JUMAPILI: 11 JANUARY 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
SOMO: MUUNDO WA SERIKALI YA KISHETANI NA MASHETANI WANAOTAWALA
SIKU
Na:
ADRIANO
MAKAZI (RP)
RP Adriano akimkaribisha mama yetu ili atupe salamu za Mwaka mpya 2015. |
Utangulizi: Somo la leo linaitwa “Muundo Wa Serikali Ya Kishetani na Mashetani
Wanaotawala Siku”. Shetani hayupombali nasi,bali yupo
hapahapa duniani na utawala wake.
A: MAJINA YA SHETANI KATIKA BIBLIA
Biblia imemtaja shetani kwa majina mablimbali kama vile ibilisi, muovu, mkuu wa ulimwengu n.k.
MATHAYO 4:1….[Kisha Yesu
alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.]….
MATHAYO 4:5…[Kisha Ibilisi
akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,]… Unaona ibilisi anadiriki kumchukua
Yesu ambaye aliviumba vitu vyote hapa duniani.
MATHAYO 4:11…[Kisha Ibilisi
akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.]…
RP Happiness Godson (Mama yetu) akiongea na Majeshi ya Bonde la Maono- Morogoro Jumapili 11/1/2015. Ni raha sana kuwa naye. |
Sehemu nyingine Biblia inamtaja shetani mahali pengine:
AYUBU 1:6..[Ilikuwa, siku moja
ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye
akaenda kati yao.]….
Biblia inamtaja shetani.
Biblia inamtaja shetani kama muovu, na ndivyo alivyo. MATHAYO 5:37…[Bali
maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa
yule mwovu.]….. Maana
yake, ukisema ndiyo iwe ndiyo, na siyo iwe siyo.
Biblia inamtaja shetani kama mkuu wa ulimwengu. Yote unayoyaona
duniani ni kazi ya shetani.
YOHANA 14:30…[Mimi sitasema nanyi
maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.]….
YOHANA 16:11…[ kwa habari ya hukumu,
kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.]…. Huyu shetani,au ibilisi, au muovu, au mkuu wa ulimwengu ndiye anayefanya maisha yako yawe jinsi
yalivyo leo.
YAKOBO 4:7…[Basi mtiini Mungu.
Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.]….Leo tutamkimbiza shetani aliyeshikilia afya yako naye
atakimbia kwa Jina la Yesu. ukimpinga shetani atakimbia tu.
Mahali pengine shetani
anaitwa ‘lusifa’, maana yake ni ‘mtoa nuru’. Watu wengi duniani humwendea
lusifa kupata nuru ya biashara, nuru ya
utawala, nuru ya kazi n.k.
Hata Yesu naye aniatwa nuru. Kumbuka shetani hupenda kuigaiga.
YOHANA 1:9…[Kulikuwako Nuru
halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.]… Maana yake, nuru halisi ilikuwepo, na
kwamba nuru isiyo halisi (kutoka kwaw shetani) pia ipo.
UKIRI
Bwana Yesu karibu kwangu kama nuru, ili giza la dunia hii lisiniweze kwa Jina la Yesu. Amen
|
Kusifu na Kuabudu katika Bonde la Maono -Morogoro, tarehe 11/1/2015. |
Wachawi wanaweka giza katika
biashara za watu, kiasi kwamba
wateja wakipita kwenye hiyo biashara hawaioni. Hii ni saa ya kuinuka na kung’aa
kwa Jina la Yesu.
Shetani anakaa hapa hapa duniani. AYUBU 1:6-7…[Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu
walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. 7
Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na
kusema, Natoka katika kuzungukazunguka duniani, na katika kutembea huku na huku
humo.]…Hata hapa
kanisani shetani anaweza kuingia na kuwafanya watu wasinzie ili wasilisikilize
neno. Ukiona usingizi unakupata, mara
moja mpinge shetani na utaona anakuachiilia kwa Jina la Yesu.
1 NYAKATI 21:1..[Tena shetani akasimama
juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.]… Kama shetani anaweza kumshawishi Daudi
mtu wa vita, je, mtawala wa nchi yako ambaye hata vita hajui ni mangapi ambayo
ameshawishiwa na shetani na akayafanya?
UFUNUO 12:12….[Kwa hiyo shangilieni,
enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi
ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.]… Huu ni udhihirisho kuwa shetani yupo
hapa hapa duniani (bahari na nchi).
