GLORY
OF CHRIST TANZANIA CHURCH (GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
MHUBIRI:
MCHUNGAJI, DKT. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI
24, DISEMBA 2017
Udhaifu ni hali ambayo ikimpata mtu kuna mambo hawezi kuyafanya. Udhaifu
wa kichawi ni hali pia inayolenga mtu asiweze kutenda mambo Fulani mtu anakuwa
hawezi kuona, kusoma, kutunga mimba, kuoa au kuolewa, hawezi kujenga nyumba,
kula nyama/samaki anakuwa mtu wakuchangua vyakula vya kula hii ni kwa sababu
wachawi wamempandia kitu ndani yake ambao ni mapepo ya udhaifu yanamtia mtu
udhaifu asiweze kufanya jambo lolote.
Udhaifu wa kichawi unalenga pia kumfunga mtu katika udhaifu asisikie habari njema iliyoambatana na Baraka
zake au nyota yake ya mafanikio na kila anapojaribu kuenenda katika hatua yoyote ya maendeleo
anashindwa au anajisikia kutoweza
kabisa kabla ya kuanza pia udhaifu wa
kichawi unaweza kumfunika mtu asipate msaada wowote kutoka kwa watu.
Kuna mwingine uwezo wa
mtu upo kwenye mikono. Wachawi wakiona
hivyo wanawahi kufunga mikono, unakuta mikono ghafla imevimba wachawi wanakuwa
wamekuweke udhahifu. Kuna wengine uwezo wao upo kwenye ndoa. Ukioa au kuolewa
wanafanikiwa. Makapuni yatafunguliwa, biashara zitaanza wachawi wanaamu kukufunika
ili usionekane. Sasa panatakiwa apatikane mtu mmoja atakayeliitia jina la Bwana
vifuniko vitaondoka. Udhaifu unakuja kwako kupitia wachawi baada ya kutoa
sadaka na kisha anatuma mashetani ndani ya maisha ya mtu, kazi, biashara.
Mathayo 8: 14-16
imeandikwa, “Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye
mkewe, amelala kitandani hawezi homa. Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye
akaondoka, akawatumikia. Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo;
akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,” Yesu aliletewa
watu wenye mapepo na aliwaponya kwa neno lake wale wote ambao walikuwa hawaweziwalikuwa
hawawezi kwasababu ya mapepo yaliyokuwa ndani yao ndivyo ilivyo hata leo Kuna mambo yamekaa ndani ya maisha yako kwa
nanmna ya kutoweza, leo nalituma neno la Bwana likavunjevunje vifungo vyote kwa
jina la Yesu.
Mathayo 4:23
imeandikwa, “Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika
masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na
udhaifu wa kila namna katika watu.” Yesu alikuwa akihubiri habari njema za ufalme, akawaponya udhaifu na
magonjwa. Yesu alikuwa anatoa mapepo kwa sababu mapepo ndio wanaoleta udhaifu
na magonjwa. Unaweza ukawa unajitahidi hata kwenye masomo, biashara, kazi lakini bado unaanguka. Lakini leo Bwana
anasema na wewe atakuinua tena katika jina la Yesu.
Udhaifu ukiondolewa neno la Bwana linakuwa limetimia na mtu
anakuwa mzima na kufanikiwa imeandikwa Mathayo
8:16-17 “Hata kulipokuwa jioni,
wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote
waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya,
akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu,
Na kuyachukua magonjwa yetu.” Yesu anabeba udhaifu wetu, kwenye ndoa,
masomo, kazi. Mathayo 9:35
imeandikwa, “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha
katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa
yote na udhaifu wa kila aina.” Hapa tunaona udhaifu upo wa kila aina,wachawi
ni wakala wa shetani, wachawi hutuma mapepo ndani ya mtu yanayopelekea udhaifu.
Mathayo 10:1
imeandikwa, “Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo
wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” Yesu
aliaanza na mapepo, kwa sababu mapepo yakitoka kansa inatoka, uvimbe unatokaa,
magonjwa yote yanatoka. Yesu aliwaita wanafunzi wake na si mkutano wote, Ili uweze
kutoa pepo ni lazima uwe mwanafunzi wa Yesu (uokoke).
Mathayo 28:16-20
imeaandikwa, “Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule
aliowaagiza Yesu. Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona
shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni
na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza
kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote
niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata
ukamilifu wa dahari.” Kufanyika kuwa mwanafunzi wa Yesu ni lazima
uokoke, wanafunzi walipewa mamlaka ya kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi. Amri ni
kibali cha kutenda.
