GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
MCHUNGAJI
KIONGOZI: DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMPILI: 17, DISEMBA, 2017
MHUBIRI: MCHUNGAJI, DKT. HAPINESS MUHIMBULA (RP)
Kwa kawaida shetani ana maeneo matatu
ya utawala. Maeneno hayo ni Bahari, Anga na Nchi kavu. Katika maeneo haya yote zina idara mbalimbali kwa ajili ya kufunga
maisha ya watu. Anweza akawa mzima mwilini lakini rohoni katekwa na maefungwa chini
ya bahari. Kupitia somo hili utajifunza kuhusu dalili za watu waliotekwa chini
ya bahari na namna ya kuwafungua. UFUNUO
WA YOHANA 12: 7-12 Imeandikwa, “Kulikuwa
na vita mbinguni; Mikaeli na malaika
zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika
zake; nao hawakushinda, wala mahali pao
hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani,
aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na
malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa
kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake;
kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za
Mungu wetu, mchana na usiku. Nao
wakamshinda kwa damu ya MwanaKondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao
hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa
hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa
maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana
wakati mchache tu.”
Mwanzo 6:1-3 Imeandikwa, “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi
usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao
binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye
ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.” Kuna maisha yanaendelea chini ya
bahari. Kuna kila kitu chini ya bahari,
magari, nyumba na vyumba vyake na kila aina ya starehe. Hawa ni mashetani wa
hali ya juu sana.
Tangu mwanzo maji yalichukua sehemu
kubwa ya dunia. Hakukuwa na utengano kati ya maji na nchi kavu. Shetani alipotupwa
chini alianzisha utawala wake huko chini. Makao makuu ya Ibilisi ni chini ya
bahari ya Hindi. Hapa Mungu anafundisha kwa habari za kuzimu ya Baharini. Kuzimu
ina mifumo ya kijeshi yenye ubunifu mkubwa kuliko majeshi ya serikali za wanadamu.
EZEKIELI 29:1-3 Imeandikwa, “Katika mwaka wa kumi, mwezi wa
kumi, siku ya kumi na mbili ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema, Mwanadamu,
elekeza uso wako juu ya Farao, mfalme wa Misri, ukatabiri juu yake, na juu ya
Misri yote; nena, useme, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe
Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto
wangu ni wangu mwenyewe, nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi yangu.” Huu
ni mto wa Farao lakini ndani yake kulikuwa na joka. Kuna wakati uliwai kupewa dawa
na mganga wa kienyeji na ukaelekezwa kuoga maji ya mto fulani.
ISAYA 27:1 Imeandikwa, “Katika siku hiyo Bwana, kwa
upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka
yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzongazonga; naye atamwua yule
joka aliye baharini.” naye atamwua Yule joka akaaye baharini. Maji ya
bahari yana muunganiko na mashetani. Lakini maji haya kila aliyeyatumia kwa
maelekezo ya waganga aliapatwa na balaa na mikosi.
UFUNUO WA YOHANA 10:1-6
Imeandikwa, “Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni,
amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama
jua, na miguu yake kama nguzo za moto. Na katika mkono wake alikuwa na kitabu
kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kuume juu ya bahari, nao wa kushoto
juu ya nchi. Naye akalia kwa sauti kuu,
kama simba angurumavyo. Na alipolia, zile ngurumo saba zikatoa sauti zao. Hata
ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika. Nami nalisikia
sauti kutoka mbinguni ikisema, Yatie muhuri maneno hayo yaliyonenwa na hizo
ngurumo saba, usiyaandike. Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari
na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, akaapa kwa yeye
aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na
nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na
wakati baada ya haya;”
Platform Ministry wakiongoza sifa na kuabudu katika ibada ya leo. |
Akaweka mguu wake juu ya bahari. Maana
yake ni kwamba shetani anakaa baharini, angani na nchi kavu. Kuzimu hii ya bahari ina malango, walinzi na
mageti yaliyofungwa kwa ustadi wa hali ya juu. Vifungo vya kuzimu ni kama vile walivyokuwa
wamefungwa wakina Paulo na Sila. Yawezekana kuna vitu au mtu aliyepelekwa
kuzimu. Kuzimu hii ina vyumba vyenye walinzi wa aina mbalimbali kuhakikisha
kila aliyefungwa hawezi kufunguliwa kutoka kuzimu. Vifungo vya namna hii
havitoki isipokuwa kwa maombi ya mwenye haki.
ISAYA 49:24-26 Imeandikwa, “Je! Aliye hodari aweza
kunyang'anywa mateka yake, au jeshi lao waliofungwa halali wataokoka? Naam,
Bwana asema hivi, Hata jeshi la wafungwa wake aliye hodari watapokonywa
mikononi mwake, na mateka yake aliye jabari wataokoka; kwa maana nitateta na
yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu. Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao
wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na
wote wenye mwili watajua ya kuwa mimi, Bwana, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako
ni Mwenye enzi wa Yakobo.” Mungu wetu ni mwenye nguvu hivyo tukiomba
kwa jina lake watafunguliwa. Kumbe kinachoweza kuwatoa watu baharini ni nguvu
ya Mungu kupitia jina la Yesu.
Baadhi ya Makutano waliompokea Yesu wakiongozwa sala ya Toba. |
ISAYA 42:22 Imeandikwa, “Lakini watu hawa ni watu
walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika
magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana
asemaye, Rudisha.” Ndio maana Mungu akamfunulia nabii Isaya kwamba kuna
watu wametekwa, kufungwa au wameuawa isivyo halali. Ndio maana Mungu akamwambia
Isaya lazima apatikane asemaye Rudisha. Mungu aliyasema haya kwa sababu anajua
bahari, mito na Maziwa yamemeza watu wengi. Lakini maombi ya kumtoa mtu
baharini ni maombi ya kivita ambayo yanahitaji kujikana.
