JUMAPILI: 18 JANUARY 2015 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo la leo linaitwa “Udongo Uliohuishwa”. Kuhuishwa ni kufanywa hai tena. Ni
kufufuliwa kwa kilichokufa. UDONGO uliohuishwa ni habari zinahusu ‘mwili’ kwa
sababu miili yetu imetokea katika ardhi,
na ndiyo maana shetani ana uwezo wa kucheza na miili yetu kwa sababu anakuwa
anacheza na ardhi.
WARUMI 4:17…[(kama ilivyoandikwa,
Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani
Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba
yamekuwako.]… Mungu
ndiye anayeshuisha.
RP Adriano akifundisha ibadani tarehe 18/1/2015 |
WARUMI 8: …[ Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa
ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu
iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.]…
1 KORINTHO 15:45…[Ndivyo ilivyoandikwa,
Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye
kuhuisha.]…
2 KORINTHO 3:6…[Naye ndiye
aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa
maana andiko huua, bali roho huhuisha.]…
EFESO 2:5…[hata wakati ule
tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani,
tumeokolewa kwa neema.]…
FILIPI 4:10….[Nalifurahi sana katika
Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama
vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi.]….
MWANZO 3:17…[Akamwambia Adamu, Kwa
kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza,
nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao
yake siku zote za maisha yako;]… Kama ardhi imelaaniwa kwa ajili ya mtu aliyetoka katika hiyo ardhi.
MWANZO 3:19…[ kwa jasho la uso wako
utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa
maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.]….
1 KORITNHO 15:47….[Mtu wa kwanza atoka
katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.]…..
MWANZO 2:7….[Bwana Mungu akamfanya
mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.]….
USHAHIDI WA KIBIBLIA KUWA ‘MTU NI UDONGO’
MWANZO 2:7...[Bwana Mungu akamfanya
mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai]…
MWANZO 3:19….[kwa jasho la uso wako
utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa
maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.]…. Shetani anajua asili ya ‘mwili’ na akitaka
kukutesa, anashika hayo mavumbi. Kwa
hiyo ni rahisi sana mashetani kuharibu mwili wa mtu kwa kuwa ni udongo tu.
ISAYA 64:8…[Lakini sasa, Ee Bwana,
wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya
mikono yako.]…
YEREMIA 18:6….[Ee nyumba ya Israeli,
je! Siwezi mimi kuwatendea ninyi vile vile kama mfinyanzi huyu alivyotenda?
Asema Bwana. Angalieni, kama udongo ulivyo katika mkono wa mfinyanzi, ndivyo
mlivyo ninyi katika mkono wangu, Ee nyumba ya Israeli.]… Udongo ukiwa mikononi mwa mfinayanzi, anawezza kuufanya chochote. Ndiyo maana tabia
za mtu zaweza kubadilika ghafla na kuwa kitu tofauti. Shertani wanaweza
kufinyanga na hicho kitu kikaonekana lakini siyo cha halisi (magonjwa, tabia za uzinzi n.k).
AYUBU 33:6…[Tazama, mimi ni mbele
ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami
nilifinyangwa katika udongo.]…
ZABURI 10:18…[Ili kumhukumu yatima naye aliyeonewa, Binadamu
aliye udongo asizidi kudhulumu.]…..
ZABURI 146:4….[Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku
hiyo mawazo yake yapotea.]….
ZABURI 90:3….[Wamrudisha mtu
mavumbini, usemapo, Rudini, enyi wanadamu.]….
Hii ndiyo maana mtu anapokufa, watu husema ‘huu
ni mwili wa fulani aliyefariki dunia’. Watu husema hivyo kwa
sababu mwili asili yake ni duniani. Mungu hakumuumba mwanadamu ili baadae afe,
bali dhambi ilipoingia duniani, ardhi ililaaniwa kwa ajili ya Adamu.
