Sunday, January 7, 2018

IPASUENI MADHABAHU YA UHARIBIFU


GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH


KANISA LA UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO


SNP DR. GODSON ISSA ZACHARIA


JUMAPILI: 7 JANUARI  2018


MHUBIRI: SNP DR GODSON ISSA ZACHARIA

Mchungaji Kiongozi Daktari Godson Issa Zacharia akifundisha neon la Mungu katika Ibada ya leo.
Uharibifu ni mpango kazi wa ibilisi. Shetani ndio mungu muovu wa dunia hii. Huyu mwaribbifu alikuja ili kuharibu. “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.(Yohana 10:10).



Huyu mwaharibufu anafanya kazi ya kuiba nyota, kinywa, mikono, kazi, ndoa, na akisha iba anaharibu. Uharibufu ni mambo maovu. Shetani hajaja ili upate kibali/uoe/kuolewa bali  uharibikiwe. Leo tutaipasua madhabahu ya uharibifu ili nyota yako irudi kwa jina la Yesu. Mwaka 2018 ni mwaka wa furaha kuu, ni mwaka wa kucheka tena, kwa jina la Yesu.



Mungu anasema ipasueni madhabahau ya uharibifu. Uharibifu ni matendo yale yanayokupelekea uharibikiwe, katika maisha yako. Shetani ndiye anayesababisha uharibifu. Uharibbifu huu unatokea kwenye madhabahu. Madhabahu ni daraja linalounganisha vitu vya ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho. Ulimwengu wa mwili ni vile vitu vilivyoumbwa vinaonekana mfano mto, milima, dhahabu na n.k. Ulimwengu wa roho ni ulimwengu ambao vitu vyake havionekani kwa macho ya kawaida. Asili yake ni roho, havionekani hata utumie vitu vya kisayansi mfano, majini, mapepo,  na n.k. Shetani yeye ni roho na hawezi kufanya kazi pekee yake. Mungu na yeye ni roho. Ili tuweze kuwasiliana na Mungu ni lazima kuwepo na daraja. Daraja linalotuunganisha na Mungu ndio linaitwa Madhabahu ya Mungu. Vitu vyote vinavyoonekana asili yake ni ulimwengu wa roho. Dunia na vyote vinavyoonekana vinatokana na ulimwengu usionekana. Kila kitu kinachoonekana leo vilitokana na ulimwengu usionekana.



Baadhi ya Makutano wakisikiliza neno  la Mungu wakati wa Ibada.

“Hapo mwanzo Mungu aliziumba (mbingu) na nchi. Nayo nchi ilikuwa (ukiwa) tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.  Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.  Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.  Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.  Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.  Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.  Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.  Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka. tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.  Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi; na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne. Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.  Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.  Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.  Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwanzo 1:1-27)



Tunaona katika mstari wa 3, 6, 7, 9, 11, 14, 20, 24 alisema na vikawepo kama alivyosema. Huu ni ulimwengu wa roho ukisema vitu vinatokea. Kama Mungu alihitaji daraja ili kutekeleza yale aliyekusudia ndivyo hivyo shetani anahitaji madhabahu ili kutenda yale anayokusudia. Kama unahitaji biashara, kazi, gari, watoto, nyumba, ili vije lazima kuwepo na madhabahu na kuhani wa madhabahu ili upokee katika ulimwengu wa mwili. Mungu alimwambia Yeremia kabla sijakuumba nalikujua, kabla hujazaliwa nalikutakasa, hii ina maana kwamba katika ulimwengu wa roho alionekana tayari ni shujaa wa Bwana.


Platform team wakiongoza kipindi cha sifa na kuabudu.

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;” Yonaha 1:12



Madhabahu ni daraja, ili shetani afanye kazi anahitaji (binadamu). Huyu ndiye kuhani wa madhabahu nap engine wanajulikana kama mawakala mfano ni wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota. Kuhani wa madhabahu anaunganisha ulimwengu wa roho na mwili. Ulimwengu wa roho una wakazi wa aina mbili. Wakazi ambao ni watakatifu hawa ndio wale wamwanio na kumtumikia Mungu Yehova. Na wakazi waovu mfano mapepo, mashetani, majini. Mfano mtu anapoota ndoto anafukuzwa kazi ghafla anafukuzwa kazi kweli. Hii ni kwa sababu kwenye ulimwengu wa roho majini yalishaharibu yanatumwa kwenye ulimwengu wa mwili ili kulitekeleza ilo na inakuwa hivyo.   



Madhabahu hii tunayoongelea leo ni madhabahu za kichawi ambazo wanazitumia kufanya uharibifu. Madhabahu nyingine zinawezekana zipo nyumbani kwako leo kwa jina la Yesu zitapasuka. Kuna mwingine akiamua kuja kanisani madhabahu inamsemesha, au inaweza kumwingia mtu ili akuzuie, huyo mtu  anakuwa  amebeba  madhabahu ya udhaifu/magonjwa ya ukoo anaona   unataka kutoroka  hivyo anakuja  kukuzuia.


