo Paulo aingie kwenye mtego lakini Mungu akamsaidia. Matendo ya Mitume 23:20-21 Imeandikwa, “Akasema Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi. Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hata watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakiitazamia ahadi kwako.”Mungu akamtuma mtu ili kumtenga mbali na mchoro wa mauti juu yake.

Showers of Glory Morogoro wakimsifu Bwana.

Wanaochora michoro ya uovu wanaishia kujenga. Wasipozuiliwa jengo lao litasismama. Na hatimaye uharibifu wao utatokea. Mwanzo 11:1-9 Imeandikwa, “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.  Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”. watu hawa walijenga ili kupingana na mpango wa Mungu. Watu hawa ndio wachawi wa leo wenye lugha moja na kila wanalokubaliana wanaweza kulitimiza na hawawezi kuzuiliwa neno.  Ndipo Bwana akaamuru kanuni ya ajabu, akasema lazima tuwachafulie usemi wao. Nawatuma waniviziao ili wawafadhaishe na kuwarudisha nyuma waovu na ramani zao. Amuru wavurugane wao kwa wao. Wachanganyane wao kwa wao. Amua mafarakano kati yao kwa jina na Damu ya Yesu.

UKIRI WA MAOMBI YA KUFUTA MICHORO YA UOVU

Sema kwa jina la Yesu Kristo, baba Mungu wa mbinguni, nina pokea uwezo na mamlaka za kufuta kila michoro ya uovu, leo nina vaa silaha zote za kufuatilia michoro ya uovu, kwenye kila nyumba ya uovu iliyo jaa michoro, nyumba za wachawi, waganga, wafuga majini, leo katika jina la Yesu ninaifatilia michoro yote mahala popote ilipo nina ichoma moto kwa jina la Yesu, Kila wasimamizi wa michoro, na wachora michoro wote nina waangamiza kwa damu ya Yesu, walio patina mashetani, mizimu, majoka nina wafyeka kwa jina Yesu, ewee jini uliye tumwa na mtu wa karibu, ndugu, rafiki, jirani niakufyeka kwa jina la Yesu. Nina wachanganya lugha zao wasielewane wao kwa wao kwa jina la Yesu, mchora mchoro na mjenzi wasielewane kwa jina la Yesu.