Monday, October 20, 2014

Ushuhuda wa FATUMA-Binti wa Miaka 8 Aliyedondoshwa na Ungo 15 Oktoba 2014

THIS IS MY STORY (USHUHUDA WA FATUMA SHABANI) - JUMAPILI 19/10/2014

Utangulizi
Fatuma Shabani (8) yupo darasa la kwanza, Morogoro maeneo ya Kihonda (jina la Shule tunalihifadhi). Alianza kutumikishwa kwenye uchawi akiwa na umri wa miaka minne tu bila hata wazazi wake kujua. 


Fatuma Shabani akifafanua jinsi ungo ulivyomdondosha
chini hapa Kihonda, Morogoro Jumatano tarehe 15/10/2014 

Ilikuwaje Fatuma kuletwa Kuombewa Kanisani? 

Siku ya Jumatano 15 Oktoba 2014, muda wa mchana, Fatuma alidondoshwa na wachawi watatu karibu na shule ya St. Monica, Kihonda. 


Hiyo  siku wote walikuwa njiani wakitafuta (kuwinda) nyama ya mwanadamu. Fatuma anasema walipokaribia maeneo ya hili Kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro, chombo chao kilikosa mwelekeo na yeye akadondoshwa chini kwenye hili eneo ambalo lipo karibu sana na Kanisa hili.


Maisha ya Kufanya Uchawi Yalianza je?

Fatuma anasema matatizo yake yalianzia Kihonda Magorofani (Morogoro), akiwa na baba yake mzazi ambaye alikuwa tayari ameshaachana na mama yake mzazi. Siku moja  alikuwa akitoka shuleni na kumkuta bibi mmoja ajulikanae hapo mtaani kwao kama Bi Mkaa. Huyu bibi alikuwa amebeba kimfuko chenye sukari ndani yake, akataka kumtuma Fatuma ili aipeleke hiyo sukari nyumba ya jirani. Hata hivyo Fatuma alikataa,  akimwambia huyu bibi aende mwenyewe au la sivyo amtume binti mwingine aliyekuwa ameongozana naye!!,


Maajabu ni kuwa Bi Mkaa alikataa kufanya hivyo, kwa kisingizio kuwa huyo binti mwingine hana akili kama za Fatuma!!!! Ili kuthibitisha hili  jambo,  huyu Bi Mkaa alizichukua kwa nguvu daftari za Fatuma na kulisoma daftari mojawapo, na kuanza kumwambia 'wewe ndio  mwenye akili'. Baada ya mabishano, hata hivyo Fatuma alimkubalia kuibeba ile sukari, na kuipeleka kwenye ile  nyumba  ya jirani aliyoelekezwa. 


Pindi tu alipofika ndani ya hii nyumba, alikutana tena na Bi Mkaa akiwa tayari yumo ndani ameketi!! Fatuma ilibidi amuulize swali 'imekuwaje umeshafika huku wakati tuliachana kule njiani?' Huyu Bi Mkaa akakataa kuwa hiyo siku hakuonana naye, akisingizia kuwa pengine aliyekutana na Fatuma njiani ni pacha wake anayefanana naye!!.



Fatuma Shabani akieleza jinsi ile nyumba ya wachawi
waliomteka ilivyokuwa imejaa 'misukule'
Ndani ya nyumba hii hali iko je?

Ndani  ya nyumba hii kulikuwemo watoto kama 20 hivi, (wengi wao wakiwa wamekatwa ndimi zao), lakini  mmojawapo wa hao watoto Fatuma aliweza kumtambua kwa jina la Denis, kwani alikuwa rafiki yake hapo mtaani. 


Huyu  Denis hata hivyo alikuwa hajakatwa ulimi. Denis alimshauri Fatuma kuwa asikubali kukaa ndani ya hiyo nyumba na huyo  bibi.  





Nani aliyekata hao watoto ndimi zao?

Fatuma anasema aliyewakata watoto hizo  ndimi zao ni Bi Moto na Bi Majivu. Hawa wawili pamoja na Bi Mkaa walikuwa wamoja katika kazi za uchawi. Bi  Mkaa akatumia  huo wasaa kumwambia Fatuma ajiunge na chama chao cha kichawi, lakini Fatuma akakataa. Kitendo cha kukataa kilimfanya yule bibi kumtishia kuwa atamkata ulimi na kichwa, na ndipo  Fatuma alipolazimika kukubaliana naye ili asipate hiyo adhabu kali kupitiliza!!!.


Fatuma alianza je Kazi ya  Uchawi?

Kwanza kabisa, Fatuma alifanywa kuwa MKUU wa wale wachawi wote. Kisha alitakiwa amtoe mama yake mzazi kafara kwa kumuua!!! Lengo la kufanya hivyo ni ili baadae akomae kwenye hii kazi. Hata hivyo kwa kuwa Fatuma alifanywa kuwa MKUU wa hiyo nyumba, aligoma kumuua  mama yake mzazi.  

Swali: Uliweza je kuwa Mkuu wakati wewe umbile na umri wako bado mdogo?
Jibu: Wakati Fatuma akiwa kule na wachawi, huuvaa mwili wa mtu mzima kabisa, na hivyo hata yule Bi Mkaa na wenzake kuna nyakati wanamuamkia Fatuma kwa heshima ya 'shikamoo'


Kupanda Ungo Je?

Fatuma ameelezea jinsi  walivyokuwa wanapanda ungo  kwa pamoja na wale bibi watatu na wachawi wengineo.  Anasema  wanajikusanya hata kama ni  wengi, na kisha  wataimba wimbo uitwao ‘Ngae’, na ndipo huo ungo hupaa angani.  Wakifika wanapoenda, humbeba mtu mlengwa, watamchezea chezea mwili wake kwa kumdhalilisha, kisha watampitisha kwenye 'pembe ya nyumba' na kwenda naye kumla nyama.



