Sunday, December 31, 2017

LIPANUE HEMA LAKO LA KUWEKEA BARAKA ZA MWAKA 2018

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH {GCTC}

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA- MOROGORO

SNP DR. GODSON ISSA ZACHARIA

JUMAPILI: 31 DISEMBA 2017

MHUBIRI: SNP DR. GODSON ISSA ZACHARIA

 
Mchungaji kiongozi Godson Issa Zacharia akifundisha somo la panua hema lako  kupokea Baraka zako za mwaka 2018
Mungu wetu ni Mungu wa ajabu sana na ametupatia imani ambayokwayo tunashinda na kufanya mambo makubwa kama nini.Imani ina tabia ya plastiki, inaweza kuongezeka kadili tutakavyo, imani yako utakavyo ipanua kupokea baraka zako ndivyo Mungu atakavyo kupatia. Ukifungua imani yako kama kikombe Mungu nimwaminifu naye atakupa kadili ulivyo weka, ukiweka jagi naye Mungu atajaza jagi lako. Kadiri utakavyo mwomba Mungu akujaze ndivyo atakavyo kupatia,kama pipa Mungu atakujazia pipa.kwa jina la Yesu.
Nabii Isaya aliona mambo mabaya yawapatayo watu katika maisha yao, ya kwamba maisha yao ni tasa, hakuna kuongezeka wala kufanikiwa, kila wanacho fanya hakizai .biashara zao hazileti faida, kazi zao hazina matunda, akatabiri kuongezeka kwa baraka za watu kwa kadiri watakavyo fungua mioyo yao kupokea kwa imani. Imeandikwa..
“ Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema Bwana.  Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.  Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena. Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote. Maana Bwana amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.  Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi wako. Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea. Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye.” (ISAYA 54:1-10)
Maelfu ya waumini wakisikiliza neno katika ibada ya leo