UFUNUO WA YOHANA 17:1-2 Imeandikwa, “Akaja mmoja wa wale malaika saba,
wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu
ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao
wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.” huyu kahaba mkuu aketiye juu ya maji. Huyu ni
shetani katika mwili wa wanadamu. Ndio maana leo kuna watu wanafanya ukahaba
kwa sababu wote wamepandwa na roho za kishetani. Huyu ni shetani anayetenda
kazi hadi kwa wachungaji. Shetani anavuvuia roho ya ukahaba na uzinzi hata kwa
watu waliokoka. Lazima tusimame imara na kupambana kwa nguvu zako zote.
TABIA ZA WATU WALIOTEKWA BAHARINI
WANAKUWA NA KIBURI SANA. Ayubu 41:1 Ieandikwa,
“Je!
Waweza wewe kumvua mamba kwa ndoana? Au,
kuufunga ulimi wake kwa kamba?” kuna watu walikuwa wanyenyekevu lakini leo
wamekuwa na kiburi sana. Ukiona dalili kama hiyo faamu kuwa mtu huyo kashatekwa
na mashetani wa baharini.
KILA BIASHARA ANAYOANZA INAHARIBIKA. Watu
wa namna kila biashara atakayofanya huwa inaharibika kwa sababu mashetani wana
tabia ya kusimamia biashara. Ndio maana kuna waganga wanaotoa ulinzi wa
biashara kwa kuelekeza watu wakuge maji ya baharini.
KUVUNJIKA KWA NDOA. Watu waliotekwa chini ya bahari wana
tabia ya kupenda kuoa wake wengi. Katika
maisha haya
kuwa na mume mmoja na wake wengi
lazima vurugu zitokee. Ndio maana kuna talaka nyingi kwa watu wa mwambao
wa Pwani. ISAYA 4:1 Imeandikwa, “Na
siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula
chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee
aibu yetu.”
Makutano wakifuatilia neno la Mungu wakati wa Ibada kuhusu mateka chini ya Bahari. |
NDOA ZA KISHETANI. Kuna mengi yanayotokea leo duniani
kwa sababu ya watu wamemilikiwa na shetani. Ndio maana mwanaume anaweza kufunga ndoa na mwanaume
mwenzake. Hata walioana katika ulimwengu wa mwili bado ndoa zao zina matatizo
makubwa. Ni kwa sababu kuna mashetani yanayotawala maisha yao na ndio maana
hakuna furaha ya ndoa. Katika dalili kama hizi fahamu kuna mashetani kutoa
baharini. Mashetani wa bahari wametumwa kuchinja na kuharibu. Mwanaume anaweza
kumpa mkewe pesa kwa ajili ya matumizi lakini mke akanunua vitu kinyume na
matarajio. Ugomvi unaanzia hapo.
WANASIMAMIA MAVAZI AU WANAONGOZA MITINDO. Haya
mashetani wa baharini yana idara maalum inayohusika na kusimamia mitindo ya
vitu mbalimbali. Kuna mashetani yaliyotumwa kwa ajili ya mitindo ya mavazi. Kuna
mitindo ya mavazi, mawigi ya aina mbalimbali, namna ya kunyoa mfano Viduku. Staili
mbalimbali za kusuka nywele.
Baharini kuna idara nyingi sana na
zinasimamia matukio ya kutisha yanayotokea duniani. Kuna idara inayohusika na
kuanguka kwa majengo yenye watu wengi ili wachinjwe na kupelekwa kuzimu. Idara nyingine
inaratibu matukio ya ajali za moto.
Mchungaji Dkt. Hapiness Muhimbula (RP) akifungua mtu kutoka vifungo vya mashetani wa baharini. |
SABABU ZA KUTEKWA CHINI YA BAHARI
DHAMBI. Hii ni sababu ya kwanza ili mtu aweze
kutekwa na ibilisi. Kwa sababu kila atendaye dhambi upungukiewa na utukufu wa
Mungu.
MATAMBIKO. Haya ni matukio ya kimila yanayoambatana
na kutoa vitu mbalimbali. Katika matambiko mtu anaweza kupeleka kitovu cha
mtoto.
MUZIKI WA DUNIA. Muziki wa kidunia una uvuvio wa
kishetani. Kila muziki na wanamuziki wake wengi wanategemea mashetani wa
baharini.
Kuna sababu nyingi sana kama Mavazi. Wengine
wametekwa kwa sababu ya kuazima nguo za watu wengine. Wengine walichukuliwa kwa
sababu ya kuoga mtoni. Wengine ni kwa sababu ya sherehe za usiku na ngoma za
kienyeji.
Ukiri: Nakataa kukaa chini ya baharini
kwa jina la Yesu. Navaa uweza na silaha za Bwana za Vita na ninapambana na
mshetani waliotumwa kutokea baharini, mtoni, ziwani na ninawaondoa wote kwa
jina la Yesu. Ninaamuru malaika wa Bwana wavae sura yangu kwa uweza wa Roho
Mtakatifu na kuvamia malango ya bahari kwa jina la Yesu. Ninavunja silaha zote
ambazo majini ya baharini wamezituma kwangu, naziondoa leo kwa jina la Yesu. Nahama
leo kutoka vifungo vya kuzimu kwa jina la Yesu.
Binti akifunguliwa kutoka vifungo vya mashetani ya baharini. |
KWA MSAADA ZAIDI NA
MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/