GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
[GCTC]
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SNP. DR. GODSON ISSSA ZACHARIA
JUMAPILI: 14, JANUARI, 2018
MHUBIRI: SNP. DR. GODSON ISSSA
ZACHARIA
Kwa
asili Ndoa ni muunganiko wa kudumu kati ya mtu mume na mke na kuwa mke na mume
au mwili mmoja. Mungu alimfunulia mtume
Paulo kuhusu ndoa. Mungu alimpa kufundisha na kuonya mengi kwa habari ya ndoa.
Mungu anaongelea kwa habari ya mtu kuungwa na mtu mwingine, Kwamba mtu akiungwa
na kahaba basi atakuwa mwili mmoja naye. Ndoa za Kishetani ni ndoa
zisizoeleweka sana kwa sababu ya watu kutokujua. Lakini ndoa za Kishetani ni
ndoa inayofungwa kati ya mwanadamu na mashetani katika ulimwengu wa roho. Imeandikwa,
“Au
hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale
wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.”
(1wakorintho 6:16-17) shetani ana uwezo wa kuvaa mwili akamfuata mtu
akamtongoza au kumwoa mtu. Ndoa hizi utazijua kwa dalili ya mambo unayoota
yakifanyika kana kwamba unafanya mapenzi lakini kwa uhalisia umefanya mapenzi
katika ulimwengu wa roho.
Ndoa
ni nini?
Ndoa
ni muunganiko wa kudumu kati ya mwanaume na mwanamke na wakawa mwili mmoja yaani mume na mke. Ndoa ni jambo
la kisheria na linatokana na agizo la Mungu kwamba kuwe na ndoa kati ya mume na
mke nasivinginevyo. Imeandikwa mwanzo 2:24,“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba
yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Mungu ndiye mwanzilishi wa jambo la
kuwepo kwa ndoa. Neno linaonyesha kwamba Mungu aliona vyema iwepo ndoa. Akasema
Adamu awe na msaidizi wake ambaye alikuwa Eva. Ndoa ni taasisi ya muhimu kwa
mujibu wa neno la Mungu. Mungu hakusema wawe watu wa jinsia tofauti maana Mungu
alikuwa na uwezo wa kusema awe mke kwa mke au mume kwa mume. Kumbe ndoa kati ya
watu wa jinsia moja sio ndoa kwa mujibu wa neno la Mungu. Imeandikwa mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema, Si vema huyo
mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Bwana Mungu
akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani,
akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu
likawa ndilo jina lake. Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na
ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia
Adamu aliyefanana naye. Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye
akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule
ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa
Adamu.” (Mwanzo 2:18-22)
Baada
ya shetani kufukuzwa kutoka mbinguni naye akaanzia jambo la taasisi ya ndoa.
Ndoa hizi ni za siri kwa sababu watu hawezi kulisema jambo hili. Hizi ni ndoa
za siri kwa sababu tendo la ndoa linafanyika rohoni lakini mtu anajiona kama
ndoto.
JE MAMBO HAYA YAPO?
Neno la Mungu linaonyesha dhahiri kwamba Mungu
aliumba wanadamu pamoja na viumbe wengine. Baada ya wanadamu kuongezeka juu ya
nchi wana wa Mungu wakaanza kuwaingilia wana wa wanadamu. Wana wa Mungu
walianza kuwaingili binti za wanadamu. Neno kuwaingilia maana yake ni kufanya
tendo la ndoa kati ya mke na mume. Lakini jambo hili halikuishia kwenye
kuwaingilia tu bali walizaa watoto pia. Na watoto wao ndio waliokuwa watu hodari
zamani. Imeandikwa mwanzo 6:1-4 “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa
nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za
wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. Bwana
akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni
nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Nao Wanefili (Wanefili
maana yake ni majitu) walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana
wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio
waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.” Hawa wanaoitwa wana wa Mungu kwenye agano la
Kale ni malaika. Imeandikwa, “wana wa Mungu waliwaona hao binti za
wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.”