Bwana anasema na wewe leo ambaye umefunga kamba fupi kwa ajili ya mafanikio yako, wewe uliyeandaa kapu dogo kwaajili ya kupokea baraka zako,uliyeandaa hema dogo kwa kupokea utajiri wako, yeye anasema hama hapo panua kamba yako, panua hema yako upate kupokea kadiri ya ukubwa wa chombo chako .Anataka upanue hema yako leo, andaa mahari  kwa ajiliya kuwekea baraka zako, panua biashara yako kwaajiri ya faida kubwa, panua mashamba yako kwa maana utaenda kuvuna kwa kiasi kikubwa, panua mtaji wako kwa maana Bwana anaenda kukupa kadiri ya ulivyo andaa chombo chako cha kupokelea,  na utapokea kwa jina la Yesu.
Mungu alisema na Joshua kwa habari ya mipaka ya wana wa Israeli, alisema kila mahali watakapo kanyaga amewapa wao, wala hakusema kwa eneo dogo,aliwamilikisha maeneo makubwa hata nchi ya Lebanoni hata mto flati. 
“Kila mahali zitakapopakanyaga nyayo za miguu yenu, nimewapa ninyi, kama nilivyomwapia Musa. Tangu jangwa hili na mlima huu, Lebanoni, mpaka mto ule mkubwa, mto wa Frati, nchi yote ya Wahiti, tena mpaka bahari ile kubwa upande wa machweo ya jua, hapo ndipo patakapokuwa mpaka wenu.” (YOSHUA 1:3-4)
Mungu anakutaka upanue mipaka yakoleo kama alivyo sema na wana wa Israeli anasema na wewe leo kuwa kila mahala utakapo kanyaga amekupa upamiliki, hivyo panua mipaka ya maeneo yako, panua mipaka ya biashara yako, panua mipaka ya elimu  yako, mipaka ya kazi yako kwa maana Bwana amekupa kila mahala  utakapo kanyaga kuwa milikiyako. Hutakufa hadi umiliki baraka zakokwa  jina la Yesu. Hakuna wa kuzuia wewe panua hema yako, panua njia zako kwa maana uwezo wa kujaza si wako, uwezo wa kujaza ni wa Bwana naatakujaza kwa jina laYesu.
Hakuna aliye acha vyote akamfuata Yesu akakosa kitu, Kwa maana Bwana anasema yule atakaye acha vyote na kumfuata atapata mara mia, kwahiyo sisi tuliye acha vyote nakuambatana na Yesu hatutakosa kitu tutapata mara miamoja kwa maana yeye alifanyika maskini ili sisi tuwe matajiiri kwa jina la Yesu.
Platform ministry wakiongoza sifa na kuabudu katika ibada ya leo
Ayubu alikua ni mtu mwenye mwili kama sisi, yeye alikua mkamilifu, na mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Alikua mtakatifu na hata Mungu akakubali utii wake naye  Mungu akambarikia kwa mali , wanyama na utajiri wa kila namna ,alimbarikia akawa na watoto wengi sana. Wewe ni nani ata usibarikiwe kama umemtumikia Mungu kwa kuacha vyote na kuishi maishamatakatifu?,  kimsingi panua hema yako ili upokee baraka zako kwa jina la Yesu. 
“Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.  Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu.  Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.”  (AYUBU1:1-4)
Tunajifunza wanawa Israeli walipokua utumwani Misri walikua wanateseka kwa mambo mabaya waliokua wanafanyiwa na Farao na majeshi yake.Mungu akasikia kilio chao akatuma mtu aende kuwatoa, wakapita katika bahari ya shamu huku majeshi ya Farao yakiendelea kuwafuatilia, hata hivyo wote wakaangamia katika bahari ya shamu.
Mtu ambaye hajaokoka nisawa na wana wa Israeli nchini misri, lakini akisha okoka kuingia kwenye wokuvu hutoka Misri kuingia kwenye baraka zake lakini shetani uendelea kumfuatilia na kufunga hatua zake na mafanikio yake, biashara yake inapungua, kazi zake kuelekea mafaniko yake zinafungwa. Kama vile Bwana alivyowatosa majeshi Farao baharini ndivyo atawatosa bahariniadui zako nawe utavuka kuingia kwenye Baraka zako, kwenye nchi ya ahadi yenye maziwa na asali kwa jina la Yesu.
Hakuna aliyewahi kumiliki pasipo kupigana; tunajifunza hata malaika walipigana kumwondoa shetani mbinguni, hata katika hali ya kawaida watu hupigana ili kumiliki. Idi Amini alipigana naTanzania chini ya Rais Julias Nyerere kwaajili ya kumiliki mipaka ya kagera. Nasisi wakristo  ilitupate kumiliki baraka zetuni lazima tupigane kwa njiaya kiroho, tunapigana kwa maombi ili wale wazuiaji waondoke kwenye mipaka yatu, tunakataa kutawaliwa  nashetani katika maisha yetu, kwa kupigana  tuna panua hema ya mafaniko, tunapanua mipaka kwa jina la Yesu.
Mtu anapozaliwa ana kuwa na baraka zake , lakini nivigumu kumiliki baraka hizo pasipo kupigana. Katikabiblia kuna mfano wa mwanamke mjane ambaye hakupanua hema yake kupoke baraka zake
“Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.  Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache. 4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge. Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina. Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo.Akamwambia, Hakuna tena chombo.Mafuta yakakoma. Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.”(2WAFALME 4:1-7)
Showers wakicheza na kumsifu Mungu katika ibada ya leo
Mume wa mwanamke huyu alikua anapenda sana madeni na mumewe alipokufa aliacha madeni hata kufika watoto wake kuuzwa kwa ajili ya madeni, pale alipokutana na nabii Elisha mwanamke huyu mjane alimwambia nabii habari za taabu yake. Elisha akamwambia nenda ukatake vyombo kwa majirani zako tena sio vichache na utie hayo mafuta. Lakini huyu hakuwa mwaminifu kwa nabii, yeye aliomba vichache na pale vilipojaa mafuta yakakata na akapata kadili ya alivyo andaa. Yaani alipata dili la kuwa bilionea akaanda mpango wa kuwa milionea.
Imani ndio itendayo kazi, kadili utakavyo amini ndivyo utakavyo pokea usitegemee maneno au uwezo wa mwanadamu, Mungu pekee ndiye atakaye nyoosha mapito yako na kukubariki. Inagharimu tu kuambatana.vile unakua mwaminifu kwa Bwana ndivyo atakavyo kubariki na kukuzidishia atakujaza kulingana na ukubwa wa hema yako, hivyo panua hema yako kwa jina la Yesu.
Mshirika akifunguliwa kutoka katika vifungo
Tunajifunza habari za Elisha jinsi alivyo ambatana na Eliya akaacha vyote na mwisho akapata Baraka, Elisha alipata vizuizi vingi lakini ile nguvu ya kuambatana aliyokua nayo ndiyo ilimwimalisha na kusonga mbele, mwishoni Eliya akamwambia Elisha omba utakacho nitakupatia,nayeElisha akaomba kupata nguvu mara mbili ya Eliya, naye Eliya alipochukuliwa vazi lake lilianguka chini naye alipolivaa akaingiwa na nguvu kadili alivyoomba. Nawe usimwache Yesu kwa maana ukiambatana na Yesu utapata baraka zako maradufu, yoyote atakaye ambatana na Bwana atapokea mara mbilikwa jina la Yesu.
======== AMEN ========
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA:
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr.Godson Zacharia
TEL: +255 719 798778 (WhatsApp&Sms only)

BLOG: Ufufuo na Uzima Morogorohttp://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/
Share:
Powered by Blogger.

Pages