UKIRI
Leo naiondoa laana katika ardhi ambayo katika hiyo ardhi mimi
nilitwaliwa, Kwa Jina la Yesu. Amen
|
MWANZO 1:24…[Mungu akasema, Nchi na
izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na
wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo]…. Ardhi inaweza kutoa vitu. Ardhi
inapokuwa imelaaniwa maana yake imezuiliwa isitoe hivyo vitu. Ndiyo maana hata
wewe unapotaka kufanya mambo makuu, ikiwemo kuondoa mapepo, mwili unakuwa mgumu
sana kukuruhusu. Hii ni kwa sababu unakuwa umezuiliwa, kwa sababu ya hiyo
laana. Wakati mwingine unataka kufanya mambo, ikiwemo kusaidia wengine lakini
unajikuta unashindwa kufanya hivyo. Ndiyo maana yamkini unaonekana haufai, au
hauna sifa, ni kwa sababu ya laana katika udongo ambao katika huo ulitwalliwa. Leo tunamfuata Mfalme wa Wafalme aliyeufanya
udongo ili atubariki tena kwa Jina la Yesu.
Laana ikiwepo mahali hakuna kitakachoota. YEREMIA 17:5….[ 5
Bwana asema hivi,
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa
kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara
nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika
nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.]….Laana inafanya nchi isikaliwe na watu.
2 SAMWELI 1:13-21…[Naye Daudi akamwambia
yule kijana aliyempa habari, Watoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni,
Mwamaleki. 14 Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako
umwangamize masihi a wa Bwana? 15 Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana,
akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. 16 Daudi
akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia
nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi a wa Bwana. 17 Basi Daudi akamwomboleza
Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya; 18(kama ilivyoandikwa katika
kitabu cha Yashari), akasema, Wana wa
Yuda na wafundishwe haya, 19 Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka! 20 Msiyahubiri
mambo haya katika Gathi, Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni; Wasije wakashangilia binti za Wafilisti, Binti za wasiotahiriwa wakasimanga. 21 Enyi
milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya
shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.]… Laana hii ya Daudi kwa mlima huu wa
Gilboa, umefanya ene hilo kuwa jangwa hadi hivi leo.
UKIRI
Mashetani wote manaoshikilia mwili wangu kwa sababu ya laana
iliyotamkwa katika nchi, leo nawasambaratisha kwa Jina la Yesu. Amen
|
MWANZO
4:11-12….[Basi
sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya
ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa
mtoro na mtu asiye na kikao duniani]…. Kilicholaaniwa hakiwezi kukupa mambo mema. Na linguine ni kuwa, laana kwenye ardhi inaweza kumfanya mtu kuwa
mtoro, na hata kama baada ya kufanya
kazi katia ardhi, matatizo hujitokeza na mshahara ule upeperushwe na upepo.
Wapo watu ambao huhama hama, na kutotulia eneo moja. Hata makanisani, wapo
ambao hawakai mahali pamoja, leo kanisa hili na kesho kanisa lile. Matokeo
yake, mahali pale ambapo Mungu amepachagua ili ukutane na Baraka zako
unapakosa.
Majeshi ya Bwana ya Bonde la Maono Morogoro wakifuatilia maandiko ya somo la "Udongo Uliohuishwa" na kumshangilia Bwana hapo tarehe 18/1/2015. |
Msubiri Bwana kwa sababu
muujiza wako upo. Kwa wanaotafuta
‘wachumba’, hapa Ufufuo na Uzima ni kisima cha Yakobo, ambapo wachumba
hupatikana kwa Jina la Yesu.
UKIRI
Ewe laana kwenye ardhi uliyenisababishia nisiwe na makao
duniani, leo nakuvunja kwa Jina la Yesu. Leo natoka mavumbini kwa Jina la
Yesu. Enyi mavumbi mniachie kwa Jina la Yesu, kwa maana mimi ni udongo lakini
uliohuishwa kwa Jina la Yesu. Naitegua mitego yote iliyotegwa mavumbini kwa
Jina la Yesu. Amen.
|
Udongo uliolaaniwa,utaushangaa sana kuziona zile adhabu alizozitoa
Mungu kwa Adamu, Eva na kwa Nyoka. MWANZO 3:13-14…[Bwana
Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka
alinidanganya, nikala. 14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya
hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko
mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;]…
Mungu anamwambia shetani kuwa mavumbi ni chakula cha shetani. Maana
yake, mtu aliyetoka katika mavumbi ya ardhi ni chakula cha shetani. Je, kuna
kupona? Yesu alipokuja duniani, alivaa
mwili kama tulivyo sisi, na
akashambuliwa katika mwili. Alipofufuka alikuwa na mwili, lakini mtu wa kwanza aliyemtokea ni Mariamu,
aliyemwabia ‘usiniguse’ kwa sababu
aliyefufuka haguswi guswi ovyo. Maaniko yanasema, tulikufa pamoja na Kristo,
tukafufuka pamoja naye….. kwa maana hiyo,
mwili wa mtu aliyeokoka na
kufufuka pamoja Kristo, hawezi kuguswaguswa na shetani, wala magonjwa yake.
