GLORY OF CHRIST
TANZANIA CHURCH (GCCT)
KANISA LA UFUFUO NA
UZIMA MOROGORO
PASTOR, DR. GODSON
ISSA ZACHARIA
JUMAPILI 15 APRILI
2018
Utangulizi:
Kamba ni silaha inayotumika kufungia vitu katika ulimwengu wa kawaida.
Lakini pia katika ulimwengu wa roho nako kuna kamba kama silaha za kishetani. Kamba
ya kuzimu yaweza kuwa jini, pepo, mizimu na majoka. Haya yote yanatumika ili
kufunga maisha ya mtu ili asifike kwenye hatima yake. Maandiko yanatuelezea
kuhusu kamba za kuzimu na kamba za mauti.“Nitamwita
Bwana astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu. Maana mawimbi ya
mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti
ikanikabili. 7 Katika shida yangu nalimwita Bwana, Naam, nikamlalamikia Mungu
wangu; Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia
masikioni mwake”. 2 Samwel 22:4 – 6
Tunajifunza kwamba kuna kamba za kuzimu, hii ina maanisha kamba hizi
zilitoka kuzimu, na chanzo chake ni kuzimu. Kamba hizi sifa yake ya pili
zinauwezo wa kuzunguka.
Kuzimu ni wapi? Kuzimu ipo hapa hapa dunia. Shetani alipohasi mbinguni
alitupwa hata nchi naye akatengeneza mahali alipoweka ufalme wake ambapo
panaitwa kuzimu. Kuzimu ni shimo lenye giza, ni shimo la mashetani, na
halionekani katika macho ya mwilini ila lipo katika ulimwengu wa roho. Kuzimu au shimo la shetani ni mahali mashetani,
mapepo, nyoka yanakaa. Pia wachawi na waganga wa kienyeji ni mahali wanapoenda
kutafuta mapepo, majoka, majini ili wayatumie kuwaangamiza watu wengi duniani.
Kamba ni nini? Kamba za kuzimu
ni majoka, mashetani, mizimu, zinakuja katika ulimwengu wa roho kama kamba na
matokeo yake yanaoneka katika ulimwengu wa mwili. Mashetani, majoka na mizimu
wanakuja duniani kufunga kazi, ndoa, biashara, shule na matokeo yake
yanaonekana katika ulimwengu wa mwilini.unapoona mwanafunzi anashindwa masomo
maana yake kuna kamba za mauti zinatenda kazi.
“Kamba za kuzimu zilinizunguka,
Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita Bwana, Na
kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu
kikaingia masikioni mwake.” Zaburi 18:5 - 6
Daudi alisema maneno hayo si kwa sababu aliona kamba ya kudu/au ya
mnazi. Bali aliona kamba katika ulimwengu wa roho. Mambo yake yalikuwa
hayasogei. Kamba hizi si za mwili, ni za rohoni hazionekani kwa macho ya mwili.
Kamba za mauti, kuzimu, hapa tunajifunza kamba inafunga kwanza ili
uangamizwe na mitego ya mauti inakukabili. Kamba inatumika kama mtego ili
ukinaswa uweze kuliwa. Kuzimu zinafanya kazi pamoja na mauti.
“Nikaona, na tazama, farasi wa
rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu
akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na
kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi”. Ufunuo 6:8
Yohana aliona maono farasi wakijivujivu na amepandwa na abiria
mwenyewe ni mauti na nyuma anafuatana na kuzimu. Mauti na kuzimu ndizo nguzo
kubwa mbili za shetani anazotumia ili kuangamiza watu. Kamba hizi si kamba za
kibinadamu bali ni za rohoni, mashetani yanaweza kugeuka na kuwa kitu chochote.
Wanaweza kugeuka wakawa kifuu cha nazi, paka, mwanaume mzuri au gari na
wewe ukapanda kumbe ni shetani.
Viumbe vya roho wanayo sifa ya kugeuka na kuvaa maumbo.
“Bwana akasema, Ni nani
atakayemdanganya Ahabu, ili akwee RamothGileadi akaanguke? Basi huyu akasema
hivi; na huyu hivi. Akatoka pepo, akasimama mbele za Bwana, akasema, Mimi
nitamdanganya. Bwana akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo
wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki
pia; ondoka ukafanye hivyo”. 1Wafalme 22:20 – 22
Pepo alikwenda kwenye kikao cha Mungu, Mungu alikuwa anauliza ni nani
atakaye enda kumdanganya mfalme Ahabu.
