JUMAPILI: 02 NOVEMBER 2014 - UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo la Jumapili ya leo linaitwa “Bila Vita Hakuna Kumiliki”. Ukiona mtu anamiliki kazi, ujue ameshapigana vita. Ukiona mtu anamiliki ndoa nzuri, ujue ameshapigana vita. Kumiliki kuna kununi yake, kama ambavyo katika hisabati zipo kanuni za kimahesabu.
RP Adriano akihubiri kwa mara ya kwanza katika Bonde la Maono Jumapili 02/11/2014 Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Mkunndi, Morogoro. |
Bwana akeshakupa Baraka yako na mahali pa kwenda, hata kama yapo majitu, bado utakatiza tu kwa Jina la Yesu. Mfalme Sihoni wa Heshboni ni yule ambaye katika Baraka zako hujitokeza na kutaka kuzuia hizo Baraka zisitokee. Mungu alimfahamu mfalme Sihoni kuwa hatowaruhusu Israeli kupita katika nchi yake. Mungu anaweza kutia moyo wa ukaidi kwa adui zako kama alivyofanya kwa mfalme Sihoni wa Heshboni.
Mungu anataka watu wake wamiliki, na ili umiliki lazima upigane vita. “Kama haumiliki, ujue unamilkiwa”. Mungu alimuumba mwanadamu ili amiliki, atawale na kutiisha.
Majeshi ya Bwana yakiliteka Viwanja vya Mkundi kwa Maombi ili kumiliki, huku baadhi ya mbao za ujenzi zikionekana |
MWANZO 1:26-27….[Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.]…. Lazima upigane, kwa sababu shetani aliiba ile asili ya kutawala. Wachawi hawapaswi kututawala, na badala yake sisi ndio tunapaswa kuwatawala wachawi. Adamu na Eva walinyang’anywa ule uwezo wa kutawala, pale walipokula tunda walilokatazwa wasile. Mungu aliwatoa nje ya bustani ya Edeni, kwa sababu angewaacha pale wangekula tunda la uzima na matokeo yake wangeishi na dhambi zao milele na milele. Admau wa Pili (Yesu Kristo) aliturudishia uweza wa kumiliki kwa njia ya damu yake msalabani.
2 KORINTHO 10:3-4….[Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)]… Kabla askari hajaenda vitani hupewa mafunzo ya kijeshi. Awali ya yote, huondolewa ile 'hali ya uraia'. Ukiwa Ufufuo na Uzima, unaondolewa ile hali ya ‘uraia’ kwanza, kwa kufundishwa namna ya kupigana kuelekea kwenye Baraka zako. Sihoni anapokuzia kama alivyofanya kwa Israeli, unapaswa kupigana naye. Sihoni ni yeyote anayekuzuia wewe usiingie kwenye afya yako, badala yake akitaka uendele kukaa katika ugonjwa wako siku hadi siku.
KUMBUKUMBU 3:1-14…[1 Ndipo tukageuka, tukakwea njia ya Bashani; na Ogu, mfalme wa Bashani, akatutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kuja kupigana huko Edrei. 2 Bwana akaniambia, Usimwogope; kwa kuwa nimemtia mkononi mwako, yeye na watu wake wote na nchi yake; nawe utamtenda mfano wa ulivyomtenda Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni. 3 Basi Bwana, Mungu wetu, akamtia mikononi mwetu na Ogu mfalme wa Bashani, na watu wake wote; tukampiga, asisaziwe cho chote. 4 Tukatwaa miji yake yote wakati huo; hapakuwa na mji tusiotwaa kwao miji sitini, nchi yote ya Argobu, ndio ufalme wa Ogu ulio katika Bashani. 5 Miji hiyo yote ilikuwa yenye maboma marefu, na malango, na makomeo, pamoja na miji isiyokuwa na maboma, mingi sana. 6 Tukaiharibu kabisa, kama tulivyomfanya huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, kwa kuharibu kabisa kila mji uliokuwa na watu, pamoja na wanawake na watoto. 7 Lakini wanyama wote wa mji, na nyara za miji, tulitwaa kuwa mawindo yetu. 8 Tukaitwaa na nchi wakati huo, katika mikono ya hao wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ng'ambo ya Yordani, tokea bonde la Arnoni mpaka kilima cha Hermoni; 9 (na hiyo Hermoni Wasidoni huiita Sirioni, na Waamori huiita Seniri); 10 miji yote ya nchi tambarare, na Gileadi yote, na Bashani yote, mpaka Saleka na Edrei, nayo ni miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani. 11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho b je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu). 12 Na nchi hiyo tuliitwaa ikawa milki yetu, wakati huo; tokea Aroeri iliyo kwenye bonde la Arnoni, na nusu ya nchi ya milima ya Gileadi, na miji iliyokuwamo, niliwapa Wareubeni na Wagadi; 13 na nchi ya Gileadi iliyobaki, na Bashani yote, maana huo ufalme wa Ogu niliwapa nusu ya kabila ya Manase; nchi yote ya Argobu, nayo ndiyo Bashani yote. (Na nchi hii yaitwa nchi ya Warefai. 14 Yairi, mwana wa Manase, alitwaa nchi yote ya Argobu, hata mpaka wa Wageshuri na Wamaaka; akaziita nchi hizo Hawothyairi, kwa jina lake mwenyewe, hata hivi leo, maana, hizo nchi za Bashani.)]…. Kwenye kila maisha ya mtu au safari yako ya Baraka, utakutana na akina Sihoni na Ogu. Bila kupigana vita, hakuna kumiliki. Kama mtu anahitaji kumpata mchumba/mume/mke/kazi, anapswa kupigana vita. Yamkini huyo mwenzio ameshikiliwa na hawa ‘wafalme mashuhuri’. Hawa Wafalme ni ambao wamejipanga ili kuona waisraeli hawamiliki. Jinsi ile ile wamlivyopigwa wafalme Sihoni na Ogu, ndivyo hata sisi tunaenda kupigana, na lazima tutaenda kushinda kwa Jina la Yesu.
