Monday, October 27, 2014

SOMO: MIPAKA ILIYOHAMISHWA-Na:- Dr. Godson Issa Zacharia (SNP)


JUMAPILI: 26 OCTOBER 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Utangulizi: Somo la Ibada ya leo linaitwaMipaka  iliyohamishwa”. Nini maana ya mipaka? Ni  sehemu au mahlai panapoonesha mwisho wa umiliki halali  wa mtu.  Ni sehemu ambapo ndani yake unakuwa na uhalali  wa kuweka utawala wako kwa uhuru bila wasiwasi wowote aukuingiliwa na mtu yeyote. Mfano: Endapo akatokea mwanaume na akamfuata mwanamke (asiye mke wake) na kuanza kumshika pua yake, au masikio yake, utasikia mwanamke huyo akimwambia ‘Ndugu, kwa hapo umevuka mipaka’. Ipo mipaka na  ramani zake hata katika serikali zetu za mitaa.


Baba (SNP Dr. Godson) aliposimama kufundisha kuhusu
Somo "Mipaka Iliyohamishwa",  tarehe 26 Oktoba 2014.

Mungu baada ya kumuumba mwanadamu,  alimpa mipaka yake ya utawala. MWANZO 1:26…[ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.]…Hii ndiyo mipaka aliyopewa mwanadamu kutawala. Vitu vyote katika nchi, angani na baharini.





MWANZO 1:28…[Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.]….Mungu hakumpa mwanadamu mipaka katika kuzaa,  ila aliwaruhusu wazaane hadi nchi iweze kujazwa na wandamu. Aliwapa wanadamu wajibu wa  ‘kutiisha na kutawala’ vyote vyenye uhai. Kila kiumbe chenye uhai tumepewa mamlaka ya kuvitiisha na kuvitawala. Endapo mwanga atarukaruka,  ni wajibu wako kumtiisha na kumtawala. Endapo ni majini,  tuna mamlaka ya kuyatiisha na kuyatawala. Hata kama hicho   kitu kitageuka na kikawa jiwe kikaanza kuongea,  tuna mamlaka ya kukitiisha na kukitawala. Kila mwenye kutawala, Mungu amemuwekea mipaka  ya  utawala wake.


Mungu aliyeumba mbingu na nchi, asingeweza kukuumba wewe na asikuwekee mipaka yako.   YOSHUA 1:3-4…[Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa. 4 Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.]….Maana yake  Mungu akikubarikia watoto, ni wewe tu kuendelea kuwa nao hadi mwisho. Endapo Mungu akikubarikia elimu, unapaswa kusoma tu upate elimu  zote  hadi uamue mwenyewe kutoendelea kusoma.




Baadhi ya Umati wa Majeshi ya Bwana wakisikiliza na kufuatilia kwa makini Somo lililotolewa na
Baba (SNP dr. Godson) Jumapili hii tarehe 26/10/2014 liitwalo "Mipaka Iliyohamishwa"


I KORINTHO 2:9 ….[lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.]… Yaani kama ni  nyumba,  zile alizokupangia Bwana ili uzipate ni nyingi mno na ambazo hata hujawahi kuziwazia. Kutiisha na kutawala ni  vitu viwili tofauti. Kwa kutiisha tu, kile ulichoatiisha lazima kikutii na kuhama. Endapo ni  ugonjwa, unpoutiisha, lazima ugonjwa huo uhame mara moja.


Mipaka ilihamishwa. Pengine wakati ukiwa kwenye disko zamani  hizo, mipaka yako ilihamishwa  enzi hizo.


Je Biblia inazungamza kuhusu mipaka kuhamishwa? ................. Ndiyo.

1. Wachawi  ndio wanaoweza  kuhamisha mipaka, kwa kuwa wao ni  mawakala wa mashetani.


LUKA 4:1- [Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, 2 akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. 3 Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. 4 Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. 5 Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. 7 Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. 8 Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.]… Unaona shetani hasemi  kuwa 'vyote ni vyangu', bali anasema  'vipo mikononi mwangu’ ikimaanisha vile alivyo navyo shetani, alivipokonya kwa mmiliki wake (mwanadamu). Shetani ndivyo alivyohamisha mipaka.


Wachawi wana uwezo wa kuchungulia mipaka ya maisha yako na kuanza kuihamisha. Endapo ni ndoa, wachawi huweza kuhamisha mipaka ya hiyo ndoa. 


Mungu anapokupa uhai wako, afya yako, mali zako, na akaja mtu akataka kuvichukua vilivyo vyako, unapswa kukataa kwa sababu vyote hivyo ni urithi wako kutoka kwa Bwana. Naboth alikataa urithi wake baada ya kubaini umetokana na huzuni zilizosonga mipaka ya huo urithi.


