GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
JUMAPILI: 10, DISEMBA, 2017
MHUBIRI: MCHUNGAJI KIONGOZI, GODFREY MWAKYUSA (SHINYANGA)
Mchungaji Godfrey Mwakyusa akifundisha neno la Mungu. |
Kwa kawaida kila unachokiona huwa kina
asili yake au kilipotoka. Kila mwanadamu amezaliwa na mwanamke na wanyama
huzaliwa na wanyama weyewe. MWANZO
1:26-28 Imeandikwa, “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano
wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na
wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na
mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke,
mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani,
na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” Mungu aliwabarikia
wakaze na kuongezeka wakaijaze nchi. Maana yake ukazae na kuongeza, na si kuzaa
tu bali uzae na kuongezeka. Chochote unachokishika kizae na kuongeka.
Kuongezeka kimasomo, mtaji, biashara, familia na ustawi.
MWANZO 3:1-6 Imeandikwa, “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko
wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi
ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke
akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya
mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije
mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya
kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa
kama Mungu, mkijua mema na mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa
chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa
katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.”
Nyoka alikuwa mwerevu akawaambia mkila
mtafanana kama yeye. Baada ya kula uwepo wa Mungu ukaondoka. MWANZO 3:12-15 imeandikwa, “Adamu
akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti
huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke
akasema, Nyoka alinidanganya, nikala. Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu
umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote
walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha
yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na
uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mungu
aliweka uadui kati ya uzao wa mwanamke na nyoka. Leo tutawaponda kwa jina la
Yesu, uzao, masomo, biashara, afya itakombolewa.
Hapa Mungu ametupa uhalali wa
kuwaganyaga uzao wa nyoka kwa jina la Yesu. Kazi iliyomezwa, ndoa, masomo leo
atatapika kwa jina la Yesu. Hata wewe umezaliwa na mwanamke bila shaka
umefungwa kwenye magereza, kwenye mashamba leo utatoka kwa jina la Yesu.UFUNUO 12:13-17 imeandikwa, “Na
joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule
aliyemzaa mtoto mwanamume. Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule
mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa
wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. Nyoka akatoa katika
kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto
ule.”
Nyoka alipomuuzi mwanamke akatupwa
mpaka nchi, na mwanamke alipokuwa akijifungua nyoka akafungua kinywa ili
ammeze. Lakini mwanamke alipewa mabawa mawili ili alombowe uzao wake. Nyoka
alitoa maji ili mwanamke akasombwe na mto ule. MATHAYO 18:18 imeandikwa, “Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga
duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani
yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” Leo tutafunga balaa zote, mikosi yote
kwa jina la Yesu.
KUTOKA 2:15-19 imeandikwa, “Basi Farao alipopata habari,
akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi
ya Midiani; akaketi karibu na kisima. Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti
saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi
la baba yao. Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena
zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.”
Farao alijua mtawala atakuwa mwanaume,
akaamua kuongea na wazalishaji mtoto akizaliwa wa kiume auwawe lakini wa kike
wamwache aishi. Lakini wakunga hawa hawakufanya matakwa ya mfalme. Mfalme
akatafuta njia nyingine ya kuwaaangamiza, katikati ya tangazo Musa alizaliwa, Musa
akaokotwa na mtoto wa Farao. Mama yake Musa alipewa kazi ya kumnyonyesha Musa
na akawa analipwa. Katikati ya magumu Mungu anaonekana.
Waamuzi 13:2-5 imeandikwa, “Palikuwa na mtu mmoja wa Sora, wa
jamaa ya Wadani; jina lake akiitwa Manoa; na mkewe alikuwa tasa, hakuzaa
watoto. Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe sasa
u tasa, huzai; lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume. Basi sasa,
jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;
kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite
juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni;
naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.” Kuna uwezekano
mtu akabeba mimba kwa uwezo wa kishetani/kijini/mganga kienyeji. Na mtoto
alipozaliwa wakaenda kunyoa na kumkata kitovu. Unapokuwa wanaweza kufuatilia
unachokifanya kwa sababu wanavitu vyako.
Unawezekana unapata matatizo kwa sababu umetokana na uzao wa mganga wa
kienyeji.
Mchungaji Mwandamizi Daktari Hapiness Muhimbula akimfungua mtu. |
Yeremia 15:1-3 imeandikwa, “Ndipo Bwana akaniambia, Hata
wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa;
watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao. Kisha itakuwa, hapo
watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, Bwana asema hivi,
Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga;
au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka. Nami
nitaamrisha juu yao namna nne, asema Bwana; upanga uue, na mbwa wararue, na
ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.”
Tunaona Samsoni alipozaliwa alikuwa na asili yake. Aliponyolewa nywele zake
asili yake ilipotea.
1 Samweli 1:1-6 imeandikwa, “Palikuwa na mtu mmoja wa Rama,
Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa
Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu naye alikuwa
na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa
Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. Na
mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na
kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo.”
Pamoja na Pennina kumchokoza Hana, Hana
hakukata tamaa. Siku moja kuhani alimkuta Hana midomo yake ikichezacheza
akamuuliza kwa nini umelewa asubuhi hii yote. Hana akamjibu mimi naumimina moyo
wangu kwa Bwana. Siku chache zilizofuata Hana akamzaa shujaa wa Bwana Samweli.
Unapochelewa kuzaa usife moyo Bwana amekuandalia jambo kubwa, endelea kuomba
utapokea sawasawa na haja ya moyo wako. Inawezezkana umepewa taarifa mbaya
kutoka kwa madaktari, hizo ni taarifa za wanadamu lakini leo yupo Yesu
atakayerudisha vyote. Mungu anasema njia zenu sio njia zangu, yeye anatuwazia
mema.