Baadhi ya Makutano walioamua kukata shauri na kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao.

Jinsi madhabahu inavyofanya kazi, madhabahu ya kichawi wanapoona unaendelea vizuri au unaenda kupona wanaongeza kafara. Kafara hizi hutolewa juu ya madhabahu za kichawi na kunuiziwa mabaya. Mfano kama walitoa njiwa wanatoa kuku. Kila wanapoongeza kafara ndivyo  nguvu ya kifungo kinavyozidi. Hata nyumba ya Ufufuo na Uzima ina madhabahu ya damu ya mwanakondo. Nguvu ya madhabahu inaongezeka kwa maombi. Maana imeandikwa maombi ni kama uvumba mbele za Mungu.



Wachawi wanaweza kujenga madhabahu. Tunaposema kuvunja ni kwa sababu madhabahu imejengwa. Ukitaka kufanya kazi lazima ujenge madhabahu watumishi wengi katika Biblia walijenga madhabahu, Musa, Ibrahimu na wengine wengi. Wewe mwenyewe unaweza kutengeneza madhabahu ndani yako. Ukiongeza nguvu za maombi kwa kuomba kwa bidii na  unanena madhabahu yako inaongezeka nguvu. Je hamjui miili yenu ni hekalu la Roho mtakatifu.



Leo tutapasua madhabahu ya kichawi na kuvunja mikono ya kuhani mwaribifu. Maana mikono yake ndo inafanya kazi kuchanganya dawa ili ubaya ukupate wewe.



“Ndipo Yeroboamu akajenga Shekemu katika milima ya Efraimu, akakaa huko. Akatoka huko akajenga Penueli. Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. Kama watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani. Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani. Tena akafanya nyumba za mahali pa juu, akafanya na watu wo wote, watu wasio wa wana wa Lawi, kuwa makuhani. Yeroboamu akaamuru kushika sikukuu katika mwezi wa nane, siku ya kumi na tano ya mwezi, mfano wa sikukuu iliyokuwa katika Yuda, akapanda juu ili kuiendea madhabahu. Akafanya vivyo katika Betheli akiwatolea dhabihu wale ng'ombe aliowafanya; akawaweka katika Betheli wale makuhani wa mahali pa juu alipokuwa amepafanya. Akatoa dhabihu juu ya ile madhabahu aliyoifanya katika Betheli, siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, mwezi aliouwaza moyoni mwake mwenyewe; akawaamuru wana wa Israeli waishike sikukuu hiyo, akapanda kuiendea madhabahu, ili kufukiza uvumba.

(1Wafalme 12:25 -33)

 
Mchungaji Kiongozi akimfungua mtu kutoka Madhabahu ya uharibifu.
Yeroboamu alibaini ya kwamba wana wa Israeli wakiomba atauwawa. Wachawi wanajua ukiomba mambo yao yataharibika na watakufa. Yeroboamu alivyoona hivyo akaamua kutengeneza madhabahu ya dhahabu na watu wa Mungu walimfuata. Na madhabahu hiyo ilionekana ni uharibifu na Mungu akamuinua mtu mmoja ili kuipasua. Leo Mungu anatafuta mtu mmoja atakayeenda kuipasua madhabahu ya uharibifu iliyojengwa na Yereboamu wa leo ili kuivunja madhabahu inayoleta kansa, magonjwa kwa jina la Yesu.


Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la Bwana, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba. Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la Bwana akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako. Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika. Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena. Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana.” (1 Wafalme 13:1-5)



Majivu yalimwagika kwa sababu ndani ya majivu kuna fedha, kazi, dhahabu, biashara, ndoa, masomo, afya, leo madhabahu ikipasuka utapokea kwa jina la Yesu. Yeroboamu alikasirika baada ya kusikia maneno ya yule mtu wa Mungu, mfalme akanyoosha mkono wake pale madhabahuni, basi mkono wa mfalme ukakatika. Mchawi anayekufuatilia maisha yako leo mkono wake ukatike kwa jina la Yesu. Huyu kuhani wa madhabahu alikuwa na kiburi kwa kuwa alikuwa anategemea majoka, mkono ulivyokatika kashuka chini akanyenyekea.


Showers of Glory wakimsifu Mungu na kucheza wakati wa Ibada ya Leo.
"Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.” (1 Wafalme 13:6)



Hapa mfalme aliomba mkono wake na akarudishiwa, hii ni ishara ya mammlaka, ukiamini utapokea nguvu na mamlaka. Ili kile wanachokitegemea kivunjike au kiondoke kabisa kwa jina la Yesu. Amua leo kuwakata mikono waliokuandalia madhabahu ya ubaya maishani kwako. Tumia nguvu iliyomo katika jina na damu ya Yesu ili upasue madhabahu ya watesi wako.
Share:
Powered by Blogger.

Pages