Sunday, October 29, 2017

KUFUNGA BIASHARA ZA KICHAWI

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

{KANISA LA UFUFUO NA UZIMA ---> MOROGORO}

JUMAPILI: 29 OKTOBA, 2017

MHUBIRI:  MCHUNGAJI, DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)

Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akifundisha neno la Mungu wakati wa Ibada ya Leo.

Biashara ni shughuli yoyote inayofanyika kihalali kwa lengo la kupata faida. Kwa kawaida biashara halali siku zote zinaruhusiwa. Kwenye biashara lazima kuwepo kuuza na kununua. Na lazima kuwepo bidhaa inayouzwa na kununuliwa. Na kwa mfanya biashara mzuri lazima alenge kupata wateja ili akishapa wateja, aweze kuuza na kupata faida.  Lakini biashara ya Kichawi sio halali kwa hiyo ni lazima ifungwe. Biashara za kichawi ni zile biashara za kuuza na kununua miili na roho za wanadamu.

Ufunuo 18: 11-13 Imeandikwa, “Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;  bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;  na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu”.


Hapa tunajifunza kwa habari ya biashara zinazoweza kufanyika juu ya nchi. Sehemu inayohusu somo hili ni ile inayoongelea biashara ya miili na roho za watu. Biashara ya kichawi nayo inatumia mfumo wa kutengeneza wateja wa biashara izo. Mfanya biashara akifanikiwa kutengeneza wateja basi amepata faida. Wafanya biashara wa kichawi wanatafuta na kuongeza wateja. Wateja wa wachawi ni wanadamu kabisa. Biashara ya kichawi huwa inamwona mwadamu yoyote kama mteja wake. Unaweza kuwa unatembea au unaishi vizuri lakini wachawi wanakutafuta.

Mwadamu ni roho inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa mwili. Biashara ya kichawi inalenga kukusanya wateja kwa nguvu kubwa. Isaya 42:22 Imeandikwa, “Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.” watu wanatekwa na kukamatwa na hatimaye kuwekwa mashimoni kwa sababu ya kazi hii ya biashara ya kichawi. Kwenye biashara hii kinacholengwa ni mwili na roho za wanadamu. Unaweza ukaibiwa uso, mikono ya pesa, kazi, nyota ya mvuto kama sehemu ya biashara za kishetani.

Ufunuo wa Yohana 18:11 imeandikwa, “Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena”. Wachawi wenyewe waliowanda/kuwika sana, kwa sababu ana bidhaa (roho za wau, mikono, nyota za watu) nyingi sana.
Baadhi ya Makutano wakifuatilia somo la leo.

Yeremia 5:26
imeandikwa, “Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu;  hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji”. Biashara ya uchawi ni biashara ya roho na mwiili. Mwili una mikono, macho tumbo na sehemu nyingine za mwili. Biashara hii ina lengo la kuongeza watu na sehemu wanapohifadhia bidhaa hizo ni kuzimu. Misukule mingi ikiwa kule ndo  inatumiwa kulima. Bishara hii ya kichawi ni biashara iliyo kamilika.

Mathayo 2:1 imeandikwa, Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema”. Hata Yesu aliwai kuonwa akiwa mdogo na wakaanza mipango ya kutaka kununua roho yake. Kumbe wachawi wanaweza kukuona ukiwa mdogo kwamba wewe umezaliwa kama mfanyabiashara mkubwa, mwalimu, Mchumi au Daktari na wakaanza kukuwinda roho yako. Ndio maana utaona watoto wanaibiwa wakiwa hospitalini. Mtoto anaweza kuwa ana uwezo mzuri kimasomo gafla anashuka katika ufaulu wake kumbe roho yake imeibiwa na kuuzwa mahali. Mtu anaweza kuwa ana nyota ya biashara akawa anauza sana kwenye duka lake gafla anafirisika, hii ni kwa sababu roho yake imeibiwa.

