GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
[GCTC]
KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SNP. DR. GODSON ISSSA ZACHARIA
JUMAPILI: 28, JANUARI, 2018
MHUBIRI: MCHUNGAJI, AMOS KOMBA (SNP
MTWARA)
Uchawi ni roho chafu
inayotokana na shetani. Kwenye Biblia neno mchawi limeandikwa mara nyingi.
Mchawi ni mtu au watu wenye roho za uchawi ndani yao. Wanaitwa wachawi kwa
sababu ndani yao kuna roho ya uchawi ndani yao. Mchawi akiona, akitembea,
akikaa na kila anachokifanya nyuma yake kuna roho ya uchawi. Wanadamu wote ni
roho ambao wanakaa ndani ya nyumba inaitwa mwili. Chochote anachokifanya ndani
yake kuna roho inamsukumiza kufanya hivyo. Ndio maana Mungu anasema usimwache
mwanamke mchawi kuishi.
“Usimwache mwanamke mchawi
kuishi.” Imeandikwa Kutoka 22:18.
“Tena mtu mume au mtu mke aliye na pepo, au
aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.”
Imeandikwa, Mambo ya Walawi 20:27
Mungu anasisitiza wachawi
hawatakiwi kusamehewa wala kuwaonea huruma. Na hutakiwi kubebea jiwe katika
ulimwengu wa mwili bali utumie upanga wa rohoni. Hii ni vita ya rohoni wala si
vita ya mwilini. Inawezekana umefika hatua ya kuolewa lakini mchawi akasema
hutapenya (ukafika Pafo). Inawezekana kuna matukio yanakupata kumbe ni matukio
ya kichawi. Kuna hatua uliyotakiwa kuifikia ila hujafika kwa sababu kuna
wachawi wametuma upepo wa kukurudisha nyuma.
Mchungaji Amos Komba akifundisha neno la Mungu. |
Hapa tunaona BarYesu alikuwa
akishindana na akitaka kutia imani ya kuicha ile imani. Mtume Paulo alikuwa
amejawa na Roho Mtakatifu ili apate uwezo wa kushindana na BarYesu akamkazia
macho. Inawezekana kuna mtu au rafiki anatembea na wewe lakini akawa na roho ya
uchawi anapotosha njia ya haki.
Viumbe na matukio ya kichawi. Hakuna uchawi kama hakuna viumbe wachafu. Wachawi wanapata nguvu
kutoka kwa shetani kwa sababu kuna viumbe wachafu.
“Kwa kuwa katika yeye vitu
vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na
visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu
vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Imeandikwa, Wakolosai
1:16
Hapa Biblia inatudhihirishia
kwamba kuna viumbe mbinguni na dunia vipo pia. Kuna viumbe vinavyoonekana na
visivyoonekana. Viumbe visivyoonekana ni pamoja na Mungu, Roho Mtakatifu
havionekani ni kwa sababu ya asili yake. Pia shetani ni kiumbe asiyeonekana
ingawa hakuwa shetani hapo mwanzo alikuwa malaika baada ya kuasi ndipo akatupwa
shimoni.
“Kisha nikaona malaika akishuka
kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani,
akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake,
asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo
yapasa afunguliwe muda mchache.” Imeandikwa, Ufunuo wa Yohana 20:1-3
baadhi ya Makutano wakifuatilia neno la Mungu wakati wa Ibada. |
Sehemu ya shetani ni kuzimu.
Ulimwengu wa roho na mwilini una kanuni. Na ndio maana ikifika jioni watu
wanaenda kulala na s kazini. Na ulimwengu wa roho una kanuni pia. Makao ya
shetani ni kuzimu wala sio ndani ya mwili wa mtu au kazini kwako.
“Kuzimu chini kumetaharuki
kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako,
Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke
katika viti vyao vya enzi.” Imeandikwa, Isaya
14:9
Inawezekanaje shetani yupo
nyumbani kwako, au tumbo unatakiwa umwambie shetani mahali pake ni shimoni.
Kuna wakati mwingine anahama kuzimu anakuja kwenye ulimwengu wa mwili. Kwenye
Biblia tunasoma Mungu huwafanya malaika zake kuwa pepo (upepo). Maana yake
malaika awe wa nuru au wa giza anaweza kujigeuza na kuwa upepo. Si kila upepo
ni upepo, na si kila kimbunga ni kimbunga.
Maana yake ni kwamba upepo
wa shetani uambatana na laana, mikosi na balaa zote. Na upepo wa Mungu
uambatana na Baraka, mafanikio, kuongezeka, afya na ustawi.
Platform Ministry wakiongoza nyimbo za sifa na kuabudu katika ibada ya leo. |
“Aliziinamisha mbingu
akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. Akapanda juu ya kerubi
akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.” Imeandikwa, 2 Samweli 22:10-11
Mungu aliruka kama mabawa ya
upepo. Kumbe Mungu anaweza na aliwai kuufanya upepo kuwa mbawa na kwazo
akaruka.
“Bwana akamwambia Musa, Nyosha
mkono wako juu ya nchi ya Misri kwa hao nzige, ili wakwee juu ya nchi ya Misri,
waile mimea yote ya nchi, yaani, vyote vilivyosazwa na ile mvua ya mawe. Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya
Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na
usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige. Na hao
nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya
Misri, walikuwa wabaya mno; hawajakuwapo nzige kama hao majira yo yote, wala
baada yao hawatakuwa wengine jinsi hiyo.” Kutoka
10:12-14
Upepo huu ulileta nzige, hapa
tunajifunza kuna upepo unavuma kuleta ugonjwa, au kuleta vitu katika ulimwengu
wa mwili. Ndani ya upepo unaweza kuleta vitu.