Wengine wataugua lakini siyo sisi tulio ndani ya Kristo, kwa maana sisi siyo
tena chakula cha shetani.
UKIRI
Kwa Jina la Yesu, nilikufa pamoja na Kristo, nikaa kaburini siku
zote tatu pamoja na Kristo, nikafufuka pamoja na Kristo siku ile ya tatu.
Ndoa yangu imefufuka pamoja na Kristo. Kazi yangu imefufuka pamoja na Kristo.
Mimi na Watoto wangu tumetoka mautini na kuingia uzimani kwa Jina la
Yesu. Amen.
|
HESABU 22:1-6…[ Kisha wana wa Israeli
wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani
karibu ya Yeriko. 2 Na Balaki mwana wa Sipori akaona mambo yote ambayo Israeli
wamewatendea Waamori. 3 Moabu akawaogopa hao watu sana, kwa kuwa walikuwa
wengi; Moabu akafadhaika kwa sababu ya wana wa Israeli. 4 Moabu akawaambia
wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote
vinavyotuzunguka, kama vile ng'ombe
arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa
Moabu zamani zile. 5 Basi Balaki akatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori,
hata Pethori, ulio kando ya Mto, mpaka nchi ya wana wa watu wake, kwenda kumwita, akisema, Tazama, kuna watu
waliotoka Misri; tazama, wanaufunika uso wa nchi, tena wanakaa kunikabili mimi.
6 Basi, njoo wewe, nakusihi unilaanie watu hawa; maana wana nguvu kunishinda
mimi. Labda nitawaweza, tupate kuwapiga, niwafukuze watoke katika nchi yangu,
kwa maana najua ya kuwa yeye umbarikiye hubarikiwa, na yeye umlaaniye hulaaniwa.]…. Laana inapokuwepo ni rahisi mno kushindwa. Mfalme Balaki hakuwa mchawi, bali
alimwendea mchawi (Balaam) ili tengeneze laana kwako. Mtu aliyebarikiwa hawezi kulaaniwa. Mtu
akeshalaaniwani rahisi kwa shetani kufanya
jambo lolote kwa mtu huyo.
KUTOKA 1:8-11…[Basi akainuka mfalme
mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. 9 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu
wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. 10 Haya! Na tuwatendee
kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana
na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.]….. Hata kama atakuja mfalme mpya
asiyemjua Yusufu, bado Baraka zako zipo pale pale. Lakini kwa kadiri
watakavyonitesa, ndivyo ambavyo nitakavyozidi kuongezeka kwa Jina la Yesu.
YOHANA 3:6…[Kilichozaliwa kwa
mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho..]… Mwili huzaa mwili na roho huzaa roho.
YOHANA 6:63…[Roho ndiyo itiayo
uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.]…
YAKOBO 2:26…[Maana kama vile mwili
pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.]….
Ibilisi anaweza kupanda kwenye udongochochote atakacho. MATHAYO
13:36-39…[Kisha Yesu akawaaga makutano, akaingia
nyumbani; wanafunzi wake wakamwendea, wakasema, Tufafanulie mfano wa magugu ya
kondeni. 37 Akajibu, akasema, Azipandaye zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu; 38
lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni
wana wa yule mwovu; 39 yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa
dunia; na wale wavunao ni malaika.]…Ndiyo maana Yesu alitupa mamlaka ya kung’oa kila pando
asilopanda Baba wa mbinguni.
UKIRI
Enyi wachawi na waganga mlionipandia balaa, magonjwa
mlionipandia, leo nayango’a yote kwa Jina la Yesu. Ewe mtawala wa dunia,
Lusifa na mashetani wako,
nakushambulia kwa Jina la Yesu.Amen
|
Laana huruhusu mlango wa shetani (adui) kuingia na kukushambulia.
