GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SNP
DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI:
18 FEBRUARI, 2018
MHUBIRI:
MCHUNGAJI, DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
Utangulizi:
Mji
ni sehemu ya makazi ya watu. Ni mahali ambapo wanadamu wanaendelea na shughuli
zao za kujiingizia kipato kila siku kwa ajili ya maisha yao. Mfano hapa
Tanzania kuna mji wa Morogoro, Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. Neno mji
Kibiblia unajumuisha nchi, mkoa, wilaya, kata na hata familia unayoishi. Kufanikiwa
kwa watu kunategemea pia mahali wanapoishi, wanachokiamini na wakimtegemea
Mungu wanafanikiwa zaidi.
Walikuwako watu wanaoishi kwenye mji
fulani ambao ulikuwa mzuri sana lakini maji ya mji huo yalikuwa yakizaa mapooza.
maji hayo walipokuwa wakinywesha ng’ombe lazima wafe, ukimwagilia mazao yanakufa,
wakinywa wanazulika. Watu hawa wakakutana na Nabii Elisha wakamwomba awasaidie juu
ya jambo hilo.
“Watu
wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri,
kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.
Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka
akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana
asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa
mapooza.” 2 Wafalme 2:19-21
Kuzaa mapooza ni sawa na kuharibu
mimba. Kila unachotengeneza hakiwezi kufika hatima yake. Ni sawa na mwanamke
ambaye kila akitunga mimba lazima iharibike. Hata hivyo jambo hili la kuzaa
mapooza halijawai kumpendeza Mungu tunayemtumikia;
“Nami
kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala
mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba,
asema Bwana wa majeshi.” Malaki 3:11
Kuzaa mapooza ni kupukutisha majani au
matunda yake. Mfano unaweza kuwa na shamba lililomea vizuri na likawa
linapukutisha matunda. Ni sawa na kuanza mradi ghafla unaharibika, unaanza
shule humalizi huko ndiko kuzaa mapooza, lakini Mungu hapendi hata mara moja
uharibikiwe yeye ameahidi ahadi ya kubarikiwa katika mambo yako yote.
“Nanyi
mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako;
nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala
aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.” Kutoka
23:25-26
Bwana atatimiza siku zako za kumiliki;
kutawala, kutiisha, na ukianza miradi mipya ifanikiwe, ukianza biashara
ifanikiwe, ukisoma ufaulu katika masomo yako na yote yanawezekana kwa yeyote
aaminiye kwa jina la Yesu.
Watu hawa walimwendea Elisha
wakamwambia mji ni mzuri ila maji yake huzaa mapooza. Mambo hayaendi, vitu
vinakufa kabla hujafaidi matunda yake. Inawezekana una ndoa nzuri; mke mzuri, lakini
ndoa haina watoto, hakuna upendo ndani ya ndoa hiyo, kama ni uchumba ulikuwa
mzuri, lakini uchumba unaingia kwenye magonjwa, au ujauzito kabla ya ndoa.
Yawezekana
mji wako ni mzuri. Mfano wa mji wa Morogoro ni mzuri ajabu na una vitu vingi
vya kuvutia, Wilaya ya Ulanga kuna madini yanaitwa Ulanga, wilaya ya Matombo
kuna madini aina ya Red ganet, Reds right na mengine mengi, Morogoro mjini kuna
dhahabu safi inapatika hapa. Kuna mbuga za wanyama mfano Mikumi, Seloue na
nyingine.
Morogoro
ina udongo mzuri sana ambao unaweza kuotesha kila aina ya mmea au mbegu nyingi
sana. Ni sehemu inayofaa kwa ajili ya uwekezaji wa Viwanda. Kuna mradi mkubwa
wa Bandari Kavu ambayo itatumika kukusanya na kusafirisha mazao kwenda ndani na
nje ya nchi. Kuna mradi wa ‘Treni iendayo Kasi’.
Mji huu ni mzuri sana lakini hatari
yake kuna mapooza., mapooza hayo ni kama yafuatayo;
·
HAKUNA AJIRA; Mji huu ulikuwa na viwanda
vingi kama Polister, Canvas Moroshoes na vingine. Viwanda hivi vingeajiri watu
wengi lakini kuna mapooza. Lazima tuombe kwa ajili ya mji wa Morogoro na viunga
vyake. Mji ni mzuri lakini hatuna miundo mbinu. Mchele wa Morogoro ni mzuri
lakini utakuta umewekewa jina ‘Mbeya Grade’.