Mtu anaweza akauzwa roho na mwili wake akawekewa jini. Mtu anaweza kuuzwa mwili, roho na viungo vyake. Pengine wanaweza kuiba roho na mwili kwa pamoja. Jifunze jambo ukimwona mtu haoni (matatizo ya macho) jua mtu huyo alikuwa na nyota ya kuona fursa. Kwa hiyo upofu huo umempata kwa sababu ya biashara za kichawi.
 
Platform na Children Ministry wakisifu na kuabudu katika ibada ya Leo.
STOO. Wafanya biashara wa kichawi wanatunza bidhaa zao kuzimu. Utasa ni matokeo ya biashara za kuuza matumbo ya uzazi kwa wanawake. Ndio maana waliokuwa tasa kwenye Biblia walizaa watu maarufu.  Mithali 27:20 Imeandikwa, “Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi.” Mithali 30:16 Imeandikwa, “Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!

Isaya 5:14 Imeandikwa, “Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo”. Kuzimu kumeongeza tama ili watu waingie kwenye maangamizo. Ndio maana wachawi wanamwona kila mwanadamu kama mteja wao. Lengo lao ni kuwameza wote waingie kwenye shimo la Kuzimu. Nahumu 3:4-6 Imeandikwa, “Kwa sababu ya wingi wa ukahaba wa yule kahaba mzuri, yule bibi wa mambo ya uchawi, auzaye mataifa kwa ukahaba wake, na jamaa za watu kwa uchawi wake. Tazama, mimi ni juu yako, asema Bwana wa majeshi; nami nitafunua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonyesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako. Nami nitatupa uchafu uchukizao juu yako, kukufanya uwe mchafu, nami nitakufanya kuwa kitu cha kutazamwa kwa dharau.” Kumbe wachawi wanaweza kuuza Mataifa na jamaa za watu, nchi inaweza kuuzwa kichawi. Ndio maana utaona ardhi ipo lakini watu hawana chakula.
SABABU YA NCHI AU MTU KUUZWA
UOVU. Mtu anaweza kuibiwa kwa sababu ya uovu wake. Isaya 50:1 Imeandikwa, “Bwana asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo naliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu”.
 
Majeshi ya Bwana wakisikiliza na kuandika somo la biashara za kichawi katika ibada ya leo.
WIVU NA HUSUDAMwanzo 37:11 Imeandikwa, “Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili”. Hizi ni habari za Yusufu aliyewai kuota ndoto. Ndoto zake zilikuwa zenye kuonyesha uwezo wa kuwa mtu mkubwa siku za usoni. Kwa kawaida mtu hamwonei wivu mtu asiyemfahamu. Yusufu aliuzwa na ndugu zake wa karibu maana yake walimwonea wivu Wachawi wakiishaona mtu anafanikiwa sana kwenye ulimwengu wa roho Mathayo 10:36 Imeandikwa, “na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake”.

 NDOTO ULIZONAZO. Ndoto ni kile kitu ambacho Mungu amekiweka ndani yako. Ndoto ni yale mambo ambayo mtu hawezi kutenda pasipokuwa na msaada kutoka kwa MUNGU. Mtu mwenye ndoto ananena mambo makubwa, nitajenga gorofa, nitamiliki viwanja na makampuni makubwa. Wachawi lazima waone wivu na kuamua kuuza roho ya mtu huyu.

Mathayo 24:14-15 Imeandikwa, “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu)” Marko 14:10-11 Imeandikwa, “Yuda Iskariote, yule mmoja katika wale Thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao. Nao waliposikia walifurahi, wakaahidi kumpa fedha. Akatafuta njia ya kumsaliti wakati wa kufaa”.
 
Majeshi ya Bwana akifunguliwa kutoka katika kifungo cha biashara ya kichawi.
Amua na ufunge biashara za kichawi kwa jina la Yesu. Unayo mamlaka ya kufunga duniani na kila ufungacho hapa duniani kitafungwa na mbinguni. Funga wachawi, waganga, wasoma nyota na madaruweshi ambao ni mawakala wa biashara za kichawi. Funga wachawi wote na stoo zote kwa jina la Yesu nawe utakuwa salama.

========== AMEN ========
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp & Sms only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro


Share:
Powered by Blogger.

Pages