2 SAMWELI 21:1-6...[Kulikuwa na njaa siku
za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa
Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa
kuwa aliwaua hao Wagibeoni. 2 Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi
Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa
Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi
yake kwa ajili ya wana wa Israeli na
Yuda;) 3 basi Daudi akawaambia hao Wagibeoni, Niwatendee nini? Na kwa tendo
gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki
urithi wa Bwana? 4 Na hao Wagibeoni wakamwambia, Si jambo la fedha wala dhahabu
lililo kati ya sisi na Sauli, au nyumba yake;
wala si juu yetu kumwua mtu ye yote katika Israeli. Akasema
Mtakayoyanena, ndiyo nitakayowatendea ninyi. 5 Wakamwambia mfalme, Yule mtu
aliyetupoteza, na kutufanyia shauri la kutuharibu, tusikae katika mipaka yo
yote ya Israeli, 6 basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi
tutawatundika mbele za Bwana katika Gibeoni, katika mlima wa Bwana. Mfalme
akasema, Nitawatoa.]…
Daudi aliingia kumilikibaada ya Sauli, na laana ya ukame ikatokea kipindi cha
utawala wa Daudi. Ndiposa Bwana akampa Daudi ufafanuzi wa ile laana. Inapokuwepo laana, mema yote huzuiliwa
yasije, hata kama utajitahidi namna gani.
Si vyema kuishi vibya na mtu
mwingine, kwani huyo mtu akiiingia mbele
za Mungu na kuongea sirini mbele za Mungu kinyume na wewe kuidai haki yake,
maneno yake hufanyika laana kwako. Yapo
mashetani yanayoingia kazini
kushikilia aina hii ya maneno. Daudi ingawa siye aliyewaua Wagibeoni,
aliwaita wale watu na kuongea nao ili kuyamaliza.
UKIRI
Mungu naomba unisaidie, kama kuna mtu aliyelia machozi ka ajili
yangu naomba unikumbushe, na unipe ujasiri wa kumfuata na kumalizana naye kwa
Jina la Yesu. Amen
|
2 SAMWELI 3:28-29…[Hata baadaye Daudi
aliposikia, akasema, Mimi na ufalme wangu hatuna hatia milele mbele za Bwana,
kwa sababu ya damu ya Abneri, mwana wa Neri; 29 na imwangukie Yoabu kichwani
pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu
mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye
kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula.]…. Katika baadhi ya koo, unapoona watu
wanatokwa damu ujue kuna laana inawafuatilia. Maana yake yupo mtu aliwahi
kuwatamka laana ya aina hiyo kwa watu wa ukoo huo. Leo ni siku kwa watu wa aina
hiyo kuzivunja laana hizo kwa Jina la
Yesu.
AYUBU 2:4-7…..[ 4 Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa
ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. 5 Lakini sasa
nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za
uso wako. 6 Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini
tunza tu uhai wake. 7 Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga
Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.]….
Shetani alikuwa anatafuta mlngo kuingia kwa Ayubu, na akeshapata mlango
huweza kuharibu apendavyo.
GALATIA 3:13...[ Kristo alitukomboa
katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana
imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; 14 ili kwamba baraka
ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho
kwa njia ya imani.]…
Leo ni siku ya kujitoa katika aina zote za laana za koo zetu, nchi yetu, ardhi zetu kwa kuwa Kristo
alifanywa laana kwa ajili yetu ili tuzipate zile Baraka za Ibrahimu na ahadi ya
Roho kwa njia ya imani.
UKIRI
Baba wa Mbinguni, ninaomba msamaha Bwana, yamkni kuna jambo
nimelifanya limeleta laana kwenye uzao wa tumbo langu, naungama uovu wangu
nilioufanya mimi, au walionitangulia,
ndugu zangu, watawala wan chi yangu, nami leo Bwana napitia uhairibifu kwa
laana hiyo, ya nchi au ukoo wangu, naomba msamaha kwako Bwana, kwa ajili ya
laana iliyoachiliwa kuja kwangu, kwenye
kazi yangu, kwenye nchi yangu,
naitumia Damu ya Yesu, Damu ya Agano Jipya, leo initakase, inene mema kwa ajili yangu. Naivunja laana
kwenye ardhi. Naitumia Damu ya Yesu
mwenye haki, kuvunja laana, inenayo mema kuliko damu ya Habili. Naiharibu laana, ya taifa, ya
ukoo, ya wachawi, ya shetani kwa Damu ya Mwanakondoo. Amen
|
ZEKARIA 5:3-4….[Ndipo akaniambia, Hii
ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye
atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama
ilivyo upande wa pili. 4 Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo
itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo
kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na
boriti zake na mawe yake.]…. Leo tunaituma laana iliyokuja kwetu irudiilkotoka kwa Jina la Yesu.
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778