Wednesday, April 19, 2017

USHUHUDA WA JOSEPHAT - DOMA

USHUHUDA WA JOSEPHAT KUTOKEA DOMA
– (MVOMERO MOROGORO)

Kijana Josephat Joseph Steven, ni mkazi wa Kata ya Doma iliyopo Mvomero (Morogoro). Kijana huyu (PICHANI KUSHOTO KWA MCHUNGAJI KIONGOZI) ana umri wa miaka 29. Ni kijana ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo mengi sana. Aliletwa kanisani Ufufuo na Uzijma Morogoro akiwa hajiwezi, na kwa mujibu wa ndugu zake, Josephat alikuwa hali chakula, hapati haja zote, akawa anakaa tu nyumbani muda wote na bila kufanya kazi yoyote ile.

Josephat (Kulia) akitambulishwa na Mchungaji Kiongozi Dr. Godson (Kushoto)


Chanzo cha matatizo aliyokuwa nayo Josephat ni ndoto aliyoiota Mwezi Novemba mwaka 2016. Katika ndoto hiyo Josephat alijiona usingizini akiitwa na watu anaowafahamu. Watu wale walimwagia maji ndotoni na kisha wakatoweka. Baada ya kuamka na kutoka nje Asubuhi aliasimulia nduguze ile jndoto na akaanza kujisikia vibaya. Kuanzia hapo matatizo yakamuanza. Akawa hataki kabisa kuonana na watu, akawa anaogopa kuwaona watu, na ndiyo maana akawa anajificha ndani mara zote.

Josephat (Katikati) na Kushoto kwake ni Binamu yake aitwae Viktoria Isaya wakitoa Ushuhuda wa Uponyaji tarehe 16/4/2017 Ufufuo na Uzima Morogoro


Ili kumsaidia, Ndugu zake walikimbilia kwa waganga wa kienyeji nwakidhani ndipo atakapoipata nafuu lakini pamoja na tiba za waganga hawa Josephat hakupata uponyaji. Kadiri alivyozitumia hizo dawa za waganga wa kienyeji ndiyo matatizo ya Josephat yalivyokuwa yanaongezeka.


Baada ya hapo Josephat alipelekwa kwa Shekhe mmoja ambaye aliwasihi endapo wangechelewa kwa wiki moja tu Josephat angefariki dunia. Shekhe aliwaambia kazi atakayoifanya ni kukihamisha kivuli cha Josephat na baadae kumsomea sala ya albadiri. Gharama ya huduma yote hii waliambiwa ni Shilingi 150,000/- . Ili kuwezesha matibabu kuanza, ndugu za Josephat walilipa nusu ya pesa hii. Pamoja na matiabu haya kuanza, hata hivyo Josephat hakupata nafuu yoyote.


Siku moja mwaka huu, binamu yake yake Josephat aitwae Viktoria Isaya alisikia redioni kuwa lipo Kanisa lililopo Morogoro (Siyo Ufufuo na Uzima) ambapo watu wanaombewa na kupata uponyaji. Binamu huyu aliwashawishi ndugu zake wampeleke kanisani nao wakakubali.


Hapo tarehe 4 March 2017 Josephat na ndugu zake walifika hapa Kanisani Ufufuo na Uzima Morogoro ili kupata msaada wa maombi. Kuanzia siku ile, Josephat hadi sasa amepona kabisa, nay eye binafsi anashuhudia kuwa amepona. Ndugu zake wanamshukuru Mungu kwa kumponya ndugu yao huyu, Josephat.


Josephat akifurahia kupona kabisa kupitia Jina la Yesu Kristo, ndani  ya Ufufuo na Uzima Morogoro,  hapo 16/4/2017


Sifa Heshima na Utukufu zimwendee Bwana Yesu.  Amen


FUATANA NASI KWA FACEBOOK  KWA KUBONYEZA HAPA CHINI:



USHUHUDA WA JOSEPHAT KUTOKA DOMA
Share:
Powered by Blogger.

Pages