(Mwanzo 6:2). Pia neno la Mungu linaonyesha pia katika kitabu cha Ayubu kuwa
malaika kwa lugha ya kiebrania ni malaika Imeandikwa “Ilikuwa, siku moja ambayo hao
wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda
kati yao.” (Ayubu 1:6, 2:1). Kwenye agano jipya wana wa Mungu ni wale
waliompokea Yesu. Imeandikwa, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;” (Yohana
1:12)
Kuna
malaika wa aina mbili malaika watakatifu
ambao walishangilia wakati wa uumbajii wa Mungu (ayubu38:4-7) na malaika
waovu au walio asi au waliotenda
dhambi na binti za wanadamu.
Matokeo
ya kuingiliana kati ya uzao wa wana wa wandamu na wana wa Mungu ilikuwa ni
kuzaa watoto. Watoto hawa ndio watu hodari nyakati hizo. Malaika Walioasi hawa ndio malaika wa shetani
ambao alitupwa nao kutoka mbinguni. Hawa wanawaingilia watu ndotoni ndio
malaika wa shetani. Malaika waliotenda dhambi wakati wa Nuhu au walioasi ndio
wanaoitwa malaika walioanguka (folen Angels). Imeandikwa Ayubu 38:4-7 “Ulikuwa
wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya!
Sema, kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama
ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu
yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?
Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa
furaha?” (Ayubu 38:4-7)
Malaika
wa shetani ndio wale wanaitwa malaika wa giza kwenye neno la Mungu. Neno la
Mungu linasema malaika hawa wa giza walifanya uasherati na watu wa Sodoma na
Gomora. Kufanya tendo la ndoa kwenye ndoto sio jambo la asili wala halitoki kwa
Mungu bali shetani. Basi maneno haya yanaonyesha kuwa ndoa za kishetani
zipo. Ndoa hizi zipo na zinafungwa
kwenye ulimwengu wa roho. Imeaandikwa Yuda 1:1-7, “Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo,
ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika Mungu Baba, na
kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo. Mwongezewe rehema na amani na upendano.
Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni
wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba
mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu
waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi,
nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo. Tena napenda
kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha
kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini. Na
malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu,
amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati
kwa jinsi moja na hawa”
Malaika
hawa wana tabia ya kujibadilisha maumbo. Malaika aweza kubadilika na kuwa
chochote. Malaika waliwahi kumtembelea Ibrahimu lakini wakiwa katika sura au
umbo la binadamu. Ibrahimu aliwapokea kama wanadamu lakini walikuwa malaika.
Hapa tunaongelea ndoa inayoweza kufungwa na shetani lakini aliyekuja kwako kama
mtu kama wewe. Mtu anaweza kukutana na msichana mzuri mpaka kijana anasema
mapigo ya moyo yalibadilika ghafla. Anaweza kupendeza kana kwamba hajawai
kufanya kazi au hana kovu ni kweli yuko vile lakini zijaribuni roho. Imeandikwa
mwanzo 18:1-3 “Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi
mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona, na
tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio
kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu,
kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.”
Unaweza
kumwona kama mwanaume au mwanamke mzuri
kumbe ni shetani katika mwili. Anaonekana kama mtu na anazo sifa zote.
Anaonekana kama mwanaume mwenye mali na anao moyo wa kujali sana. Anaweza
anafanya hayo yote lakini si kwamba ni mtu bali ndani yake ni joka. Ndoa za
kishetani ni janga la watu wote wa mataifa yote.
DALILI
AU ATHARI ZA NDOA ZA KISHETANI.
MADHARA
KWA MTU AMBAYE HAJAOA AU HAJAOLEWA
i)
Kama
ni mwanamke hapendi wanaume hata mara moja. Akitokea mwanaume anataka
kumchumbia binti, utasikia maneno ya huyu binti haijuzu dunia kuyasikia. Hawezi
kukaa au kufanya kazi na wanaume. Wadada wanakuwa na maneno ya kutisha, mfano
mdada mmoja alikuwa akisema yeye mwanaume akimsumbua lazima atammwagia maji ya
moto. Mdada Mzuri lakini haolewi. Maana yake huyu amevalishwa vazi la uzee ili
mashetani waweze kumtumia kimapenzi. Haya yote yanatendeka kwa sababu ya ndoa
za kishetani
ii)
Kama
ni mwanaume, hapendi kukaa na wanawake. Huyu tayari ana jini jike wa ndotoni.
