GLORY OF CHRIST TAN ZANIA CHURCH
(GCTC)
KANISA
LA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO
PASTOR DR. GODSON ISSA ZACHARIA
JUMAPILI: 18 MACHI, 2018
Utangulizi:
Mtego kwa asili ni kama silaha ya
kunasa mtu ambayo ni lazima iwekwe sehemu ya kificho ili kumnasa mtu bila yeye kujua.
Mtego huwekwa kwa namna ya uzuri ili usiweze kuutambua. Mitego ya kichawi ni
mitego inayotegwa na wanadamu wenye roho za kichawi ndani yao. Hii ni mitego
inayotokana na mawakala wa shetani. Kwa kawaida kuna wanadamu wanaomtegemea
Mungu na wengine wanamtegemea shetani. Kwa asili shetani na mawakala wake kazi
yao ni kutengeneza uharibifu. Mitego ya kichawi ni silaha inayotegwa na wachawi
ili kumnasa mtu. Silaha hii ni kama wavuvi wanavyotumia nyavu kuvua samaki.
AINA ZA UCHAWI
Uchawi
wa kurithi; huu ni uchawi ambao unarithiwa toka kizazi kimoja mpaka kingine
aidha ndani ya familia au ukoo. Inawezekana bibi/babu/shangazi/mama alikuwa
mchawi akikaribia kufa anarithisha wengine ile mikoba ya kichawi.
Kuna uchawi wa ziwani yaani mtoto akizaliwa
akinyonya tu anaanza kuwanga tangu utoto wake.
Uchawi wa kitabu uhawi huu unaumia kitabu kuloba, unakutandan
ya majianawekewa kombe limeandikwa.
Uchawi wa kununua; mtu anaenda kununua uchawi anafundishwa na
kuanza kuroga. Uchawi huu unafanyka juu ya watukwa sababuhetai anavuvia hii
roho ndni yao. Kuna watu wanategwa leo
ili waumie, wachangayikiwe, wakose kazi.
Watu wamekuwa wachawi kwa sababu ya
kurithi. Wengine wamekuwa wachawi tangu wakiwa watoto sana (tangu wakati wa
kunyonya au ziwani). Wengine ni wanatumia uchawi wa Kitabu. Huu ni uchawi
unaotegemea maandishi yaliyoandikwa kwenye lugha ya kiarabu. Mwingine ni uchawi
wa kununua. Mtu analipa na kununua uchawi, na baadae lazima ajifunze na
hatimaye anakuwa mchawi. Uchawi huu wote unategemea nguvu kutoka kwa shetani.
“Maana
moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.” Maombolezo 3:33
Mungu hapendi kuwangamiza wala
kuwatesa watu. Sehemu ambayo kuna uchawi kuna umaskini, yaani kama ni mji
unakuta hakuna furaha, nyumba, pesa hakuna. Leo Bwana Yesu akakuokoe na mkono wa kichawi. Wachawi
wnaweza kukutegea mitego ili uliwe nyama. Ili unaswe mchawi anaangalia pale
ambako hauna taarifa na hujui lolote. Mchawi anaangalia pale ambako huwezi
kujua ndio unapotegwa. Kila penye uchawi pamejaa matukio ya kutisha na ya
kushangaza.
Anayetega mtego huwa anauweka mahali
ambapo huwezi kujua ili ukamatwe au unaswe vizuri. Mtego unategwa pale ambapo
huna taarifa. Mtegaji huwa anaweka mtego mahali usipotarajia. Kwa kawaida
mtegaji huwa anaweka kitu cha kukuvutia bila kujua. Unaweza ukanaswa kwenye
kazi, miradi na kwa kile unachofanya. Mashetani wanakutega wakati usioutarajia
na mtego lazima ukunase kwa ghafla. Mtego lazima ufichwe ili mtu aweze kunaswa.
“Maana
mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya,
na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati
mbaya, unapowaangukia kwa ghafula.” Mhubiri 9:12
Mitego huwa inawalenga wanadamu. Na
mitego huwa wanategewa watu wanaokaa duniani. Wategaji huwa wanakuwekea roho ya
hofu na kukuchimbia mashimo.
“Hofu,
na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.” Isaya 24:17
Kwa asili mitego utegwa katika siri.
Kumbe ili shetani aweze kumnasa mtu lazima utegwe sehemu ya siri. Mtego
unawekwa kwa namna ya uzuri lakini ndani yake kuna ubaya. Kinaweza kuwa kitu
lakini nyuma yake kuna uovu ndani yake.
“Utanitoa
katika wavu walionitegea kwa siri, Maana Wewe ndiwe ngome yangu.” Zaburi 31:4
Neno la Mungu linasisitiza zaidi
kwamba mitego huwa haiwezi kukaa sehemu za wazi. Kwa hiyo mtego huwekwa sehemu
za faragha ili usiweze kutambua kama umetegwa. Mitego huwa inawekwa kulingana
na unyonge wa mtu. Mtu kama ana unyonge wa kupenda wasichana, pombe au sigara,
kwa hiyo mtu atawekewa mtego kupitia unyonge wake. Na mashetani wakiona
hawawezi kukutega wanaanza kukuwekea roho ya unyonge. Ulikuwa unaweza kuomba
kwa muda mrefu lakini kasi yako inapungua. Mpaka unakuja kushtuka, kumbe ulisha
chelewa.
“Huotea
faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu
mnyonge, Akimkokota wavuni mwake” Zaburi 10:9
Mitego mara zote utegwa faragani. Na
mitego hii huwa wanategewa watu wale waliokamilika. Watu walio wakamilifu ni
wale wana wa Mungu au waliokoka. Ukiona mtu alikuwa na bidii ya kumtafuta Mungu
lakini ikapungua ghafla. Jua kuna mtego mtu huyo aliwekewa faraghani na
amenaswa.