Pepo akasema yeye atakwenda, Mungu akamuuliza jinsi gani atakavyo mdanganya?
Pepo akasema ataondoka na kuwa pepo wa uongo kwenye vinywa vya manabii wote. Hivyo
pepo wanao uwezo wa kugeuka na kuwa namna wanavyotaka kuwa, wanaweza wakawa
uvimbe, au ugonjwa wowote. Pepo anaweza kuwa kamba na kuingia kwako ili wafunge
ndoa, shule, kazi n.k.
Kazi ya kamba ya kuzimu. Kamba
hizi asili yake ni kuzimu
Ø
Kumfunga
mtu; Kufungwa maana yake ni kuondolewa uhuru wa kutenda. Au kuondolewa
uwezo wa kitu ulichokuwa unakifanya hapo awali. Akifungwa mtu anakuwa
ameondolewa uhuru. Ukisikia mtu amefungwa magereza maana yake ameondolewa uwezo
wake wa kutenda kama atakavyo. Kama alikuwa anaweza kuamua ale au avae nini
lakini kamba ikiwepo hawezi kuamua tena.
Mtu anapofungwa anaondolewa
uhuru wa kuomba, ukifungwa akili unakuwa huwezi kufanya maamuzi ya haraka
haraka ya maisha yako. Kazi ikifungwa huwezi kuona kazi mbele yako. Zinafunga
kazi, fedha, kuoa, kuolewa, biashara. Unakuta kijana amemaliza shahada ya kwanza
anakaa kwa mjomba anaangalia Tv lakini hafikirii hata kujishughulisha na kazi
ndogo ndogo.
Wengine wameondolewa uwezo wa
kutunga mimba, uwezo wa biashara, unaondolewa uwezo wa kutenda yale unayotaka kufanya.
Kuzimu inakufahamu inaweza kufungwa uso, macho, akili n.k. Kwa jina la la Yesu
ewe kamba ya kuzimu uliyotumwa ukae kwenye uso, mikono, miguu leo nakutangazia na
kufungua leo kwa jina la Yesu. Mwovu (ibilisi au abadoni au apolioni) akitaka
akuangamize haraka na vizuri anakufunga
kwanza ili usifurukute.
“Akatoka tena katika mipaka ya
Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya
mipaka ya Dekapoli. Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee
mikono. Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake,
akatema mate, akamgusa ulimi, akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia,
Efatha, maana yake, Funguka. Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi
wake kikalegea, akasema vizuri.” Marko 7:31 – 35
Hapa tunajifunza kamba za
kuzimu zilikuwa zimemfunga ulimi na masikio yake. Hapa tunajifunza kamba
zinauwezo wa kufunga sehemu mbalimbali za mwili, macho, miguu, mikono. Anayekufunga
ni mwovu. Na kila mtu atafungwa kulingana na sehemu ya umahili wake.
“Aliyeufanya ulimwengu ukiwa,
akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?” Isaya 14:17
Ilimpasa kila mmoja kuwa makini maana Mkono wa Bwana ulipita katikati ya makutano ili kuzifungua kamba za kuzimu. |
Ukiwa umefungwa unakosa uhuru wa kuchagua kitu cha kufanya. Mfano kila
mtu ameamua kuvaa nguo uliyovaa, lakini kuna mwingine amefungwa mapato amevaa
nguo aliyovaa ni kwa sababu huna namna bali umevaa. Au mwingine anakula chakula
si kwa sababu anakipenda ni kwa sababu hana mapato ya kununua ukipendacho. Unakuta
mtu mwingine amesoma na ana shahada mbili anashindwa kuandika hata maandiko ya
mradi ni kwa sababu akili imefungwa. Anakubali kuwa mkusanyaji takwimu. Huyu anakuwa
amefungwa kamba katika akili. Aliyefunga ndiyo mwenye uwezo wa kukufungua na
asipotokea mwenye nguvu kuliko yeye hakuna wa kukufungua.
“Amin, nawaambieni, yo yote
mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua
duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” Mathayo 18:18
Akipatikana mwenye nguvu kuliko yeye ataweza kukufungua kamba. Shetani
akikukufunga kwa muda mrefu, unakuwa na mazoea yaleyale ukifunguliwa unawaza
bado umefungwa. Unatakiwa utoke uende kutafutafuta, mfano kuandika barua za
kuomba kazi. Mungu alijua watu wamefungwa akamtoa mwanae wa pekee ili aje
afungue wafungwa waende zao.