Platform Ministry wakiongoza sifa na kuabudu katika ibada ya leo. |
Zaburi 138:7 imeandikwa, “Nijapokwenda kati ya shida
utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa
kuume utaniokoa.”
Ayubu 2:3-7 imeandikwa, “Bwana akamwuliza Shetani, Je!
Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye
duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu;
naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake,
ili nimwangamize pasipokuwa na sababu. Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi
kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini
sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele
za uso wako. Bwana akamwambia Shetani,
Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana,
akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hata utosi wa kichwa.”
Shetani alimpiga Ayubu kwa majipu. Unatakiwa ujiulize huo uvimbe au mirija
imeziba inawezekana ni kama Ayubu alivyopigwa na majipu na shetani.
Matukio ya kichawi
ndani ya biblia yaliowapata watu.
Ububu na uziwi uliompta mtu tangu alipozaliwa. Marko 9:14-27 imeandikwa, “Hata
walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi
wakijadiliana nao; mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio,
wakamsalimu. Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? Mtu mmoja katika mkutano
akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; na kila ampagaapo,
humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na
wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. Akawajibu, akasema, Enyi kizazi
kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni
kwangu. Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye
akaanguka chini, akagaagaa, akitokwa na povu. Akamwuliza babaye, Amepatwa na
haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na
katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na
kutusaidia. Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. Mara
babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini
kwangu. Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo
mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala
usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama
amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua
naye akasimama.”
Huyo pepo akimpagawa anambwagwa chini, anamuagushwa chini
kichawi. Pia alikuwa anatokwa na povu kama kifafa lakini ni ukifafa wa kichawi.
Pia alikuwa anatiwa kusaga meno na kukonda kutokana na mapepo. Unaweza kuwa unakula
sana lakini unakondo kichawi, leo pokea mwili wako kwa jna la Yesu. Shetani/pepo
anao uwezo wa kugeuka na kuwa Ukimwi/kukonda. Pepo anaweza kutia wasiwasi,
hofu. Mathayo 11:18 imeandikwa, “Maana
Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo.” Hapa tunaona mapepo
yanaweza kumfanya mtu ashindwe kula na kunywa.
Pepo anao uwezo wa kutupa kwenye moto au maji(marko 9:22). Moto
na maji ni dalili ya kuangamiza. Unakuta kazi, nyumba, ndoa imetupwa kwenye
maji au kwenye moto leo warudishe kwa jina la Yesu. Pepo anaweza kumfanya mtu
aonekane ame kufa ili watu wote wadhani umeshakufa. Bwana akushike mkono uinuke
tena kwa jina la Yesu.
Udhaifu wa ulemavu, Luka
13:10-16 imeandikwa, “Siku ya sabato alikuwa akifundisha katika
sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu
muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu
alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka
mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. Basi mkuu wa
sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu,
akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe
katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki,
kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng'ombe wake au punda wake siku ya sabato katika
zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu,
ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo
hiki siku ya sabato?”
Huyu mwanamke alikuwa amepindana lakini ni pepo wa udhaifu
aliyeingia ndani yake na kuleta udhaifu. Inawezekana masomo, ndoa, biashara
yako vimepindana, haiwezi kunyooka lakini leo Bwana atanyoosha mkono wake
kwenye mambo yako tena yanyooke.
Yohana 5:1-10 imeandikwa, “Baada ya hayo palikuwa na
sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu. Na huko Yerusalemu
penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina
matao matano. Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu,
viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke. Kwa maana kuna wakati ambapo
malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye
aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa
umempata.] Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka
thelathini na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa
hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Majeshi ya Bwana akifunguliwa kutoka kwenye udhaifu wa kichawi |
Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia
birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka
mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu
akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si
halali kwako kujitwika godoro.” Inawezekana kuna ugonjwa unakusumbua kwa muda mrefu na
hakuna yeyeto anayejua leo utapokea uzima kutoka kwa Yesu.
Zabari 103:3 imeandikwa, “Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,” Bwana anataka akakuponye leo, kwa kupigwa
kwakke Yesu sisi tupata kupona. Isaya 53:3
imeandikwa, “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye
sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala
hatukumhesabu kuwa kitu.”
KWA MSAADA ZAIDI NA
MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
(WhatsAssp & SMS only)
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/