“Wapate
kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.” Zaburi 64:4
Ifike wakati ambao wachawi wakikuona
waogope. Ifike wakati ambao wachawi wakitaja jina lako waungue kwa sababu ya
nguvu iliyo ndani yako. Kataa kuwa Mkristo legelege. Jifunze kuomba kwa bidii
ili usiweze kuvamiwa na mashetani.
Kwa kawaida mtego unafichwa, huwa
hauwekwi sehemu iliyo wazi. Unaweza kuona njia ni nzuri lakini kumbe kuna
mtego. Wachawi siku zote wanaweka mitego kwenye njia ya kuyaendea mafanikio
yako. Ndio maana unaweza kuona mtu ameenda kwenye usaili na akakataliwa.
Inaweza kuwa njia ya kwenda kwenye masomo, biashara, huduma, miradi au ndoa
lakini imewekewa mitego na tanzi. Watu wanawekewa kamba na kunaswa kwa hizo
kamba. Kuna mtu amekuja kama rafiki kumbe ni mtego kwako.
“Wenye
kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea
matanzi.” Zaburi 140:5
Mungu hapendi kuona wanadamu wakitegewa
mitego. Na Mungu ametoa laana kwa wachawi kwa sababu ya mitego yao.
“Na
alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.” Kumbukumbu
27:24
“Watendao
uovu wamenitegea mtego, Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.” Zaburi 119:110
“Unilinde
na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu.” Zaburi 141:9
“Maana
Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.” Zaburi 91:3
“Nafsi
yetu imeokoka kama ndege Katika mtego wa wawindaji, Mtego umevunjika, nasi
tumeokoka.” Zaburi 124:7
NAMNA
WACHAWI WANAWEZA KUTEGA MITEGO.
Wachawi wanaweza kutega mtego njia
panda, uvunguni, chumbani, mezani kwako, ofisini au Gari unalotumia. Pengine
wanaweza kufukia mtego karibu na mlango wa nyumba yako. Wachawi wanaweza kutega
mtego kwenye biashara, masomo, kazi, uchumi au ndoa yako.
Wachawi wanaweza kutega nafsi ya
mwanadamu. Nafsi ya mtu ikinaswa ni hatari. Nafsi ya mtu ikinaswa mtu anapoteza
utashi wa kutenda na hawezi kuthubutu. Unaweza kujisikia moyoni mwako kutenda
uovu lakini jua hapo kuna mtego. Wachawi wanatumia nyenzo kama HIRIZI, ZINDIKO
au LESO ili kumnasa mtu.
“Useme,
Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo
vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za
watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe?”
Ezekieli 13:18
Ni hakika kwamba mtu anaweza kunaswa
kwenye mtego wa uovu. Mitego hii inaweza kuelekezwa kwenye shule, kazi,
uchumba, biashara au ndoa yako. Mitego hii huwa inalenga kukurudisha nyuma.
Yawezekana ulikuwa unaelekea kwenye mafanikio au hatima ya maisha yako lakini
huwezi kwenda kwa sababu ya mtego wao. Mtego unaweza kuwekwa kuzunguka nyumba
yako, biashara au ofisi yako na ukanaswa kabisa.
“Maana
katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mitego;
hutega mtego, na kunasa watu. Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao
zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. Wamewanda sana, wang'aa;
naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate
kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji. Je! Nisiwapatilize kwa mambo hayo?
Asema Bwana; na nafsi yangu, je! Nisijilipize kisasi juu ya taifa la namna
hii?” Yeremia 5:26-29
Ni hakika kwamba mitego haiwezi
kuonekana kwa macho lakini ipo na inatenda kazi. Kwa kawaida mitego uambatana
na matanzi. Hizi zote za mashetani zinazotumika kuhakikisha kwamba mtu hawezi
kuyafikia mafanikio yake. Kuna vitu umejaribu lakini hujawai kupata faida. Kuna
hali ya ugumu unayoipitia kwa sababu kuna mtu ameweka mtego mahali. Lakini Imeandikwa
Bwana atakuokoa na mtego wa mwindaji. Tena imeandikwa kwamba kila silaha
itakayofanyika juu yako haitafanikiwa.
Kama mvuvi anavyovua samaki ndivyo
wategao mitego walivyo. Mvuvi akishaweka wavu majini, samaki walionaswa huwa
wanatolewa ndani na kuwekwa nchi kavu ili wapoteze uhai. Hata wachawi wako vilevile,
wakishamnasa mtu kwa wavu au mitego yao, hatua ya pili ni kumvua mtu. Maana
yake ni kwamba baada ya kunaswa kinachofuatwa ni kuchinja na kuharibu. Wanaweza
kunasa akili, mapato, kazi, nyota ili wale matunda ya kazi yako. Lakini unaweza
kuwatoroka kwa jina la Yesu. Wapige na utoke kwenye himaya yao kwa jina la
Yesu.
“Mwivi
haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha
wawe nao tele.” Yohana 10:10
Children Ministry pamoja na Showers of Glory Morogoro wakipiga Salute kama salamu ya wana wa Ufufuo na Uzima. |
KWA
MSAADA ZAIDI NA MAOMBEZI WASILIANA NASI KUPITIA
FACEBOOK: Pastor Dr Godson Issa
Zacharia
Follow us on INSTAGRAM: pastordrgodson
Follow us on YOUTUBE: Pastor Dr.
Godson Zacharia
TEL: +255 719 798 778