Sunday, March 18, 2018

MITEGO YA KICHAWI


GLORY OF CHRIST TAN ZANIA CHURCH (GCTC)
 KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 18 MACHI, 2018  
 
Mchungaji Kiongozi Dr. Godson Issa Zacharia akifundisha somo kuhusu Mitego ya kichawi.
Utangulizi:
Mtego kwa asili ni kama silaha ya kunasa mtu ambayo ni lazima iwekwe sehemu ya kificho ili kumnasa mtu bila yeye kujua. Mtego huwekwa kwa namna ya uzuri ili usiweze kuutambua. Mitego ya kichawi ni mitego inayotegwa na wanadamu wenye roho za kichawi ndani yao. Hii ni mitego inayotokana na mawakala wa shetani. Kwa kawaida kuna wanadamu wanaomtegemea Mungu na wengine wanamtegemea shetani. Kwa asili shetani na mawakala wake kazi yao ni kutengeneza uharibifu. Mitego ya kichawi ni silaha inayotegwa na wachawi ili kumnasa mtu. Silaha hii ni kama wavuvi wanavyotumia nyavu kuvua samaki.

AINA ZA UCHAWI
Uchawi wa kurithi; huu ni uchawi ambao unarithiwa toka kizazi kimoja mpaka kingine aidha ndani ya familia au ukoo. Inawezekana bibi/babu/shangazi/mama alikuwa mchawi akikaribia kufa anarithisha wengine ile mikoba ya kichawi.
Kuna uchawi wa ziwani yaani mtoto akizaliwa akinyonya tu anaanza kuwanga tangu utoto wake.
Uchawi wa kitabu uhawi huu unaumia kitabu kuloba, unakutandan ya majianawekewa kombe limeandikwa.
Uchawi wa kununua; mtu anaenda kununua uchawi anafundishwa na kuanza kuroga. Uchawi huu unafanyka juu ya watukwa sababuhetai anavuvia hii roho ndni yao. Kuna watu wanategwa  leo ili waumie, wachangayikiwe,  wakose   kazi.
Watu wamekuwa wachawi kwa sababu ya kurithi. Wengine wamekuwa wachawi tangu wakiwa watoto sana (tangu wakati wa kunyonya au ziwani). Wengine ni wanatumia uchawi wa Kitabu. Huu ni uchawi unaotegemea maandishi yaliyoandikwa kwenye lugha ya kiarabu. Mwingine ni uchawi wa kununua. Mtu analipa na kununua uchawi, na baadae lazima ajifunze na hatimaye anakuwa mchawi. Uchawi huu wote unategemea nguvu kutoka kwa shetani.

“Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.” Maombolezo 3:33
Mungu hapendi kuwangamiza wala kuwatesa watu. Sehemu ambayo kuna uchawi kuna umaskini, yaani kama ni mji unakuta hakuna furaha, nyumba, pesa hakuna. Leo Bwana Yesu  akakuokoe na mkono wa kichawi. Wachawi wnaweza kukutegea mitego ili uliwe nyama. Ili unaswe mchawi anaangalia pale ambako hauna taarifa na hujui lolote. Mchawi anaangalia pale ambako huwezi kujua ndio unapotegwa. Kila penye uchawi pamejaa matukio ya kutisha na ya kushangaza.

Baadhi ya Makutano wakimwabudu Mungu wakati wa Ibada ya Leo.
Anayetega mtego huwa anauweka mahali ambapo huwezi kujua ili ukamatwe au unaswe vizuri. Mtego unategwa pale ambapo huna taarifa. Mtegaji huwa anaweka mtego mahali usipotarajia. Kwa kawaida mtegaji huwa anaweka kitu cha kukuvutia bila kujua. Unaweza ukanaswa kwenye kazi, miradi na kwa kile unachofanya. Mashetani wanakutega wakati usioutarajia na mtego lazima ukunase kwa ghafla. Mtego lazima ufichwe ili mtu aweze kunaswa.

“Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafula.” Mhubiri 9:12

Mitego huwa inawalenga wanadamu. Na mitego huwa wanategewa watu wanaokaa duniani. Wategaji huwa wanakuwekea roho ya hofu na kukuchimbia mashimo.
“Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.” Isaya 24:17

Kwa asili mitego utegwa katika siri. Kumbe ili shetani aweze kumnasa mtu lazima utegwe sehemu ya siri. Mtego unawekwa kwa namna ya uzuri lakini ndani yake kuna ubaya. Kinaweza kuwa kitu lakini nyuma yake kuna uovu ndani yake.
“Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu.” Zaburi 31:4

Neno la Mungu linasisitiza zaidi kwamba mitego huwa haiwezi kukaa sehemu za wazi. Kwa hiyo mtego huwekwa sehemu za faragha ili usiweze kutambua kama umetegwa. Mitego huwa inawekwa kulingana na unyonge wa mtu. Mtu kama ana unyonge wa kupenda wasichana, pombe au sigara, kwa hiyo mtu atawekewa mtego kupitia unyonge wake. Na mashetani wakiona hawawezi kukutega wanaanza kukuwekea roho ya unyonge. Ulikuwa unaweza kuomba kwa muda mrefu lakini kasi yako inapungua. Mpaka unakuja kushtuka, kumbe ulisha chelewa.

“Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Akimkokota wavuni mwake” Zaburi 10:9
 
Katikati ya Ibada mitego iliteguliwa na dada huyu akawekwa huru kwa Jina la Yesu
Mitego mara zote utegwa faragani. Na mitego hii huwa wanategewa watu wale waliokamilika. Watu walio wakamilifu ni wale wana wa Mungu au waliokoka. Ukiona mtu alikuwa na bidii ya kumtafuta Mungu lakini ikapungua ghafla. Jua kuna mtego mtu huyo aliwekewa faraghani na amenaswa.

“Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.” Zaburi 64:4

Ifike wakati ambao wachawi wakikuona waogope. Ifike wakati ambao wachawi wakitaja jina lako waungue kwa sababu ya nguvu iliyo ndani yako. Kataa kuwa Mkristo legelege. Jifunze kuomba kwa bidii ili usiweze kuvamiwa na mashetani.

Kwa kawaida mtego unafichwa, huwa hauwekwi sehemu iliyo wazi. Unaweza kuona njia ni nzuri lakini kumbe kuna mtego. Wachawi siku zote wanaweka mitego kwenye njia ya kuyaendea mafanikio yako. Ndio maana unaweza kuona mtu ameenda kwenye usaili na akakataliwa. Inaweza kuwa njia ya kwenda kwenye masomo, biashara, huduma, miradi au ndoa lakini imewekewa mitego na tanzi. Watu wanawekewa kamba na kunaswa kwa hizo kamba. Kuna mtu amekuja kama rafiki kumbe ni mtego kwako.
 
Platform team wakimwabudu Mungu wakati wa Ibada ya leo.
“Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.” Zaburi 140:5

Mungu hapendi kuona wanadamu wakitegewa mitego. Na Mungu ametoa laana kwa wachawi kwa sababu ya mitego yao.
“Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.” Kumbukumbu 27:24

“Watendao uovu wamenitegea mtego, Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.” Zaburi 119:110

“Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu.” Zaburi 141:9
“Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.” Zaburi 91:3

“Nafsi yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.” Zaburi 124:7

NAMNA WACHAWI WANAWEZA KUTEGA MITEGO.

Wachawi wanaweza kutega mtego njia panda, uvunguni, chumbani, mezani kwako, ofisini au Gari unalotumia. Pengine wanaweza kufukia mtego karibu na mlango wa nyumba yako. Wachawi wanaweza kutega mtego kwenye biashara, masomo, kazi, uchumi au ndoa yako.

Wachawi wanaweza kutega nafsi ya mwanadamu. Nafsi ya mtu ikinaswa ni hatari. Nafsi ya mtu ikinaswa mtu anapoteza utashi wa kutenda na hawezi kuthubutu. Unaweza kujisikia moyoni mwako kutenda uovu lakini jua hapo kuna mtego. Wachawi wanatumia nyenzo kama HIRIZI, ZINDIKO au LESO ili kumnasa mtu.
 
Mchungaji Kiongozi akifungua watu kutoka mitego ya kichawi
“Useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?” Ezekieli 13:18

Ni hakika kwamba mtu anaweza kunaswa kwenye mtego wa uovu. Mitego hii inaweza kuelekezwa kwenye shule, kazi, uchumba, biashara au ndoa yako. Mitego hii huwa inalenga kukurudisha nyuma. Yawezekana ulikuwa unaelekea kwenye mafanikio au hatima ya maisha yako lakini huwezi kwenda kwa sababu ya mtego wao. Mtego unaweza kuwekwa kuzunguka nyumba yako, biashara au ofisi yako na ukanaswa kabisa.

Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego; hutega mtego, na kunasa watu. Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji. Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo? Asema Bwana; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna hii?” Yeremia 5:26-29
 
Baadhi ya Makutano wakimchezea Bwana baada ya kutegeua Mitego ya Kichawi. 
Ni hakika kwamba mitego haiwezi kuonekana kwa macho lakini ipo na inatenda kazi. Kwa kawaida mitego uambatana na matanzi. Hizi zote za mashetani zinazotumika kuhakikisha kwamba mtu hawezi kuyafikia mafanikio yake. Kuna vitu umejaribu lakini hujawai kupata faida. Kuna hali ya ugumu unayoipitia kwa sababu kuna mtu ameweka mtego mahali. Lakini Imeandikwa Bwana atakuokoa na mtego wa mwindaji. Tena imeandikwa kwamba kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa.

Kama mvuvi anavyovua samaki ndivyo wategao mitego walivyo. Mvuvi akishaweka wavu majini, samaki walionaswa huwa wanatolewa ndani na kuwekwa nchi kavu ili wapoteze uhai. Hata wachawi wako vilevile, wakishamnasa mtu kwa wavu au mitego yao, hatua ya pili ni kumvua mtu. Maana yake ni kwamba baada ya kunaswa kinachofuatwa ni kuchinja na kuharibu. Wanaweza kunasa akili, mapato, kazi, nyota ili wale matunda ya kazi yako. Lakini unaweza kuwatoroka kwa jina la Yesu. Wapige na utoke kwenye himaya yao kwa jina la Yesu.

“Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Yohana 10:10
 
Children Ministry pamoja na Showers of Glory Morogoro wakipiga Salute kama salamu ya wana wa Ufufuo na Uzima.
KWA MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr. Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778
BLOG: Ufufuo na Uzima Morogoro       http://ufufuonauzimamorogoro.blogspot.com/






Share:
Powered by Blogger.

Pages