Utangulizi: Somo la Ibada ya leo linaitwa “Madhabahu Imepasuka”.
Neno madhabahu ni daraja
linalounganisha ulimwengu wa mwili na
ule ulimwengu wa roho. Wanadamu wote tunaishi
katika ulimwengu wa vitu vinavyoonekana,
ambao ni ulimwengu wa mwili. Upo pia ulimwengu wa roho ambao ni ulimwengu wa vitu
visivyoonekana.
Ulimwengu wa vitu visivyoonekana ndio uliosababisha
ulimwengu wa vitu vinavyoonekana. Wakazi wa ulimwengu usionekana hawawezi
kuonekana kwa macho ya kawaida, si kwa sababu ni wadogo, la hasha!!. Dunia na vyote vyenye kuonnekana vimetokea
kutokana na ulimwengu ule usioonekana. Mungu (ambaye ni roho) ndivyo alivyoumba dunia na viumbe vyote
kwa njia hii, kwa neno lake.
Matukio yote yanayotokea katika ulimwengu wa mwili yanakuwa na asili yake kutokea kwenye ulimwengu wa roho. Mungu (kwa sababu ni roho) akitaka kukuletea Baraka wewe huhitaji DARAJA ambalo Mungu atalitumia kukufikia. Daraja hili ndilo huitwa MADHABAHU. Madhabahu huwepo ili pasiwepo kizuizi cha mtu na Mungu katika kufanya mawasiliano. Mawakala wa Mungu ni kama wachungaji ambao husimama katika madhabahu za Mungu kuleta ujumbe wa Mungu maishani mwa mtu. Madhabahu za Mungu humsogeza Mungu sana karibu na watu wake.
Kwa sababu shetani ndiye 'mungu wa madhabahu za uharibifu'. Ikumbukwe kuwa, ndani ya madhabahu mipango ya Baraka au Uharibifu hufanyika.
Katika kila madhabahu, yupo KUHANI wa madhabahu. Huyu hukaa katikati kuunganisha pande zote mbili. Endapo umekuwa unaombewa kanisani, na ukeshapata nafuu hali ile ya zamani inakurudia tena, ujue kuna kuhani wa madhabahu anayesimamia hali yako hiyo.
MWANZO 1:1-27... Utaona Mungu alitamka tu maneno,
na ikawa hivyo jinsi alivyotamka. Mungu alianzia na
yasiyoonekana na kufanya kuwepo kwa vinavyoonekana. Ulimwengu wa roho una viumbe
wake ambao hatujawahi kuwaona kwa macho, ni
kama vile, Mungu, malaika watakatifu, malaika wachafu, mashetani n.k.
Matukio yote yanayotokea katika ulimwengu wa mwili yanakuwa na asili yake kutokea kwenye ulimwengu wa roho. Mungu (kwa sababu ni roho) akitaka kukuletea Baraka wewe huhitaji DARAJA ambalo Mungu atalitumia kukufikia. Daraja hili ndilo huitwa MADHABAHU. Madhabahu huwepo ili pasiwepo kizuizi cha mtu na Mungu katika kufanya mawasiliano. Mawakala wa Mungu ni kama wachungaji ambao husimama katika madhabahu za Mungu kuleta ujumbe wa Mungu maishani mwa mtu. Madhabahu za Mungu humsogeza Mungu sana karibu na watu wake.
Vivyo hivyo, kanuni hii
pia hutumiwa na shetani (kwa sababu shetani ni
roho) kuweza kuingia hapa duniani na kufanya kazi zake za
uharibifu. Shetani anahitaji daraja la
kumfanya aingie katika mipango ya maisha
yako. Shetani haji hapa duniani ili kukuletea Baraka maishani
mwako. Imeandikwa katika YOHANA 10:10… [Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.]….
Shetani ili aweze kufanikisha uharibifu
huu, anahitaji Madhabahu. Shetani naye anao mawakala wake ambao ni wachawi, waganga wa
kienyeji, wasoma nyota n.k . ambao nao kazi zao ni kuleta uharibifu maishani mwa
watu. Madhabahu za shetani humsogeza mtu karibu na shetani.
Katika Biblia madhabahu ziliwahi kujengwa. Wafuatao walijenga madhabahu kwa ajili ya Bwana:-
- NUHU: Mwanzo 8:20...[Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.]
- MUSA: Kutoka 17:15 ..[Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yehova-nisi* (Yehova-nisi maana yake ni Bwana ni bendera yangu); akasema, Bwana ameapa; Bwana atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.]...
- IBRAHIMU: Mwanzo 12:7..[Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea.]...
KWA
NINI TUNAOMBA ILI MADHABAHU HIZI ZIPASUKE?
Kwa sababu shetani ndiye 'mungu wa madhabahu za uharibifu'. Ikumbukwe kuwa, ndani ya madhabahu mipango ya Baraka au Uharibifu hufanyika.