KUMBUKUMBU 34:1-6…[ Musa akapanda kutoka
uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. Bwana
akamwonyesha nchi yote ya Gileadi hata Dani; 2 na Naftali yote, na nchi ya
Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi; 3 na
Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari. 4 Bwana
akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo,
nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini
hutavuka huko. 5 Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya
Moabu, kwa neno la Bwana. 6 Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili
Bethpeori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo.]….Pamoja na kwamba Mungu alimzika Musa,
tunaona katika kitabu cha YUDA 1:9…[Lakini
Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya
mwili wa Musa,hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na
akukemee.]…. Huu ni
mwili wa Musa, lakini kwa nini
shetani anataka kuuchukua huu mwili?
Shetani ni roho, lakini jambo la kujiuliza,
kwa nini shetani ahangaike na
mwili huu? Hata wakati wa Yesu, wale
wanawake walipoenda makaburini wakaukosa mwili
wa Yesu, bila kujua kuwa Yesu amaefufuka, walianza kulia wakisema kuna
watu wameuiba mwili wa Bwana Yesu. Hawa wanawake wasingeweza kuongea mambo kama
haya endapo haikuwepo desturi ya miili ya waliokufa kuibiwa.
1YOHANA 5:19…[Twajua ya kuwa sisi tu
wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.]… Shetani anashikilia akili za watu.
Ndiyo maana hata ukimhubiria mtu habari
za Yesu, utajikuta wewe unamwelkeza hivi, lakini fikra zake zikombali na wewe.
2KORINTHO 4:4..[ambao ndani yao mungu
wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya
utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.]….Injili imefichwa
kwa wanaopotea ili waendelee kupotea zaidi. Shetani anaitaawala dunia, lakini
wewe na mimi ambao tumemwamini Yesu
Kristo hatupo chini ya utawala wa shetani.
UKIRI
Ninakuja kiunyume na
mashetni wote wanaoitawala dunia katika Jina la Yesu, kwa maana imeandikwa
mtiini mungu mpingeni shetani naye atawakimbia. Amen
|
B: UHAKIKA KUWA SHETANI ANA SERIKALI YAKE
EFESO 2:1-2…[Nanyi mlikuwa wafu kwa
sababu ya makosa na dhambi zenu; 2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata
kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule
atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;]….Serikali ya shetani haifanyi kazi kwa wale waliokoka.
Anatenda kazi katika wana wa uasi. Shetani aliasi mbinguni,vivyo hivyo
unapokuwa katika uasi ujue unakaa chini ya shetani. Kawaida, hukumu ya uasi ni
kifo. Uasi huanzi ndani ya moyo. Kile unachowaza, hakuna awezaye kukijua. Watu
wengi hawajui kwa nini shetani anaitwa mfalme. Watu maranyingine huonekana
wakiwabusu wafalme, au kuwainamia n.k.
shetani naye hupenda kufanyiwa hivyo hivyo.
2 KORINTHO 11:12-15…[Lakini nifanyalo
nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba
katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi. 13 Maana watu kama hao
ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume
wa Kristo. 14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa
malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe
mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.]… Kama ukiimkuta kobe amezaa, hawezi kuzaa
sungura. Kobe huzaa kobe. Ukimkuta kobe ana kitoto cha sungura, ujue
amekaiba. Shetani anaweza kujiegeuza na
kuwa kama malaika wa nuru kumbe siyo.
Shetani anaitwa kuwa ni ‘baba wa uongo’. Maana ya neno baba ni ‘mwanzilishi’. Hata
tunapomwita Mungu kuwa ni ‘baba’ hatumaanishi kuwa Mungu ana jinsi ya kiume.
Kwa hiyo, shetani anapoitwa baba maana yake ni mwanzilishi wa uongo.
YOHANA 8:44….[Ninyi ni wa baba yenu,
Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji
tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani
yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na
baba wa huo.]….
Maneno haya Yesu alikuwa anaongea na
Wayahudi. Maana yake shetani ana watoto na anaendelea kuzaa hadi leo.
Kazi huwa inamshuhudia mtu. Ndiyo maana Yesu aliwaambia wayahudi kuwa hata kama hawamuamini, basi wazisadiki
kazi zake.
Zipo njia tatu za kuweza kubaini / kushuhudia mambo: La kwanza ni ‘Neno
la Mungu’. Neno la Mungu huweza kumthibitisha mtu. Jambo linguine ni ‘muda’.
Kwa kutumia muda, unaweza kumpima mtu afaaye na asiyefaa katika maisha
yako (yawe ya ndoa, biashara, kazi n.k).
1 YOHANA 3:9-10…[Kila mtu aliyezaliwa
na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi
kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.10 Katika hili watoto wa
Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki
hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.]…. Ina maana ibilisi ana watoto na Mungu
ana watoto.