1 Samweli 1:10-18 imeandikwa, “Naye huyo mwanamke alikuwa na
uchungu rohoni mwake, akamwomba Bwana akalia sana. Akaweka nadhiri, akasema, Ee
Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka,
wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume,
ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe
hautamfikilia kichwani kamwe. Ndipo Eli
akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako. Hana
akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni,
mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za Bwana. Basi
huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana
tena.” Hana alipokuwa anaomba, Kuhani akamwambia
Bwana akupe sawasawa na haja yako. Hii inatufundisha kuwa neno la Kuhani ni la
muhimu wakati wa uhitaji wako. 1 SAMWELI
1:20 Imeandikwa, “Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua
mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake Samweli, akisema, Kwa kuwa
nimemwomba kwa Bwana.” Mungu alimpa mtoto wa kiume na Hana alitimiza
nadhiri kwa kumtoa Bwana.
Vita ya uzao ni vita ya kufa na
kupona, ndo maana shetani ameachilia waume na wake wa kipepo. Unapokuwa umelala
unaingiliwa kwenye ndoto. Inawezekana una watoto baharini au unanyonyesha
ndotoni, katika hali ya kawaida huwezi kupata ujauzito katika ulimwengu wa
mwili. Dalili za mtu aliyefunga ndoa za kipepo Kiuno, mguu wa kushoto unakufa
ganzi, ukiota unatoka bichi (out). Shetani anafanya hivi kwa sababu anataka
uzao wake uchanganyike na uzao wa mwanadamu ili aweze kutenda kazi kwa urahisi.
Ni kwa nini wanaume au wanawake wa kipepo, sababu ni kama zifuatazo, inawezekana
nyota yako inang’aa. Inawezekana
nyota yako ya uzao wako. Hivyo wanakuchukua ili ukazae kule kuzimu. Kuna mwanaume kakupenda kwa sababu ya nyota
yako, anapokuingilia kimwili usiku yeye anafanikiwa katika kazi zake. Katika
ulimwengu wa roho mnaoneka ni mwili mmoja ni kwa sababu ya agano. Ukiingia
katika siku zako unapatwa na maumivu
makali, hii hali si ya kawaida unatakiwa ushughulikie. Leo hii wanatumia
kucha, mawigi na kope za bandia. Kucha na kope zimetolewa kwa maagano ya kuzimu
ili wapate malikia wengi duniani.
MWANZO 11:30 Imeandikwa, “Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na
mtoto.” MWANZO 25:21 Imeandikwa
“Isaka
akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana
akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.” Baba alichelewa kuzaa na
mtoto alichelewa pia. Kumbe ukichelewa unatakiwa uendelee kuliitia jina la
Bwana na ukipokea Baraka zako jina lako linabadilika. LUKA 1:5 Imeandikwa, “Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi,
palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa
mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elisabeti.” Alipojifungua mtoto
aliitwa Yohana, jina limebeba Baraka za mtu.
ISAYA 14:29b imeandikwa, “Maana katika shina la nyoka
atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye.” Zaburi 22:10 imeandikwa, “Kwako
nalitupwa tangu tumboni, Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.”
Unakuta tangu tumboni wengine washaanza kunywa makombe, dua. Unakuta mtu
anakula mkaa, udongo kumbe mama yake alivyokuwa mjamzito alikuwa anakula
udongo. Ukiona mtu anakula udongo ujue tumboni kwake kuna joka. Leo ukatae kula
vyakula vya kipepo kwa jina la Yesu.
ZABURI 58:3 imeandikwa, “Wasio haki wamejitenga tangu
kuzaliwa kwao; Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.” Unakuta mtu
anaongea uongo kumbe ni asili yake tangu
tumboni. Kataa kila asili ambayo umeipata kutoka kwa mama yako ambayo si nzuri kwa
jina la Yesu. LUKA 1:13 -15 Imeandikwa,
“Lakini
yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo
Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Nawe
utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. Kwa
sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa
Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.” Namna Yohana alivyopokea
Roho mtakatifu tangu tumboni.
LUKA 1:39-43 Imeandikwa, “Basi, Mariamu akaondoka siku
hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,
akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Ikawa Elisabeti aliposikia
kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake;
Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa
wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno
hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?” Kumbe mtu anaweza kupokea
roho kupitia sauti ya mtu. Mtu anaweza kupata matatizo au Baraka kupitia
salamu. WAEBRANIA 1:7 imeandikwa “Na
kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake
kuwa miali ya moto.” ZABURI
104:4 imeandikwa, “Huwafanya
malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali.” Unakuta unapata
fursa nzuri lakini zinapotea, umenyang’anywa kinywa.
Mchungaji Kiongozi Daktari Godson Issa Zacharia akimfungua mtu na uzao wake umekuwa salama kwa jina la Yesu. |
ISAYA 6:8 imeaandikwa, “Kisha nikaisikia sauti ya
Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo
niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.” Mungu alikusudia kuokoa uzao kwa
kumtoa mwanawe wa pekee. YOHANA 6:16-17
imeandikwa, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana
Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu
uokolewe katika yeye.” Mungu aliupenda ulimwengu, kutoa kunaendana na
kupenda. Mungu alimtoa mwanawe ili upate uzima tele. Kazi, ndoa, masomo,
biashara yako iwe na uzima tele. Lazimisha ulimwengu wa roho ukuachilie ili
uongezeke. Kila unachokianza maana yake kizae na kuongezeka.7
KWA MSAADA ZAIDI NA
MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: pastor:dr.godson
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/