·
WATU WAZEMBE. Hakuna bidii ya kazi; Watu wa
mji wa Morogoro ni wazembe kupita kawaida. Ni watu wasioweza kujishughulisha
ili kupata kipato. Ni watu wenye nguvu lakini hawawezi kuboresha maisha yao.
Maana yake kuna kuna jambo kwenye ulimwengu wa roho linaloitwa Maji yenye kuzaa
mapooza. Watu wamefungwa akili hawawezi kuwa na mipango ya kukomboa uchumi wao.
Ni wageni waliojenga Morogoro kuliko wenyeji.
·
WATU WANAAMINI UCHAWI SANA; watu wanaamini
sana uchawi, Hii ni roho inayotenda kazi sana. Uzembe ni matokeo ya roho ya
uchawi. Mtu akianza ujenzi, vita inaanza na inakuwa kali. Watu wengi wamejaa hofu ya uchawi. Wengine
wana mashamba lakini hawawezi kulima kwa sababu ya roho hiyo ya uchawi.
Imeandikwa Usimwache
mwanamke mchawi kuishi leo tutawashinda wachawi wote kwa jina la Yesu.
·
ROHO YA UMASKINI; utatona morogoro kuna
umaskini wa hali ya juu utamkuta mtu mzima kabisa anakaanga karanga anatembeza
mji mzima lakini ukimwambia achukue shamba alime kwa mara moja awe tajiri
hataki. Watu wengi wameamini uchawi sana kuliko Mungu. Mzunguko wa fedha ni
mdogo sana. Watu wana ugumu wa maisha. Shule za Kimataifa (International School)
ipo moja tu. Maana yake watu wengi wamelogwa akili hawawezi kuona fursa ya
biashara iliyoko mbele yao.
MIGOGORO; migogoro ya wakulima na wafugaji ina pelekea kumwaga damu, hakuna maelewano kati ya wananchi wa kawaida na wafugaji. Wakulima wakilima mazao yao mifugo inapitishwa kwenye mashamba. Wakulima wakiwakamata wanyama wanaua hata kusababisha ugomvi. Hayo yote yana sababishwa na maji yasiyofaa ya rohoni yenye kuleta kuzaa mapooza.
Platform Ministry wakiongoza nyimbo za kuabudu katika ibada ya leo. |
MIGOGORO; migogoro ya wakulima na wafugaji ina pelekea kumwaga damu, hakuna maelewano kati ya wananchi wa kawaida na wafugaji. Wakulima wakilima mazao yao mifugo inapitishwa kwenye mashamba. Wakulima wakiwakamata wanyama wanaua hata kusababisha ugomvi. Hayo yote yana sababishwa na maji yasiyofaa ya rohoni yenye kuleta kuzaa mapooza.
·
MAFURIKO; kila mwaka mafuriko yanapotokea
kuna watu wanakufa kwa maji, mali za watu zinaharibika mifugo na mazao
yanaharibika kutokana na mafuriko, pia aina nyingine ya mafuriko yanayochukua
kazi za watu afya za watu kwa sababu ya ile roho inayoleta kuzaa mapooza.
Maji haya ni ya rohoni, Elisha
aliletewa chombo ndani yake kulikuwa na chumvi, akaenda kwenye chanzo cha
mapooza akarusha chumvi na akasema “Bwana
asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza”.
Bwana anasema leo katika jina la Yesu anatangaza, analituma neno la Bwana
liende kwenye kazi, biashara, ndoa kama kuna roho ya kuzaa mapooza inaondolewa kwa
jina la Yesu, nuru ikaangaze mbele yako kwa jina la Yesu.
Morogoro hakuna maji; lakini hapo
mwanzo maji yalikuwa yanatiririka kwenye milima kuelekea mabondeni, lakini sasa
hakuna maji yanayotiririka tena milimani. Morogoro wa imekumbwa na magonjwa ya
ajabu ajabu kama vile kipindupindu, lakini watu wa Morogoro si wachafu.
WAKOMBOAJI
WA MJI
Watu wanao ukomboa mji, si watu wenye
fedha sana, si waliotoka kwenye ukoo mzuri, au wamesoma sana, au wanakaa kwenye
nyumba nzuri, bali ni wale wenye utayari, wako tayari kujihatarisha kwa ajili
ya kuukomboa mji, ni watu waliochoka kukaa kwenye hali fulani na wakaamua
kupiga hatua kuelekea kwenye utatuzi wa matatizo, ni mashujaa wa imani
waliojipanga kuvipiga vita kwa ajili ya miji yao.