Katika kila madhabahu, yupo KUHANI wa madhabahu. Huyu hukaa katikati kuunganisha pande zote mbili. Endapo umekuwa unaombewa kanisani, na ukeshapata nafuu hali ile ya zamani inakurudia tena, ujue kuna kuhani wa madhabahu anayesimamia hali yako hiyo.
Madhabahu inayo KAFARA, ambayo ni chakula cha
madhabahu. Kwetu sisi wakristo, hatuna
haja tena ya kutoa sadaka za wanyama ili
kuwa kafara kwa sababu YESU Kristo tayari alifanyika Kafara ya mwisho.
Kinachotokea kwa mtu amabaye anaombewa na hali yake ya zamani kumrudia tena ni kuwa, wachawi huongeza nguvu kwa kutoa kafara nyingine kubwa kuliko ile ya awali. Matokeo yake ni kuwa mtu anarudiwa na hali yake ya zamani, na anapokuja kuombewa tena kafara ya Bwana Yesu hufanya kazi upya tena. Sadaka ya Madhabahu husababisha NGUVU ya Madhabau kuongezeka.
Wachawi wanapoona shida yako imeisha kwa sababu ya maombi yako, huongeza sadaka, na hata ile shida ambayo ilikuwa imeondoka humrudia huyo mtu tena. Pengine mtu alikuwa anaumwa mguu, na sadaka iliyokuwa imetolewa ni njiwa. Wachawi huongeza ukubwa wa sadaka, pengine mara hii wakamtoa ng’ombe, na ile shida ya mguu huongezeka na kuwa siyo mguu tu, bali pamoja na mgongo. Katika vikao vyao, wachawi hujadiliana ni sadaka ya aina ipi itafuatia endapo mguu na mgongo wake mtu huyu vitaponywa kutokana na maombi. Ndiposa wachawi huamua kutoa 'sadaka ya mtu'.
Kinachotokea kwa mtu amabaye anaombewa na hali yake ya zamani kumrudia tena ni kuwa, wachawi huongeza nguvu kwa kutoa kafara nyingine kubwa kuliko ile ya awali. Matokeo yake ni kuwa mtu anarudiwa na hali yake ya zamani, na anapokuja kuombewa tena kafara ya Bwana Yesu hufanya kazi upya tena. Sadaka ya Madhabahu husababisha NGUVU ya Madhabau kuongezeka.
Wachawi wanapoona shida yako imeisha kwa sababu ya maombi yako, huongeza sadaka, na hata ile shida ambayo ilikuwa imeondoka humrudia huyo mtu tena. Pengine mtu alikuwa anaumwa mguu, na sadaka iliyokuwa imetolewa ni njiwa. Wachawi huongeza ukubwa wa sadaka, pengine mara hii wakamtoa ng’ombe, na ile shida ya mguu huongezeka na kuwa siyo mguu tu, bali pamoja na mgongo. Katika vikao vyao, wachawi hujadiliana ni sadaka ya aina ipi itafuatia endapo mguu na mgongo wake mtu huyu vitaponywa kutokana na maombi. Ndiposa wachawi huamua kutoa 'sadaka ya mtu'.
Hata hivyo,
hata kama wachawi watatoa sadaka za mamia ya watu, hazitaweza kuizidi ile kafara ya YESU, kwa
sababu "Yesu alikuwa mtakatifu", hakuwa na
dhambi. Hata kama wachawi watasababisha ajali na kuua watu wote kwenye basi, hizo bado ni sadaka za watenda dhambi,
walevi, wezi n.k. ambazo haziwezi kulinganishwa na ile kafara ya Bwana Yesu Kristo ya pale msalabani.
Leo tunaifuata hiyo madhabahu na kuipasua ili isiwepo
kabisa kwa Jina la Yesu. Madhabahu hizi zikeshapasuka, wachawi hawatakaa waione tena madhabahu yao ya uharibifu. Mfano mzuri: Ukitaka kuzuia au
kumaliza magari yote ya 'Toyota' hapa duniani kote, itakuwa kazi bure kuanza
kukusanya na kuharibu magari ya Toyota dunia nzima. Cha kufanya ni kupanda
ndege na kupasua pasua mitambo yote ya magari haya kule kule Japan. Leo tuna
kazi moja tu ya kufanya. Kazi yenyewe ni
kupasua madhabahu za shetani.