UKIRI
Ninakataa kuwa mtotoo wa ibilisi kwa Jina la Yesu, Kwa kuwa
imeandikwa Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, nakataa klutenda
dhambi kwa Jina la Yesu. Amen
|
Shetani katika serikali yake ana majeshi. Ndiyo maana shetani aliptimuliwa mbinguni alipigana vita. Kwa
hivyo basi, vita ya kumpiga shetani si lelemama. YOHANA 12:7-9…[Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika
zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika
zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule
joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani,
audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa
pamoja naye.]….Hapa
tunaziona timu mbili: Timu ya malaika Mikaeli na ile ya Joka (Lusifa). Shetani
(Lusifa) alikuwa mwimbaji mzuri tu
mbinguni na hata hivyo akawa na mbinu za kupigana. Iweje mtu leo hii
anajiita mwimbaji, lakini hajui kupigana vita vya kiroho? Katika mstari wa 8 imeandikwa “nao
hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.” Lazima shetani ashindwe kwenye
familia zetu, ukoo, kazi n.k. ili
ashindwe duniani na awe ameshindwa kwenye maisha yetu.
EFESO 6:12…[Kwa maana kushindana
kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya
wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.]… Kwa hiyo serikali hii ya shetani
inaonekana kuwa ni ya kijeshi jeshi tu.
UKIRI
Ewe shetani uliyejenga katika maisha yangu, achia maisha yangu
kwa damu ya mwanakondoo. Amen
|
Shetani anaitwa mfalme, na chini yake ana falme ambazo anazipa
amri ya kipi kifanyike. Yesu naye ni
Mfalme wa Wafalme, kimaanisha kila
mfalme na ufalme vyote vipo chini yake. MATHAYO
9:28-32 ….[Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya
Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali
mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. 29 Na tazama, wakapiga kelele,
wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula
wetu? 30 Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha. 31 Wale
pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi
la nguruwe. 32 Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na
kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.]….
LUKA 8:26-30 …[Wakafika pwani ya nchi
ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya. 27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu
mmoja wa mji ule, mwenye pepo, hakuvaa nguo siku nyingi, wala hakukaa nyumbani,
ila makaburini. 28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake,
akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi
usinitese. 29 Kwa kuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke mtu yule. Maana
amepagawa naye mara nyingi, hata alilindwa kifungoni na kufungwa minyororo na
pingu; akavikata vile vifungo, akakimbizwa jangwani kwa nguvu za yule pepo. 30
Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo
wengi wamemwingia.]….
Jeshi la pepo wachafu lilikaa ndani ya huyu mtu makaburini. Kila unapliona
jeshi, ujue kuna mtawala (mfalme). Mwaka
huu wale waliokuzuia kupita kuelekea
hatimayako wataiachia hiyo njia kwa Jina la Yesu.
Serikali ya shetani imegawanyika katka sehemu kuu mbili:
(i). Serikali ya shetani inayofanua kazi rohoni.
Aina hii ya serikali huleta udhaifu, magonjwa n.k.
(ii). Serikali ya shetani kwenye ulimwengu wa
mwili. Hawanimashetani wanaovaa miili na
kuwa mwanadamu.
MWANZO 18:2- ….[Akainua macho yake
akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga
mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, 3 akasema, Bwana
wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa
wako. 4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.
5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo
mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.]…… Malaika wanaweza kuja na kula,kuoa
n.k kama wafavyo wanadamu. Wenyeji wa Sodomana Gomora nao wakaona kuanza
kuwatamani kufanya nao tendo la ndoa. Ina maana basi kuwa, kama malaika wa
Bwana wanaweza kuvaaa miili, hata mashetani nao wanaweza kufanya vivyo hivyo.
MATHAYO 3:7….[Hata alipoona wengi
miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi
wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?]….Kumbe duniani hapa upo uzao wa nyoka;
Mungu akupe macho ya rohoni ilikuweza kuawabaini wanaokuja kwako lakini
kumbe ni wauzao wa nyoka, kwa
sababu hata katika uzao wa nyoka
LUKA 3:7…[Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea
ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira
itakayokuja?]…..