Mamia ya mashujaa waliompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. |
Neno
kuhusuru maana yake ni kuzungukwa au kuzingirwa na hakuna mtu kutoka nje wala
kuingia ndani, hakuna chochote kupita kutoka nje au kuingia ndani. Shida ya
kuzungukwa huwezi kupata hela, wala chakula, ndicho kilichotokea kwa wana wa
Israeli. Watu hawa walizungukwa pande zote na adui hawakuwa mpaka wakaishiwa
chakula.
Mfalme wa Shamu aliizunguka na kuihusuru
Samaria njaa ikawa kubwa sana katika mji, njaa ilipozidi wakakosa chakula hata
kufikia kutokosa watoto kwa ajili ya kuwala. Mfalme aliposikia haya alirarua
mavazi yake akapaza sauti yawezekanaje kuwepo na nabii katika mji huu na watu
wafe kwa kukosa chakula? Akaagiza mtu akilete kichwa cha Elisha kama asipotoa
unabii juu ya mji wa samaria. Hapa tunajifunza kuwa kuna baadhi ya majibu
yanapatikana kwa mtumishi wa Bwana pekee.
Kuna mambo ambayo wafalme wanaweza
kuyafanya na mengine hawawezi, kuna mambo ambayo Raisi anaweza kuyafanya
mengine hawezi, kuna mambo ambayo baba yako anaweza kukutendea lakini mengine
hawezi. Lakini nakutangazia yupo mfalme Yesu hapa anaweza kukusaidia tena na
kukutoa kwenye roho ya kuzaa mapooza kwa jina la Yesu.
Ukiwa
mtumishi wa Bwana ni lazima uombe mpaka mtu afunguliwe, kuna watu wanaumwa na wengine wamechizika wapo milembe ndio
maana Mungu anataka watu kama wewe ili
uwasaidie watu wapate kuwa huru
kwa jina la Yesu.
WATU WENYE UKOMA. Ni kawaida sana kwa watu wanyonge
kudharauliwa. Usiogope kukataliwa kwako kwa sababu Mungu anakuandaa kuwa
shujaa. Ni wewe utakayetumika kuleta ukombozi wa familia, ukoo, kanisa na jamii
kwa ujumla. Pamoja na ukoma wao, hawa ndio waliotumika kuleta ukombozi wa mji.
Watu hawa wakasema Haya, na tuliendee jeshi. Wakoma hawa wanatufundisha nguvu
ya kuthubutu kuanza jambo. Hii ni tabia watu mashujaa. Kumbe ukithubutu
kufanya, wale waliokuzuia watakimbia wao wenyewe. Mtu huyu akitembea anakuwa na
kishindo kikubwa kwa uwezo wa Bwana. Kuna faida ya kuchukua hatua ili
kuzimiliki Baraka zako.
“Elisha
akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii,
kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa
shekeli, langoni pa Samaria. Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea
mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya
madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe
utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. Basi walikuwapo watu wanne wenye
ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?” 2
WAFALME 7:1-4
Muumini akifunguliwa katika ibada ya leo. |
“Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna
njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende
tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa
tu. Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami;
na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. Kwa maana Bwana alikuwa
amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi,
kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli
amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. Kwa
hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi
zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate
kujiponya nafsi zao. Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo,
waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na
mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile
vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. Ndipo wakaambiana, Mambo haya
tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata
kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba
ya mfalme. Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika
kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila
farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. Na
mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme. Mfalme akaondoka usiku,
akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami.
Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni,
wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini. Na
mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na
watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa
kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama
mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone. Basi wakatwaa
magari mawili na farasi zake; mfalme akawatuma kuwafuata Washami, akasema,
Enendeni, mkaangalie.”
2 WAFALME 7:5 - 12
Children Ministry wakimchezea Bwana Yesu katika ibada ya leo. |
“Wakawafuata mpaka Yordani; na kumbe! Njia
yote ilikuwa imejaa mavazi na vyombo, walivyovitupa Washami, wapate kukimbia
upesi. Watu wale waliotumwa wakarudi, wakamwambia mfalme. Basi watu wakatoka,
wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa
shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la Bwana.”
2 Wafalme 7:15-16”.
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA
NASI KUPITIA
FACEBOOK:
Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow
us on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson Zacharia
TEL:
+255 719 798 778
(WhatsAssp
& SMS only)