Majeshi ya Bwana,marika yote, wakubwa kwa watoto wakiwa wametawanyika kufanya Maombi ya Kushindana ili kumiliki. |
WAEFESO 6:10-12 [10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.]… Biblia inasema ‘mzidi’ maana yake, kila iitwapo leo lazima upige hatua ya vita vyako. Kama hakuna vita, kwa nini tuvae silaha? Vipo vitu vinne ambavyo vimetajwa hapa: falme, wakuu wa giza, mamlaka na majeshi ya pepo wabaya. Vita yako inategemea wewe unapigana na nini. Endapo vita yako ni juu ya falme, ujue vita yako ni kubwa sana, kwa sababu penye mfalme lazima pana majeshi yanayomlinda huyo mfalme‼!
Wakati mwingine vita ya mtu
inakuwa juu ya mizimu. Kawaida, mizimu ni
mashetani yanayotawala na kumiliki wanaukoo kwenye makabila ya Afrika‼! Mashetani haya
huhakikisha kuwa watu wa ukoo husika
wanapitia maisha yanayofanana fanana. Mfano, endapo mama katika ukoo wa mizimu anazaa
kabla ya ndoa, itakuwa hivyo hivyo hata kwa mabinti wake kuzaa kabla ya
kuolewa‼ Ili uweze kutoka kwenye hali kama hii, inabidi upigane vita
ili baadae utoke kwenye huo ukoo na kuingia
katika ukoo wa Bwana Yesu.
Miavuli Juu, Miavuli Chini!!! Hii ndiyo staili yetu, tukiwa kwetu - Bonde la Maono,Mkundi - Morogoro, tarehe 02/11/2014 |
Mashetani yapo na yemejigeuza na kuitwa kwa majina tofauti. Mfano, maeneo yote ambayo Waarabu walikaa au wanakaa sasa hivi, aina ya mashetani yanayotawala maeneo hayo ni ‘majini’. Mashetani wengine aina ya ‘majoka’, yapo na yanaijua hata Biblia kwa sababu yana asili ya mbinguni (UFUNUO 12:7-12). Mashetani aina ya majoka, yanaweza kugeuka na kuwa kitu chochote kwa sababu yana uwezo wa kuwa kama malaika. Ndiyo maana, kuna nyakati ambapo tatizo la mtu haliishi haraka, kwa sababu aina hii ya mashetani (majoka) yanapotumwa kwa mtu, humshikilia mtu yakitaka asiweze kutoka katika shida yake.
MAOMBI:
Kwa Jina la Yesu, leo ni siku yangu ya kushindana na nitashinda kwa Jina la Yesu. Amen
|
Katika Biblia, kila aliyepigana, jina lake lilibadilika. Imeandikwa:
YEREMIA 51:20-24…[Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; 21 na kwa wewe nitamvunjavunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunjavunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; 22 na kwa wewe nitawavunjavunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunjavunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunjavunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; 23 na kwa wewe nitamvunjavunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunjavunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunjavunja maliwali na maakida. 24 Nami nitamlipa Babeli, na wote wakaao ndani ya Ukaldayo, mabaya yao yote, waliyoyatenda katika Sayuni mbele ya macho yenu, asema Bwana.]… Bwana akitaka ampige Ogu anakutumia wewe. Ndiyo maana Mungu akamwambia Musa, mtashindana nao, siyo kwamba Mungu atafanya hivyo, lahasha, bali atamtumia Musa na Waisraeli wote kupigana na kuwashinda maadui zote‼!
Kwa hiyo huu siyo wakati wa kumlilia Mungu na kumuomba akupiganie au akutetee‼! Silaha nazo hutofautiana, nyingine ni mawe, mishale, machine guns, nyingine ni mabomu ya nyuklia‼! Biblia inasema, “Amelaaniwa mtu yule asiyetumia silaha yake kumwaga damu”….. Leo mashetani yote ni saizi yetu. Kila jini linalojipitisha katikati yetu lazima tutumie silaha zetu kumwaga damu za hilo jini kwa Jina la Yesu.
Baadhi ya Majeshi ya Bwana Morogoro wakifuatillia kwa makini somo la Jumapili hii tarehe 02/11/2014 liitwalo "Bila Vita Hakuna Kumili" |
MAOMBI:
Bwana Mungu wa Mbinugni ninakuja kwako leo kwa Jina
la Mwanakondoo. Ninaomba msamaha kwa maovu yote niliyotenda kwa Jina la
Yesu. Naomba unipe neema mchana huu wa leo katika Jina la Yesu. Nifanye kuwa rungu
lako, nifanye kuwa silaha zako kwa Jina la Yesu. Unifanye kuwa mtu wa vita katika
Jinala Yesu, kwa maana bila vita hakuna kumiliki. Nahitaji kumiliki
afya, nahitaji kumiliki utajiri katika
Jina la Yesu. Roho Mtakatifu uniongoze katika njia, na mahali
pa kupenya katika Jina la Yesu. Amen
|
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi, Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior
Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778