1KORINTHO 15:24-28…[Hapo
ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote,
na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui
wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 27
Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote
vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo. 28 Basi,
vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa
chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.]…
UKIRI
Asante Yesu kwa ajili ya siku zetu, asnate Bwana kwa nunipa
maaraifa ili niwe na silaha ya kumshinda adui yangu shetani. Asante
RohoMtakatifu kwa Kunifundisha,kuniongoza na ukanikumbushe yote pindi
itokeapo vita mbele yangu ili nipate
ushindi katika Jina la Yesu. Amen
|
C: MASHETANI WAKUU WATATU WANAOTAWALA
DUNIA
Wa kwanza ni Lusifa
mwenyewe. Biblia imemuita majina tofauti
tofauti (ibilisi, mkuu wa ulimwengu, muovu, shetani).
Wa pili ni Beelzebuli,
ambaye ni mkuu wa mapepo. Huyu ni mwana wa iblisi. Ndiye anawatawala mapepo na
kuwapa majukumu yao. MATHAYO 12:22-29
… [Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu;
akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. 23 Makutano wote wakashangaa,
wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? 24 Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema,
Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo. 25 Basi Yesu akijua mawazo
yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa;
tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. 26 Na
Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake
utasimamaje? 27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa
nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. 28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa
Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. 29 Ama awezaje mtu
kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake,
asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.]…. Mwaka huu 2015 ndivyo amabvyo watu
wengi wataulizia kukuhusu wewe,
wakistaajabu umewezaje kutoka na kwenda kwa Jina la Yesu.
Wa Tatu ni Ashtorethi: Maandiko yanasema ‘walijenga
nguzo juu ya Ashtorethi’. Watawala wengi hujenga tawala zao juu
ya huyu Ashtoreshi. Kanisa limejengwajuu ya mwamba ambaye ni Yesu Kristo. 1 WAFALME 11:5 …[Kwa
kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo
la Waamoni.], na pia
katika
D. MAPEPO YANAYOTAWALA SIKU
(i).
JUMAPILI
Kimsingi hii ni siku inayoitwa Sunday, yaani ‘siku ya jua’. Siku hizi zilipewa majina na wanadamu.
Mamlaka nyingi zikitaka kuleta jambo la kimamlaka huileta siku ya Jumapili.
Hili jambo halifanyiki kwa kuzuia wakristo wasipige kura. La hasha.
UKIRI
Kwa jina la Yesu naifyatua mipango yao ya kuipangia siku ya
Jumapili kwa Jina la Yesu. Nashambulia mashetani wote wanaoitawala Jumapili
yangu kwa damu ya Mwanakondoo, ninawafunga wakose nguvu juu ya maisha yangu,
na Jumapili zote ninazitiisha kwa Jina la Yesu. Wanaokaa vikao vya uharibifu,
vyote navisambaratisha kwa Jina la Yesu, kwa maana imeandikwa Bwana ni mtu wa
vita, Bwana ndilo Jina lake. Amen
|
Mashetani wanaitawala siku ya Jumapili kwa kila saa, kuanzia asubuhi saa moja hadi saa 12 jioni.
Hii ni kuzuia hata wanaotaka kwenda kanisani washindwe lakini kuwezesha mipango
ya uovu ifanyike bila kikwazo. Yanakuwepo mashetani ya kuleta ‘aibu’ kwa mtu
siku hii. Ndiyo siku ambayo hata wachawi
hukusanyika. Hufanya hivyo kuiga kile ambacho wana wa Mungu wanakifanya, kama
inavyoonekana pia katika AYUBU 1:1-6. Yapo mashetani ambayo hufanya ‘ahadi’ zao
za kishetani siku hii.
Muda wa saa moja: yapo mapepo ya kumsahmbulia mtu kimwili au kiroho.
Muda wa saa mbili: ni wakati mzuri kumdanganya mwanaume au
mwanamke kwa jambo lolote.
Muda wa saa tatu: Mtu mwenye cheo, au mpango wa kibiashara
Muda wa saa nne: Ni saa nzuri ya mauzo lakini ni saa mbaya kwa wanaotumia mapepo. Wahindi
kwa mfano, ikifika saa nne Mhindi hukaa mwenyewe
Muda wa saa sita: Ni mzuri wa kutapeli
Muda wa saa nane: Ni saa nzuri kwa wachawi kuongea na mtotoo aliye tumboni
Muda wa saa tisa: Ni saa nzuri ya kufunga ndoa za
kishetani
Muda wa Saa kumi: Muda wa kupongezana kwa wachawi. Ni muda
wa kumpa mtu mnyonge zawadi.
UKIRI
Ninafyatua masaa yote ya kishetani, naimilikisiku ya Jumapili na masaa yake kwa
Jina la Yesu. Ninaikamata Jumapili na watwala wote wanaotawala siku hii,
naubomoa utawala wa mapepo wanaoitawala Jumapili kwa Jina la Yesu. Amen.
|
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778