SNP (Dr.  Godson) akiomba kinyume na wachawi wote
wenye kuwateka watu na kuwafanya misukule

Sasa mkeshamla Nyama nini kinafuatia?

Fatuma anasema wakeshamtoa huyo mtu ndani, hubakisha 'kivuli' cha huyo mtu kitandani mwake. Watu  watadhani aliyelala kitandani ni mtu mwenyewe, kumbe ni 'gogo' tu lenye sura ya huyo mtu.  Watu  wakiamka  asubuhi  wanakuta huyo mtu amefariki dunia, na kuanza kulia ovyo!!. 


Endapo watu hawa wataita majirani zao, Bi Moto ambaye ndiye mhusika mkuu hujitokeza, atalia machozi 'kama waombolezaji' wengine na kuwaambia watu  kwamba maadamu huyu mtu amekufa kwa hiyo ni vyema maandalizi ya kumzika yafanyike mara moja!!. Mazishi ya hili 'mtu-gogo' hufanyika haraka haraka, na baada ya mazishi ya huyo mtu ndipo nyama yake huenda kuliwa rasmi.


Fatuma amewataja watu ambao walishaliwa nyama kwa majina yao, na amewakumbuka kama wawili hivi (ambao majina yao tunayahifadhi). Fatuma aliwahi kuhusika na kudondosha magari kwa njia ya ajali, na kusababisha majeraha kwa watu waliokuwemo kwenye hayo  magari.



Hapo Mtaani Fatuma anajulikana je?

Majirani zake walianza kumhisi huyu mtoto kuwa ni mchawi. Wakati mwingine wapo watu waliokuwa wanamuona Fatuma kana kwamba anazo 'pembe' za mnyama kichwani  mwake!! Kitendo hiki kilitishia maisha ya mtoto huyu. 


Waganga wa Kienyeji walisaidia je?

Baada ya maneno na uvumi  wa uchawi wa Fatuma kuenea hapo mtaani, ndipo ambapo wazazi wake walimpeleka huyu mtoto kwa mganga wa kienyeji mtaani kwao ili kubaini tatizo lipo je. Hata hivyo wachawi wale watatu (Bi Mkaa, Bi Moto na Bi Majivu) walimfuata Fatuma huko huko, mganga akawa hawaoni, na kisha wakampa 'kipigo kikali sana' yule mganga wa kienyeji. Kipigo alichokipata mganga huyu kilimfanya awakataze kabisa wazazi wa Fatuma kuwa wasimrudishe tena mtoto huyu nyumbani kwake kuaguliwa!!


Mtaa wake kwa sasa wanamuogopa Fatuma kwa sababu hizi. Wazazi nao wanaogopa kuishi naye kwa sababu wale wachawi wanamfuatilia,  na hapo hapo majirani wanamuwinda ili wamuadhibu kwa kujihusisha na nguvu za giza (uchawi). 



Mamia ya Majeshi ya Bwana yakimponda shetani na mawakala wake (wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota n.k) wanaofanya kazi za uharibifu hapa duniani,  kama ambavyo kamera yetu iliwashuudia wakati Fatuma akitoa ushuhuda wake.



Je Shuleni kwake na Darasani kwake hali ikoje?

Fatuma akiwa darasani wachawi wale wamekuwa wanamfuatilia na kumwambia hii siyo kazi waliyomtuma aifanye. Fatuma anasema zipo siku ambapo Bi Moto hujibadili umbile lake na kukaa  darasani kama mtoto mdogo, kwa hiyo hata mwalimu akimwangalia anadhani ni Fatuma kumbe siyo yeye. Hata mwandiko wa  Fatuma siyo wa kawaida yake, kwa sababu ya kuandikiwa na hawa bibi (Bi Mkaa, Bi Moto na Bi Majivu).


Nini kilitokea Jumatano tarehe 15 Oktoba 2014?

Fatuma anasema walipokatisha tu eneo la Kanisa la Saa ya Ufufuo na Uzima - Morogoro, mchana wa hiyo siku ya Jumatano, chombo chao (ungo) ulikosa nguvu na mwelekeo na kuanza kuyumba. Baadae kidogo chombo hicho kilichosheheni wachawi kilimdondosha chini Fatuma, na wale wengine wakaendelea na safari yao.



Baba (SNP Dr. Godson) akimuuliza Fatuma maswali ili atoe
ufafanuzi wa kilichotokea hadi adondoshwe kwenye ungo.
Alivyookotwa,  Fatuma aliletwa kanisani, na kufanyiwa maombi ya kurudishwa kutoka utumwa wa shetani. Mama mzazi (ambaye awali alishakosa msaada kwa waganga wa kienyeji) ndiye aliyeamua kumleta hapa kanisani. Kanisa limebidi kuchukua jukumu la kumhifadhi huyu mtoto kutokana na vitisho vya majirani zake wakidhani Fatuma ni mchawi kwa kupenda, kumbe alilazimishwa na wachawi kuishi maisha ya aina ile bila hiari yake. 



Mambo aliyoshuhudia Fatuma yalimshangaza sana mama yake mzazi, na hivyo kuamini  kuwa 'hakika katika YESU, kila jambo linawezekana'.


© Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Kihonda VETA, Morogoro.
 /or
Contact our Senior Pastor:
 Dr. Godson Issa Zacharia
 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778

Share:
Powered by Blogger.

Pages