“Roho wa Bwana yu juu yangu,
Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,
Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza
mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” Luka 4:18-19
Katika Biblia Daudi amepitia vifungo vingi vya kamba. Kamba za kuzimu
wakati mwingine ni kamba za mauti. Kamba hizi zinaweza kumfunga mtu aliye hai
na akaanza kupata matatizo na kuelekea kufa.
“Kamba za mauti zilinizunguka,
Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;” Zaburi 116:3
Kamba za mauti zikikupata unaanza kupata na taabu za kuzimu. Kamba
ikifungwaa unaishia kupata mimba na kutoka, unapata kazi na kufukuzwa, unaanza
biashara inakufa.
“Kamba za
mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.” Zaburi 18:4
Kamba za mauti zinatakiwa zikatwe, na kamba za
kuzimu zinatakiwa kufunguliwa. Kamba za kuzimu zinamfanya mtu asiweze kabisa. Unafungwa
kwenye ndoa, unafungwa kwenye elimu unafungwa kila mahali. Kamba za mauti
zikija una pata mafuriko ya uovu, unapata taabu, maumivu, mafuriko ya uovu. Mafuriko
ni kitu kinakuja kwa wingi na hakipimiki. Maovu yakiwa mengi unapata hofu, na
hatimaye unakufa. Watu wengi wameharibikiwa ni kwa sababu wanapata hofu ya
mambo yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Kuna mwingine anapata hofu ya usiku.
“Kwa kuwa
hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa
wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.” Warumi 8:15
Hofu haitoki kwa Mungu, bali ni roho inayotoka kwa
shetani. Kwa sababu hiyo Mungu alimtoa Yesu Kristo ili aje kufungua kamba za
kuzimu.
“Basi, kwa
kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo
hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani,
Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa
katika hali ya utumwa.” Waebrania 2:14 -15
Mungu alimaua kumleta Yesu akaja kwa mwili na nyama
kupitia mauti yake Yesu Kristo ili aweze kuharibu zile nguvu za mauti alizokuwa
nazo shetani. Unakuta mtu anapewa msaada anakataa ni kwa sababu alipitia shida
nyingi sana anakataa anahisi ni mtego anakuwa na hofu. Kamba za uso, kamba za
mikono, kamba za mizimu ya ukoo/familia kwa jina la Yesu nazifungua leo kwa
jina la Yesu. Japo kamba zimetoka kuzimu ila Bwana ametupa uwezo wa kufungua
kamba hizo, ufungue familia yako ufungue watoto wako kwa jina la Yesu.
“Nami
nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu;
wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na
lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.” Mathayo
16:18 – 19
Hapa maandiko yanatuambia kuzimu ina milango, kwa
hiyo kamba zinaruhusiwa kupita kwenye malango hayo. Bwana amesema atakupa
funguo za kufunga malango hayo.
Yesu alitumwa ili kuwafungua walio fungwa na kuwaweka huru. Binti huyu alifunguliwa kutoka kamba za kuzimu na mauti. |
“Bali wote
waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio
jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi
ya mtu, bali kwa Mungu.” Yohana 1:12-13
Ukizaliwa na Bwana utapewa ufunguo. Hapa tunaona
ukifanyika kuwa mtoto wa Mungu utapewa funguo ya kufungua kamba za mauti, kamba
za kuzimu.
Utazaliwaje? Mtu
anazaliwa mara ya pili kwa kumpokea Yesu kuwa na BWANA na Mwokozi wa maisha
yake.
“Kwa sababu,
ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya
kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata
kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Warumi 10:9-10
Hawa ni baadhi ya Makutano waliokuwa tayari kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. |
Ukimpokea na
ukimkiri Yesu kwa kinywa chako
unapata uwezo wa kufungua kamba za mauti. Yamkini kuna kamba mpya, ambazo
hujazijua bado wamezitumia hatimaye umeharibikiwa na kuibiwa. Ukimpokea Yesu
anakupa funguo itakayofungua kila kitu, ambapo lolote utakaloliomba utalipokea
kwa jina la Yesu. Fungua kamba na vitu vyako vyote ukafanikiwe kila mahali kwa
jina la Yesu.
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA
NASI KUPITIA
FACEBOOK:
Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow
us on INSTAGRAM: pastordrgodson
TEL:
+255 719 798 778