Sunday, December 3, 2017

KUWATOWA WALIOFUNGWA KATIKA NYUMBA YA GIZA

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

JUMAPILI : 3, DESEMBA, 2017

MHUBIRI: MCHUNGAJI, DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
Mchungaji kiongozi akiwa katika ibada


MITHALI 7: Imeandikwa, “Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.” MITHALI 2:18 Imeandikwa, “Maana nyumba yake inaelekea mauti, Na mapito yake yanakwenda kwenye wafu.” Mungu anatuambia katika neno takatifu kwamba kuzimu kuna nyumba ambayo ndani yake kuna njia inayoelekea kuzimu. Tumejifunza mara nyingi kuhusu habari za kuzimu kwamba ina mikono, makomeo, macho na vyumba pia. Tuonaona kuzimu kuna vyumba kama maandiko matakatifu yanavyo sema kuna vyumba vya mauti. Kuna nyumba nyingine ukikaa unaweza kusikia harufu ya mauti. Kwenye nyumba hiyo kuna njia inayoelekea kuzimu ambako kuna vyumba ambavyo ni mauti. Njia hiyo inaongaza kazi, fedha zako, ndoa yako kuelekea mauti. Unaweza kuona mtikisiko wa ndoa, biashara, huduma na miradi kumbe ni roho ya mauti imeingia.

Nyumba za giza ni nyumba ambazo hazionekane katika ulimwengu wa mwili. Hizi ni nyumba za rohoni ambazo zinatumiwa na shetani pamoja na mawakala wake. Hizi ndio nyumba zinazotumika kufungia maisha ya watu. Chanzo cha nyumba za kuzimu huwa ni katika ulimwengu wa mwili, Inawezekana umejenga katika kiwanja kilichonuiziwa au ni sehemu iliyowahi kutumika kama madhabahu ya wachawi. Nyumba zilizojengwa kwenye viwanja hivi mara nyingi utasikia mtu anasema kasikia harufu ya mauti.
Utajuaje kwenye nyumba unayokaa wachawi walikuwa wanafanya mikutano hapo? Unakuta baadhi ya watu usiku wanakosa usinginzi, au mabundi yanalia usiku, kumbe ilikuwa njia yao ya kushukuia kuzimu. Mtu akipita bila yeye kujua ni njia ya kuzimu. Mashetani yanambeba wanampleka moja kwa moja kuzimu kwenye vumba vya mauti. Mauti kazi yake kubwa ni kuua tu. Mauti ina harufu 2 WAKORINTHO 2:16 meandikwa, “katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?” kuna harufu ya mauti kwenye kazi, kwenye ndoa. Ukiri: kwa jina la Yesu nakataa harufu ya mauti kwenye kazi, ndoa, biashara naweka uzima kwenye kazi, kwenye ndoa.

Makutano wakisikiliza neno la Mungu kwa makini


Kuzimu kuna vyumba vya mauti, na kama mbinguni kuna vyumba vya uzima. Maana shetani anaigiza kwa kuchukua nakala ya kile alichokiona katika Ufalme wa mbinguni. Kama kuna makomeo na milango maana yake kuna vyumba na wakiwakamata watu wanawafungia huko. Nyumba hizi za kuzimu ni zile zile zinazofunga kazi yako, ndoa, shule hata nafsi ya mtu. Hizi nyumba zinatumika kama magereza, watu wanawafungia kule na wanawekewa walinzi wa kishetani ili wasitoke. Watu hawa wanalishwa vitu vichafu kama pumba, mawe na mkaa. Ukiona mtu unaumwa sana huponi, au magonjwa ya kupitiliza jua kuna sehemu yako kama nafsdi, mwili au roho imebebwa na kufungiwa kwenye nyumba ya giza. Tunaona chumba cha giza kina mateso, unatakiwa kuvivunja hivyo vyumba vya mateso na mauti kwa jina la Yesu Kristo.

Kuna watu wamenaswa kwenye mashimo, matope, wanaweka majumba ambayo yana utelezi. Lakini leo Bwana atakutoa huko kwenye nyumba ya giza, nyumba yeyote ya uganga, uchawi leo kwa jina la Yesu. Umenaswa kwenye magonjwa ya macho, ukimwi, kansa, leo nayashusha kwa jina Yesu. Ndani ya nyumba kubwa kuna vyumba vidogovidogo, kimojawapo cha mauti ya elimu, mauti ya miguu, mauti ya kuiba miguu, kingine ni mauti kuleta ugomvi kwenye familia.

Isaya 14:17 imeandikwa, “Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?” Pia katika Isaya 42:6 – 7 imeandikwa, “Mimi, Bwana, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.” Kumbe kuna macho yaliyofungwa, mtu anaota akiwa kwenye chumba gizani. Waliofungwa wapo mashimo , makaburi. Lakini Mungu anasema Isaya 26:19 imeandikwa, “Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.” Kuna watu wamekufa mazingira tatanishi, Bwana anasema utaishi tena, ndoa, kazi, biashara, elimu na familia itaishi tena.
Mtu akifunguliwa kutoka chumba cha giza

Kama kuna mtu amaekufa mazingira tata mlete kanisani, na mwingine hajafa ndo anaelekea kufa mlete katika nyumba ya Ufufuo na Uzima, maana wengine wanaanza kufa taratibu. Bwana anasema maiti zitasimama, zitafufuka tena. Amua kuvivunja vyumba vya mauti nawe utakuwa mzima kwa jina la Yesu.


KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/
Share:
Powered by Blogger.

Pages