MITHALI 22:28…[Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako.]…


MITHALI 23:10… [Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima;]…


HOSEA 5:10...[Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.]….

MAOMBI
Yeyote aliyehamisha mipaka amwagiwe ghadhabu ya Bwana kwa Jina la Yesu. Amen






Showers of Glory wakimwimbia Bwana Yesu 26/10/20114



MIPAKA HUHAMISHWA JE?

Endapo Mungu alikusudia wewe uishi miaka 80,  wachawi hupenda kufupisha maisha yako  ili usifikie  huo umri. 


Endapo Mungu alikusudia uwe Mbunge ukiwa na miaka 45,  ule  muda ukikaribia,  wachawi hufanya uganga wao ili ugue, ukose sauti ya kufanyia kampeni, na mwishowe usiweze kufikia hilo lengo la ubunge. 


Pengine Mungu alikusudia mtu  awe Mkurugenzi mahali fulani,  lakini  akianza masomo yake ya kumfikisha kwenye hilo lengo, wachawi wanamfanya asiweze kufaulu  vizuri akiwa hata form 4. Halafu baadae, ile nafasi iliyokusudiwa inatoweka isiwe yake tena!!!.


Showers of Glory Walivyonaswa na Kamera yetu wakimwimbia Bwana Yesu.


MAOMBI:
Leo yeyote anayehamisha mipaka  yangu,  nakufyeka kwa Jina  la Yesu. Mipaka ya elimu, mipaka ya kazi, mipaka ya biashara, mipaka ya fedha,  mipaka ya ndoa ...... Niachie kwa jina la Yesu. Amen


2. Mtu anapoacha kuwa mwaminifu akatenda dhambi, mashetani huingia ndani mwake.

Hii ni  sawa na kumfungulia shetani milango. Unaweza kuwa umeokoka lakini  hujui jinsi ya kusimamia mipaka yako.  Ayubu  alikuwa mtakatifu wa Bwana, lakini  shetani alipokuja mbele za Mungu alimwambia kwamba, ‘Ayubu hamchi Mungu bure, bali ni kwa sababu Mungu amewekea wigo mali na vitu vya Ayubu’.


Mtu unapokuwa umeokoka, Bwana anakuwekea wigo, na pale ukiacha kuwa mwamifu ukatenda dhambi,  malaika wema huondoka na kuwapisha wale malaika wachafu toka kuzimu waingie ndani mwako kukuzunguka kama mfungwa. Ni vyema uache dhambi na kuanza maisha mtakatifu ukiwa na Yesu.


ZIPI DALILI ZA  MTU AMBAYE  MIPAKA ILISHA HAMISHWA?

·        Mtu huyo huishi  kwa huzuni.  Mungu hapendi kummhuzunisha mtu. Endapo mtu anaishi kwa  huzuni, ujue tayari mipaka ya maisha yake imehamishwa.


·        Mtu  anakuwa na hofu. Hofu ya mambo yajayo humjia mtu. Mtu anawaza, kwa kuwa  zamani aliwahi kutoa ujauzito (abortion) kabla ya kuokoa, anaanza kujiuliza maswali itakuwa je maisha ya  ndoa,  watoto watapatikana kweli?


MAOMBI:

Naikataa roho ya hofu ya mambo  niliyotenda zamani  kwa Jina la Yesu. Leo Bwana anaenda kuitanua ile mipaka iliyopindishwa kwa Jina la Yesu. Hofu iniachie kwa Jina la Yesu. Amen 


·        Hawezi kudiriki  kufanya makubwa. Watu wa aina hii hutamka kuwa ‘usinie kufanya makuu’.  Shetani hufunga ufahamu wa wasioamaini ili isiwazukie nuru ya Injilli.  Kinachoanza siyo fedha mfukoni mwako. A poor man does not think beyond his nose. Bwana analiangalia  neno  lake ili alitimizie.  Endapo unawaza biashara za kuuza karanga, ndivyo utakayopewa. Lakini ukiwa na mawazo ya kufanya biashara kubwa kubwa za super markets,  ndivyo utakavyopewa na Bwana.  Ukiwaza madogo unapewa madogo. Yule mama mjane, nabii alimwambia una nini nyumbani  kwako? Akaanza kutaja vitu vidogo alivyo navyo,  hadi  pale nabii alivyomwambia aende nyumba za majirani na kukusanya vyombo vya kutosha ili vijazwe mafuta!!!


·        Hawezi kuwa  na mipango ya maisha ya baadae. Mtu wa aina hii huwa hajui kesho yake itakuwa je‼!.


·        Mtu  wa aina hii hujaa wasiwasi. Nyakati zote mtu wa aina hii  hujaa wasiwasi kwa sababu hana uhakika na maisha yake,  kiafya,  katika kazi n.k.


