Pages

Sunday, December 24, 2017

UDHAIFU WA KICHAWI

GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)

KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

MHUBIRI: MCHUNGAJI, DKT. GODSON ISSA ZACHARIA

JUMAPILI 24, DISEMBA 2017
Mchungaji kiongozi Dkt.Godson Issa Zacharia, akihubiri katika ibada ya leo.
Udhaifu ni hali ambayo ikimpata mtu kuna mambo hawezi kuyafanya. Udhaifu wa kichawi  ni hali pia inayolenga  mtu asiweze kutenda mambo Fulani mtu anakuwa hawezi kuona, kusoma, kutunga mimba, kuoa au kuolewa, hawezi kujenga nyumba, kula nyama/samaki anakuwa mtu wakuchangua vyakula vya kula hii ni kwa sababu wachawi wamempandia kitu ndani yake ambao ni mapepo ya udhaifu yanamtia mtu udhaifu asiweze kufanya jambo lolote.

Udhaifu wa kichawi unalenga pia kumfunga mtu katika udhaifu  asisikie habari njema iliyoambatana na Baraka zake au nyota yake ya mafanikio na kila anapojaribu kuenenda  katika hatua yoyote ya maendeleo anashindwa  au anajisikia kutoweza kabisa  kabla ya kuanza pia udhaifu wa kichawi unaweza kumfunika mtu asipate msaada wowote kutoka kwa watu.

 Kuna mwingine uwezo wa mtu  upo kwenye mikono. Wachawi wakiona hivyo wanawahi kufunga mikono, unakuta mikono ghafla imevimba wachawi wanakuwa wamekuweke udhahifu. Kuna wengine uwezo wao upo kwenye ndoa. Ukioa au kuolewa wanafanikiwa. Makapuni yatafunguliwa, biashara zitaanza wachawi wanaamu kukufunika ili usionekane. Sasa panatakiwa apatikane mtu mmoja atakayeliitia jina la Bwana vifuniko vitaondoka. Udhaifu unakuja kwako kupitia wachawi baada ya kutoa sadaka na kisha anatuma mashetani ndani ya maisha ya mtu, kazi, biashara.

Mathayo 8: 14-16 imeandikwa, “Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,” Yesu aliletewa watu wenye mapepo na aliwaponya kwa neno lake wale wote ambao walikuwa hawaweziwalikuwa hawawezi kwasababu ya mapepo yaliyokuwa ndani yao  ndivyo ilivyo hata leo  Kuna mambo yamekaa ndani ya maisha yako kwa nanmna ya kutoweza, leo nalituma neno la Bwana likavunjevunje vifungo vyote kwa jina la Yesu.

Majeshi ya ufufuo na uzima wakisikiliza neno kwenye ibada ya leo.

Mathayo 4:23 imeandikwa, “Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.” Yesu alikuwa akihubiri habari  njema za ufalme, akawaponya udhaifu na magonjwa. Yesu alikuwa anatoa mapepo kwa sababu mapepo ndio wanaoleta udhaifu na magonjwa. Unaweza ukawa unajitahidi hata kwenye masomo, biashara, kazi  lakini bado unaanguka. Lakini leo Bwana anasema na wewe atakuinua tena katika jina la Yesu.

Udhaifu ukiondolewa neno la Bwana linakuwa limetimia na mtu anakuwa mzima na kufanikiwa imeandikwa Mathayo 8:16-17Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,  Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.” Yesu anabeba udhaifu wetu, kwenye ndoa, masomo, kazi. Mathayo 9:35 imeandikwa, “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” Hapa tunaona udhaifu upo wa kila aina,wachawi ni wakala wa shetani, wachawi hutuma mapepo ndani ya mtu yanayopelekea udhaifu.

Mathayo 10:1 imeandikwa, “Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” Yesu aliaanza na mapepo, kwa sababu mapepo yakitoka kansa inatoka, uvimbe unatokaa, magonjwa yote yanatoka. Yesu aliwaita wanafunzi wake na si mkutano wote, Ili uweze kutoa pepo ni lazima uwe mwanafunzi wa Yesu (uokoke).

Mathayo 28:16-20 imeaandikwa, “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Kufanyika kuwa mwanafunzi wa Yesu ni lazima uokoke, wanafunzi walipewa mamlaka ya kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi. Amri ni kibali cha kutenda.
Platform Ministry wakiongoza sifa na kuabudu katika ibada ya leo.

Zaburi 138:7 imeandikwa, “Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa.”
Ayubu 2:3-7 imeandikwa, “Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu. Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.  Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake.  Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.” Shetani alimpiga Ayubu kwa majipu. Unatakiwa ujiulize huo uvimbe au mirija imeziba inawezekana ni kama Ayubu alivyopigwa na majipu na shetani.
Matukio ya kichawi ndani ya biblia yaliowapata watu.


Ububu na uziwi uliompta mtu tangu alipozaliwa. Marko 9:14-27 imeandikwa, “Hata walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao; mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu. Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaagaa, akitokwa na povu. Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama.
Children Ministry wakicheza na kusifu katika ibada ya leo.
Huyo pepo akimpagawa anambwagwa chini, anamuagushwa chini kichawi. Pia alikuwa anatokwa na povu kama kifafa lakini ni ukifafa wa kichawi. Pia alikuwa anatiwa kusaga meno na kukonda kutokana na mapepo. Unaweza kuwa unakula sana lakini unakondo kichawi, leo pokea mwili wako kwa jna la Yesu. Shetani/pepo anao uwezo wa kugeuka na kuwa Ukimwi/kukonda. Pepo anaweza kutia wasiwasi, hofu.  Mathayo 11:18 imeandikwa, “Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.” Hapa tunaona mapepo yanaweza kumfanya mtu ashindwe kula na kunywa.
Pepo anao uwezo wa kutupa kwenye moto au maji(marko 9:22). Moto na maji ni dalili ya kuangamiza. Unakuta kazi, nyumba, ndoa imetupwa kwenye maji au kwenye moto leo warudishe kwa jina la Yesu. Pepo anaweza kumfanya mtu aonekane ame kufa ili watu wote wadhani umeshakufa. Bwana akushike mkono uinuke tena kwa jina la Yesu.

Udhaifu wa ulemavu, Luka 13:10-16 imeandikwa, “Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato.  Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng'ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?

Huyu mwanamke alikuwa amepindana lakini ni pepo wa udhaifu aliyeingia ndani yake na kuleta udhaifu. Inawezekana masomo, ndoa, biashara yako vimepindana, haiwezi kunyooka lakini leo Bwana atanyoosha mkono wake kwenye mambo yako tena yanyooke.
Yohana 5:1-10 imeandikwa, “Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu. Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.] Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Majeshi ya Bwana akifunguliwa kutoka kwenye udhaifu wa kichawi
Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo. Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.” Inawezekana kuna ugonjwa unakusumbua kwa muda mrefu na hakuna yeyeto anayejua leo utapokea uzima kutoka kwa Yesu.
Zabari 103:3 imeandikwa, “Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,” Bwana anataka akakuponye leo, kwa kupigwa kwakke Yesu sisi tupata kupona. Isaya 53:3 imeandikwa, “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro       http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/