Yupo Mfalme
aliyewahi kujenga madhabahu za kuwatesa wana wa Israeli, jina lake ni Yeroboamu. Imeandikwa:
1
WAFALME 12:25-27 …[Ndipo Yeroboamu
akajenga Shekemu katika milima ya Efraimu, akakaa huko. Akatoka huko akajenga
Penueli. 26 Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya
Daudi. 27 Kama watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana
huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu,
mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. 28
Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu,
akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo
miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. 29 Akamweka
mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani. 30 Jambo hili likawa
dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani. 31
Tena akafanya nyumba za mahali pa juu, akafanya na watu wo wote, watu wasio wa
wana wa Lawi, kuwa makuhani. 32 Yeroboamu akaamuru kushika sikukuu katika mwezi
wa nane, siku ya kumi na tano ya mwezi, mfano wa sikukuu iliyokuwa katika Yuda,
akapanda juu ili kuiendea madhabahu. Akafanya vivyo katika Betheli akiwatolea
dhabihu wale ng'ombe aliowafanya; akawaweka katika Betheli wale makuhani wa
mahali pa juu alipokuwa amepafanya. 33 Akatoa dhabihu juu ya ile madhabahu
aliyoifanya katika Betheli, siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, mwezi
aliouwaza moyoni mwake mwenyewe; akawaamuru wana wa Israeli waishike sikukuu
hiyo, akapanda kuiendea madhabahu, ili kufukiza uvumba.]…
Yeroboamu alibaini kuwa endapo wana
wa Israeli wataendelea kwenda Yerusalemu kuomba watakuja baadae kumuua, na
kutafakari cha kufanya, kwa kutengeneza 'miungu wawili wa dhahabu'. Kwa nini alitumia dhahabu" Alitumia dhahabu kwa sababu ni madini yanayotamaniwa
sana na watu, tena yenye thamani. Madhabahu hii ilisababisha
chukizo kwa Mungu, na kitendo cha watu
kuiabudu miungu hii, matatizo yao
ya awali yakawarudia upya kwa sababu walimuacha Mungu wa ukweli.
MAOMBI:
Leo, tunazipasua madhabahu, zilizotengenezwa kwa mikono ya waovu, kwa Jina la Yesu. Amen
|
1
WAFALME 13:1-10…[Na tazama,
akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye
Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. 2 Basi mtu huyo
akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu,
madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi,
jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza
uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako. 3 Akatoa ishara siku
ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na
majivu yaliyo juu yake yatamwagika. 4 Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia
maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli,
alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake
aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena]….
Kunyoosha mkono kwa huyu mfalme ni sawa na kitendo cha wachawi wanapotamani
kukuadhibu wewe unapoomba kinyume nao.
MAOMBI:
Ninaamuru kwa Jina la Yesu, wanaokunyooshea mateso
mikono yao ikatike kwa Jina la Yesu, wanaokunyooshea taabu mikono yao ikatike
kwa Jina la Yesu, wanaokunyooshea shida,
mikono yao ikatike kwa Jina la
Yesu. Amen
|
1
WAFALME 13:5-6…[Madhabahu
ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu
wa Mungu kwa neno la Bwana. 6 Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu,
Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena.
Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama
ulivyokuwa kwanza.]… Ukitaka kumkamata aliyetumwa utakatika mkono. Ukitaka
kumkamata mchungaji utakatika mkono. Ukitaka kumkamata RP utakatika mkono. Ukitaka
kumkamata AP utakatika mkono. Ukitaka kumkamata MP utakatika mkono. Ukitaka
kumkamata Shepherd utakatika mkono. Ukitaka kumkamata MP utakatika mkono. Ukitaka
kumkamata Shepherd utakatika mkono. Ukitaka kumkamata Shepherd on Training utakatika
mkono. Ukitaka kumkamata Potential Shepherd utakatika mkono.
Leo tunaiweka adhabu. Wale wale waliokutesa waje na kuomba ili
uwaombee‼ Lazima wafike mahali pa kujua kuwa, madhabhu zikeshapasuka,
mikono yao haitaweza kurudishwa na
wachawi wenzao tena. Kama madhabahu hii
isinekuwa imepasuka, mfalme huyu
angeendelea na kiburi chake.
Musa alikumbana na kisa cha madhabahu za kichawi kama hizi. Alipotengeneza nyoka, Farao
na wachawi wake wote walitengeneza vijoka vyao tena vingi. Kila muujiza ambao
Musa aliufanya mbele ya Farao, wachawi wake nao waliufanya vivyo hivyo. Mungu
alipoona kuwa 'tegemeo la hawa watu' ni
wazaliwa wao wa kwanza ambao
huwatumia kwenye kafara zao za kichawi,
basi aliamuru kuua kila mzaliwa
wa kwanza wa Misri ili pasiwepo tena sadaka ya madhabahu zao za kutumia wazaliwa wao wa kwanza!!.
Madhabahu inayoleta uharibifu kwako ni muhimu
ipasuke siku ya leo. Usikubali uingie nyumbani
mwa Bwana na kurudi nyumbani
kwako na ile madhabahu inayotengeneza shida yako kila wakati.
Leo tunataka mtunza madhaabhu aone jinsi hiyo
madhabahu inavyopasuka. Kumbuka kwamba, imeandikwa kuwa “Hamjui kuwa miili yenu
ni mahekaluya roho mtakatifu?” Endapo mtu ni
mtenda dhambi, Mungu hutoka ndani mwake, na badala yake wachawi huweka
kituo ndani ya mwili wa mtu huyo kwa njia ya roho za mashetani.
MAOMBI:
Asante Bwana Yesu kwa kuniwezesha kuweko
nyumbani mwako leo. Asante Yesu kwa kuniokoa siku ya leo. Amen
|
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Kihonda VETA, Morogoro.
/or
Contact our Senior Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778