·        Hawezi kuwaza kufanya kitu kipya. Mtu wa aina hii hujipima kwa  kipimo cha wale wengine waliomzunguka.  Mtu mwenye mipaka  iliyo salama huenda tu bila kuangalia wale waliomzunguka. Musa alisonga mbele, akawa wa kwanza kuipiga bahari nayo ikagawanyika kupisha njia kwa wana wa Israeli, kitu ambacho hapo awali hakikuwahi kufanyika!!!. 

     
     Hata sasa, wapo wanaoambiwa na ndugu zao  kwamba ‘katika ukoo wetu hayupo mtu aliwahi  kuoa mzungu, utaanza je wewe kufanya hivyo‼!’ Au wengine husema ‘katika ukoo wetu hayupo mtu aliwahi  kuhama kwenye hii dini yetu, utaanza je wewe kufanya hivyo‼!’


Mipaka ya mtu ikipanuka, mambo   ambayo  yalikuwa hayafanyiki, yataanza kufanyika kwa Jina la Yesu. Hii ni kwa sababu “Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu  yote”.


1 NYAKATI 4:9-10 ..[Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni. 10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.]…  Unapozaliwa mahali na kukuta mipaka imefinnywa lazima ushtuke. Usipofanya hivyo, utachukuliwa na ile hali  halisi. Kumbe kupanua mipaka ni  mpango wa Bwana.


KUTOKA 23:25…[Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.]…Mtu mwenye kunia madogo hawezi kunia makubwa.


MAOMBI:
Mimi  ninakataa kuwaza madogo, Kwa Jina la Yesu, nakataa kuishi kwa hofu, kwa Jina la Yesu. Hofu yoyote iliyokuja kwangu kwa sababu ya mipaka kuhama,  leo  naishambulia kwa Jina la Yesu. Amen



Mipaka ikiwa imeminywa hauwezi kuisimamia. Wapo wanaosogeza mipaka ya watu  wengine (makazini, kwenye ndoa, biasharani n.k.), na hao ni wachawi tu!!.


YEREMIA 51:20…[Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;]… Yesu ni Mungu aliye hai na anaishi  hata sasa. Anataka akutumie wewe kama silaha zake. Leo ni siku ya kupanua mipaka yetu kwa Jina la Yesu.


MIPAKA ILIYOHAMISHWA ITAPANULIWA JE?

Njia pekee ya kufanya hivyo (kupanua mipaka yako) ni "kupigana"


KUTOKA 13:17-18….[Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri;18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha.]…. Ulikuwepo mwendo wa siku nne tu kutoka  Misri hadi nchi ya Ahadi. Endapo wangepita ile njia ya urahisi,  vita ile ingewashinda. Mungu  aliwapitisha wana wa Israeli njia ndefu kwa sababu walikuwa 'hawajui  jinsi  ya kupigana'.


Pengine ulitakiwa uoelwe ukiwa na miaka 25, lakini Mungu  amesababisha upite jangwani na mwishowe ukaolewa na miaka 38.  Ni kweli umeolewa lakini umechukua muda mwingi jangwani. Unamiliki ghorofa, kweli. Lakini umeanza kulimiliki ukiwa na miaka 70, kiasi  kwamba hata kupanda juu unaomba msaada wa wajukuu zako wakushike  mikono wakati wa kupanda ngazi za ghorofani. 


Uwezo wa mtu kupigana ndiyo siri ya kumiliki vitu vyake  na mipaka yake mapema.


EFESO 6:11-12…[Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.]… Unapopigana, aliyeshikkilia mipaka yako anaachilia haraka kwa Jina la Yesu. zipo falme zenye kuhamisha mipaka yetu ya elimu,  ndoa, biashara,  mafanikio.  Silaha hazipatikani endapo hakuna vita. Uwezo wetu wa kupigana vita unatuwezesha kumiliki  na kuwafanya walioshikilia mipaka  yetu waachilie.


Baadhi ya Umati wa watu waliopania kuipanua mipaka yao iliyohamishwa, kwa kufanya maamuzi ya Kuokoka
Jumapili tarehe 26/10/2014 ndani ya Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro.


Endapo mtu haujaokoka, leo ni siku muhimu sana  kwako  kuhamia kwa Yesu na kushirikiana na wale watakaopanua mipaka yao  wenyewe siku ya leo.

© Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Kihonda VETA, Morogoro.
 /or
Contact our Senior Pastor:
 Dr. Godson Issa Zacharia
 (Ufufuo Na Uzima – Morogoro)

Cellphone: (+255) 757 550878 / +255 719798778
Share:
Powered by Blogger.

Pages