“Kisha upepo ukavuma kutoka kwa
Bwana, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao ukawaacha wakaanguka
karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, na kama kiasi
cha mwendo wa siku moja upande huu, kuizunguka, nao wakafikilia kiasi cha
dhiraa mbili juu ya uso wa nchi.” Hesabu
11:1
kila upepo unamahali unapotokea,
upepo huu ulivuma ukaleta kware pande za baharini walianguka karibu na kambi
kwa mwendo wa siku moja. Huu upepo ulileta chakula. Unawezaa kuamuru upepo
ulete amani kwenye ndoa yako, maisha yako. Inawzekana unafanya biashara lakini
unapata hasara kumbe kuna pepo imevuma.
“1. Ikawa, hapo Bwana alipopenda
kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali
pamoja na Elisha. 11. Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama!
Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya
akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.” 2 Wafalme 2:1,11
Upepo ulivuma kama gari la moto,
kama farasi, upepo wa kisulisuli ulimbeba Eliya mpaka mbinguni. Tunajifunza
kwamba upepo unaweza kuwatenganisha watu na watu wao. Wachawi wanaweza kutuma
upepo uje kukubeba ukakutupe kwenye matatizo.
Upepo unaweza ukabeba nyota ya mafanikio na hatima yako.
“Ikawa siku zile mojawapo
alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo
ya ziwa. Wakatweka matanga. Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka
tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari. Wakamwendea,
wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka,
akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari. Akawaambia,
Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakaamka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu
basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?” Luka 8:22-25
Kuna mahali unatakiwa kuvuka ila
huwezi kwenda kwa sababu kuna Baraka zako kule. Yesu na wanafunzi wake walikuwa
wanavuka kwenda ng’ambo walipanda chomboni Yesu alilala usingizi, wakiwa
wanavuka upepo ukavuma wanafunzi walimwamsha Yesu. Kilichokuwa kinataabishwa ni
chombo, chombo hicho kilitakiwa kikuvushe mpaka ng’ambo. Chombo ni kifaa
kinachoweza kukuvusha wewe. Inawezekana ndoa yako ndio chombo, shule ndio
inataabishwa, ndio inayotakiwa ikufiishe ng’ambo.
Ukiri: Kuanzia leo kwa jina la Yesu kila pepo iliyotumwa kwangu
kunitaabisha, kunikwamisha, kunipindisha, kunichelewesha, leo nakunyamazisha
kwa jina la Yesu. Ewe mwongozaji wa upepo, unayeongeza mwendo wa upepo
nakuapisha kwa jina la Yesu.
Mchungaji Amos Komba akimwokoa mtu kutoka nguvu ya upepo wa kishetani. |
“Ilikuwa, siku moja ambayo hao
wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda
kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu
Bwana, na kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea
huku na huku humo. Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo
mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu
mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani
akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira
kwa ukingo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi
za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini
nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za
uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo
wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka
mbele za uso wa Bwana.” Ayubu
1:6-12
Shetani alituma matukio, lakini
alipogusa nyumba yake alianguka na kurarua mavazi yake.
“Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao
na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao
mkubwa; mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga
hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi
peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari.” Ayubu 1:18-19
Upepo ulivuma wa nguvu na
umetokea jangwani, na kwani nini jangwani ni kwa sababu jangwani ni shimoni. Jangwa
lina nguvu ya kuzuia/kutatanishwa vitu vya rohoni. Wacahawi kwa nanmana ya
kafara wanaouweza wa kuita mapepo na kuyageuza yakawa upepo wakayatuma kwenye
maisha yako. Haya ni matukio ya kichawi, leo sema na upepo, upepo una akili na
masikio nao utatii.
NAMANA YA KUSHINDA MATUKIO YA KICHAWI
1. Kuokoka; ni kwa sababu ukiokoka
unapewa uwezo (unapewa mamlaka) wa kufanyika kuwa watoto wa Mungu. Ukiwa mtoto
wa Mungu unapata sifa ya kulindwa na malaika wa Mungu. Zaidi unakuwa na nguvu
ya kuyaamuru mashetani na yakakutii.
“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa
damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.”
Yohana 1: 12-13.
“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini,
atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa
pepo; watasema kwa lugha mpya;” Marko 16:15-17
2. Mamlaka; Ni ile hali ya kuwa na uwezo
na nguvu ya kutenda. Unaweza ukaamini usiwe na mamlaka, wanafunzi wa Yesu
walikuwa wameokoka. Neno la Mungu linasema naye Yesu aliwaita wale Thenashara
akawapa amri (mamlaka). Tembea, omba na ongea kwa mamlaka nao upepo utakutii
kwa jina la Yesu.
Mchungaji Dkt. Godson Issa Zacharia akiwafungua kutoka matukio ya kishetani. |
“Akawaita
wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo
wachafu; ” Marko 6:7
Kuitwa ni
kuokolewa, na hii amri ni mamlaka. Ukiomba tumia mamlaka. Omba kwa mamlaka
maana wewe ni mwana wa Mungu.
3. Maombi ya Kushindana; haya ni
maombi ambayo ni vita ya rohoni. Wewe unatakiwa uombe ushindane na ule upepo.
Upepo wa usaliti ulishavuma mbinguni mpaka nao wakashindana wakamtupa shetani
nje. Na wewe ili kushinda unatakiwa kushindana na vita inaanzia kwenye
ulimwengu war oho na hatimaye utashinda na mwilini.
“Kulikuwa
na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka
naye akapigana nao pamoja na malaika zake;” Ufunuo wa Yohana 12:7
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI
KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson
Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)