Majini haya yanasababisha cijana wengi kuchelewa kuoa. Kwa hiyo kijana huyu
hawezi kuoa. Hata akichumbia lazima baadae atakuwa na sababu ya kufanaya uchumba
uvunjike.
iii)
Kama
ni Mwanamke, anakuwa na maumivu makali wakati wa Hedhi. Mwanamke anasikia
maumivu kabla na wakati wa hedhi kiasi ambacho dawa zote haziwezi kumfanya
apone. Hii ni kwa sababu yapo majini yanasimamia ndoa.
iv)
Kuvunja
Uchumba. Kijana ipo ndoa na cheti cha ndoa kwenye ulimwengu wa roho, akianzisha
uchumba lazima uvunjike. Na utakuta anayevunja ni Kijana mwenyewe. Hii ni kwa
sababu yupo mume au mke wa kiroho anayehakikisha ndoa yake ya rohoni haiwezi
kuingiliwa na mtu mwingine.
v)
Anavunja
au kuharibu vitu vyake mwenyewe. Awe mke au mume lazima awe na tabia ya
kuharibu vitu au mali zake mwenyewe bila sababu. Hii ni kwa sababu kuna mke au
mume wa rohoni. Hata ni mashetani yanayosabaisha vurugu kwenye familia. Ni kazi
ya shetani kuharibu vitu vya watu. Anaweza kuwa mfanyakazi mzuri na mwenye
umahili katika kazi hiyo lakini anaamua kuacha. Imeandikwa,Yohana 10:10 “Mwivi
haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele.”
vi)
Anatabia
ya kuacha vitu. Anaweza kuwa kijana mahili wa ushonaji lakinianaamua kuacha bial sababu za msingi.
Mtu huyu anaacha kazi ili Yule mume au mke wa rohoni amfanye huyu kuwa
mtegemezi wake.
KWA
WALE WENYE NDOA.
i)
Huwa
Anakosa Furaha wakati wa Tendo la Ndoa. Awe mke au mume lazima ajisikie maumivu makali
sana wakati wa tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu yupo mke wa rohoni anayezuia
isiwepo furaha kati ya wanandoa ili yeye ammiliki vizuri kwenye ulimwengu wa
roho. Na utakuta mke au mume anaota anafanya tendo la ndoa na afurahia sana.
ii)
Unahisi
kumpenda mwenzio akiwa mbali. Mtu mwenye ndoa anakuwa na hasira mwenzi wake
akirudi nyumbani. Lakini mume au mke akiwa mbali ndo ulalamika kumhitaji. Hii
yote ni mifumo ya ibilisi ambayo Yesu alikuja ili kuivunja. Imeandikwa, “atendaye
dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi
hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” (1
Yohana 3:8)
iii)
Anakuwa
Mlevi. Mwnaume anapandikizwa roho ya ulevi ili apoteze ule moyo wa uwajibikaji
katika fsmilia yake. Lakini pia mtu akilewa sana na pombe ikawa sehemu ya
maisha yake hawezi kufanya tendo la ndoa. Hii ni kwa sababu kuna mwanamke au
mume wa rohoni. Kumbuka lengo la ndoa za
kishetani ni kutaka kuvunja ndoa za mwilini.
iv)
Roho
ya kushindwa. Huwezi kufanya jambo ukafanikiwa. Kila unachoanza lazima kiishie
njiani, iwe kazi, biashara, shule lazima hawezi kufanikiwa. Ukipata mtu wa
kukusaidia lazima aondoke kabala hajakusaidia au anakufa kabla msaada wako
haujawa timilifu.
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI
KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: Pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/