JUMAPILI: 14 DECEMBER 2014
- UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
Utangulizi: Somo la leo linaitwa “Mji wa Uharibifu”. Ni vizuri kufahamu kuwa ipo miji ya
uharibifu ambapo wachawi, waganga wa kienyeji, washirikina, wasoma-nyota,
wapigaramli na washirika wao wote hukaa humo. Leo tutaenda kuibomoa miji hii
kwa Jina la Yesu.
ISAYA 19:18…[Katika siku hiyo
itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na
kumwapia Bwana wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu.]…Tunapoongelea Misri tunaizungumzia
Afrika. Maana ya miji mitano katika
Misri ni kuwa itakuwepo miji mitano Barani
Afrika. Biblia inasema kuwa katika hiyo
miji mitano, mmoja utakuwa ni mji
wa uharibifu. Kwa nini uwepo mji wa aina hii? Kwa sababu shetani hapendi kuona mambo mema
yakifanyika, na katikati ya mema shetani hupenyeza uharibifu. Kumbuka hata
katika mitume 12 wa Yesu Kristo, shetani alijipenyeza na kumuingia mmoja wao
aitwae Yuda Iskariote ili kuleta uharibifu.
Katika Biblia Misri ilibarikiwa na kuwa kama kimbilio la watu
kwenda nyakati za shida na njaa.
Tunamuona Ibrahimu alikimbilia Misri njaa ilipozidi, na hata mwanae Isaka alifanya vivyo hivyo.
Watoto wa Isaka vivyo hivyo, njaa ilipowapata,walikimbilia Misri na kumkuta Yusufu ndugu yao akiwa amefanywa
Waziri Mkuu wa Misri. Kwa hiyo basi, mataifa yanaonekana yakija Afrika kupata
chakula. Misri imebarikiwa hivyo kwa kitendo cha kuwapokea
Wayahudi (Israel). Yesu Kristo akiwa
kabla ya kusulubiwa Golgotha,
alipokelewa msalaba wake na Simoni wa Kirene (ambaye ni kutoka Afrika)
kudhihirisha kuwa Afrika ndiko ambapo moto wa Injili utatokea nyakati hizi za
mwisho na kufanya mataifa yote duniani kuwa falme za mwanakondoo.
Sehemu nyingine mji huu unaitwa’Mji wa Ghasia” (ISAYA 22:2…[Ewe
uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha; Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa
upanga, Wala hawakufa vitani.])… Unapoona ghasia zinatokea bungeni au
katika mita yetu ujue zinatokea kule. Sehemu nyingine uniatwa mji wa machafuko
(ISAYA 24:10…[Mji
wa machafuko umebomolewa; kila nyumba imefungwa, asipate kuingia mtu awaye yote.])… Yanapotokea machafuko ya ndoa,
machafuko makazini, ujjue yote
huanmzai hapo. Na zipo nyumba katika huumji,
na wachawi hutumia aina hizi za nyumba zishikilie watu. Unaweza kumuona
mtu katika mwili lakini kumbe anakuwepo mara mbili. Kila mji unaouona unakuwa na uongozi wake
(wakuu wa kuutawala mji) ambao huzuia vinavyoingia ndani ya mji,kama ambavyo
Dnieli alizuia na Mfalme wa Anga la Uajemi ili majibu yake yasimjie Danieli.
Mungu anapenda sisi tuombe ili
kupata majibu ya kile tunachomuomba
kama katika MATHAYO 7:7. Hata hivyo wapo mashetani wakaao katika miji ya
uharibifu ambao huzuia majibu ya maombi yetu.
Tangia siku ya kwanza ulipoanza
kuomba hitaji lako, Bwana ameshakujibu lakini wenyeji wa miji
ya uharibifu huyazuia hayo majibu ili yakufikie ukiwa tayari mzee wa
miaka 80. Yakija katika muda huo, majibu
ya aina hii yanakosa maana. Leo kila
mmoja adhamirie kuibomoa hii miji kwa Jina la Yesu ili tupate majibu yetu kwa
wakati wa Bwana.
Kimsingi wachawi huwa hawana sababu ya maana ya kumsababishia mtu
matatizo. Watu wa aina hii huweka ‘vikao vya uharibifu’ na kupanga namna ya
kukuangamiza. Hawa hujifungia ndani ili kutengeneza mango wa maangamizi. Mara nyingi watu wa aina hii huwa ndugu wa karibu au wa ofisi makazini.
Ndiyo maana Biblia husema Adui wa mtu ni
wale wa nyumbani mwake.
2 WAFALME 6:8…[Basi, mfalme wa Shamu
alikuwa akifanya vita na Israeli. Akafanya mashauri na watumishi wake, akasema,
Kituo changu kitakuwapo mahali Fulani]… Ujue hata wewe
kuna mtu/watu wanafanya vita na biashara yako.
Kuna watu wanapanga ajali kwa ajili
yako ingawa hujui. Si vizuri kwenda kwa mazoea. Haujui adui wakoamepanga
aina gani ya vita dhidi yako. Kuna watu wanapanga kituo cha watu wengine kwa maisha
yao.
MAOMBI
Kila aliyepenga shauri juu ya ndoa yangu, au juu ya watoto
wangu, Bwana auoyooshe mkono wake kinyume nao, ili mashauri yao yawarudie wao wenyewe kwa Jina la Yesu. Amen
|
2 WAFALME 6:9..[Yule
mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, kusema, Jihadhari, usipite
mahali fulani; kwa sababu ndiko
wanakoshukia Washami.]…
Shetani amejipanga lakini hata Yesu Kristo naye amejipanga kwa ajili yako. Kuna
wakati wa kujihadhari. Si vyema kwenda
bila hadhari.
MAOMBI:
Naagiza mtego wa ajili waliokutegea uwanase wenyewe kwa Jina la
Yesu. Mungu na akuokoe na mtego wa wawindaji kwa Jina la Yesu kwa sababu Yesu
Kristo ameshinda vita na kuzimu. Amen
|
2 WAFALME 6:10...[Mfalme
wa Israeli akapeleka watu mpaka mahali pale alipoambiwa na yule mtu wa Mungu,
na kuhadharishwa; akajiokoa nafsi yake, si mara moja, wala si
mara mbili. 11
Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili;
akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionyesha, ni mtu yupi miongoni
mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?]… Unapoambiwa jambo hukimbilii tu. Kwa niniMfalme wa
Shamu afadhaike? Ni kwa sababu kituo
alichopanga uharibiifu hakikutokea,
zaidi ya mara tatu. Alipanga
magonjwa, akaugua mwanae wa kwanza
akafa. Alipanga ajali, badala yake ajali ikatokea nyumbani kwake mwenyewe. Na
iwe hivyo hivyo kwa Yule ndugu yako aliyepanga mabaya kwako, yamrudie yeye na
familiayake na wafadhaike kwa Jina la
Yesu. Tunaye Roho Mtakatifu wa kutujulisha mambo yote ya sirini yaliyopndwa juu
yetu kwa Jina la Yesu.
Platforms wakiongoza Majeshi ya Bwana katika Sifa na Kubadu Bonde la Maono -Morogoro tarehe 14/12/2014 |
Mungu amemficha mwanadamu ili asiyaone baadhi ya mambo yaliyopangwa maishani mwake. Laiti
mtu angejua mambo /matukio ambayo yalikuwa yatokee kwake kila siku maishani mwake na ambayo Bwana anamuepusha, angepiga magoti na
kumshukuru Mungu kusema 'asante’. Tazama
Bwana amekuwezesha kwa miezi yote ya mwaka kuishi vizuri, na kukuepusha na mabaya yaliyopangwa kukupata kipindi hicho. Mwezi wa Desemba ni
mwezi wa kumpa Bwana shukurani kwa ukarimu ambao
Bwana ameufanya katika maisha yako. Lazima uwe na moyo wa shukrani.
Muombe Mungu ili mwaka 2015 uwe ni "mwaka
wa kutiisha, kumiliki na kutawala" kwa Jina la Yesu.
Majeshi ya Bwana Bonde la Maono Morogoro wakifuatilia kwa makini somo "Mji wa Uharibifu" tarehe 14/12/2014. |
Huu ni wakati wa kumpa sifa Bwana kwa matendo makuu aliyofanya
maishani mwetu. Daudi alisema ni ‘heri
kuwa nyumbani mwa Bwana kuliko
miaka elfu moja kwenye karamu za waovu’. Mungu
aliweka siku moja tu ya saa 12
kwa ajili ya kumwabudu. Ni vizuri kuja
nyumbani kwake, na kusogeza mioyo ya shukrani kwake.
© Information Ministry
(Ufufuo Na Uzima - Morogoro)
Mtaa wa Nguvu Kazi,
(Minara Mitatu), Mkundi-Morogoro.
/or
Contact our Senior Pastor:
Dr. Godson Issa Zacharia
(Ufufuo Na Uzima – Morogoro)
Cellphone: (+255) 757
550878 / +255 719798778